Thursday, May 23, 2013

WARSHA YA WAZI KUJADILI MATOKEO YA UCHAMBUZI WA KINA WA MAENEO YA KIPAUMBELE YA KITAIFA


Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi (Ikulu) inawatangazia na kuwaalika wadau na wananchi wote kuhudhuria Warsha ya Wazi (Open Day) kupata maelezo, kujadili na kutoa maoni juu ya miradi na program zitakazotekelezwa na Serikali kwa kipindi cha miaka mitatu (2013/14 hadi 2015/16) katika maeneo ya kipaumbele yaliayoainishwa katika Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/12 – 2015/16).

Miradi hiyo inatokana na uchambuzi wa kina uliofanywa na wataalamu wa kitanzania kwa kutumia mfumo mpya wa kimaabara (labs).

Huu ni mfumo ambao Serikali imeuanzisha ili kuhakikisha ushirikishwaji mpana wa wadau na wananchi kwa ujumla katika utekelezaji wa miradi ya kipaumbele ya Kitaifa.

Warsha hiyo ya wazi itafanyika kesho Ijumaa tarehe 24/05/2013 katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa mkabala na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) jijini Dar es Salaam kuanzia saa 3:00 asubuhi.

Wote mnakaribishwa!

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano

Ikulu

DAR ES SALAAM

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.