Tuesday, March 30, 2021

Balozi Brigedia Jenerali Ibuge: Tuendelee Kudumisha Mahusiano ya Kidiplomasia na Biashara.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge amehimiza Ofisi za Balozi zinazoiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nje ya Nchi kuendelea kukuza na kudumisha ushirikiano wa Kidiplomasia na biashara katika maeneo yao ya uwakilishi. Balozi Brigedia Jenerali Ibuge amesema hayo leo alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Qatar Mhe. Fatma M. Rajab na Balozi wa Tanzania nchini Oman Mhe. Abdallah Abas Kilima. 

“Mnadhamana na jukumu kubwa la kuendelelea kudumisha na kukuza mahusiano ya kidiplomasia na biashara katika maeneo yenu ya uwakilishi ili kuendelea kuvutia kwa uwingi wawekezaji na watalii nchini. Jukumu letu la kutumikia wananchi wa Tanzania tulifanye kwa moyo, kujituma, maarifa na uzalendo”. Amesema Balozi Brigedia Jenerali Ibuge.

Balozi Brigedia Jenerali Ibuge vilevile ameeleza dhamira ya Wizara ya kuendeleza viwanja vya Serikali vilivyopo maeneo mbalimbali nje ya nchi ili viweze kuiingizia Serikali mapato na kuipunguzia matumizi yanayotokana na gharama za pango la ofisi na makazi kwa watumishi wanaofanya kazi katika maeneo hayo.

Mheshimiwa Balozi Abdallah Kilima na Fatma Rajab kwa nyakati tofauti wameishukuru Wizara na Serikali kwa ujumla kwa ushirikiano mzuri wanaoendelea kuupata na kuahidi kuwa wataendelea kufanyakazi kwa bidii na weledi katika kulinda na kutetea maslahi ya nchi na kuleta manufaa kwa nchi.  


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge na Mhe. Abdallah Abas Kilima Balozi wa Tanzania nchini Oman wakiwa kwenye mazumgumzo yaliyofanyika katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge na Mhe. Fatma M. Rajab Balozi wa Tanzania nchini Qatar wakiwa kwenye mazumgumzo yaliyofanyika katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge na Mhe. Fatma M. Rajab Balozi wa Tanzania nchini Qatar wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mazungumzo yaliyofanyika jijini Dodoma

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge na Mhe. Abdallah Abas Kilima Balozi wa Tanzania nchini Oman wakiwa katika picha pamoja baada ya mazungumzo yaliyofanyika jijini Dodoma






Monday, March 29, 2021

MABALOZI WANAOIWAKILISHA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NJE YA NCHI WAHIMIZWA KUONGEZA JUHUDI ZA KUTAFUTA MASOKO

Mabalozi wanaoiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nje ya Nchi wameelekezwa kujipanga, kushiriki na kutafuta fursa zitakazowezesha bidhaa mbalimbali za Tanzania kupata masoko ya uhakika katika nchi walizopo.

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi wakati akizungumza na mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi na kuongeza kuwa , Ilani ya Chama cha Mapinduzi inatamka bayana juu ya diplomasia ya uchumi sambamba na kuimarisha sauti ya Tanzania na taswira yake katika medani ya uhusiano wa kikanda na kimataifa. 

Prof. Kabudi ameongeza kuwa ili kufanikisha hilo Balozi zinapaswa kuimarisha ushiriki wa Tanzania katika jumuiya nyingine za kimataifa zikiwemo, Indian Ocean Rim Association, Indian Ocean Tuna Commission, South South Commission, South West Indian Ocean Fisheries Commission.

Aidha amewataka Mabalozi hao kuzingatia maelekezo ya Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi aliyoyatoa wakati akizundua Baraza la Wawakilishi ya kutaka Uchumi wa Bluu kupitia uvuvi wa Bahari Kuu unakuwa na manufaa kwa Wananchi hususani katika kuongeza mapato, ajira na kukuza uchumi kwa kuzingatia kuwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ni ya Muungano. 

Pia Prof. Kabudi amesema Serikali inatambua na kuthamini mchango unaotolewa na Watanzania waishio nje ya nchi (Diaspora) katika maendeleo ya Taifa na kuzielekeza Balozi zianze na ziboreshe kanzi data ya Diapora ikiwa ni pamoja na kuwahimiza kuanzisha Jumuiya zao. 

