Tuesday, March 31, 2015

Ujumbe kutoka Chuo cha Kijeshi cha Nigeria watembelea Wizara ya Mambo ya Nje


Mwakilishi wa Katibu Mkuu na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,  Bw.Elibariki Maleko(katikati) akizungumza kuukaribisha Ujumbe kutoka  Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha nchini Nigeria (hawapo pichani) ulipokutana na Watendaji wa Wizara kwa ajili ya kujifunza masuala mbalimbali yanayohusu Sera ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa. Ujumbe huo unaongozwa na  Brigedia Generali Jimoh (wa pili kushoto) na upo nchini kwa ziara ya mafunzo. Wengine katika picha ni  Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, Bw.James Lugaganya ( kushoto), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Bw. Innocent Shiyo (wa pili kulia) na  Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Bi.Maulidah Hassan.

Mwenyeji wa Ujumbe huo  kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Brigedia Jenerali Mwemnjudi (mwenye nguo nyeupe) pamoja na Mwambata wa Jeshi katika Ubalozi wa Nigeria hapa nchini Brigedia Jenerali Erick Angaye wakimsikiliza Bw. Maleko (hayupo pichani)
Sehemu ya Maafisa wa Jeshi kutoka Nigeria wakifuatilia kwa makini maelezo kutoka kwa Bw. Maleko
Maofisa na Wanachuo wa Chuo cha Kijeshi cha Nigeria wakati wa mkutano huo
Mmoja wa wanachuo akiuliza swaliwakati wa mkutano huo
Kiongozi wa msafara wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha nchini Nigeria, Brigedia Jenerali Jimoh akimkabidhi zawadi ya nembo ya chuo hicho Bw. Maleko 
Picha ya pamoja.

Picha na Reuben Mchome

Monday, March 30, 2015

Picha na Matukio ya Ufunguzi wa Jengo la Tanzania Jijini New York


Jengo la ghorofa sita la Ofisi za Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. Jengo hilo lipo karibu na Ofisi za Umoja wa Mataifa anuani namba 307 East 53rd Street, 4th Floor, New York, N.Y. 10022. 

Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi akifurahia jambo baada ya kuwatambulisha Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Mhe. Mahadhi Juma Maalim na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue kwa mabalozi wa nchi za Kiafrika waliohudhuria uzinduzi wa jengo hilo.

Balozi Ombeni Sefue akisalimiana na baadhi ya Watanzania waishio Jijini New York wakati wa uzinduzi wa jengo. Balozi Sefue aliwahi pia kuwa Balozi wa Tanzania hapa New York kwenye Umoja wa Mataifa na pia Washington DC. 
Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakiangalia picha ya utalii wa Tanzania iliyopo kwenye eneo la mapokezi la jengo jipya la Tanzania jijini New York Marekani wakati wa ufunguzi.

Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Bw. Alfred Swere, Mhasibu wa Ubalozi wa Tanzania Washington D.C. ambaye pia alikuwa mhasibu wa Ubalozi wa NY wakati jengo hilo likinunuliwa. Wengine pichani ni baadhi ya watumishi wa Serikali Bw. Noel Kaganda, Bw. Lucas Suka, Mkurugenzi wa Ugavi na Manunuzi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Watanzania waliofika kwenye uzinduzi huo.


Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Bi. Roselinda Mkapa mfanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa. Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Celestine Mushy na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mindi Kasiga. 

Mhe. Rais Jakaya Kikwete kwenye picha na wana diaspora waishio New York. (kutoka kushoto) Bw. Meck Khalfan aliyebuni power bank PUKU, mwanamitindo Flaviana Matata na Rosemary Kokuhilwa pia mwanamitindo wa Kitanzania anayefanya shuguli za ujasiriamali jijini New York, Marekani. 
Baadhi ya Maafisa wa Ubalozi ambao walishiriki kwenye uzinduzi huo. (kushoto-Kulia) Noel Kaganda, Justin Kisoka na Alfred Swere. 

Baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (kutoka kushoto) Noel Kaganda (kwa sasa ni Mshauri wa Mhe. Sam Kutesa, Rais wa Kikao cha 69 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ), Baraka Luvanda (kwa sasa ni msaidizi wa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Ikulu Dar es salaam), Mindi Kasiga (kwa sasa Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa) na Togolani Mavura (kwa sasa ni Msaidizi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ikulu).

