Saturday, May 31, 2014

PRESIDENT KIKWETE CONGRATULATES NEWLY ELECTED PRESIDENT OF MALAWI H.E PETER MUTHARIKA

H.E. PETER MUTHARIKA
PRESS RELEASE
H.E. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania has sent a congratulatory message to H.E. Peter Mutharika President of the Republic of Malawi. 

The message reads as follows;

“H.E. Peter Mutharika,
 President of the Republic of Malawi,
 Lilongwe,
         MALAWI.

          Your Excellency,
I have received with great pleasure, the news of your election as the new President of the Republic of Malawi following the general elections held on 20th May 2014. I would like, on behalf of the People and Government of the United Republic of Tanzania and on my own behalf, to extend to Your Excellency, our sincere congratulations on your impressive victory and that of your Party, the Democratic Progressive Party. 

Your victory in these heavily contested elections is a clear testimony of the trust and confidence that the people of Malawi have bestowed on you and your exemplary leadership.

I wish you every success as you take up the responsibilities and challenges of the leadership of your great nation. It is my hope that during your tenure of office, the people of Malawi will enjoy greater prosperity and development. It is equally my hope that under your able leadership, the excellent bilateral relations existing between our countries and their people will be strengthened further and taken to even higher heights.

I look forward to working closely with Your Excellency not only in fostering our bilateral relations but also to concert our efforts in the cause for peace and stability in our region and the African Continent as a whole. 

Please accept, Your Excellency, my best wishes for your personal good health and peace and prosperity for the people of Malawi. 
Dr. Jakaya Mrisho Kikwete
PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA”

ISSUED BY: 

THE MINISTRY OF FOREIGN AFFAIRS AND INTERNATIONAL COOPERATION, 

DAR ES SALAAM.


31ST MAY, 2014.

Friday, May 30, 2014

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki ziarani nchini


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akimpokea kwa furaha Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Mhe. Ahmet Dovutoglu ambaye yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu yenye lengo la kukuza na kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Uturuki.
Mhe. Membe akiwa ameongozana na Mhe. Dovutoglu mara baada ya kumpokea wakielekea katika Hoteli ya Hyatt Regency kwa ajili ya mazungumzo rasmi.
Mhe. Membe na Mhe. Dovutoglu wakiwa na Wajumbe waliofuatana nao wakati wa mazungumzo rasmi.
Mhe. Membe kwa pamoja na Mhe. Dovutoglu wakizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano ikiwa ni pamoja na kuangalia namna Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) linaweza kushirikiana na Shirika la Ndege la Uturuki (Turkish Airlines) 
Mhe. Waziri Membe akizungumza.
Baadhi ya Wakurugenzi na Kaimu Wakurugenzi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa pamoja na Waandishi wa habari wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani)
Mhe. Dovutoglu nae akizungumza wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari
Mkutano ukiendelea
Mhe. Membe kwa pamoja na Mhe. Dovutoglu wakijibu maswali ya waandishi wa habari.
Picha na Reginald Philip

Thursday, May 29, 2014

Maadhimisho ya siku ya walinda Amani ya Umoja wa Mataifa yafanyika Dar

Waziri wa Ulinzi Dkt. Hussein Mwinyi akihotubia katika maadhimisho ya siku ya walinda Amani wa Umoja wa Mataifa yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja.

Mabalozi wakimsikiliza Waziri Mwinyi (hayupo pichani).
Dkt. Mwinyi akiweka Shada katika mnara wa Mashujaa kuashiria kuwakumbuka walindaamani waliopoteza maisha duniani kote. 

Mabalozi mbalimbali wanao ziwakilisha Nchi zao hapa nchin nao walihudhuria maadhimisho hayo
Waziri waulinzi Dkt. Mwinyi akiagana na mabalozi waliohudhuria maadhimisho hayo

Dkt. Mwinyi akiagana na walinda Amani mara baada ya kumalizaka kwa sherehe hizo 

Waziri wa Ulinzi akiongea na waandishi wa habari.

Picha na Hassara Kilalika


Konga mano la Nyumba kufanyika Dubai

Balozi Mdogo wa Tanzania nchini Dubai Bw. Omari Mjenga akifanya mazungumza na Nehemiah Mchechu (kulia) Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) alipo mtembelea Ofisini kwake Jijini Dubai, mazungumzo hayo yalihusu maandalizi ya Kongamano la uwekezaji katika sekta ya nyumba litakalofanyika Jumeirah Madnat Hotel Dubai. Kongamano  hilo limeandaliwa na Ubalozi Mdogo wa Tanzania uliopo Dubai kwa kushirikiana na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika Kongamano hilo makampuni makubwa ya sekta ya nyumba dubai na mengine kutoka Nchi za Muungano wa Ukanda wa Mashariki ya Kati yatashiriki.

