Na Mwandishi Wetu, Dar
Tanzania
na Kenya zimedhamiria kumalizia kuondoa vikwazo vya kiutawala vilivyosalia
ifikapo Disemba 2021 baada ya kuondoa vikwazo 46 visivyokuwa vya kikodi.
Hayo
yamesemwa wakati wa mazungumzo baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) na Balozi wa Kenya Nchini
Tanzania Mhe. Dany Kazungu jijini Dar es Salaam ambapo takwimu zinaonesha urari
wa biashara kati ya Nchi hizo umeongezeka mara sita zaidi baada ya kuondolewa
kwa vikwazo hivyo.
Kutokana
na hatua hiyo, Tanzania imeonekana kunufaika zaidi kwa kuondolewa kwa vikwazo
hivyo kwa kuuza zaidi bidhaa zake nchini Kenya.
“Hii
ni ishara nzuri kwa Tanzania lakini pia ni fursa kwa Tanzania na Kenya kuondoa
umaskini kwa watoto wetu na ndugu zetu kupata ajira kwa wingi katika sekta ya
biashara,” Amesema Mhe. Kazungu
Pia
Balozi Kazungu amemueleza Waziri Mulamula kuhusu azma ya Rais wa Kenya Mhe.
Uhuru Kenyatta kufanya ziara rasmi hapa nchini na kisha kuhudhuria sherehe za
Uhuru tarehe 9 Disemba 2021 ambapo alialikwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipotembelea Kenya mapema mwaka huu.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula
amesema Tanzania inaheshimu makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano wa awali wa
kuondo vikwazo hivyo na dhamira ni kuwa ifikapo Disemba 2021 vikwazo vya
kiutawala navyo viwe vimeondolewa ili kukuza zaidi mahusiano ya Kidiplomasia na
Biashara baina ya Tanzania na Kenya.
“Tumekubaliana
kuhakikisha ifikapo mwezi Disemba 2021 vikwazo vyote vya kitawala viwe vimetatuliwa……….azma
yetu ni kuhakikisha kuwa kila kitu kinakuwa sawa kwa Ustawi wa Diplomasia na
biashara baina ya Tanzania na Kenya,” amesema Balozi Mulamula.
Katika
tukio jingine, Balozi Mulamula amekutana kwa mazungumzo na Mwakilishi wa
Taasisi ya Sister Cities ya Marekani Bi. Ronda Pierce katika Ofisi Ndogo za
Wizara Jijini Dar es Salaam
Balozi
wa Kenya Nchini Tanzania Mhe. Dany Kazungu akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) walipokutana
kwa mazungumzo katika Ofisi ndogo za Wizara leo Jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata
Mulamula (Mb) akimuleleza jambo Balozi wa Kenya Nchini Tanzania Mhe. Dany
Kazungu walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi ndogo za Wizara leo Jijini Dar
es Salaam
Mazungumzo
baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi
Liberata Mulamula (Mb) na Balozi wa Kenya Nchini Tanzania Mhe. Dany Kazungu yakiendelea
katika Ofisi ndogo za Wizara leo Jijini Dar es Salaam
Mwakilishi
wa Taasisi ya Sister Cities ya Marekani Bi. Ronda Pierce akimueleza jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) walipokutana kwa
mazungumzo katika Ofisi ndogo za Wizara leo Jijini Dar es Salaam
Mazungumzo
baina ya wakilishi wa Taasisi ya Sister Cities ya Marekani Bi. Ronda Pierce na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) yakiendelea katika
Ofisi ndogo za Wizara leo Jijini Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.