Mkutano wa Makatibu Wakuu wanaoshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango katika Jumuiya ya Afrika Mashariki unafanyika jijini Arusha, Tanzania tarehe 4 Novemba 2021.
Mkutano
huu na mkutano wa ngazi ya wataalamu uliofanyika tarehe 1 na 2 Novemba 2021 ni
sehemu ya mikutano ya awali kwa ajili ya maandalizi ya Mkutano wa 32 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta
linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango utakaofanyika jijini Arusha tarehe 5 Novemba 2021.
Mikutano
hii ya awali pamoja
na mambo mengine ina jukumu la kupitia na kuwasilisha agenda na mapendekezo ya
masuala mengine ya kikanda yatakayojadiliwa katika mkutano wa Baraza la Mawaziri la Kisekta
linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango.
Ujumbe
wa Tanzania kwenye mkutano wa Makatibu Wakuu unaongozwa na Katibu Mkuu, Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Laurean Ndumbaro
ambaye amemuwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine.
Viongozi
wengine walioambatana na Dkt. Ndumbaro katika mkutano huo ni pamoja na; Naibu
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Evaristo Longopa, Katibu Mkuu, Wizara ya Biashara na
Maendeleo ya Viwanda – Zanzibar, Dkt. Islam Seif Salum, Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Harshil Adballah, na Afisa Mtendaji Mkuu,
Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) Bw. Nicodemus Mkama.
|
Mwenyekiti wa Mkutano wa Makatibu Wakuu ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Kenya, Mhe. Dkt. Kevit Desai (wa pili kushoto) akiongoza Mkutano wa Makatibu Wakuu unaofanyika jijini Arusha tarehe 4 Novemba 2021 kwa ajili ya maandalizi ya Mkutano wa 32 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango utakaofanyika jijini Arusha tarehe 5 Novemba 2021. |
|
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Laurean Ndumbaro (kulia) akiongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Makatibu Wakuu wanaoshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango katika Nchi za Afrika Mashariki, Kushoto ni Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Evaristo Longopa. |
|
Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu, Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda – Zanzibar, Dkt. Islam Seif Salum, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Harshil Adballah, na Afisa Mtendaji Mkuu, Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) Bw. Nicodemus Mkama wakifuatilia mkutano. |
|
Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi na Mkurugenzi wa Uendelezaji wa Sera Ofisi ya Rais, Menejementi ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi Agnes Meena wakifuatilia mkutano.
|
Kutoka Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi idara ya Sera na Mipango katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Justin Kisoka na Afisa Biashara Mkuu katika Wizara ya Viwanda na Biashara, Bw. Abdul Chacha wakifuatilia mkutano.
| Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia mkutano. |
|
|
Ujumbe wa Burundi |
|
Ujumbe wa Kenya |
|
Ujumbe wa Uganda |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.