Saturday, February 15, 2025

MAKATIBU WAKUU EAC WAJADILI NISHATI, PETROLI NA MADINI


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayesimamia masuala ya Afrika Mashariki Balozi Stephen P. Mbundi akichangia hoja kwenye Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati, Petroli na Madini la EAC katika ngazi ya Makatibu Wakuu uliofanyika jijini Arusha.


Makatibu Wakuu wanaosimamia Sekta ya Nishati, Petroli na Madini katika Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wamekutana jijini Arusha katika mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati, Petroli na Madini la EAC kujadili masuala muhimu ya pamoja yanayohusu sekta hizo. 

Mkutano huo pamoja na musuala mengine umepokea na kujadili ripoti ya maendeleo ya sekta ya nishati ya umeme, petroli, madini na nishati jadidifu iliyotokana na mkutano wa Wataalam uliyofanyika tarehe 10 -12 Februari 2025. 

Miongoni mwa taarifa iliyojumuisha kwenye ripoti hiyo ni pamoja na; taarifa ya hali ya upatikanaji na hatua iliyofikiwa kwenye usambazaji wa nishati ya umeme katika nchi wanachama, na utelekelezaji wa miradi ya pamoja ya kuzalisha na kusambaza umeme ukiwemo mradi wa kuzalisha umeme kwa nguvu za maji wa Nsongezi wa 39MW unaotarajiwa kutelezwa kwa pamoja baina ya nchi ya Tanzania, Rwanda na Uganda

Mbali na hayo mkutano huo unalenga kuibua maeneo mapya ya ushirikiano kupitia miradi na programu mbalimbali ilikuongeza ufanisi katika maeneo muhimu ikiwemo upatikanaji na usambazaji, usimamizi na utafutaji wa rasilimali hizo ili kurahisisha upatikanaji wake kwa wananchi na kuleta tija zaidi katika ukuaji wa maendeleo ya kijamii na uchumi wa Jumuiya. 

Akifungua mkutano huo, Mwenyekiti wa Baraza hilo ambaye pia ni Katibu Mkuu anayesimamia masuala ya Afrika Mashariki katika Jamhuri ya Kenya Bw. Abdi Dubati ameeleza kuwa mkutano huo ni mwendelezo wa jitihada za Wakuu wa Nchi wanachana wa Jumuiya, za kuhahikisha sekta ya nishati inaimarika ili kuchagiza maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika Jumuiya. 

“Wote tunatambua kuwa sekta ya nishati, petrol na madini zinamchango wakipekee katika maendeleo ya uchumi wa Jumuiya yetu, hivyo nitoe rai kwetu sote kwa umoja wetu kutumia fursa hii na utaalamu wetu katika kuhakikisha wananchi wetu wanapata nishati ya uhahikika kwa bei nafuu huku tukitilia mkazo zaidi kwenye kutafuta na kuhimiza matumizi yanishati mbadala”. Alisema Dubati. 

Mkutano huo wa ngazi ya Makatibu Wakuu ni Maandalizi ya Mkutano wa 17 wa Mawaziri wa Nishati, Petroli na Madini unaotarajiwa kufanyika kesho tarehe 14 Februari 2025 katika Makao Makuu ya Jumuiya ya EAC jijini Arusha.

Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo Ngazi ya Makatibu Wakuu ulijumuisha Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Mhandisi Felchesmi Mramba, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi- Zanzibar Bw. Zahor Alharousy, Katibu Mkuu Wizara ya Madini Mhandisi Yahaya Samamba, ukiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayesimamia masuala ya Afrika MasharikiBalozi Stephen P. Mbundi. 
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Mhandisi Felchesmi Mramba Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati, Petroli na Madini la EAC katika ngazi ya Makatibu Wakuu uliofanyika jijini Arusha.

