Saturday, December 31, 2011

Taarifa ya Msiba wa Bwana Aziz Sheween

Marehemu Aziz Sheween (kushoto) akiwa kwenye mazungumzo ya kikazi na Mwana wa Mfalme wa Saudi Arabia (HRH Prince Alwaleed Bin Talal bin Abdulaziz Alsaud) wakati wa uhai wake.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. John Haule, anasikitika kutangaza kifo cha Bw. Aziz Sheween, Afisa Mambo ya Nje Mkuu Daraja la I katika Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, kilichotokea huko Riyadh, Saudi Arabia. Taratibu za kusafirisha mwili wa marehemu kuja nyumbani kwa mazishi zinaendelea na pindi zitakapokamilika taarifa rasmi itatolewa. Tunawapa pole familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki, watumishi wa Wizara na wote walioguswa na msiba huu mzito.

Wednesday, December 28, 2011

Katibu Mkuu Apokea Msaada Kutoka kwa Watanzania waishio Zambia


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John M. Haule, akipokea msaada wa fedha kiasi cha Sh. 1,118,600.00/- kutoka kwa Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Bibi Justa Nyange, kwa ajili ya waathirika wa ajali ya Meli ya MV Spice iliyotokea Zanzibar mwezi Septemba, 2011. Msaada huo umetolewa na Watanzania wanaoishi nchini Zambia.

Naibu Waziri Mambo ya Nje Asaini Kitabu cha Maombolezo Leo Ubalozi wa Korea

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Mahadhi  J. Maalim akisalimiana na Kaimu Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea leo jijini Dar es Salaam, alipofika kusaini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo Jenerali Kim Jong-Il.


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Mahadhi J. Maalim akisaini Kitabu cha Maombolezo kwenye Ubalozi Mdogo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea leo jijini Dar es Salaam, kufuatia kifo cha aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo Jenerali Kim Jong-Il.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Mahadhi J. Maalim akimfariji Kaimu Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea Mhe. Kim Yong Su leo jijini Dar es Salaam, alipofika kusaini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo Jenerali Kim Jong-Il.

Friday, December 23, 2011

Waziri Membe azindua album ya Christina Shusho

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe akizungumzia uimbaji wa Christina Shusho na muziki wa injili nchini Tanzania wakati akizindua albamu mpya iitwayo Nipe Macho jijini Dar es salaam leo tarehe 23.12.2011.

Mhe. Bernard Membe akifurahia jambo wkati wa uzinduzi wa album ya Nipe Macho ya muimbaji wa injili Christina Shusho. Katikati ni mshereheshaji wa uzinduzi huo MC Harris.

Muimbaji Christina Shusho akiimba wimbo wake wa  Nipe Macho wakati wa uzinduzi wa album uliofanyika Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.

Waziri Membe akutana na Mabalozi Wateule Leo

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe leo amekutana na Mabalozi Wateule walioapishwa wiki hii kushika vituo mbalimbali vya uwakilishi nje ya nchi kwenye Chuo Cha Diplomasia ambapo wanahudhuria kozi ya utambulisho kabla ya kuanza kazi rasmi. Pamoja nao ni Mabalozi Wastaafu, Wakufunzi na baadhi ya viongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje.

Thursday, December 22, 2011

Naibu Waziri amuaga Balozi wa Zambia Nchini Tanzania


Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Mahadhi Juma Maalim akizungumza na Balozi wa Zambia nchini Tanzania Mhe. Mavis Muyunda alipofika ofisini kwake kumuaga leo tarehe 22.12.2011.

Balozi Mavis Muyanda akimkabidhi zawadi Mhe. Mahadhi Juma Maalim, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ofisini kwake leo kama ishara ya kumuaga. Balozi Muyanda anatarajiwa kuondoka nchini kesho tarehe 23.12.2011 baada ya kumaliza muda wake kazi nchini Tanzania.

