Wafanyabiashara maarufu nchini Oman wanatarajiwa
kufanya ziara nchini tarehe 25 Novemba 2025 kwa ajili ya kukamilisha taratibu
za kupata eneo mkoani Tanga la kukusanyia mifugo hai ya kusafirisha Oman
kupitia bandari ya Tanga. Wafanyabiashara hao ambao ni Mkurugenzi
Mwendeshaji wa Abu Suleiman Al-Darai Trading &Services, Bw. Mohamed S. Aldarai; Afisa Mtendaji Mkuu wa
Desert Cold Store LLC, Dkt. Munawar H. Pardhan; Mkurugenzi wa Desert Cold Store
LLC, Bw. Aasim M. Pardhan na Mkurugenzi wa IKTIMAl Trading Company LLC, Bw. Salem
Al Dighaishi awali walikuwa wanasafirisha nyama iliyogandishwa tani 240 kwa
mwezi kutoka nchini walifanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Oman,
Mhe. Abdallah Kilima hivi karibuni kuhusu taratibu za utekelezaji wa biashara
yao hiyo.
Mhe. Balozi aliwapongeza
wafanyabiashara hao kwa kuonesha nia ya kufanya biashara na Tanzania kwani
itasaidia kubadilisha urari wa biashara kati ya nchi hizi mbili ambao kwa sasa
inaonesha Oman inauza zaidi nchini Tanzania. Aliwaahidi wafanyabiashara hao
kuwa atawakutanisha na Mamlaka husika nchini Tanzania akiwemo Mkurugenzi wa
Idara ya Diplomasia ya Uchumi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Balozi Edwin Rutageruka ili kukamilisha taratibu husika.
Wafanyabiashara hao walielezea malengo
yao ya baadaye ni kufanyabiashara ya kusafirisha matunda kutoka nchini kwenda
Oman na nchi nyingine za ghuba, jambo ambalo litasaidia wakulima wa Tanzania
kupata soko na kuondoa uharibifu wa matunda yanayoharibika kwa kukosa soko. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.