Meza Kuu wakiongoza mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati, Petroli na Madini la EAC katika ngazi ya Makatibu Wakuu uliokuwa ukiendelea katika Makao Mkuu ya Jumuiya jijini Arusha.
Makatibu Wakuu wanaosimamia Sekta ya Nishati, Petroli na Madini katika Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kutia saini ripoti ya Mkutano wao uliofanyika jijini Arusha. 
Sehemu ya ujumbe wa Tanzania wakifuatilia mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati, Petroli na Madini la EAC katika ngazi ya Makatibu Wakuu uliokuwa ukiendelea katika Makao Mkuu ya Jumuiya jijini Arusha.
Mkurugenzi wa Idara ya Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Abdillah Mataka akifuatilia Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati, Petroli na Madini la EAC katika ngazi ya Makatibu Wakuu uliofanyika jijini Arusha.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi- Zanzibar Bw. Zahor Alharousy, akifuatilia Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati, Petroli na Madini la EAC katika ngazi ya Makatibu Wakuu uliofanyika jijini Arusha.

EAC YAIPONGEZA TANZANIA KWA MAANDALIZI YA KONGAMANO NA MAONESHO YA PETROLI

Waziri wa Madini Mhe. Antony Mavunde (Mb.) akichangia hoja kwenye Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati, Petroli na Madini la EAC uliofanyika Makao Makuu ya Jumuiya hiyo jijini Arusha.

Tanzania, Rwanda na Uganda zakubaliana kusaini hati ya makubaliano ya ujenzi wa Kufua Umeme Nsongezi wa 39MW

Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati, Petroli na Madini la Jumuiya ya Afrika Mashariki umeipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kukamilisha maandalizi ya Kongamano na Maonesho ya 11 ya Petroli ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yatakayofanyika tarehe 5 hadi 7 Machi 2025 jijini Dar es Salaam.

Pongezi hizo zimetolewa kwenye mkutano wa Baraza hilo uliofanyika katika Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) jijini Arusha.

Uenyeji wa Tanzania katika Kongamano hilo unatokana na Maamuzi ya Mkutano wa 16 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati uliofanyika Februari 14, 2024 ambao uliamua Tanzania kuwa Mwenyeji wa Kongamano na maonesho hayo.

Kongamano na Maonesho hayo ni mkakati unaolenga kutangaza fursa zilizopo katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu rasilimali za mafuta na gesi asilia na kuielezea jiolojia ya ukanda wa Afrika Mashariki ili kuvutia uwekezaji, kuendelezaji wa miundombinu, udhibiti wa uharibifu wa mazingira, usimamizi wa taarifa za mafuta na gesi asilia.

Pia linalenga kutangaza maeneo mapya ya utafutaji na kutangaza maendeleo yaliyopatikana katika sekta ya nishati katika ukanda. 

Malengo mengine ni kubadilishana uzoefu kuhusu sera, sheria, kanuni na utaalamu unaotumika kwenye sekta ya nishati, kuhamasisha uwekezaji, utafutaji, uzalishaji na uendelezaji wa mafuta na gesi asilia. Vilevile Kongamano hilo linatoa fursa ya kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini na katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Kongamano na maonesho hayo yanatoa fursa adhimu kwa Tanzania kutangaza fursa za uwekezaji katika sekta ya Nishati hususan katika sekta ndogo ya mafuta na gesi na hivyo kuongeza wigo wa kupata wawekezaji kwenye sekta hiyo. 

Mbali na hayo, Mkutano 17 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati, Petroli na Madini la EAC limepokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa miradi na programu mbalimbali katika sekta ya nishati, petroli na madini ikiwemo Mradi wa Kufua Umeme wa Nsongezi wenye Megawati 39 kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Kagera utakaotelezwa kwa pamoja baina ya Tanzania, Rwanda na Uganda. 

Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati, Petroli na Madini uliongozwa na Waziri wa Madini Mhe. Antony Mavunde (Mb.), Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga (Mb.), Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi- Zanzibar Bw. Zahor Alharousy na Viongozi wengine waandamizi wa Serikali.
Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga (Mb.) akifuatilia Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati, Petroli na Madini la EAC uliofanyika Makao Makuu ya Jumuiya hiyo jijini Arusha
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi- Zanzibar Bw. Zahor Alharousy akifuatilia Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati, Petroli na Madini la EAC uliofanyika Makao Makuu ya Jumuiya hiyo jijini Arusha
Meza Kuu wakiongoza mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati, Petroli na Madini la EAC katika ngazi ya Makatibu Wakuu uliokuwa ukiendelea katika Makao Mkuu ya Jumuiya jijini Arusha.


