Friday, May 31, 2013

Tanzania signs a Memorandum of Understanding for the Kinyerezi Power Project


The Deputy Secretary in the Ministry of Finance Dr Servacius Likwelile and Sumitomo Corporation Senior Official signs a Memorandum of Understanding (MoU) for Kinyerezi 240 MW combined cycle power project at SUMITOMO Corporation Headquarters in Tokyo, Japan on May 31, 2013.  Witnessing the signing ceremony is President Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania and Mr. Kuniharu Nakamura, President of the SUMITOMO Corporation. 

The Deputy Secretary in the Ministry of Finance Dr Servacius Likwelile exchanges Memorandum of Understanding with Sumitomo Corporation Senior Official. (All Photos by Freddy Maro of the State House)


Rais Kikwete amteua Mtendaji Mkuu wa Kwanza wa Kusimamia Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Programu na Miradi ya Maendeleo nchini


Japan kuangalia uwezekano wa kugharimia Reli ya Kati


Japan yatangaza mabilioni kusaidia Tanzania


Tanzania yaunga mkono ombi la Japan kuhusu Olimpiki


Mhe. Membe awasilisha Hotuba ya Bajeti Bungeni

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akiwasilisha Bungeni Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014. Hotuba hiyo iliwasilishwa tarehe 30 Mei, 2013.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) akifuatilia kwa makini Hotuba ya Wizara ilipokuwa ikiwasilishwa Bungeni na Mhe. Membe (hayupo pichani)


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule (wa sita mstari wa mbele) akiwa na Naibu Katibu Mkuu, Balozi Rajabu Gamaha (kushoto kwa Katibu Mkuu) pamoja na Wakuu wa Idara, Vitengo na Taasisi za Wizara wakifuatilia kwa makini mwenendo wa Bunge mjini Dodoma.

Wakurugenzi wengine kutoka Wizarani na Taasisi wakiwa Bungeni Mjini Dodoma

Baadhi ya Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini na Wageni wengine wakifuatilia kwa makini Hotuba ya Mhe. Membe (hayupo pichani) Bungeni leo akiwemo Mkuu wa Mabalozi na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Mhe. Juma Khalfan Mpango na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU), Mhe. Balozi Filberto Ceriani Sebregondi.

Baadhi ya Wanafunzi wanaosomea Shahada ya Uhusiano wa Kimataifa katika Chuo Kikuu cha Dodoma wakifuatilia Hotuba ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa iliyowasilishwa na Mhe. Membe.

Mhe. Juma Nkamia (Mb.), Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwasilisha Hotuba kwa niaba ya Kamati hiyo huku Mhe. Membe na Mhe. Maalim wakifuatilia.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai (Mb.) akiahirisha Kikao cha Bunge leo tarehe 30 Mei, 2013.

Mhe. Membe akiwaeleza Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini sababu zilizopelekea Kikao cha Bunge kuahirishwa.

Mhe. Membe akiteta jambo na Balozi Sebregondi.

Wananchi kutoka Vijiji mbalimbali vya Mkoa wa Lindi wakiwemo kutoka Jimbo la Mtama linalowakilishwa na  Mhe. Membe wakipata picha ya pamoja mara baada ya kusikiliza Hotuba ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Mhe. Membe akisalimiana na baadhi ya Wananchi kutoka Lindi.

Mhe. Maalim akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wananchi kutoka Jimbo la Muyuni, Zanzibar waliofika Bungeni kufuatilia Hotuba ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushiririkiano wa Kimataifa

Picha zaidi za Mhe. Maalim na wananchi kutoka Jimbo la Muyuni, Zanzibar.

Thursday, May 30, 2013

HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA - 30 MEI, 2013

Hotuba Ya Bajeti Nje 2013
President Kikwete arrives in Tokyo for TICAD meeting Kikwete arrives in Tokyo for TICAD meeting:
Daily News - -  President Jakaya Mrisho Kikwete has arrived in Tokyo, Japan on Wednesday, ready to attend the 5th Tokyo international Conference on African Development (TICAD-V), scheduled to be held on June 1 to 3 this year, at the invitation of the Japanese Prime Minister Shinzo Abe. The meeting will be attended by leaders from Africa, Japan as well as development partners including the World bank, African Development Bank, United Nations, African Union and the United Nations Development Programme (UNDP). 


President Kikwete's Speech for the Regional Oversight Mechanism - DRC Peace


Wednesday, May 29, 2013

Mhe. Membe aongoza kikao cha Menejimenti ya Wizara cha maandalizi ya uwasilishaji wa Bajeti Bungeni

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akiwa na Naibu Waziri, Mhe. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) wakipitia Makabrasha kabla ya kuanza kwa kikao na Menejimenti ya Wizara ikiwa ni maandalizi ya mwisho kabla ya uwasilishaji wa Hotuba ya Bajeti ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014 itakayowasilishwa Bungeni tarehe 30 Mei, 2013. Kikao hicho kilifanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara mjini Dodoma tarehe 29 Mei, 2013

Mhe. Membe akiongoza kikao hicho cha maandalizi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule na Balozi Rajabu Gamaha, Naibu Katibu Mkuu wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) wakati wa kikao hicho.

Wakuu wa Idara, Vitengo na Taasisi za Wizara wakifuatilia masuala mbalimbali katika makabrasha wakati wa kikao na Mhe. Waziri. Kutoka kulia ni Bw. Dushhood Mndeme, Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Balozi Irene Kasyanju, Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria, Bw. Gabriel Mwero, Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi, Bw. Lucas Suka, Mkuu wa Kitengo cha Ugavi, Bw. Lupakisyo Mwakitalima, Mhasibu Mkuu na Bibi Rehema Twalib, Mkurugenzi wa Taasisi ya Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM).

