Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye amewasili leo mchana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam akitokea Zanzibar na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Amos Makalla. Mhe. Ndayishime ameambatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb).
Mara
baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam, Mhe. Ndayishimiye alielekea katika
Stesheni ya Pugu na kapata taarifa fupi kuhusu mradi wa Reli ya Kisasa (SGR)
inayojengwa kutoka Dar es Salaam – Morogoro, Morogoro – Makutupora na Mwanza –
Isaka ikiwa ni jumla ya Kilomita 1063 za njia kuu na njia za kupishania.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Reli, Bw. Masanja Kadogosa amemueleza Mhe. Ndayishimiye kuwa
hadi sasa ujenzi wa SGR (kipande cha Pugu - Morogoro) umefikia asilimia 94 na
kuwa unaendelea vizuri.
Aidha,
mara baada ya kupata taarifa fupi kuhusu mradi wa ujenzi wa SGR, Mhe. Rais
Ndayishimiye ametembelea bandari kavu eneo la Kwala Mkoani Pwani.
Mhe.
Ndayishimiye amesema kuwa eneo la bandari kavu (Kwala) litakuza biashara kati
ya Tanzania na Burundi na litatusaidia kupunguza gharama za usafiri na fedha
zitakazookolewa zitaenda kwenye miradi mingine.
“Mradi
huu pia utapunguza gharama za bidhaa mbalimbali Nchini Burundi, kwetu sisi
Burundi, mtu akikupa eneo amekuthamini sawa na kukuunga undugu kwenye familia
yake,” amesema Mhe. Ndayishimie.
Awali
akitoa taarifa ya eneo hilo, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa
(Mb) amesema eneo hilo lina ukubwa wa hekta 502, kati ya hizo hekta 10
zimetengwa kwa ajili ya Serikali ya Burundi.
“Dhumuni
la kutenga eneo hili ni kupunguza msongamano wa mizigo kutoka bandari ya Dar es
Salaam,” Amesema Prof. Mbarawa na kuongeza kuwa ujenzi wa miundombinu ya eneo
hili utakapokamilika utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 37.23
Kwa
upande wake Waziri wa Mambo ya NJe na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi
Liberata Mulamula (Mb) amesema kuwa kupitia mradi wa ujenzi wa bandari kavu eno
la Kwala utasaidia kuimarisha uhusiano wa Tanzania na Burundi pamoja na ukanda
wa Afrika Mashariki kwa ujumla.
Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Amos Makalla. mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam akitokea Zanzibar. Mhe. Ndayishime katika ziara yake ameambatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb).
Rais wa
Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb), Waziri wa
Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa (Mb) na baadhi ya Mabalozi
wakimsikiliza Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania Bw. Masanja Kadogosa
alipokuwa akitoa taarifa fupi kuhusu maendeleo ya ujenzi wa Reli ya Kisasa
(SGR) wakati Mhe. Ndayishimiye alipowasili leo katika Stesheni ya Pugu ikiwa ni
muendelezo wa ziara yake ya kikazi ya siku tatu hapa nchini
Rais wa
Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb), Waziri wa
Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa (Mb) na baadhi ya Mabalozi
wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Bandari ya Tanzania Bw. Eric Hamissi alipokuwa
akitoa taarifa ya eneo la Bandari Kavu (Kwala) mkoani Pwani leo
Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb)
akitoa hotuba yake kwa wananchi wa Kwala kabla ya mkaribisha Rais wa Jamhuri ya
Burundi kuongea na wananchi wa eneo la Bandari Kavu (Kwala) mkoani Pwani
Rais wa
Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye akihutubia wananchi wa Kwala
wakati alipotembelea eneo la Bandari Kavu leo mkoani Pwani
Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye akipokea nakala ya hati ya eneo lenye ukubwa wa hekta 10 zilizotengwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya Serikali ya Burundi kutoka kwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa (Mb)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.