Ujumbe wa Tanzania, Uganda na Rwanda wakionesha hati ya makubaliano (MOU) ya ujenzi wa Kufua Umeme wa Nsongezi 39MW.




Sehemu ya ujumbe wa Tanzania wakifuatilia Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati, Petroli na Madini la EAC uliofanyika jijini Arusha
Sehemu ya ujumbe wa Tanzania wakifuatilia Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati, Petroli na Madini la EAC uliofanyika jijini Arusha

Monday, February 10, 2025

MKUTANO WA 17 WA BARAZA LA MAWAZIRI LA KISEKTA LA NISHATI, PETROLI NA MADINI LA EAC WAANZA JIJINI ARUSHA


Mkurugenzi wa Idara ya Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Bw. Abdillah Mataka katika Wizara ya Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki akichangia hoja kwenye Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati, Petroli na Madini la EAC uliokuwa ukiendelea katika Makao Makuu ya Jumuiya jijini Arusha.

Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati, Petroli na Madini la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) umenza leo tarehe 10 Februari 2025 katika Makao Makuu ya Jumuiya hiyo jijini Arusha. 

Mkutano huo wa siku tano kuanzia Februari 10 hadi 14, 2025 utafanyika katika ngazi tatu; ngazi ya Wataalamu tarehe 10 -12 Februari 2025, ngazi ya Makatibu Wakuu tarehe 13 Februari 2024 na kuhitimishwa katika ngazi ya Mawaziri tarehe 14 Februari 2025.

Mkutano huo unatarajiwa kupokea na kujadili taarifa mbalimbali za maendeleo ya sekta ya nishati, petroli na madini katika Jumuiya na kuweka mikakati ya pamoja ya kutatua chagamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo ili kuhakikisha nchi wanachama wananufaika kutokana na mchango wa sekta hizo, vilevile kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya uhakika, nafuu na endelevu katika Jumuiya. 

Ili kufikia adhima hiyo mkutano huo utaangazia agenda mbalimbali ikiwemo; hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa maamuzi ya baraza la hilo la sekta, matumizi ya nishati safi, salama na ufanisi wake, Mkutano na Maonyesho ya 11 ya Petroli ya Afrika Mashariki yanayotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam tarehe 5-7 Machi 2025 na kuhuisha taarifa za utekelezaji wa miradi ya kuunganisha na kusambaza nishati katika Jumuiya. 

Akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano huo wa ngazi ya wataalamu Mkurugenzi wa Sekta za Uzalishaji wa Sekretariati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Bw. Jean Baptiste Havugimana ameeleza kuwa licha ya mafanikio yaliyofikiwa katika sekta hiyo bado mchango na weledi wa wataalamu wa sekta hizo muhimu katika kukuza uchumi wa Jumuiya unahitajika ili kutatua changamoto zilizopo na hatimaye kufikia malengo yanayotarajiwa na Jumuiya. 

Havugimana ametoa rai kwa watalamu hao kujikita katika kujadili na kuyapatia ufumbuzi wa kudumu masuala muhimu yatakayojili katika mkutano huo kwa manufaa ya Jumuiya.

Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo wa ngazi ya wataalamu unaongozwa na Bw. Abdillah Mataka Mkurugenzi wa Idara ya Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii katika Wizara ya Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 

Mkutano huo unaotarajiwa hutimishwa tarehe 14 Februari 2025 katika ngazi ya Mawaziri wanaosimamia sekta ya nishati, petroli na madini umehudhiriwa na wajumbe kutoka Nchi zote saba (7) wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) Bw. Haji  Haji akifuatilia Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati, Petroli na Madini la EAC uliokuwa ukiendelea katika Makao Makuu ya Jumuiya jijini Arusha.

Mkurugenzi wa Sekta za Uzalishaji wa Sekretariati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Bw. Jean Baptiste Havugimana akichangia hoja kwenye Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati, Petroli na Madini la EAC uliokuwa ukiendelea katika Makao Makuu ya Jumuiya jijini Arusha.
Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati, Petroli na Madini la EAC ukiendelea katika Makao Makuu ya Jumuiya jijini Arusha.




