Na Mwandishi Wetu, Dar
Tanzania
imezihakikishia Kampuni za Kifaransa kuwa mazingira ya biashara na uwekezaji ni
salama na kuwasihi kuwekeza kwa wingi hapa nchini.
Akiongea
na Waandishi wa Habari mara baada ya kumalizika kwa kongamano lililowakutanisha
Mawaziri wa Kisekta, wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Ufaransa Jijini Dar
es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi
Liberata Mulamula (Mb) amesema Serikali imewahakikishia wafanyabishara na
wawekezaji wa kampuni za Kifaransa kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inajenga na
inaendelea kuboresha mazingira rafiki ya uwekezaji kwa kuondoa kero mbalimbali
zilizokuwa zinawakabili wawekezaji hapa nchini.
“Serikali
ya Awamu ya Sita iko serious….. na tuna azma kubwa ya kuhakikisha kwamba
tunajenga mazingira rafiki ya kuweza kuwekeza na kuondoa kero zote ambazo
zimekuwa zinajitokeza….na makampuni mengine yameeleza hizo kero lakini
tunafurahi kuona kero hizo tayari zimeanza kuondolewa,” amesema Balozi Mulamula
Balozi
Mulamula ameongeza kuwa Wafaransa wamekuwa na uhusiano mzuri na Tanzania kwa
muda mrefu na hivi sasa wamekuwa na shauku ya kufanya biashara na kuwekeza kwa
wingi hapa nchini…..ambapo takwimu zinaonesha watalii kutoka Ufaransa kuja
Tanzania kila mwezi ni zaidi ya watalii 7000 wanaokuja kutembelea vivutio
mbalimbali hapa nchini, hivyo ni changamoto kwetu kuchangamkia fursa hii
adhimu.
Kwa
upande wake, Waziri wa Biashara za Kimataifa na Uwekezaji wa Ufaransa, Mhe.
Franck Riester amesema Ufaransa inatambua jitihada zinazofanywa na Serikali ya
Tanzania ikiwa ni pamoja na kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji mambo
ambayo pia yanatiliwa mkazo na serikali ya Ufaransa.
“Ufaransa
imedhamiria kuongeza ushirikiano na Tanzania na kama mlivyoshuhudia leo
tumeanzisha safari za ndege za moja kwa moja kutoka Paris hadi Zanzibar ambao
ulisimama tangu mwaka 1974, huu ni mwanzo mzuri” amesema Mhe. Riester
Mhe.
Riester ameongeza kuwa wataendelea kuwaeleza na kuwahamasisha wafanyabiashara
na wawekezaji wa Ufaransa juu ya fursa mbalimbali zinazopatika Tanzania ikiwemo
katika sekta ya Nishati, Utalii, Viwanda, Usafirishaji pamoja na Uwekezaji ili
kuja kuwekeza na kukuza ucbumi wa pande zote mbili.
Mawaziri
wa Kisekta waliohudhuria kongamano hilo ni Waziri wa mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb), Waziri wa Maliasili
na Utalii Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb), Waziri wa Nishati, Mhe. January
Makamba (Mb) Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (Mb)
Waziri wa Uwekezaji – Zanzibar Mhe. Mudrick Soraga, Waziri wa Viwanda na
Biashara Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb) na Waziri wa Ofisi ya Rais Uwekezaji
Mhe. Geoffrey Mwambe (Mb).
Kampuni
zilizoshiriki katika kongamano hilo ni pamoja na; CMA-CGM, Bolloré, Airbus, Thales,
Lagardére, Total, Chama cha Wafanyabiashara wa Ufaransa-Tanzania, Engie pamoja
na Maurel & Prom.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula
(Mb) akiongea na washiriki wa Kongamano lililowakutanisha Mawaziri wa Kisekta, wafanyabiashara
na wawekezaji kutoka Ufaransa Jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Biashara za Kimataifa na Uwekezaji wa Ufaransa, Mhe. Franck Riester akiongea
na washiriki wa Kongamano lililowakutanisha Mawaziri wa Kisekta, wafanyabiashara
na wawekezaji kutoka Ufaransa Jijini Dar es Salaam
Mawaziri
wa Kisekta pamoja na Wafanyabiashara na Wawekezaji kutoka Ufaransa wakiendelea
na Kongamano Jijini Dar es Salaam
Mawaziri
wa Kisekta pamoja na Wafanyabiashara na Wawekezaji kutoka Ufaransa wakiendelea
na Kongamano Jijini Dar es Salaam
Wafanyabiashara na Wawekezaji kutoka Ufaransa wakiendelea
na Kongamano Jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Biashara za Kimataifa na Uwekezaji wa Ufaransa, Mhe. Franck Riester akiongea
na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kumalizika kwa Kongamano
lililowakutanisha Mawaziri wa Kisekta, wafanyabiashara na wawekezaji kutoka
Ufaransa Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb)
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula
(Mb) akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa Kongamano
lililowakutanisha Mawaziri wa Kisekta, wafanyabiashara na wawekezaji kutoka
Ufaransa Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Biashara za Kimataifa na
Uwekezaji wa Ufaransa, Mhe. Franck Riester
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.