Saturday, April 29, 2023

BALOZI MBAROUK ASHIRIKI SIKU YA UHURU WA AFRIKA KUSINI AITA WAWEKEZAJI WAJE NCHINI

Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akisalimiana  na Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania Mhe.  Noluthando Mayende- Malepe alipowasili  kuhudhuria hafla ya maadhimisho ya miaka 29 ya Uhuru wa Jamhuri ya Afrika Kusini yaliyofanyika jijini Dar es Salaam

Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk akisalimiana na  Balozi Mstaafu Mhe. Getrude Mongela walipokutana katika hafla ya maadhimisho ya miaka 29 ya Uhuru wa Jamhuri ya Afrika Kusini yaliyofanyika jijini Dar es Salaam


Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania Mhe.  Noluthando Mayende- Malepe akizungumza kuwakaribisha wageni waliohudhuria hafla ya maadhimisho ya miaka 29 ya Uhuru wa Jamhuri ya Afrika Kusini yaliyofanyika jijini Dar es Salaam

Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (kushoto) akizungumza katika maadhimisho ya miaka 29 ya Uhuru wa Jamhuri ya Afrika Kusini yaliyofanyika jijini Dar es Salaam wanaomsikiliza ni baadhi ya Wanadiplomasia wanaowakilisha nchi zao hapa nchini.

Baadhi ya wageni waliohudhuria hafla ya maadhimisho ya miaka 29 ya Uhuru wa Jamhuri ya Afrika Kusini iliyofanyika jijini Dar es Salaam wakifuatilia hafla hiyo
Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akiongoza wanadiplomasia waliohudhuria hafla ya  maadhimisho ya miaka 29 ya Uhuru wa Jamhuri ya Afrika Kusini kukata keki malum kwa ajili ya maadhimisho hayo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akisindikizwa na Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania Mhe.  Noluthando Mayende- Malepe (kulia kwa Naibu Waziri) alipohudhuria hafla ya maadhimisho ya miaka 29 ya Uhuru wa Jamhuri ya Afrika Kusini iliyofanyika jijini Dar es Salaam




Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb.) ameshiriki hafla ya maadhimisho ya miaka 29 ya Uhuru wa Jamhuri ya Afrika Kusini iliyofanyika jijini Dar es Salaam na kuwaita wawekezaji wengi zaidi waje kuwekeza nchini.

 

Akizungumza katika hafla hiyo Mhe. Balozi Mbarouk amesema Tanzania itaendelea kushirikiana na Afrika Kusini kuendelea kuuenzi uhusiano wa kidugu na wa kihistoria uliopo kati ya nchi hizo ambao uliasisiwa na viongozi waasisi wa mataifa hayo.



Tanzania itaendelea kutumia fursa za uwekezaji zinazopatikana nchini Afrika Kusini na nitoe  wito kwa wawekezaji wengi zaidi wa Afrika Kusini waje Tanzabia kuwekeza hasa ikizingatia kuna fursa katika maeneo ya kilimo, uzalishaji, mifugo, viwanda vya dawa, usafiri, utalii, madini na viwanda vya kusindika mazao ya chakula,”alisema.

 

Amesema wakati Taifa la Afrika Kusini likiadhimisha siku ya uhuru wake Tanzania itaendelea kushirikiana na Afrika Kusini ili kuhakikisha nchi zote zinanufaika na uwepo wa uhusiano huo.

Amesema ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Afrika Kusini umeoneshwa zaidi na ziara ya kitaifa aliyoifanya nchini Afrika Kusini Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na kufanyika kwa  mikutano ya pamoja kati ya nchi hizi.

 

Akizungumza katika  hafla hiyo Balozi wa Afrika Kusini nchini Mhe. Noluthando Mayende- Malepe amesema Afrika Kusini inajali na kuthamini mchango mkubwa ambao Tanzania imetoa katika harakati za ukombozi wa nchi hiyo na kuifanya Tanzania kuwa nyumbani kwa wapigania uhuru wa Afrika Kusini.

 

“Tunaishukuru sana serikali na wananchi wa Tanzania kwa mambo yote ambayo Tanzania imeifanyia Afrika Kusini  wakati wote hadi kufikia kupata uhuru wetu, kwakweli sisi tunawashukuru sana, niwahakikishie kuwa Afrika Kusini itaendelea kuuthamini mchango wenu katika uhuru wetu na tutaendelea kuuenz uhusiano wa kidugu na wa kihistoria uliopo kati ya nchi zetu mbili hizi, alisema.

 

Ameahidi kuwa Tanzania na Afrika Kusini zitaendelea kushirikiana katika mambo mengi ambayo nchi mbili hizi zimekuwa zikiyafanya.

 

Hafla hiyo ilihudhuriwa na waheshimiwa Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini.

 












Friday, April 28, 2023

WAZIRI TAX AMUAGA BALOZI WA RWANDA NCHINI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) amemuaga Balozi wa Jamhuri ya Rwanda nchini Mhe. Meja Jenerali Charles Karamba, baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini.