Maafisa Mambo ya Nje na Wasaidizi wa Viongozi wa Serikali,  Bw. Togolani Mavura ; Msaidizi wa Rais Hotuba na Bw. Adam Issara; Msaidizi wa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, wakipitia hotuba za viongozi wakati wa uzinduzi wa jengo la Tanzania jijini New York, Marekani.   

Sunday, March 29, 2015

Rais Jakaya Kikwete azindua jengo jipya lenye Ofisi za Uwakilishi wa Tanzania Umoja wa Mataifa

Rais Kikwete akikata utepe pamoja na Mhe. Mahadhi Juma Maalim, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa  na viongozi wengine, kufungua rasmi jengo la ghorofa sita la Ofisi za Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani leo Machi 29, 2015

Juu na chini ni Jengo la ghorofa sita la Ofisi za Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani.  

Rais Kikwete akisaini kitabu cha wageni baada ya kufungua rasmi jengo hilo. Anayeshuhudia ni Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania Katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi 
Rais Kikwete akiandaliwa kwa picha ya pamoja na viongozi wa Wizara, Mhe. Mahadhi (aliyekaa kulia), Naibu Waziri - Nje, Balozi Tuvako Manogi, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa na Balozi Ramadhani Mwinyi (kwanza kushoto), Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa.

Baadhi ya wafanyakazi wa Ubalozi (Home based staff) kwenye picha ya pamoja na Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete baada ya ufunguzi wa Jengo la Tanzania.

Baadhi ya Wafanyakazi (local based staff) kwenye picha ya pamoja na Mhe. Rais Kikwete. Pia kwenye mstari wa kwanza ni Col. Mutta (wa kwanza kulia) Mwambata Jeshi wa Tanzania nchini Marekani na Canada, ambaye alihudhuria sherehe hizo NY ambapo Mwambata Jeshi wa Umoja wa Mataifa yuko masomoni. 

Viongozi mbalimbali waliohudhuria sherehe hizo za ufunguzi.

Mh. Membe atoa somo kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Tusiime

Wazir wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Tusiime kuhusu masuala mbalimbali ya kitaifa na kimataifa ambapo wanafunzi hao walipata nafasi ya kumuuliza maswali na kuyajibu kabla hajafungua maabara ya sayansi na maktaba na mahafali ya tano ya kidato cha sita ya shule hiyo. Wengine wanaoonekana ni wageni alioambatana nao na walimu wa Tusiime.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Akisikiliza maelezo kutoka kwa mwanafunzi wa kidato cha pili sekondari ya Tusiime, Khadija Suleiman kuhusu namna ya kuchuja maji wakati Waziri alipofungua rasmi maabara ya kisasa ya sayansi na maktaba na mahafali ya tano ya kidato cha sita ya shule hiyo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, akipata maelezo kutoka kwa Angela Shanira wa kitado cha tano sekondari ya Tusiime Tabata kuhusu masuala mbalimbali ya kisayansi kwenye maabara ya shule hiyo wakati Waziri alipofungua rasmi maabara ya kisasa ya sayansi na maktaba na mahafali ya tano ya kidato cha sita ya shule hiyo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, akikata utepe kuzindia maabara ya kisasa ya sayansi na maktaba ya shule ya sekondari Tusiime kabla yajatoa vyeti kwa wahitimu wa kitado cha tano wa shule hiyo. Wengine ni kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi, Dk. John Mbogoma kulia kwa Waziri ni Mkurugenzi wa shule hizo, Albert Katagira, Meneja wa shule Jane Katagira, na Mkuu wa shule ya sekondari Tusiime, Emil Rugambwa.