Wednesday, January 29, 2025

UGANDA KUENDELEA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA TANZANIA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Robinah Nabbanja amesema Serikali yake itaendelea kuimarisha ushirikiano wa kindugu uliopo na Tanzania hususan kwenye nyanja zinazochochea maendeleo ya wananchi ikiwemo kilimo na biashara.

 

Mhe. Nabbanja ametoa kauli hiyo alipotembelea Kiwanda cha Mbolea cha Itracom Fertilizer Limited kilichopo eneo la Nala jijini Dodoma, Januari 29, 2025 ikiwa ni sehemu ya ziara yake nchini baada ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati kwa niaba ya Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni uliomalizika jijini Dar es Salaam, Januari 28, 2025.

 

Mhe. Nabbanja ambaye aliwasili jijini Dodoma kwa kutumia usafiri wa Treni ya SGR amesema kuwa, uwekezaji wa kiwanda hicho cha mbolea ni mkombozi kwa wakulima wote wa Afrika Mashariki ambao sasa wanatakiwa kuzalisha mazao yao kwa kutumia mbolea hiyo asilia ambayo inazalishwa kwa utaalam na ubora wa hali ya juu  ili kuongeza uzalishaji wa kibiashara.

 

Pia amesisitiza umuhimu wa Serikali hizi mbili kuendelea kuwekeza kwenye masuala ya kilimo cha umwagiliaji, udhibiti wa magonjwa na wadudu, utafutaji wa mitaji na masoko kwa wakulima, elimu kwa wakulima ya matumizi bora ya mbolea  pamoja na kuingia ubia na wadau mbalimbali hususan kwenye masuala ya teknolojia ya kilimo.

 

“Tanzania na Uganda zimebarikiwa kuwa na ardhi nzuri ya kilimo. Naamini Mwenyezi Mungu alijua ipo siku tutailisha dunia. Hivyo ni wajibu wetu kuhakikisha tunawawezesha wakulima wetu ili walime kwa tija ikiwemo kuwahimiza kutumia mbolea kwa uzalishaji mkubwa wa kibiashara kwa faida zaidi” alisema Mhe. Nabbanja.

 

Aidha, Mhe. Nabbanja aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuwa na sera nzuri inayowawezesha watanzania kuajiriwa kwa wingi kwenye viwanda vya wawekezaji kutoka nje kama ilivyofanyika katika kiwanda hicho cha mbolea ambapo zaidi ya watanzania 800 wameajiriwa kiwandani hapo.

 

Mhe. Nabbanja alitumia nafasi hiyo pia kuelezea furaha yake ya kusafiri kwa kutumia Treni ya Reli ya Kisasa ya SGR na kuahidi kurudi tena Tanzania wakati mwingine ili kufurahia maendeleo makubwa ya miundombinu yanayokamilishwa hapa nchini.

 

“Nimefurahia kusafiri kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma kwa SGR. Naiushukuru na kuipongeza Serikali ya Tanzanua kwa hatua hii. Na sisi tayari Mhe. Rais Museveni alizindua mradi huo na tupo katika hatua za mwisho kukamilisha njia ya SGR,” alifafanua Mhe. Nabbanja.

 

Kwa upande wake, Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Selemani Jafo amemshukuru Mhe. Nabbanja kwa kutembelea kiwanda hicho ili kujionea uwekezaji mkubwa unaofanywa hapa Tanzania na kwamba Serikali ya Tanzania itaendelea kuweka mazingira mazuri ili kuvutia wawekezaji wengi zaidi kuja nchini kwa manufaa ya watanzania.

 

Pia ameongeza kusema,  Mhe. Nabbanja kama kiongozi wa juu wa Uganda  amenonesha nia ya nchi yake kutumia mbolea inayozalishwa kiwandani hapo na kuitaja hatua hiyo kama chachu ya kukuza na kuimarisha ushirikiano wa kibiashara baina ya Tanzania na Uganda kupitia makubaliano chini ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na yale ya Eneo Huru la Biashara Barani Afrika.

