Friday, July 29, 2016

Waziri Mahiga akutana na Balozi wa DRC nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt Augustine Mahiga akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Jean Pierre Tshampanga Mutamba, alipomtembelea Wizarani Jijiji Dar es Salaam. Katika Mazungumzo yao Mhe Waziri alieleza Serikali ya Tanzania inafanya jitihada za makusudi kuhakikisha wafanyabiashara kutoka nchini Congo hawapati shida katika kusafirisha bidhaa zao kupitia Bandari ya Dar es Salaam.
Mhe. Mutamba akizungumza ambapo alieleza umuhimu wa kufanyika vikao vya Tume ya Pamoja kati ya Tanzania na DRC, pamoja na kuweka makubaliano yatakayowezesha wafanyabiashara kunufaika na kuweza kukuza uchumi wa mataifa yao badala ya kuwa na tozo nyingi zinazorudisha nyuma biashara zao.
Wakati mazungumzo yakiendelea
Waziri Mahiga akiagana na Mhe. Balozi Mutamba

Waziri Mahiga akutana na Balozi wa Saharawi nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akimkaribisha Balozi wa Saharawi nchini Mhe. Brahim Salem Buseif alipomtembea katika ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam na kufanya naye mazungumzo tarehe 29 Julai, 2016
Mhe. Waziri Mahiga akizungumza na Mhe. Buseif, ambapo katika mazumgumzo yao alimpa pole kwa  msiba wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Tawala cha Polisario cha nchini Saharawi. Pia alisisitiza kuwa mataifa haya mawili yataendelea kuimarisha ushirikiano katika masuala mbalimbali.
Mhe. Buseif akizungumza ambapo alieleza kuwa nchi ya Saharawi ipo tayari kushirikiana na Tanzania na kuishukuru kwa kuiunga mkono katika masuala mbalimbali.
Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samuel Shelukindo pamoja na Afisa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia mazungumzo.
Mazungumzo yakiendelea.

Mtanzania atunukiwa Tuzo ya Juu ya Malkia wa Thailand

Profesa Pauline Peter Mella aliyetunukiwa Tuzo ya Juu ya Malkia wa Thailand Srinagarindra kwa kutambua mchango wake kwenye sekta ya afya, akizungumza wakati wa hafla fupi ya kumpongeza iliyoandaliwa na Ubalozi wa Thailand nchini kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Tuzo hiyo inatolewa  na Malkia wa Thailand Srinagarindra kwa kutambua mchango wa watu mbalimbali kwenye sekta ya afya. Profesa Mela ambaye kitaaluma ni Muuguzi kwa sasa ni Mkufunzi katika Chuo Kikuu cha masuala ya Tiba cha Hubert Kairuki cha Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wageni waalikwa wakimsikiliza Profesa Pauline Peter Mella hayupo pichani. Wa pili kutoka kulia ni Balozi Mteule wa Thailand nchini, Mhe. Prasittiporn Wetprasit
Profesa Pauline Peter Mella akiwa ameshikilia Tuzo yake kwenye picha ya pamoja na Balozi Mteule wa Thailand hapa nchini mwenye makazi yake nchini Nairobi Mhe. Prasittiporn Wetprasit na familia yake.

Profesa Mella akiwa katika picha ya pamoja na wageni waalikwa

Waziri Mahiga apokea Nakala za Hati za Utambulisho za Mabalozi Wateule nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga (Mb.), akipokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Italia hapa nchini, Mhe. Roberto Mengon. Hafla hiyo ilifanyika katika Ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Waziri Mahiga akizungumza na Balozi Mteule wa Italia hapa nchini mara baada ya kupokea Nakala zake za utambulisho. Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa Idara ya Amerika na Ulaya Balozi Joseph Sokoine akifuatiwa na  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Itifaki, Bw. James Bwana .