Friday, March 27, 2015

Tanzania yaikabidhi Malawi msaada kwa ajili ya Wahanga wa mafuriko

Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. Patrick Luciano Tsere (kulia) akikabidhi  Dawa za Binadamu na Mahindi  kwa Bw. Paul Chiunguzeni, Katibu Mkuu na pia Kamishna  anayeshughulikia masuala ya Maafa aktika Ofisi ya Makamu wa Rais wa Malawi  ikiwa  ni sehemu ya msaada wa Tani 1,200 za Mahindi na Dawa za Binadamu zilizotolewa na Serikali ya Tanzania kwa nchi hiyo kufuatia mafuriko makubwa yaliyoikumba nchi hiyo mwezi Januari 2015. 
Bw. Paul Chiunguzeni, Katibu Mkuu na pia Kamishna anayeshughulikia masuala ya Maafa katika Ofisi ya Makamu wa Rais wa Malawi akitoa hotuba ya shukrani kwa Serikali ya Tanzania kwa msaada huo wa Mahindi na Dawa za Binadamu.
Mhe. Balozi Tsere akiwa katika picha ya pamoja na Bw. Chiunguzeni. Wengine katika picha ni Mwambata wa Jeshi katika Ubalozi wa Malawi nchini Tanzania, Ufulu Kalino (kushoto) akifuatiwa na Kanali Rugeumbiza kutoka JWTZ ambaye alikuwa msimamizi wa zoezi la usafirishaji wa msaada huo kutoka Tanzania na Luteni Kanali B.B. Kisinda (wa tatu kulia) kutoka JWTZ ambaye alikuwa Kiongozi wa Msafara pamoja na Makamanda wa JWTZ.
Balozi Tsere akizungumza machache kabla ya kukabidhi msaada huo
Balozi Tsere akiteta jambo na Bw. Chiunguzeni.
Balozi Tsere akitoa ufafanuzi kwa Waandishi wa Habari kuhusu msaada uliotolewa na Serikali ya Tanzania.
=============================================

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TANZANIA YAIKABIDHI MALAWI MSAADA KWA AJILI YA WAHANGA WA MAFURIKO

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekabidhi Tani 1,200 za Mahindi na Dawa za Binadamu kwa Serikali ya Malawi ikiwa ni msaada wake kwa wahanga wa mafuriko yaliyotokea nchini humo mwezi Januari mwaka huu na kusababisha maafa makubwa.

Msaada huo umekabidhiwa hivi karibuni na Mhe. Patrick Luciano Tsere, Balozi wa Tanzania nchini Malawi kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na kupokelewa na Katibu Mkuu na Kamishna wa Idara ya Maafa, Bw. Paul Chiunguzeni kwa niaba ya Serikali ya Malawi. Aidha, msafara uliopeleka msaada huo kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), uliongozwa na  Luteni Kanali B.B. Kisinda.

Katika hotuba yake fupi wakati wa makabidhiano, Balozi Tsere alisema kwamba msaada huo umetolewa na Tanzania ikiwa ni agizo kutoka kwa  Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na kuguswa kwake na maafa hayo makubwa na pia kuitikia wito uliotolewa na Rais wa nchi hiyo Mhe. Prof. Arthur Bingu Mutharika kwa Jumuiya ya Kimataifa na watu mbalimbali wenye uwezo kutoa msaada kwa wahanga hao wa mafuriko.

Aidha,  Balozi  Tsere alieleza kwamba, Malawi na Tanzania ni nchi jirani, marafiki na zinazoshirikiana katika masuala mbalimbali ikiwemo majukwaa ya kimataifa kama vile Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Umoja wa Afrika (AU) na Umoja wa Mataifa.

“Hivyo, kwa kutambua mahusiano hayo ya ujirani mwema na udugu baina ya nchi hizi na watu wake, Tanzania imeona ni jambo jema kushirikiana na jirani yake katika kupunguza athari za maafa hayo kwa wahanga hao kwani siyo vyema kuona jirani yako amepatwa na matatizo na kisha unakaa kimya” alisema Balozi Tsere.

Mhe. Tsere aliongeza kwamba ingawa msaada huo hautoshelezi kutatua tatizo hilo kabisa bado utaweza kusaidia wahanga hao na kupunguza tatizo lililopo kwa kiasi Fulani

Malawi ilikumbwa na mafuriko mwezi Januari mwaka huu. Mafuriko hayo yalisababisha maafa makubwa ikiwemo watu kupoteza maisha, nyumba kuharibiwa na mazao mashambani kusombwa na maji. Kwa hivi sasa familia katika maeneo yaliyokumbwa na mafuriko hayo hazina mahali pa kuishi na zinahitaji msaada wa chakula na kumekuwa na magonjwa ya mlipuko katika maeneo hayo kama vile kipindupindu.