 

Naye Mkurugenzi Mtendaji  wa Kiwanda hicho, Bw. Nduwimana Nazaire ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuhakikisha miundombinu muhimu kwa uendeshaji wa kiwanda hicho ikiwemo barabara, maji na umeme inakuwepo na inafanya kazi wakati wote na kwa uhakika.

 

Akitoa neno la shukrani, Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Meja Jenerali Paul Simuli ameishukuru Serikali ya Uganda kwa ushirikiano mkubwa wanaoupata katika kutekeelza majukumu yao nchini humo na kumshukuru Mhe. Nabbanja kwa kutenga muda na kukitembelea kiwanda hicho ili kujionea uzalishaji mkubwa unaofanywa kiwandani hapo.

 

Mbali na Mhe. Jafo, Viongozi wengine wa Serikali walioshiriki ziara hiyo ni pamoja Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Mhe. Dennis Londo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.Mhe. Rosemary Senyamule.

 

Kiwanda cha Itracom Fertilizer Limited kilianza uzalishaji rasmi mwaka 2022 ikiwa ni matokeo ya ziara ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Burundi. Kiwanda hicho hadi kufikia mwezi Juni 2025, kina lengo la  kuzalisha Tani milioni moja za mbolea huku kikiajiri zaidi ya Watanzania 800.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Selemani Jafo akimpokea Waziri Mkuu wa Uganda, Mhe. Robinah Nabbanja alipowasili katika Kiwanda cha Mbolea cha Itracom Fertilizer Limited kilichopo eneo la Nala jijini Dodoma kwa ajili ya kujionea shughuli zinazotekelezwa katika Kiwanda hicho.
Mhe. Nabbanja akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Mhe. Dennis Londo mara baada ya kuwasili jijini Dodoma

Mhe. Nabbanja akizungumza mara baada ya kutembelea kiwanda hicho
Mhe. Nabbanja akihutubia
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Selemani Jafo akizungumza 
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule akizungumza
Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Paul Simuli akizungumza 
Mhe. Nabbanja akiwa ameongozana na Mhe. Londo mara baada ya kupokelewa
Mhe. Nabbanja akisalimiana na Mkurugenzi wa Kiwanda cha Itracom Fertilizer Limited, Bw. Nduwimana Nazaire
Kikundi cha burudani wakati wa mapokezi ya Waziri Mkuu wa Uganda jijini Dodoma
Mhe. Nabbanja akiteta jambo na Viongozi wa Seriklai waliofika kumpokea alipowasili Dodoma akiwemo Mhe. Londo (wa pili kushoto)
Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Simuli
Mhe. Nabbanja akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kiwanda cha Mbolea cha Itracom Fertilizer Limited, Mhe. John Chiligati
Afisa Mambo ya Nje Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Seif Kamtunda akishiriki ziara ya Mhe. Nabbanja
Shehena ya mbolea
Mhe. Nabbanjana wakati wa ziara yake katika Kiwanda cha Itracom Fertilizer Limited
Mhe. Nabbanjana akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali wakati wa ziara yake katika Kiwanda cha Itracom Fertilizer Limited

Mhe. Nabbanjana wakati wa ziara yake katika Kiwanda cha Itracom Fertilizer Limited
Mhe. Nabbanja akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Fredrick Sumaye walipokutana katika Stesheni za SGR jijini Dodoma mara baada ya Mhe. Nabbanja kuwasili
Mhe. Nabbanja akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Dodoma. Aliyesimama pembeni ni Mhe. Londo
Mhe. Nabbanja akipokelewa baada ya kuwasili Dodoma kwa Treni ya SGR
Wageni waalikwa wakishiriki Mkutano wa Mhe. Nabbanja na Viongozi wa Kiwanda cha Mbolea cha Itracom Fertilzer Limited
Mhe. Nabbanja akizungumza wakati wa ziara yake katika Kiwanda cha Itracom Fertilizer Limited
Shehena ya Mbolea ikipakiwa kwenye lori kabla ya  kusafirishwa kwa ajili ya usambazaji nchini