Mazungumzo yakiendelea


Tuesday, May 27, 2014

Waziri Membe aliwasilisha Bajeti ya Wizara Bungeni Dodoma

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akiwasilisha Bungeni  Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa mwaka wa fedha 2014/2015 mjini Dodoma tarehe 27 Mei 2014
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule (wa tatu kutoka kushoto) akiwa na Naibu Katibu Mkuu, Balozi Rajabu Gamaha (wa kwanza kulia) pamoja na Mke wa Waziri, Mama Dorcas Membe na Mkurugenzi wa Chuo cha Diplomasia, Balozi Mohammed Maundi wakifuatilia kwa makini Hotuba ilikuwa ikitolewa na Mhe. Membe (hayupo pichani) Bungeni.
Katibu Mtendajii wa Jumuiya ya Maedneleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika, Dkt. Stergomena Tax (katikati) akiwa na wageni wengine wakifutilia Hotuba ya Makadirio ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa mwaka 2014/2015
Baadhi ya Wawakilishi kutoka Balozi za nchi mbalimbali zilizopo hapa nchini wakifuatilia Hotuba ya Mhe. Membe (hayupo pichani)
Baadhi ya Wanafunzi kutoka Vyuo Vikuu vya Mzumbe, SAUT, UDSM, UDOM na CFR wanaochukua Kozi za Uhusiano wa Kimataifa wakifuatilia hotuba ya Mhe. Membe.
Baadhi ya Wakurugenzi na Wakurugenzi Wasaidizi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje wakifuatilia hotuba ya Mhe. Membe

Watendaji  kutoka Wizara ya Mambo ya Nje wakifuatilia hotuba.
Watendaji wengine kutoka Wizara ya Mambo ya Nje wakifuatilia Hotuba ya Mhe. Membe.
Wajumbe wakimsikiliza Mhe. Membe
Mwakilishi kutoka Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Betty Machangu (Mb.) akiwasilisha Hotuba kwa niaba ya Kamati hiyo
Mhe. Membe (kushoto) akiwa na Naibu wake Mhe. Dkt. Mahadhii Juma Maalim (Mb.) wakifuatilia hotuba wakati Mhe. Machangu (hayupo pichani) akiwasilisha
Waziri Kivuli wa Mambo ya Nje kutoka Kambi ya Upinzani, Mhe. Ezekiel Wenje nae akiwasilisha hotuba ya kambi yake.
Mhe. Membe akiongozana na Mhe. Wenje kutoka Bungeni mara baada ya kipindi cha mchana kumalizika.
Mhe. Membe, Mama Dorcas Membe (wa nne kutoka kushoto) katika picha ya pamoja na Dkt. Tax  wakiwa nje ya Viwanja vya Bunge mara baada ya kipindi cha mchana kumalizika
Mhe. Membe akimtambulisha Mhe. Wenje kwa Balozi wa DRC hapa nchini Mhe. Juma Mpango
Mhe. Membe katika picha ya pamoja na wanafunzi aliowaalika  kutoka vyuo vikuu mbalimbali nchini 
Katibu Mkuu, Bw. Haule akimpongeza Mhe. Maalim mara baada ya Bajetii ya Wizara kupitishwa na Bunge
Mhe. Maalim akifurahia jambo na Mhe. John Shibuda (Mb.)
Mhe. Membe akipongezwa na Mkewe Mama Dorcas mara baada ya Bunge kupitisha Hotuba ya Wizara
Picha ya Pamoja 

Baadhi ya Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa

Sunday, May 25, 2014

Sherehe za Kuadhimisha Siku ya Afrika Zafana jijini Dar es Salaam

Brass band ikiongoza maandamano ya wanadipolomasia wa nchi za Afrika, watumishi wa Serikali ya Tanzania, wanafunzi na wageni wengine waalikwa kwenda Viwanja vya Karimjee kuadhimisha Siku ya Afrika.

Wanafunzi wakiwa wamebeba bendera mbalimbali za nchi za Afrika na ile ya Umoja wa Afrika wakiwa katika maandamano kuelekea Viwanja vya Karimjee.

Waheshimiwa Mabalozi wa Nchi za Afrika nchini Tanzania wakiwa katika maandamano ya kuadhimisha Siku ya Afrika

Waheshimiwa Mabalozi wakiendelea na maandamano
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb) aliyevaa suti ya rangi ya kijivu akipokea maandamno katika Viwanja vya Karimjee 

Burudani ya ngoma katika Viwanja vya Karimjee kusherehekea Siku ya Afrika


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt Mahadhi Juma Maalim akiwahutubia watu waliohudhuria sherehe za Siku ya Afrika. Naibu Waziri alipongeza kaulimbiu ya maadhimisho hayo ambayo ni Kilimo na Usalama wa Chakula. Alisema usalama wa Chakula ni changamoto ambayo  lazima nchi za Afrika zichukuwe juhudi za pamoja kukabiliana nayo

Wanadiplomasia na wananchi wengine wakimsikiliza Naibu Waziri.

Balozi wa Kenya akichangia mada Kilimo na Usalama wa Chakula.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Dkt. Yamungu Kayandabila naye akitoa neno wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afrika

Balozi Sweden nchini Tanzania alipata fursa pia ya kuchangia mada katika maadhimisho hayo 


Picha ya pamoja ya Mabalozi na Mabalozi wastaafu mara baada ya sherehe za kuadhimisha Siku ya Afrika kukamilika

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim akihojiwa na wana habari


Picha ya pamoja kati ya Dkt. Maalim na Wanadipolomasia.



Picha na Reginald Philip