IMETOLEWA NA: WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, DAR ES SALAAM.

27 MACHI, 2015

PRESS RELEASE

Presidente of German Joachim GauckPRESS RELEASE

President of the United Republic of Tanzania, His Excellency Jakaya Mrisho Kikwete has sent a condolence message to H.E. Joachim Gauck, President of the Federal Republic of Germany following the crash of Germanwings Airbus A320, on 24th March 2015.

The message reads as follows:-

“H.E. Joachim Gauck,
President of the Federal Republic of Germany,
Berlin,
GERMANY.

Your Excellency,

It is with great sadness that I have learned about the crash of the Germanwings Airbus A320 which occurred on 24th March, 2015 with 150 passengers on board, among them, 67 German Nationals.

On behalf of the Government and the People of the United Republic of Tanzania, I wish to convey to you and through you to the people of the Federal Republic of Germany, particularly the bereaved families our heartfelt condolences.

At this time of grief and profound sadness, our hearts and prayers are with the families of the deceased and the People of the Federal Republic of Germany.

Please accept your Excellency, the assurances of my highest consideration.

Issued by the Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation of the United Republic of Tanzania. 
25th March 2015

PRESS RELEASE

King of Spain, H.M Felipe VI

PRESS RELEASE

President of the United Republic of Tanzania, His Excellency Jakaya Mrisho Kikwete has sent a condolence message to the King of Spain, H.M. Felipe VI following the tragic plane crash that involved Germanwings Airbus A320 in southern French Alps on 24th March 2015.

 The message reads as follows:

‘‘His Majesty,
Felipe VI,
King of Spain,
Madrid
SPAIN.

Your Majesty,

I have received with profound sorrow and shock the sad news about the tragic plane crash that involved Germanwings Airbus A320 in southern French Alps on 24th March 2015 and caused the loss of lives of 150 people, including 45 Spanish nationals.

On behalf of the Government and People of the United Republic of Tanzania, and indeed on my behalf, I wish at this difficult time, to express our deepest sympathies and condolences to you and through you to the bereaved families and relatives.

We pray that the Almighty God gives the families and relatives of the deceased, the strength to endure this moment of agony.

Please accept, Your Majesty, the assurance of my highest consideration”.

Issued by the Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation of the United Republic of Tanzania.

25th March, 2015

Thursday, March 26, 2015

Rais Kagame awasili Dar es Salaam kushiriki Mkutano wa Uwekezaaji wa Ukanda wa Kati

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe.Bernard K. Membe (Mb) akisalimiana na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame  alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam. Mhe. Rais Kagame yupo nchini kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Ukanda wa Kati kuhusu Uwekezaji na Viwanda unaofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Rais Kagame akipokea shada la maua kutoka kwa mtoto Elizabeth Jackson kama ishara ya kumkaribisha nchini Tanzania.
Rais Kagame akikagua gwaride la heshima 
Rais Kagame na Waziri Membe wakiangalia burudani ya ngoma za asili uwanjani hapo.
Waziri Membe akiwa ameongozana na Rais Kagame mara baada ya kukagua gwaride na kushuhudia ngoma za asili.Picha na Reginald Philip.

Wednesday, March 25, 2015

Rais Kikwete afungua Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Ukanda wa Kati


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akifungua Mkutano wa Wakuu wa Nchi zinazounda Ukanda wa Kati yaani Tanzania, Uganda, Burundi, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). Ufunguzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam ulihudhuriwa na Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Burundi, Mhe. Pierre Nkurunziza na Mawaziri waliowawakilisha Marais wa DRC na Rwanda. Pamoja na mambo mengine mkutano huo ulijadili umuhimu wakuendelea kuimarisha miundombinu ya nchi za Kanda ya Kati hususan barabara, reli na bandari ili kukuza uwekezaji na maendeleo kwa ujumla.
Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Museveni nae akizungumza wakati wa mkutano huo.
Rais wa Burundi, Mhe. Pierre Nkurunziza nae akizungumza.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (kushoto) akiwa na Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Samwel Sitta na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe wakifuatiliaufunguzi wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Ukanda wa Kati.
Sehemu ya wageni waalikwa wakati wa ufunguzi wa mkutano huo
Marais na Mawaziri waliowawakilisha viongozi wao wakiwa katika picha ya pamoja.