Na Mwandishi Wetu,
Waziri
wa Nishati Mhe. January Makamba (Mb), amewasilisha Ujumbe Maalum wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa Rais wa Umoja wa
Falme za Kiarabu (UAE) Mhe. Khalifa Bin Zayed Al Nahyan.
Mhe.
Makamba amewasilisha ujumbe huo Maalum kupitia kwa Waziri wa Nchi
anayeshughulikia Mambo ya Nje, Mhe. Sheikh Shakhbout bin Nahyan Al Nahyan,
tarehe 24 Oktoba 2021 katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa ya UAE.
Waziri
Makamba yupo nchini Umoja wa Falme za Kiarabu kwa ziara ya kikazi kwa lengo la
kuimarisha ushirikiano katika masuala Mafuta na Gesi.
Waziri Makamba ameambatana na Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Falme za Kiarabu, Mhe. Mohamed Mtonga, Kamishina wa Nishati na Gesi kutoka Wizara ya Nishati pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Petroli Nchini (TPDC).
Waziri
wa Nishati Mhe. January Makamba akizungumza na Waziri wa Nchi anayeshughulikia
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa UAE Mhe. Sheikh Shakhbout bin
Nahyan Al Nahyan |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.