Monday, July 31, 2017

Waziri Mahiga akutana na Mchungaji Ongere

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akisalimiana na Mchungaji John Oscar Ongere ambaye alifika ofisini kwa Mhe. Waziri kujadili maandalizi ya Kongamano kubwa la uwekezaji linalotarajiwa kufanyika nchini mwezi Novemba 2017..Kongamano hilo litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam litajumuiya wafanyabiashara wakubwa kutoka kote duniani na wa hapa nchini kujadiliana namna bora ya kutumia fursa lukuki za uwekezaji zilizopo hapa nchini.

Mchungaji Ongere akifanya maombi kwa ajili ya kuiombea nchi amani na utulivu ili iweze kukua kiuchumi
Picha ya pamoja
 Balozi wa Iran
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Iran nchini Tanzania, Mhe. Mousa Farhang ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo.  Mazungumzo yao pamoja na mambo mengine walijadili maandalizi ya sherehe za kumuapisha Rais Mteule wa Iran, Mhe. Hassan Rouhani zitakazofanyika Tehran tarehe 05 August 2017.

Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia mazungumzo hayo, Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Bi. Zainab Angovi-Mrutu, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Bw Ayoub Mndeme na Katibu wa Waziri, Bw. Gerald Mbwafu.

Ujumbe aliofuatana nao Balozi wa Iran ukifuatilia mazungumzo.

Saturday, July 29, 2017

Balozi Mahiga apokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi mteule wa Uganda

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb) akipokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Uganda nchini Tanzania, Mhe. Richard Tumusiime Kabonero katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Kagera, leo tarehe 29/07/2017. Waziri Mahiga yupo Mkoani Kagera kwaajili ya kuhudhuria Mkutano wa Ujirani mwema Kati ya Tanzania na Uganda. 
Waziri Mahiga akizungumza na Balozi Mteule Kabonero
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mej.Gen. Salum M. Kijuu ( wa pili kutoka kulia), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga ( wa kwanza kushoto), Balozi wa Tanzania nchini Uganda Mhe. Grace Mgavano (wa pili kutoka kushoto) na Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Afrika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, nao walikuwepo kushuhudia tukio hilo
Balozi Mgavano akisalimiana na Balozi Mteule Kabonero
Waziri Mahiga akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya kupokea nakala za utambulisho za Balozi Mteule Mhe. Kabonero.

Friday, July 28, 2017

KIKAO CHA MAKATIBU WAKUU CHA UJIRANI MWEMA BAINA YA TANZANIA NA UGANDA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Aziz Mlima akizungumza wakati akifungua mkutano wa ujirani mwema kati ya Tanzania na Uganda, ngazi ya Makatibu Wakuu. Mkutano huo unao jadili pia masuala ya mpaka umefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa ELCT Mjini Bukoba, Mkoani Kagera.
Ujumbe kutoka nchi ya Uganda wakifuatilia kwa makini hotuba ya Dkt. Mlima (hayupo pichani),  alipokuwa akizungumza wakati wa ufunguzi.
Ujumbe wa upande wa Tanzania nao wakimsikiliza kwa makini Dkt. Mlima (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, wa kwanza kutoka kulia ni Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Gerson Mdemu (wa kwanza kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome, na wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi Dr. Florens Turuka
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Uganda  Balozi Patrick Mugoya naye akizungumza kwenye ufunguzi  wa Mkutano huo kati ya Tanzania na Uganda kwa ngazi ya Makatibu wa Kuu.
Dkt. Mlima (katikati) akitoa miongozo ya kikao hicho, wa kwanza kulia ni Bw. Suleiman Salehe (kulia), Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Afrika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na wa kwanza kushoto ni  Balozi Mugoya.
Sehemu ya Ujumbe wa Tanzania ukisikiliza  kwa makini miongozo iliyokuwa inatolewa na Dkt. Mlima (hayupo pichani).
Sehemu ya Makatibu wa Kuu upande wa Uganda, nao wakisikiliza kwa makini miongozo iliyokuwa ikiendelea kutolewa na Dkt. Mlima (hayupo pichani), wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Uganda, na kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Mazingira Uganda.
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kagera Naibu Kamishina Jeremiah M. Nkondo (wa kwanza kulia) pamoja na Naibu Afisa Uhamiaji Mkoa wa Kagera Bw. Butenge  Christopher.


