Bw. John Michael Haule |
TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bw. John Michael Haule, kuwa Balozi mpya wa Tanzania nchini Kenya.
Kabla
ya uteuzi huu, Bw. Haule alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa kuanzia mwaka 2011 hadi uteuzi huu.
Aidha, Rais Kikwete amemhamisha
kituo Balozi
Batilda Burian kutoka Nairobi, Kenya kwenda Tokyo, Japan kujaza
nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Salome Sijaona ambaye anarejea nyumbani baada ya
kustaafu.
Imetolewa na:
Imetolewa na:
Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
05 Februari, 2015
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.