Wakurugenzi wa Idara za Sera na Mipango Bw. James Lugaganya (kushoto), Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (katikati) na Mashariki ya Kati, Balozi Simba Yahya (kulia) wakiendelea na kikao.

Mkurugenzi wa Chuo cha Diplomasia, Balozi Mohammed Maundi (kushoto) na Bw. Andy Mwandembwa, Kaimu Mkuu wa Itifaki wakimsikiliza Mhe. Waziri (hayupo pichani)

Wakurugenzi wakiendelea kupitia makabrasha hatua kwa hatua wakati wa kikao hicho. Kutoka kushoto ni Balozi Bertha Semu-Somi, Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora, Balozi Naimi Aziz, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda na Balozi Vincent Kibwana, Mkurugenzi wa Idara ya Afrika.

Bw. Omar Mjenga (kushoto), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Ausralasia na Bw. Khamis Kombo, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje Zanzibar wakifuatilia kikao kwa makini

Wajumbe wengine kutoka Wizarani na Taasisi za Wizara wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) wakati wa kikao hicho. Kushoto ni Bw. Charles Bekoni, kutoka Chuo cha Diplomasia, Bibi Mary Kyando kutoka APRM na Bw. Kombo Hamis

Kikao kikiendelea

Ijue Wizara ya Mambo ya Nje (Sehemu ya Pili)


Tanzania Yaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Dkt. Emmanuel Nchimbi (Mb), akitoa hotuba katika sherehe ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani Duniani ilyofanyika kwenye Viwanja vya Mashujaa, Mnazi Mmoja, Dar es Salaam

Mwakilishi wa Bw. Alberic Kacou, Mratibu Mkazi wa UNDP nchini Tanzania, Bw. Richard Regan ambaye ni Mwakilishi wa Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) nchini Tanzania naye akitoa hotuba katika sherehe hizo.
Dkt. Emmanuel Nchimbi akisalimiana na Mwakilishi kutoka Jeshi la Wananchi wakati wa sherehe hizo

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi akisalimiana na wanajeshi waliowahi kulinda amani katika nchi mbalimbali duniani.

Bw. Nathaniel Kaaya, (R) Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akibadilishana Mawazo na Kaimu Balozi wa Uturuki wakati wa kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani.

Picha zote na Reginald Philip KisakaSaturday, May 25, 2013

OAU/AU IMEFANIKIWA: MEMBE

OAU/AU IMEFANIKIWA: MEMBE

Na Ally Kondo

Umoja wa Afrika (OAU/AU) umepata mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake mjini Addis Ababa, Ethiopia tarehe 25 Mei, 1963.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) katika sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Umoja huo iliyofanyika katika Viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2013.

Mhe. Membe alieleza kuwa, AU imefanikiwa kutimiza lengo la kuzikomboa nchi zote za Bara la Afrika isipokuwa Saharawi kutoka katika tawala za kikoloni. Alisema katika kufanikisha hilo, Tanzania imechangia kwa kiasi kikubwa kwani, Makao Makuu ya Ukombozi ya AU yalikuwa hapa nchini.

Kuhusu Demokrasia na Utawala Bora katika nchi za Afrika, Mhe. Waziri alisema kuwa AU imeweka utaratibu mzuri wa kuhakikisha kuwa wanachama wake wanaheshimu utawala wa sheria kwa kuweka sheria kali za kukomesha tabia ya kuingia madarakani kwa njia ya mapinduzi ya kijeshi. Sheria hizo ni pamoja na; nchi inayotawaliwa kijeshi kusimamishwa uanachama wa AU, kuwekewa vikwazo vya kiuchumi pamoja na Kiongozi wa Mapinduzi kutoruhusiwa kuwania nafasi ya Urais katika uchaguzi wa kidemokrasia.

Kutokana na msimamo huo, AU imefanikiwa kupunguza matukio ya mapinduzi katika nchi za Afrika tangu ilipoanzishwa. “Afrika imeshuhudia matukio ya mapinduzi matano katika kipindi cha miaka mitano iliyopita ukilinganisha na matukio 34 yaliyotokea kabla ya kipindi hicho”. Mhe. Membe alisikika akisema.

Katika kukabiliana na migogoro inayozuka mara kwa mara katika nchi za Afrika, alisema kuwa, AU imebadilisha kipengele ambacho kilikuwa kinakataza nchi za Afrika kuingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine. Hivyo, kutokana na mabadiliko hayo nchi za Afrika sasa zinaweza kuingia katika nchi nyingine kulinda amani.

Kwa upande wa maendeleo ya kiuchumi, Mhe. Waziri alisema kuwa hatua kubwa imefikiwa, hususan kupitia Jumuiya za Kiuchumi za Kikanda, kama vile SADC, EAC na ECOWAS. Hata hivyo alibainisha kuwa, ukosefu wa miundombinu imara kama barabra na reli, kuunganisha Bara zima la Afrika ni kikwazo katika kufikia malengo ya kiuchumi kwa nchi nyingi za Afrika.

Sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Umoja wa Afrika (OAU/AU) zilipambwa na shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwasha mwenge wa AU, maandamano na burudani kutoka vikundi mbalimbali vya utamaduni. Aidha, sherehe hizo zilihudhuriwa na Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimatafa hapa nchini, wanafunzi na wananchi.