...Nakala za Hati za Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Korea

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb.), pia akipokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Jamhuri ya Watu wa Korea (DPRK) hapa nchini, Balozi Kim Yong Su hafla iliyofanyika katika Ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam hivi karibuni

...Nakala za Utambulisho za Balozi wa Thailand

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (Mb.), amepokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mpya wa Thailand hapa nchini mwenye makazi yake nchini Nairobi Balozi Prasittiporn Wetprasit (kushoto) leo katika Ofisi yake jijini Dar es Salaam
Waziri Mahiga akimweleza jambo Balozi Mteule, Mhe. Wetprasit mara baada ya kupokea nakala zake za utambulisho.

...Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi wa Somalia

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb.), akiisoma Nakala ya Hati ya  Utambulisho  ya a Balozi Mpya wa Jamhuri ya Somalia hapa nchini Balozi Mteule wa Somalia nchini, Mhe. Mohammed Hassan Abdi mara baada ya kuipokea. Tukio hilo lilifanyika Wizarani hivi karibuni.
Dkt. Mahiga akizungumza na Balozi Mohammed Hassan Abdi mara baada ya kupokea nakala zake
Waziri Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Hassan Abdi

Waziri Mahiga ashiriki hafla ya kuwaaga Mabalozi

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga (Mb), akizungumza kwenye hafla  ya kuwaaga Mabalozi wa nchi za Ireland, Canada na Uingereza wanaomaliza muda wao wa uwakilishi nchini. Kutoka kushoto ni  Mhe. Fionnuala Gilsenan, Balozi wa Ireland, Mhe. Alexandre Leveque, Balozi wa Canda na Mhe. Dianna Melrose, Balozi wa Uingereza. Katika mazungumzo hayo Dkt. Mahiga aliwashukuru kwa kuendeleza na kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Mataifa yao hapa nchini hususan katika kuchangia miradi mbalimbali ya  maendeleo. 
Waziri Mahiga akiendelea kuzungumza.
Mkurugenzi wa Idara ya  Ulaya na Amerika, Balozi Joseph Sokoine akitoa neno la shukrani. 
Waziri Mahiga akimkabidhi picha yenye mchoro wa ndege zilizochorwa kwa ustadi wa hali ya juu
Balozi wa Canada akipokea zawadi
Balozi Melrose naye akipokea zawadi yake
Dkt. Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi  hao
Picha ya pamoja

Thursday, July 28, 2016

Waziri Mahiga aagana na Mabalozi waliomaliza muda wa kazi nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Balozi wa Uingereza hapa nchini, Mhe. Dianna Melrose alipokuja Wizarani kumuaga mara baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini.
 Katika mazungumzo yao Waziri Mahiga alimpongeza Balozi Melrose kwa kuiwakilisha nchini yake vema na kuendeleza mahusiano mazuri kati ya Tanzania na Uingereza. Kwa upande wa Balozi Melrose, alisema anaishukuru Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Serikali kwa ujumla kwa ushirikiano aliokuwa anaupata kipindi chote cha uwakilishi wake.
Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine(wa kwanza kushoto) pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga (wa kwanza kulia) na Afisa Mambo ya Nje, Bi. Mona Mahecha nao wakifuatilia kwa makini mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea.
Mazungumzo yakiendelea

=====================================

Wakati huo huo Mhe. Waziri Mahiga alikutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Canada nchini.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza  na Balozi wa Canada nchini, Mhe Alexandre Leveque alipokuja Wizarani kumuaga mara baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini. Mhe. Mahiga alimpongeza na kumshukuru kwa kuendelea kushirikiana na Tanzania katika sekta mbalimbali zikiwemo Elimu na Biashara. Pia Mhe . Alexandre Leveque alitumia fursa hiyo kuishukuru Wizara kwa ushirikiano katika kipindi chake chote cha uwakilishi hapa nchini.
Mkurugenzi wa Idara ya Amerika na Ulaya Balozi Joseph Sokoine(wa kwanza kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga (wa kwanza kulia) na Afisa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Lilian Kimaro wakifuatilia mazungumzo hayo kwa makini.
Balozi Mahiga akiagana na Balozi Leveque mara baada ya kumaliza mazungumzo

=========================================

 .... Mazungumzo na Balozi wa Ireland hapa nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Balozi wa Ireland nchini, Mhe. Fionnuala Gilsenan alipokuja Wizarani kuaga mara baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini. Mhe. Mahiga alimpongeza na kumshukuru kwa kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Ireland katika sekta mbalimbali. Kwa upande wa Mhe. Gilsenan alitumia fursa hiyo kuishukuru Wizara na Serikali kwa ujumla kwa ushirikiano.

