Sunday, May 25, 2014

Sherehe za Kuadhimisha Siku ya Afrika Zafana jijini Dar es Salaam

Brass band ikiongoza maandamano ya wanadipolomasia wa nchi za Afrika, watumishi wa Serikali ya Tanzania, wanafunzi na wageni wengine waalikwa kwenda Viwanja vya Karimjee kuadhimisha Siku ya Afrika.

Wanafunzi wakiwa wamebeba bendera mbalimbali za nchi za Afrika na ile ya Umoja wa Afrika wakiwa katika maandamano kuelekea Viwanja vya Karimjee.

Waheshimiwa Mabalozi wa Nchi za Afrika nchini Tanzania wakiwa katika maandamano ya kuadhimisha Siku ya Afrika

Waheshimiwa Mabalozi wakiendelea na maandamano
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb) aliyevaa suti ya rangi ya kijivu akipokea maandamno katika Viwanja vya Karimjee 

Burudani ya ngoma katika Viwanja vya Karimjee kusherehekea Siku ya Afrika


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt Mahadhi Juma Maalim akiwahutubia watu waliohudhuria sherehe za Siku ya Afrika. Naibu Waziri alipongeza kaulimbiu ya maadhimisho hayo ambayo ni Kilimo na Usalama wa Chakula. Alisema usalama wa Chakula ni changamoto ambayo  lazima nchi za Afrika zichukuwe juhudi za pamoja kukabiliana nayo

Wanadiplomasia na wananchi wengine wakimsikiliza Naibu Waziri.

Balozi wa Kenya akichangia mada Kilimo na Usalama wa Chakula.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Dkt. Yamungu Kayandabila naye akitoa neno wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afrika

Balozi Sweden nchini Tanzania alipata fursa pia ya kuchangia mada katika maadhimisho hayo 


Picha ya pamoja ya Mabalozi na Mabalozi wastaafu mara baada ya sherehe za kuadhimisha Siku ya Afrika kukamilika

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim akihojiwa na wana habari


Picha ya pamoja kati ya Dkt. Maalim na Wanadipolomasia.



Picha na Reginald Philip


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.