Thursday, January 28, 2016

Naibu Katibu Mkuu akutana kwa mazungumzo na Balozi wa Comoro nchini

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Balozi Ramadhani Mwinyi Muombwa akutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Comoro nchini, Mhe. Ahmed El Badaoui Mohamed Fakih. Mazungumzo hayo yalijikita katika kuboresha mahusiano kati ya Tanzania na Comoro.  
Maafisa wa Ubalozi wa Commoro nao wakifuatilia kwa makini mazungumzo kati ya Balozi Fakih na Balozi Muombwa (hawapo pichani), wa kwanza kutoka kulia ni Naibu Balozi Bw. Bacar Salim na kulia ni Afisa Mwandamizi wa Ubalozi huo Bw. Failladhu Mbae Charif.
Balozi Fakih naye akimwelezea jambo Balozi Muombwa (Kulia) wakati wa mazungumzo yao.

Picha na Reginald Philip



Wednesday, January 27, 2016

India marks 67th years of Independence

Permanent Secretary for the Ministry of Foreign Affairs, East Africa, Regional and International Cooperation, Dr. Aziz Ponary Mlima addresses distinguished invited guests including members of the Diplomatic Community, Government Officials and representatives from private sector during the celebration to mark 67 years of India Independence. In his speech, Dr. Mlima insisted the importance of Tanzania and India to deepen and strengthen diplomatic and economic cooperation with a focus on increasing investment and trade volumes.The celebrations was hosted by the Indian High Commission in Dar es Salaam.  
Indian High Commissioner, H.E Sandeep Arya delivers his speech in the celebration of the 67th Anniversary of the Independence of India. The event took place at Hyatt Regency, Kilimanjaro Hotel in Dar Es Salaam yesterday.
Deputy Permanent Secretary for the Ministry of Foreign Affairs, East Africa, Regional and International Cooperation, Amb. Ramadhani Mwinyi Muombwa (second left) was among the senior government officials who attended the ceremonies.
Permanent Secretary (R) and Indian High Commissioner toasting for the progress and prosperity of their Nations.
Former President of the United Republic of Tanzania, Alhaji Ali Hassan Mwinyi (with a red tie) was also present at the ceremonies. On his left is the former Prime Minister of the United Republic of Tanzania, Hon. Dr. Salim Ahmed Salim.
Indian High Commissioner (L) receives invited guests at the ceremonies hall.


Permanent Secretary, Dr. Mlima (R) chats with ambassadors prior to the official opening of an event.

Tuesday, January 26, 2016

Dkt. Mlima akutana na Katibu Mkuu wa EAC

Katibu Mkuu wa Sekretariati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Richard Sezibera (kushoto) akutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dkt. Aziz P. Mlima. Dkt. Sezibera alikutana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje kwa madhumuni ya kusalimia pamoja na kutoa taarifa fupi ya masuala mbalimbali yanayoendelea katika Jumuiya.
Kutoka kushoto ni Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje ambao ni Mkurugenzi wa Siasa, Ulinzi na Usalama, Bw. Stephen Mbundi; Mhandisi John Kiswaga; Bw. Amos Tengu na Bw. Antony Ishengoma wakifuatilia mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea.

Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje akutana na Kaimu Mkurugenzi wa TAKUKURU

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Aziz Mlima (kulia), amekutana na kufanya mazungumzo na Kaimu Mkurugenzi wa TAKUKURU, Bw. Valentino Mlowola. Mazungumzo hayo yalifanyika Wizarani tarehe 26 Januari, 2016.
Mazungumzo yakiendelea huku Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi  Baraka Luvanda na Afisa Mambo ya Nje, Bw. Elisha Suku (wa kwanza kulia) wakifuatilia.

Picha na Reginald Philip 

Nafasi za Kazi UNEP.

For information on how to apply for a job, go to Application Process.
Applications from women candidates are strongly encouraged.
The United Nations does not charge a fee at any stage of the recruitment process (application, interview meeting, processing, training or any other fees). The United Nations does not concern itself with information on bank accounts.