Akiongea wakati wa hafla ya kumuaga Balozi Karamba iliyofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam, Dkt. Tax amempongeza Balozi Karamba kwa kumaliza muda wake wa uwakilishi salama na kumpongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya katika kukuza na kudumisha uhusiano mzuri na wa kindugu baina ya Tanzania na Rwanda katika kipindi chake cha uwakilishi nchini. 

Aidha, Mhe. Tax ameeleza kwamba, wakati wa Uwakilishi wake, Balozi Karamba amechangia Kwa kiasi kikubwa kukuza ushirikiano wa Tanzania na Rwanda katika maeneo mbalimbali ikiwemo, biashara na Uwekezaji, Nishati, uchukuzi na ujenzi, na yapo maeneo ambayo nchi hizi mbili zitaendelea kushirikiana kwa ukaribu na maeneo mengine Tanzania itaendelea kubadilishana uzoefu na Rwanda.

Naye, Mhe. Balozi Karamba ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kumpa ushirikiano wa kutosha wakati wa kipindi chake cha uwakilishi hapa nchini.

Mhe. Balozi ameelezea kufurahishwa na uhusiano mzuri uliopo baina ya nchi hizi mbili na kupongeza hatua mbalimbali ambazo Tanzania imeendelea kuzichukua katika kuimarisha mahusiano hayo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Rwanda nchini ambaye amemaliza muda wake wa uwakilishi nchini, Mhe. Meja Jenerali Charles Karamba. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam. 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Rwanda nchini ambaye amemaliza muda wake wa uwakilishi nchini, Mhe. Meja Jenerali Charles Karamba. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam. 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika picha ya pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Rwanda nchini ambaye amemaliza muda wake wa uwakilishi nchini, Mhe. Meja Jenerali Charles Karamba

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika picha ya pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Rwanda nchini ambaye amemaliza muda wake wa uwakilishi nchini, Mhe. Meja Jenerali Charles Karamba pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Naimi Aziz


NJE SPORTS CHUPUCHUPU KUTWAA UBINGWA WA KARATA

Timu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Nje Sports) iliyopo jijini Morogoro kushiriki katika michezo mbalimbali inayoendelea mjini hapo kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Mei Mosi imejitosa kuwania ushindi katika mchezo wa karata na drafti. 

Katika michezo hiyo iliyochezwa kwa nyakati tofauti ilianza na hatua ya makudi na kufuatiwa na robo fainali, nusu fainali, na fainali. 

Kwa upande wa mchezo wa karata Nje Sports iliwakilishwa na Bw. Peter Ndatila na Bi. Nyanzala Lupeja. Bi. Lupeja ambaye aliwakilisha upande wa Wanawake - Nje Sports alifanikiwa kufika hatua fainali na kuibuka mshindi wa 4 baada ya kuonesha umahiri wa hali ya juu uliomfanya kuvuka hatua ya makundi, robo na nusu fainali. Bi. Lupenja kupitia kundi B2 alifanikiwa kufuzu baada kujikusanyia alama 6 katika michezo 6 aliyocheza. 

Wakati huo huo ushindani mkali hulioshuhudiwa kwa upande wa Wanaume katika mchezo huo, ulitosha kufifisha juhudi na makali ya Bw. Ndatila na kumfanya ashindwe kufuzu katika hatua ya makundi. Bw. Ndatila alifanikiwa kujikusanyia alama 5 katika kundi D baada ya kusuluhu katika michezo yote 5 aliyocheza. Wachezaji wawili waliofanikiwa kufuzu kwenda robo fainali katika kundi hilo walijikusanyia alama 8 na 7 katika michezo 5 iliyochezwa.

Kwa upande wa mchezo wa drafti Nje Sports iliwakilishwa na Bw. Shaban Maganga ambaye licha ya kuonesha makali yake na kutoa upinzani mkali katika mchezo huo hakufanikiwa kuvuka kwenda hatua ya makundi. Bw. Maganga alijikusanyia alama 6 katika kundi E na kushika nafasi ya 4 kati ya washiriki 7 wa kundi hilo. Wachezaji wawili waliofanikiwa kupita kwenda robo fainali katika kundi hilo walijikusanyia alama 11 na 10 katika michezo 6 iliyochezwa.

Mashindano hayo ya michezo kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya Mei Mosi yanatarajiwa kuhitimishwa katika siku hizi mbili za mwishoni mwa Juma (Ijumaa na Jumamosi) mjini Morogoro, ambapo watumishi, wakazi wa Morogoro na maeneo jirani watapata fursa ya kutazama fainali katika michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, mpira wa pete, riadha na kuvuta kamba. 
Usajili wa washiriki wa mchezo wa drafti ukiendelea kwenye mashindano ya kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Mei Mosi uliofanyika kwenye uwanya wa Jamhuri mjini Morogoro
Mchezaji wa drafti wa Nje Sports Bw. Shaaban Maganga akijisajili kushiriki mchezo uliofanyika katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro
Mchezaji wa karata wa Nje Sports Bw. Shaaban Maganga (kushoto) akimkabili mpinzani wake katika mchezo wa karata uliofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro
Mchezo ukiendelea
Mchezaji wa karata wa Nje Sports Bi. Nyanzala Lupeja (kulia) akimkabili mpinzani wake katika mchezo wa karata uliofanyika Jamhuri mjini Morogoro
Mchezaji wa karata wa Nje Sports Bi. Nyanzala Lupeja (kushoto) akimkabili mpinzani wake katika mchezo wa karata uliofanyika Jamhuri mjini Morogoro
Mchezaji wa karata wa Nje Sports Bw. Peter Ndatila akimkabili mpinzani wake katika mchezo wa karata uliofanyika Jamhuri mjini Morogoro
Mchezo ukiendelea
Mchezo ukiendelea