Wizara ya Mambo ya Nje yamkabidhi Waziri Mkuu michango ya Madawati

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akikabidhi hundi ya michango ya madawati kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa. Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika tarehe 28 Julai, 2016 katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chamazi iliyopo Mbagala nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Ally Hapi akipokea Hundi ya michango ya Madawati kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe. Geofrey Mwambe kutoka kwa  Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa. Mhe. Mwambe kabla ya uteuzi wake wa kuwa Mkuu wa Wilaya alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta ya Uzalishaji katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Waziri Mkuu, Mhe.Kassim  Majaliwa akihutubia hadhara iliyohudhuria kushuhudia makabidhiano ya michango ya Madawati yaliyotolewa na Ubalozi wa Kuwait pamoja na Jumuiya ya Mabohora iliyopo nchini. Katika hotuba yake aliwahimiza wanafunzi wa Shule ya Msingi Chamazi kusoma kwa bidii pamoja na Walimu ambao aliwaeleza kuwa serikali ya awamu ya tano inafanyia kazi malalamiko yao na itahakikisha wanalipwa stahili zao zote.
Mhe. Waziri Mahiga akihutubia wananchi katika hafla hiyo ambapo alieleza kuwa Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje (waliopo Wizarani na katika ofisi zetu za Ubalozi) wamekabidhi michango yenye thamani ya fedha taslim za Kitanzania shilingi 100, 176,825.52 katika kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli katika kuboresha sekta ya elimu nchini.
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akisalimiana na Mhe. Waziri Mahiga mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Shule ya Msingi Chamazi, pembeni kwa Waziri Mahiga ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje  na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Susan Kolimba. 
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiwa pamoja na viongozi waliokaa meza kuu wakati wimbo wa Taifa ukipigwa.
Mhe. Waziri Mkuu akisalimia sehemu ya Wanafunzi wa shule ya Msingi Chamazi.
Mhe. Waziri Mkuu akiwasalimia sehemu nyingine ya Wanafunzi hao

Wakurugenzi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja Mhe. Waziri Mkuu
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Waziri Mkuu pamoja na meza kuu.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan Mwinyi akimkaribisha Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem Al- Najem katika hafla ya makabidhiano ya madawati, ambapo Ubalozi wa Kuwait umechangia jumla ya madawati 600.
Msemaji na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi Mindi Kasiga (Kushoto) akiwa na Kaimu Mkuu wa Itifaki Bw. James Bwana wakiratibu hafla hiyo ya makabidhiano
Mhe. Waziri Mahiga akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Mhe. Humphrey Polepole, kulia kwa Mhe. Polepole ni Mkuu wa Wilaya ya Kindononi Mhe. Ally Hapi na Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Ramadhan Madabida.
=================================================


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), ameipongeza Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa kuitikia wito wa Serikali wa kuchangia madawati kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu nchini.


Mhe. Majaliwa ametoa pongezi hizo leo wakati wa hafla ya kupokea mchango wa Madawati wa Wizara zilizofanyika katika Shule ya Msingi Chamazi Jijini Dar es Salaam.Katika hotuba yake Mhe. Waziri Mkuu alisema kuwa anaipongeza Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki chini ya uongozi wa Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga kwa juhudi za kuwashirikisha wadau wanaofanya kazi kwa karibu na Wizara hiyo wakiwemo Mabalozi, Watumishi na Jumuiya mbalimbali za kimataifa katika kutekeleza wito wa Serikali na hatimaye kufanisha azma hiyo

“Nampongeza Balozi Mahiga kwa mbinu alizotumia za kuwashawishi Mabalozi, Watumishi na Jumuiya mbalimbali za kimataifa na hatimaye leo napokea madawati hayo ambayo ni msaada mkubwa kwa wanafunzi wa Wilaya hii ya Temeke ambayo ina idadi kubwa ya watu na wanafunzi pia” alisema Mhe. Majaliwa.

