Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili
kushoto-mstari wa pili), Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico,
Liberata Mulamula (nyuma ya waziri) wakimsikiliza kwa makini Rais Barack
Obama (hayupo pichani) wakati alipokuwa anatoa hotuba yake katika
Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani
uliofanyika katika Ukumbi wa Loy Henderson wa Wizara ya Mambo ya Nje,
jijini Washington DC nchini humo leo. Mkutano huo uliowashirikisha
Mawaziri wanaoshughulika na masuala ya usalama kutoka mataifa mbalimbali
duniani, Maafisa Waandamizi wa Umoja wa Mataifa (UN), Vyama vya Kiraia
na Sekta Binafsi ulijadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupambana na
vurugu na ugaidi dunaini. Katika hotuba yake, Obama alisema mapambano
dhidi ya watu wenye msimamo mkali hayawezi kulinganishwa na mapambano
dhidi ya waislamu, hivyo hakuna dini yoyote inayowajibika kwa ugaidi,
isipokuwa watu ndio wanaowajibika kwa vurugu na ugaidi. Picha zote na
Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.