Job TitleLevelJob IDJob NetworkJob FamilyDepartment/OfficeDuty stationDeadline
ADMINISTRATIVE OFFICER P-352332Management and AdministrationAdministrationUnited Nations Environment Programme                                                                COPENHAGEN24/03/2016
SENIOR PROGRAMME MANAGEMENT OFFICER P-550054Economic, Social and DevelopmentProgramme ManagementUnited Nations Environment Programme                                                                GENEVA20/03/2016
SENIOR PROGRAMME MANAGEMENT OFFICER P-552647Economic, Social and DevelopmentProgramme ManagementUnited Nations Environment Programme                                                                NAIROBI12/03/2016
Associate Programme Management Officer (Marine: Project Post), P-252040Economic, Social and DevelopmentProgramme ManagementUnited Nations Environment Programme                                                                ABU DHABI19/02/2016
Programme Management Officer P-348410Economic, Social and DevelopmentProgramme ManagementUnited Nations Environment Programme                                                                NAIROBI14/02/2016
SENIOR PROGRAMME MANAGEMENT OFFICER P-549433Economic, Social and DevelopmentProgramme ManagementUnited Nations Environment Programme                                                                NAIROBI11/02/2016
SENIOR COORDINATION OFFICER (Project Post) P-550630Economic, Social and DevelopmentProgramme ManagementUnited Nations Environment Programme                                                                TOYAMA10/02/2016
DEPUTY COORDINATOR, Mediterranean Action Plan P-550553Economic, Social and DevelopmentProgramme ManagementUnited Nations Environment Programme                                                                ATHENS07/02/2016
SENIOR ADMINISTRATIVE OFFICER P-550105Management and AdministrationAdministrationUnited Nations Environment Programme                                                                NAIROBI07/02/2016
SPECIAL ASSISTANT, ADMINISTRATION [Cancelled] P-349435Management and AdministrationAdministrationUnited Nations Environment Programme                                                                NAIROBI05/02/2016

Dr. Mlima Meets Assistant Secretary General of the United Nations


Permanent Secretary for the Ministry of Foreign Affairs, East Africa, Regional and International Cooperation, Dr. Aziz Ponary Mlima (right) is in the official discussions with the Assistant Secretary General – Political Affairs of the United Nations, Mr. Taye Brook Zerihoun who paid a courtesy visit at the Ministry recently. The two discussed the importance of enhancing cooperation between the United Nations and the Southern Africa Development Community (SADC)  especially in the area of conflict prevention and resolution.
Officials from the Ministry of Foreign Affairs listening  attentively to the ongoing discussion between Dr. Mlima and Mr.Zerihoun (not in the photo). First from left is the Director of Regional  Cooperation Department, Amb. Innocent Shiyo followed by Head of Government Coomunication Unit, Ms. Mindi Kasiga; Director of Political, Defence and Security Department, Mr. Stephen Mbundi and Acting Director of Africa Department, Mr. Merdad Ngaiza.

UN Resident Coordinator and UNDP Representative in Tanzania, Mr. Alvaro Rodriguez (R) with his colleague in the office also attended the discussions.


Photos by Reginald Philip

Friday, January 22, 2016

Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje akutana kwa mazungumzo na Balozi wa New Zealand nchini

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Aziz Mlima amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa New Zealand nchini mwenye makazi yake nchini Afrika Kusini Mhe. Richard Mann, katika mazungumzo yao Balozi Mann alitumia fursa hiyo kumpongeza Balozi Mlima kwa uteuzi na aliishukuru Wizara kwa ushirikiano anaoupata katika utendaji utekelezaji wake wa majukumu. Kwa upande wa Balozi Mlima alimweleza kuwa wataendelea kushirikiana vyema na nchi ya New Zealand katika sekta mbalimbali katika kukuza uchumi.   
Mkutano ukiendelea kati ya Balozi Mlima (katikati) na Balozi Mann huku Bw. Khatibu Makenga (kulia), Afisa Mambo ya Nje akifuatilia


Picha na Reginald Philip

Balozi Haule akutana na Balozi wa Hungary.


Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. John Michael Haule  akikabidhi zawadi kutoka Tanzania kwa  Balozi wa Hungary nchini mwenye makazi yake Nairobi, Mhe. Laszlo Mathe mara baada ya kukutana kwa mazungumzo Jijini Nairobi. Serikali ya Hungary imetoa nafasi 30 za masomo kwa Tanzania kwa miaka mitatu kuanzia mwaka huu. Wawakilishi hao wa Nchi pia walizungumzia ushirikiano wa kiuchumi, ambapo Hungary imeahidi kushawishi wawekezaji kuanzisha miradi ya ubia ya viwanda itakayolenga uhamishaji wa teknolojia kwa Tanzania

Waziri Mahiga azindua Kitabu cha Dkt. Salim Ahmed Salim.

 Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb), mwenye tai ambaye ndiye alikuwa Mgeni Rasmi katika hafla ya uzinduzi wa kitabu cha Dkt. Salim Ahmed Salim (Salim Ahmed Salim: Son of Afica), kitabu kinachozungumzia historia iliyotukuka ya Dkt. Salim ndani ya Tanzania, Afrika na Duniani kwa ujumla, wakiwa wameshikilia kitabu hicho baada ya kuzinduliwa rasmi tarehe 21-01-2016, katika hafla iliyofanyika katika hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam. 


 Waziri Mahiga akimpongeza Dkt. Salim, muda mfupi baada ya kuzindua kitabu chake.
 Waziri Mahiga akikata utepe, kama ishara ya kuzindua kitabu hicho.
Hivi ndivyo uso wa kitabu hicho unavyoonekana.

 Dkt. Salim Ahmed Salim (kulia), na Mwakilishi wa Kituo cha Kutatua Migogoro Barani Afrika, (Centre for Humanitarian Dialogue-CHD), Bw. Mohamed Omary wakionyesha Fremu yenye Mashairi ya kumsifu Dkt. Salim, huku Waziri Mahiga akishuhudia tukio hilo.

Mhariri wa kitabu hicho, Dkt. Jackkie Cilliers akizungumza katika hafla hiyo.
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb), ambaye ndiye alikuwa Mgeni Rasmi katika hafla ya uzinduzi wa kitabu cha Dkt. Salim Ahmed Salim (Salim Ahmed Salim: Son of Afica),akimzungumzia historia iliyotukuka ya Dkt. Salim Ahmed Salim, kabla ya uzinduzi wa kitabu hicho.
 Balozi wa Afrika Kusini hapa nchini, Mhe. Thami Mseleku (kushoto) akiwa pamoja na Balozi wa Rwanda hapa nchini, Mhe. Eugene Segore Kayihura nao wakifuatilia uzinduzi wa kitabu hicho.
Dkt. Salim Ahmed Salim, akitoa maneno ya Shukrani kwa heshima aliyopewa kwa Mwandishi wa kitabu hicho lakini kwa wadau wote waliohudhuria hafla hiyo ya uzinduzi wa kitabu chake.

 Aliyekua Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula (Katikati), akiwa na wageni mbalimbali wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho.
Mwanasheria nguli, Profesa Issa Shivji, akitoa muhtasari kitabu hicho kwa wadau mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo.
Muongozaji wa shughuli hiyo, Bw. Hamza Kasongo akiendelea na kazi yake.

Waziri Mahiga akifurahia jambo na Dkt. Salim.
 Aliyekua Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe akisalimiana na baadhi ya wageni waliohudhuria hafla hiyo.

Dkt. Salim akizungumza jambo wakati wa hafla hiyo.

Mgeni Rasmi, Waziri  Augustine Mahiga akizungumza  na vyombo vya habari mara baada ya kuzindua kitabu cha Dkt. Salim katika hafla iliyofanyika tarehe 21-01-2016 katika hoteli ya New Africa jijini Dar es Salim.
==============================
PICHA NA REUBEN MCHOME.