RAIS KAGAME AHITIMISHA ZIARA YA KIKAZI NCHINI

Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Mheshimiwa Paul Kagame akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam wakati akiondoka kurejea nchini Rwanda


Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Mheshimiwa Paul Kagame akiagana na viongozi mbalimbali katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kabla ya kurejea nchini Rwanda

Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Mheshimiwa Paul Kagame akiagana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam

Viongozi mbalimbali wakiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax wakimuaga Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Mheshimiwa Paul Kagame katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam

Ndege ya Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Mheshimiwa Paul Kagame na ujumbe wake ikiwa tayari kuondoka katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kurejea nchini Rwanda

Ndege ya Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Mheshimiwa Paul Kagame na ujumbe wake ikiondoka katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kurejea nchini Rwanda



 

Thursday, April 27, 2023

RAIS SAMIA NA RAIS KAGAME WAKUBALIANA KUIMARISHA BIASHARA

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Ikulu Jijini Dar es Salaam 

Rais wa Jamhuri ya Jamhuri ya Rwanda, Mhe. Paul Kagame akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Ikulu Jijini Dar es Salaam 

WATANZANIA WALIOKWAMA SUDAN WAWASILI NCHINI SALAMA






Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) akisalimiana na mmoja wa Watanzania waliorejeshwa na Serikali kutoka Sudan ambako kuna mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kati ya Jeshi la Sudan na Jeshi la Msaada wa Haraka (RSF). Mtanzania huyo amepata changamoto za kiafya kwa kupata mshituko kufuatia matukio ya mapigano hayo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) akiongea na Balozi wa Tanzania nchini Sudan, Mhe. Silima Kombo Haji baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kutoka Sudan ambako kuna mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kati ya Jeshi la Sudan na Jeshi la Msaada wa Haraka (RSF)

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) wa pili kulia; Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo (kulia); Balozi wa Tanzania nchini Sudan, Mhe. Silima Kombo Haji na Mkurugenzi wa Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Naimi Aziz wakiwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere baada ya kuwapokea Watanzania waliorejeshwa na Serikali kutoka Sudan ambako kuna mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kati ya Jeshi la Sudan na Jeshi la Msaada wa Haraka (RSF).

Watanzania waliorejeshwa na Serikali kutoka Sudan ambako kuna mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kati ya Jeshi la Sudan na Jeshi la Msaada wa Haraka (RSF) wakiwa wanakamilisha taratibu za uhamiaji ili waweze kukutana na familia zao zilizokuwa zinawasubiri uwanjani hapo

Watanzania waliorejeshwa na Serikali kutoka Sudan ambako kuna mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kati ya Jeshi la Sudan na Jeshi la Msaada wa Haraka (RSF) wakiwa wanakamilisha taratibu za uhamiaji ili waweze kukutana na familia zao zilizokuwa zinawasubiri uwanjani hapo

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) akiongea na baadhi ya wazazi waliofika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuwapokea vijana wao waliorejeshwa na Serikali kutoka Sudan.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) akiongea na vyombo vya habari vilivyofika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kushuhudia tukio la kuwapokea Watanzania waliorejeshwa na Serikali kutoka Sudan.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) akiongea na familia zilizofika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuwapokea wapendwa wao walirejeshwa na Serikali kutoka Sudan. 







 

RAIS KAGAME AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI

Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Mheshimiwa Paul Kagame,  awasili nchini kwa Ziara ya Kikazi ya siku mbili tarehe 27 - 28 April, 2023. Mheshimiwa Rais Paul Kagame na Ujumbe wake  amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Dkt. Stergomena Tax (Mb.)

Katika mapokezi hayo Dkt. Tax aliambatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu – Zanzibar Mhe. Jamal Kassim Ali, Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Amos Makala, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo, Balozi wa Rwanda Nchini, Mhe. Meja Jenerali Charles Karamba na viongozi mbalimbali waandamizi wa Serikali.

Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Mheshimiwa Paul Kagame akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ziara ya kikazi ya siku mbili na kupokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Dkt. Stergomena Tax

Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Mheshimiwa Paul Kagame akipokea zawadi ya maua baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ziara ya kikazi ya siku mbili

Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Mheshimiwa Paul Kagame akisalimiana na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ziara ya kikazi ya siku mbili

Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Mheshimiwa Paul Kagame akisalimiana na Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ziara ya kikazi ya siku mbili



Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Mheshimiwa Paul Kagame akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Dkt. Stergomena Tax