Na Mwandishi wetu, Dar
Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa
Korea (DPRK) zimekubaliana kuimarisha misingi ya uhusiano wa kidiplomasia baina
ya mataifa hayo kwa maslahi mapana ya pande zote mbili.
Ahadi
hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Balozi Liberata Mulamula pamoja na Balozi wa Korea Kaskazini mhe. Kim Yong Su walipokutana
leo kwa mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Waziri
Mulamula amesema Tanzania na Korea Kaskazini zitaendelea kushikiana katika kuimarisha
zaidi misingi ya uhusiano baina ya nchi hizo kwa kuzingatia Sera ya Mambo ya
Nje ya Tanzania.
“Nimemhakikishia
Balozi wa Korea Kaskazini kuwa sisi misingi yetu ya Sera ya Mambo ya Nje
(Tanzania) haijabadilika iko vilevile, na tutaendelea kuimarisha uhusiano wetu,
amesema Waziri Mulamula.
Kwa
upande wake Balozi wa Korea Kaskazini hapa nchini, Mhe. Kim Yong Su amesema
kuwa Korea na Tanzani ni marafiki wa muda mrefu na kwa mkutano wetu tumejadili
namna ya kuboresha uhusiano wetu wa kidiplomasia.
Balozi
Kim Yong Su amesema kuwa pamoja na mambo mengine wamekubaliana kuboresha
uhusiano wa kidiploasia kwa maslahi ya pande zote mbili.
“Ushirikiano
wa Korea Kusini na Tanzania ni mzuri na imara ………. naahidi kuwa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Watu wa Korea itaendelea kushirikiana na Tanzania kiutamaduni,
kisiasa, kiuchumi, ulinzi na kilimo hii ikiwa ni jitihada za kuimarisha
ushirikiano wetu kwa maslahi ya mataifa yetu,” amesema Balozi Su.
Balozi
Su ameongeza kuwa Korea Kaskazini inapongeza jitihada mbalimbali ambazo
zimekuwa zikichukuliwa na Tanzania katika kuhakikisha inasonga mbele
kimaendeleo katika nyanja za kiuchumi pamoja na kuimarisha/kuboresha diplomasia
na mataifa mengine duniani.
“Nampongeza
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada
mbalimbali anazaochukua katika kuimarisha uchumi wa Tanzania na wananchi wake
pamoja na kidiplomasia,” ameongeza Balozi Su.
Tanzania
na Korea Kaskazini zilianzisha uhusiano wa kidiplomasia Aprili, 1992, ambapo nchi
hizi zimekuwa zikishirikiana kidiplomasia katika sekta ya elimu, afya, sayansi
na utamaduni pamoja na utalii.
Katika
tukio jingine, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Balozi Liberata Mulamula amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi wa
Heshima wa Kazakhstan nchini Tanzania Bw. Ameir Nahdi ambapo viongozi hao
wajejadili masuala mbalimbali ikiwemo za biashara na uwekezaji katika sekta za mafuta
na gesi, kilimo pamoja na uchimbaji na uchakataji wa madini na utalii.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiongea
na Balozi wa Korea Kaskazini nchini Mhe. Kim Yong Su katika Ofisi Ndogo za
Wizara Jijini Dar es Salaam
Balozi
wa Korea Kaskazini hapa nchini Mhe. Kim Yong Su akimuelezea jambo Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula walipokutana
kwa mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Mkutano
wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata
Mulamula na Balozi wa Korea Kaskazini hapa nchini Mhe. Kim Yong Su ukiendelea
katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula katika
picha ya pamoja na Balozi wa Korea Kaskazini hapa nchini Mhe. Kim Yong Su mara
baada ya kumaliza mkutano wao leo katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akizungumza
na Mwakilishi wa Heshima wa Kazakhstan nchini Tanzania Bw. Ameir Nahdi katika
Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam
Mwakilishi
wa Heshima wa Kazakhstan nchini Tanzania Bw. Ameir Nahdi akiongea na Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula wakati
walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.