Friday, January 22, 2016

Waziri Mahiga azindua Kitabu cha Dkt. Salim Ahmed Salim.

 Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb), mwenye tai ambaye ndiye alikuwa Mgeni Rasmi katika hafla ya uzinduzi wa kitabu cha Dkt. Salim Ahmed Salim (Salim Ahmed Salim: Son of Afica), kitabu kinachozungumzia historia iliyotukuka ya Dkt. Salim ndani ya Tanzania, Afrika na Duniani kwa ujumla, wakiwa wameshikilia kitabu hicho baada ya kuzinduliwa rasmi tarehe 21-01-2016, katika hafla iliyofanyika katika hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam. 


 Waziri Mahiga akimpongeza Dkt. Salim, muda mfupi baada ya kuzindua kitabu chake.
 Waziri Mahiga akikata utepe, kama ishara ya kuzindua kitabu hicho.
Hivi ndivyo uso wa kitabu hicho unavyoonekana.

 Dkt. Salim Ahmed Salim (kulia), na Mwakilishi wa Kituo cha Kutatua Migogoro Barani Afrika, (Centre for Humanitarian Dialogue-CHD), Bw. Mohamed Omary wakionyesha Fremu yenye Mashairi ya kumsifu Dkt. Salim, huku Waziri Mahiga akishuhudia tukio hilo.

Mhariri wa kitabu hicho, Dkt. Jackkie Cilliers akizungumza katika hafla hiyo.
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb), ambaye ndiye alikuwa Mgeni Rasmi katika hafla ya uzinduzi wa kitabu cha Dkt. Salim Ahmed Salim (Salim Ahmed Salim: Son of Afica),akimzungumzia historia iliyotukuka ya Dkt. Salim Ahmed Salim, kabla ya uzinduzi wa kitabu hicho.
 Balozi wa Afrika Kusini hapa nchini, Mhe. Thami Mseleku (kushoto) akiwa pamoja na Balozi wa Rwanda hapa nchini, Mhe. Eugene Segore Kayihura nao wakifuatilia uzinduzi wa kitabu hicho.
Dkt. Salim Ahmed Salim, akitoa maneno ya Shukrani kwa heshima aliyopewa kwa Mwandishi wa kitabu hicho lakini kwa wadau wote waliohudhuria hafla hiyo ya uzinduzi wa kitabu chake.

 Aliyekua Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula (Katikati), akiwa na wageni mbalimbali wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho.
Mwanasheria nguli, Profesa Issa Shivji, akitoa muhtasari kitabu hicho kwa wadau mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo.
Muongozaji wa shughuli hiyo, Bw. Hamza Kasongo akiendelea na kazi yake.

Waziri Mahiga akifurahia jambo na Dkt. Salim.
 Aliyekua Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe akisalimiana na baadhi ya wageni waliohudhuria hafla hiyo.

Dkt. Salim akizungumza jambo wakati wa hafla hiyo.

Mgeni Rasmi, Waziri  Augustine Mahiga akizungumza  na vyombo vya habari mara baada ya kuzindua kitabu cha Dkt. Salim katika hafla iliyofanyika tarehe 21-01-2016 katika hoteli ya New Africa jijini Dar es Salim.
==============================
PICHA NA REUBEN MCHOME.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.