Na Mwandishi wetu, Dar
Wafanyabiashara
na Wawekezaji kutoka Jamhuri ya Czech wameonesha nia ya kuwekeza katika sekta
ya kilimo hasa Pamba pamoja na viwanda vya nguo hapa nchini.
Akibainisha
kuhusu utayari wa Wafanyabiashara na Wawekezaji wa Czech, kuwekeza hapa nchini,
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Czech Mhe. Miloslav Staŝek amesema
wamefurahishwa sana na mazingira ya biashara hapa Tanzania na wapo tayari
kuwekeza katika sekta kilimo na viwanda.
Mhe.
Staŝek ameyasema hayo wakati alipokutana kwa mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji
wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Dkt. Maduhu Kazi leo jijini Dar es
Salaam.
Katika
ziara yake ya kikazi hapa nchini, Mhe. Staŝek ameambatana na viongozi
mbalimbali wa Jamhuri ya Czech akiwemo Naibu Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya
Czech, mhe. Karel Tyll pamoja na Wafanyabiashara na Wawekezaji kutoka nchini
humo.
Waziri
wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Czech Meh. Miloslav Staŝek amesema yeye pamoja na
wajumbe alioongozana nao wamejadiliana na uongozi wa TIC na kupata fursa ya
kutambua masuala mbalimbali ya kuongeza ushirikiano ili kuimarisha sekta ya
uwekezaji kati ya Czech na Tanzania kwa maslahi ya pande zote mbili.
“Mimi
na Timu yangu tumejadili mambo mbalimbali ya kuwekeza hapa Tanzania ikiwa ni
pamoja na utengezaji wa ndege, kilimo, teknolojia pamoja na viwanda.
“Moja
ya kampuni niliyoambatana nayo inauzoefu mkubwa katika uzalisha dawa na vifaa
tiba, hivyo kampuni hii itakapo pata fursa ya kuwekeza hapa Tanzania itasaidia
kuimarisha mahusiano yetu pamoja na kuboresha sekta ya afya,” Amesema mhe. Staŝek.
Mhe.
Staŝek ameongeza kuwa wamekubaliana na uongozi wa TIC pamoja na Waziri wa
Viwanda na Biashara kutafuta namna bora ya kuwaunganisha wafanyabiashara wa
Tanzania na wale wa Czech ili kutoa fursa kwa kampuni mbalimbali za Czech kuja
kuwekeza kwa wingi hapa Tanzania na wafanyabiashara wa Tanzania kuwekeza nchini
Czech kwa maslahi ya pande zote mbili.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Dkt.
Maduhu Kazi amesema kuwa mara baada ya mazungumzo ya awali, wawekezaji hao
wameonsha nia kubwa sana ya kuwekeza katika Pamba na viwanda vya nguo hapa
nchini.
“Wameonesha
uwezo mkubwa katika biashara na uwekezaji kwenye maeneo ya ufundi wa ndege ambapo
baadae kutakuwa na mafunzo mbalimbali ya kubadilishana ujuzi na fursa za uwekezaji……...lakini
pia wamevutiwa na sekta ya kilimo hasa katika viwanda vya kutengeneza mafuta ya
kula,” Amesema Dkt. Kazi
Nae
Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Mhe. Dkt. Abdallah Possi amesema kuwa
lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa tunatangaza fursa za biashara na
uwekezaji.
“Fursa
za kupata wafanyabiashara kutoka Zchec zinazidi kuongezeka hapa nchini, hivyo
nitoe rai kwa sekta binafsi kuchangamkia fursa za biashara na uwekezaji,”
Amesema Dkt. Posi
Pamoja
na mambo mengine, viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali yaliyolenga kukuza
na kuimarisha sekta ya uwekezaji baina ya Tanzania na Czech hapa nchini.
Waziri
wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Czech Mhe. Miloslav Staŝek akiongea na uongozi wa
Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), ulioongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Dkt.
Maduhu Kazi leo jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Dkt. Maduhu Kazi akimueleza
jambo Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Czech Mhe. Miloslav Staŝek wakati
Waziri Staŝek alipotembelea taasisi hiyo leo jijini Dar es Salaam
Balozi
wa Tanzania nchini Ujerumani, Mhe. Dkt. Abdallah Possi (wa kwanza kulia) akieleza jambo wakati wa
mkutano baina ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Czech Mhe. Miloslav
Staŝek na uongozi wa TIC
Waziri
wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Czech Mhe. Miloslav Staŝek akimueleza jambo
Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo walipokutana kwa mazungumzo leo
jijini Dar es Salaam
Mkutano
ukiendelea
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.