Mhe. Waziri Mkuu aliongeza kusema kuwa, Serikali imetekeleza kikamilifu azma ya kutoa elimu bure kwa tija ambapo shule zimefanikiwa kuandikisha wanafunzi wengi wa darasa la kwanza mwaka huu kuliko ilivyokuwa hapo awali. Aidha, alieleza kuwa Serikali inaendelea kumaliza changamoto zilizotokana na ongezeko hilo ikiwa ni pamoja na kuendelea kuongeza madawati, vyumba vya madarasa na kuboresha maslahi ya Walimu.

“Azma ya Serikali ya Elimu bure imekuwa na tija kwani wazazi wameandikisha kwa wingi watoto wao ambapo nimeambiwa shule hii ya Chamazi imeandikisha zaidi ya wanafunzi 700 wa darasa la kwanza, hayo ni mafanikio makubwa na kinachotakiwa ni Serikali kutekeleza mkakati wake wa kumaliza changamoto  zilizopo ili kuendana na ongezeko hilo” alisisitiza Waziri Mkuu.

Vilevile Mhe. Majaliwa alitumia fursa hiyo kuwaasa wazazi na walezi kuhakikisha wanafuatilia kwa karibu maendeleo ya watoto wao shuleni ikiwa ni pamoja na kutimiza wajibu wao wa msingi wa kuwapatia chakula, mavazi na vifaa kwa ajili ya kujifunzia.

Aidha, Mhe. Waziri Mkuu alitoa wito kwa wananchi na wadau mbalimbali bila kujali dini, rangi, kabila wala itikadi za kisiasa kuendelea kuchangia maendeleo ya nchi hususan katika sekta ya elimu ili kuwawezesha watoto wa kitanzania kupata elimu bora.

Awali akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga alisema kuwa ili kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli na kwa kutambua umuhimu wa elimu kwa maendeleo ya nchi, Wizara ilihamasika na kuhakikisha inachangia sekta hiyo ya elimu ili kufikia malengo yaliyokusudiwa. 

Wakati wa hafla hiyo Wizara ilimkabidhi Waziri Mkuu jumla ya Shilingi milioni mia moja zilizochangwa na Watumishi wa Wizara, madawati 600 kutoka Ubalozi wa Kuwait hapa nchini na mengine 105 kutoka Jumuiya ya Mabohora nchini. Kati ya fedha hizo shilingi milioni 85 zilikabidhiwa kwa ajili ya kutengeneza madawati kwa ajili ya Shule za Wilaya ya Temeke huku milioni 15 zikipelekwa Wilaya ya Manyoni kwa ajili ya madawati.

-Mwisho-
 
Wednesday, July 27, 2016

Tanzania na Korea Kusini kuimarisha ushirikiano

Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbelwa Kairuki (katikati) akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa masuala ya Afrika na Mashariki ya Kati wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Korea Kusini, Bw. KWON Hee-seog (hayupo pichani). Mazungumzo hayo rasmi ambayo yalijikita katika kujadili masuala ya ushirikiano baina ya Tanzania na Korea Kusini yalifanyika katika Ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Julai, 2016. Wengine katika picha ni Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia mazungumzo.
Mkurugenzi wa masuala ya Afrika na Mashariki ya Kati kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea Kusini, Bw. Kwon Hee-seog (kulia) akizungumza ambapo alieleza nia ya Serikali ya Korea katika kuendelea kuimarisha ushirikiano na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hususan katika sekta ya elimu, biashara, uwekezaji na masuala ya utamaduni. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi masuala ya Mashariki ya Kati wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Korea ni Bw. JO Joosung.
Bw. Kwon Hee- seog akiwa pamoja na wajumbe aliofuatana nao wakifuatilia mazungumzo.
Mkutano ukiendelea