|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimsikiliza Balozi wa Korea ya Kusini aliyemaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini Mhe. Tae-ick Cho wakati alipokwenda kumuaga Mhe. Waziri katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam |
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimueleza jambo Balozi wa Korea ya Kusini aliyemaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini Mhe. Tae-ick Cho katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam |
|
Balozi wa Korea ya Kusini aliyemaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini Mhe. Tae-ick Cho akimkabidhi zawadi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula alipofika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam kumuaga
|
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimkabidhi zawadi ya picha ya jahazi Balozi wa Korea ya Kusini aliyemaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini Mhe. Tae-ick Cho katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
|
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwa na Balozi wa Korea ya Kusini aliyemaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini Mhe. Tae-ick Cho katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Caesar Waitara. |
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata
Mulamula (Mb) amekutana na kumuaga Balozi wa Korea ya Kusini aliyemaliza muda
wake wa uwakilishi hapa nchini Mhe. Tae-ick Cho katika Ofisi Ndogo za Wizara
Jijini Dar es Salaam.
“Katika kipindi chake cha uwakilishi ameiwakilisha vyema nchi yake na
kufurahishwa na namna ushirikiano baina ya Tanzania na Korea ya Kusini
ulivyoimarika hasa katika miradi ya maendeleo ya kimkakati na nimemuomba aendelee
kuwa Balozi mzuri wa Tanzania huko aendako,” amesema Balozi Mulamula.
Nae Balozi wa Korea ya Kusini aliyemaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini,
Mhe. Tae-ick Cho ameipongeza Tanzania kwa hatau mbalimbali za maendeleo ya
kiuchumi, kijamii na kisiasa ambazo imekuwa ikizichukua chini ya Uongozi
imara wa Rais Samia Suluhu Hassan.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.