“Natambua kazi hiyo inaendelea na kwa sasa tuna data za diaspora takriban 98,658 na kuna jumuiya 77 za diaspora. Nichukue fursa kusisitiza umuhimu wa Balozi zetu kuboresha na kuharakisha zoezi hili kwa kubuni njia mbalimbali za kuwaandikisha”. Amesema Prof. Kabudi

Mkutano huo wa Prof. Palamagamba John Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi umehudhuriwa pia na Naibu Waziri, Mhe William Tate Ole Nasha, Katibu Mkuu Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, Wakurugenzi na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palagamba John Kabudi (Mb) akisisitiza jambo kwenye Kikao kazi na Mabalozi wanaoiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sehemu mbalimbali Duniani pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo kilichofanyika jijini Dodoma

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.  William Tate Olenasha (Mb) akizungumza na Mabalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanaoiwakilisha nchi sehemu mbalimbali Duniani pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo kwenye kikoa kazi kilichofanyika jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge akisisitiza jambo katika Kikao kazi katika ya Mhe. Prof Kabudi na Mabalozi wanaoiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sehemu mbalimbali Duniani pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo kilichofanyika jijini Dodoma.

Sehemu ya Mabalozi na Wakuu wa Idara na Vitengo wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palagamba John Kabudi (Mb) kwenye Kikao Kazi kilichofanyika jijini Dodoma. 

Sehemu nyingine ya Mabalozi na Wakuu wa Idara na Vitengo wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palagamba John Kabudi (Mb) kwenye Kikao Kazi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wanaoiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sehemu mbalimbali Duniani mara baada ya Kikao kazi kilichofanyika jijini Dodoma.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo baada ya Kikao Kazi kilichofanyika jijini Dodoma
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wanaoiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sehemu mbalimbali Duniani mara baada ya kuhitimisha Kikao kazi kilichofanyika jijini Dodoma.

TANGAZO LA FURSA ZA UFADHILI WA MASOMO




 

VACANCY ANNOUNCEMENT


 

Friday, March 26, 2021

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AONGOZA VIONGOZI, WANANCHI KUMUAGA HAYATI JPM

 Habari picha za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza viongozi mbalimbali wa Serikali, taasisi binafsi, mashirika ya kimataifa, dini na wananchi kutoka Chato na mikoa jirani katika mazishi ya aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kijijini kwake Chato mkoani Geita.































Thursday, March 25, 2021

MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR AONGOZA WAKAZI WA GEITA NA MIKOA JIRANI KUMUAGA JPM

 Na Mwandishi Wetu, Geita

Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdullah amewaongoza wakazi wa Geita na mikoa jirani kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati John Pombe Magufuli katika uwanja wa Magufuli Chato mkoani Geita.

 

Akizungumza katika shughuli hiyo ya kuuaga mwili wa hayati Magufuli Wilayani Chato, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa kamati ya mazishi kitaifa amewasihi Watanzania kuendelea kushikamana katika kulijenga taifa, ambalo Magufuli ameliacha salama na lenye heshima.

Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, amesema ni wajibu wa viongozi na Watanzania kuungana kuenzi mazuri yote aliyofanya Hayati Magufuli na kuendeleza sera zake za kuchapa kazi, kupiga vita rushwa na ubadhirifu na kuweka mbele uzalendo na maslahi ya taifa.

Mazishi ya Hayati Dkt. Magufuli yatafanyika Ijumaa Machi 26, 2021 katika makaburi ya familia kijijini kwake Chato mkoani Geita.

Mawaziri mbalimbali pamoja na viongozi waandamizi wa Serikali wakiwa katika uwanja wa Magufuli tayari kwa zoezi la kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa Magufuli Chato mkoani Geita


Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi-Zanzibar, Mhandisi Zena Ahmed Said akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge katika uwanja wa Magufuli wakati wa zoezi la kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli Chato mkoani Geita


Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Bashiru Ally akiteta jambo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) katika uwanja wa Magufuli wakati wa zoezi la kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli Chato mkoani Geita


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli Chato mkoani Geita


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akisaini kitabu cha maombolezo katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chato kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli Chato mkoani Geita


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli Chato mkoani Geita


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akisaini kitabu cha maombolezo katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chato kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli Chato mkoani Geita


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akisaini kitabu cha maombolezo katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chato kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli Chato mkoani Geita