Tanzania kuimarisha mipaka yake na nchi jirani

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi (Mb.), katikati, anaongoza ujumbe wa Tanzania kwenye ziara ya kutembelea na kujifunza juu ya mipaka iliyopo kati ya Tanzania na Uganda. Watatu kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Isaack Kamwele, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Suzan Kolimba (wa tatu kutoka kulia), Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Aziz Mlima (wa pili kutoka kulia), Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe Gerson John Mdemu (wa kwanza kulia) na wa kwanza kushoto ni Bw. Deogratias Nholope, wakitizama Mto Kagera ulipopita.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Suzan Kolimba akisalimiana na wanakijiji wanaoishi mpakani mwa Tanzania na Uganda, mara baada ya kuwasili kwenye eneo hilo na kujionea alama za mipaka.
Mhe. Lukuvi pamoja na ujumbe wa Manaibu Waziri wakisalimiana na wanakijiji wa pande zote mbili, ambapo wananchi hao walionekana kufurahishwa na ziara hiyo.
Mhe. Lukuvi pamoja na ujumbe alioambatana nao, wakiwemo wataalamu kutoka sekta mbalimbali nchini Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja.
Mhe. Lukuvi akijadiliana jambo na Manaibu Waziri alioambatana nao kwenye ziara ya kujifunza na kujionea mipaka iliyopo kati ya Tanzania na Uganda. Wa pili kutoka kulia ni Mhe. Dkt. Susan Kolimba Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mhandisi Isaack Kamwelwe Naibu Waziri wa Maji (wa pili kutoka kulia), na Naibu Waziri wa TAMISEMI, Utumishi na Utawala Bora Mhe. Jafo Selemani Said (wa kwanza kulia).
Ziara ikiendelea ambapo Ujumbe ulioongozwa na Mhe. Lukuvi alipata fursa ya kutembelea majengo yanayotumika kwenye kukagua mizigo na kukusanya ushuru wa forodha kati ya Tanzania na Uganda yanayopatikana eneo la Mtukula.
Picha ya pamoja ya ujumbe wa viongozi na wataalam wa Tanzania ulioongozwa na Waziri Lukuvi wakiwa kwenye moja ya alama iliyopo mpakani mwa Tanzania na Uganda.

Thursday, July 27, 2017

Balozi Mero amkaribisha Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu Professa Mussa Assad New YMork

Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Modest Mero akimkaribisha Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali Professa Mussa Assad kwenye ofisi za uwakilishi Jijini New York Marekani hivi karibuni. 

http://www.mwananchi.co.tz/habari/CAG-awasilisha-ukaguzi-mashirika-ya-Umoja-wa-Mataifa/1597578-4034028-j2vri7/index.html

TAARIFA YA KIFO CHA BI. LOVENESS HERMAN, MTANZANIA MWENYE URAIA WA UBELGIJI

 
Mwenye picha katika kitambulisho hapo juu ni Bi. Loveness Herman (69), Mbelgiji mwenye asili ya Tanzania ambaye alifariki huko Liege, Ubelgiji tokea tarehe 18 Mei 2017. Marehemu Loveness Herman kabla ya kuhamia Ubelgiji na kuchukuwa uraia wa nchi hiyo katika miaka ya 1980 alikuwa akiishi Dar es Salaam. Tokea alipohamia Ubelgiji, Marehemu alikuwa akiishi peke yake na hakuwahi kupata mtoto. Kwa taarifa hii, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kupitia Ubalozi wake wa Brussels inawatafuta ndugu zake ili iwape taarifa kamili za msiba huo
Kwa maelezo zaidi  piga simu katika namba hii +3226406500 au barua pepe brussels@nje.go.tz.

                             

Kaimu Balozi wa Saudi Arabia atembelea Wizara ya Mambo ya Nje

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akiwa katika mazungumzo na Kaimu Balozi wa Saudi Arabia nchini, Bw. Bandar Abdullah Alhazani ofisini kwake jijini Dar es Salaam. Masuala yaliyojadiliwa katika mazungumzo hayo ni pamoja na uhusiano kati ya Tanzania na Saudi Arabia ambao ulielezwa kuwa ni mzuri.

Waziri Mahiga akisoma barua aliyokabidhiwa na Kaimu Balozi ambayo ni mwaliko kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia ikimwalika kufanya ziara ya kikazi nchini humo katika muda utakaopangwa baadaye. Mhe. Mahiga anaalikwa nchini Saudi Arabia kufuatilia utekelezaji wa masuala yaliyoafikiwa wakati Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia alipofanya ziara hapa nchini mwezi Machi 2016.

Mazungumzo yanaendelea



Wednesday, July 26, 2017

Tanzania calls for immediate solution on Diplomatic crisis in Gulf Countries


PRESS STATEMENT

Tanzania calls for immediate solution on Diplomatic crisis in Gulf Countries

The united Republic of Tanzania is supporting the initiatives taken by the Amir of Kuwait HH Sheikh Sabah Al-Jaber Al-Sabah’s mediation efforts to address the Gulf crisis and the exploration of possible solution methods.

The diplomatic crisis began in June 5th 2017 when Saudi Arabia, United Arab Emirates, Bahrain, and Egypt abruptly cut off diplomatic relations with Qatar by withdrawing ambassadors and imposing trade and travel bans.

Tanzania call for unity and stability of the Gulf region and it emphasis that a solution should be found within the framework of the Gulf Cooperation Council and in that regards, it joins and support the initiative of the State of Kuwait that called for the crisis to be resolved through peaceful negotiations.

We therefore, appeal to the Gulf Nations to quickly resolve their disputes in peaceful and diplomatic manner.


Issued by Government Communication Unit, Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation

26 July, 2017

Hafla ya kumuaga Balozi wa Israeli nchini Mhe. Yahel Vilan

  
 Balozi Innocent Shiyo Mkurugenzi wa Idara ya Afrika akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Balozi Augustine Mahiga kwenye hafla ya kumuaga Balozi wa Israel Nchini aliyemaliza muda wake Mhe. Yahel Vilan,  tarehe 22 Julai,2017-  Hyatt, Dar es salaam.


Balozi Innocent Shiyo akimkabidhi zawadi Mhe.Balozi Yahel Vilan kwa niaba ya Mhe. Waziri Mahiga katika hafla hiyo.

Balozi Innocent Shiyo na Balozi Vilan pamoja na wageni wengine wakiwa katika hafla hiyo.

Tuesday, July 25, 2017

Balozi Mahiga apokea Nakala za Hati za Utambulisho za Mabalozi Watatu


Balozi Mteule wa Jamhuri ya Indonesia

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb) akipokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Jamhuri ya Indonesia nchini Tanzania, Mhe. Prof. Ratlan Pardede ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akiwa katika mazungumzo na Balozi Mteule wa Jamhuri ya Indonesia nchini Tanzania, Mhe. Prof. Ratlan Pardede. Katika mazungumzo hayo, Mhe. Waziri aliisifu Indonesia kwa hatua ya maendeleo iliyofikia katika nyanja mbalimbali ikiwemo sekta ya kilimo na kuelezea matumaini yake kuwa ujio wa Mhe. Balozi utasaidia kuimarisha mahusiano kati ya Tanzania na Indonesia yatakayosaidia Tanzania kujifunza kutokana na maendeleo ya Indonesia.
 
Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia mazungumzo hayo. Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Autralasia, Bi Justa Nyange, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Bi. Mindi Kasiga na Afisa Dawati, Bw. Emannuel Luangisa

 Mwakilishi wa Papa, Tanzania


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb) akipokea Nakala za Hati za Utambulisho za Mwakilishi Mteule wa Papa nchini Tanzania, Mhashamu Marek Solczynski ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akiwa katika mazungumzo na Mwakilishi Mteule wa Papa nchini Tanzania, Mhashamu Marek Solczynski.
Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia mazungumzo hayo. Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Bi Mary Matari, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Bi. Mindi Kasiga na Afisa Dawati, Bw. Ceaser Waitara.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Mwakilishi Mteule wa Papa nchini Tanzania, Mhashamu Marek Solczynski mara baada ya kuwasili Wizarani kwa ajili ya kuwasilisha Nakala za  Hati za Utambulisho.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akibusu pete ya Mwakilishi Mteule wa Papa nchini Tanzania, Mhashamu Marek Solczynski kabla ya kupokea Nakala za  Hati za Utambulisho.


Balozi Mteule wa Ujerumani
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb) akipokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Shirikisho la Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. Dkt. Detlef Wachter ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akiwa katika mazungumzo na Balozi Mteule wa Shirikisho la Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. Dkt. Detlef Wachter. Katika mazungumzo hayo, Mhe. Waziri aliishukuru Ujerumani kwa msaada mkubwa inaotoa kwa Tanzania, hususan katika kulinda rasilimali ikiwemo hifadhi za Taifa na kusisitiza umuhimu wa makampuni makubwa ya Kijerumani kuja kuwekeza nchini.

Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia mazungumzo hayo. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Itifaki, Bi. Grace Martin, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Bi. Mindi Kasiga na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Bi Mary Matari.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Balozi Mteule wa Shirikisho la Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. Dkt. Detlef Wachter mara baada ya kuwasili Wizarani kwa ajili ya kuwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho.

Picha ya pamoja.