Balozi Mavis Muyunda akiagana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Bi. Zuhura Bundala nje ya Jengo la Wizara alipofika kuagana na uongozi baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini Tanzania.

Wednesday, December 21, 2011

Mabalozi wapya wakaribishwa Wizara ya Mambo ya Nje

Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bwana John Haule leo amewakaribisha rasmi Mabalozi Wateule kwenye Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambapo Wakuu wa Idara na Votengo walieleza kwa kifupi kazi za Wizara kwa ujumla. 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bwana John Haule akiongoza kikao cha utambulisho kati ya Mabalozi Wateule na Uongozi wa Wizara Leo tarehe 21.12.2011

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara Bwana D. Mndeme akijitambulisha kwa mabalozi wapya wa Wizara.

Balozi Mteule nchini Misri, Mhe. Mohamed Hamza akijitambulisha kwenye Mkutano huo. Kushoto ni Balozi Batilda Burian anayeenda nchini Kenya.

Balozi Mteule wa Tanzania nchini Oman Mhe. Ali Saleh akijitambulisha kwa uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Balozi Mteule wa Tanzania nchini Msumbiji Mhe. Shamim Nyanduga

Balozi Mteule wa Tanzania nchini Uganda Mhe. Ladislaus Komba akijitambulisha
Katibu Mkuu wa Wizara Bwana John Haule akiongea na Mabalozi Wateule. Wa kwanza kushoto ni Mhe. Batilda Burian, Balozi Mteule wa Tanzania nchini Kenya.

Mhe. Grace Mujuma (wa kwanza Kulia), Balozi Mteule wa Tanzania nchini Zambia  

Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani Bw. Gabriel Mwero akijitambulisha kwa mabalozi wapya.


Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda Bw. Adrian Miyaye akijitambulisha.

Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bw. Katinda E. Kamando akijitambulisha kwa mabalozi wapya wa Wizara.


Kaimu Mkurugenzi Idara ya Asia na Australasia Bi. Naimi Aziz akijitambulisha kwa mabalozi wapya wa Wizara.

Monday, December 19, 2011

Mabalozi Waapishwa Ikulu Leo

Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Kwanza wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali, Waziri na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakiwa katika picha ya pamoja na mabalozi wapya ambao leo wameapa Ikulu jijini Dar es salaamFriday, December 16, 2011

Ikulu yatangaza Mabalozi watakaowakilisha Tanzania kwenye nchi Nane

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

UTEUZI WA MABALOZI

_________________________

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, amewateua wafuatao kuwa Mabalozi:-
Mhe. Phillip MARMO, ameteuliwa kuwa Balozi nchini CHINA. Kabla ya hapo Mhe. Marmo alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge.

Dkt. Deodorus B. KAMALA, ameteuliwa kuwa Balozi nchini BELGIUM. Kabla ya hapo Mhe. Kamala alikuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Dkt. Batilda S. BURIAN, ameteuliwa kuwa Balozi nchini KENYA. Kabla ya hapo Mhe. Dkt. Burian alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira).

Dkt. Ladislaus C. KOMBA, ameteuliwa kuwa Balozi nchini UGANDA. Kabla ya hapo Dkt. Komba alikuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii.

Bibi Shamim NYANDUGA, ameteuliwa kuwa Balozi nchini MSUMBIJI. Kabla ya hapo Bibi Nyanduga alikuwa Naibu Mkuu wa Itifaki, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. 

Bibi Grace J.E. MUJUMA, ameteuliwa kuwa Balozi nchini ZAMBIA. Kabla ya hapo Bibi Mujuma alikuwa Kaimu Mkurugenzi, Ushirikiano wa Kikanda (Regional Co-operation), Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Bwana Mohamed H. HAMZA, ameteuliwa kuwa Balozi nchini MISRI. Kabla ya hapo Bwana Hamza alikuwa Mkurugenzi wa Mambo ya Nje, ZANZIBAR, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Ndugu Ali A. SALEH, ameteuliwa kuwa Balozi nchini OMAN. Kabla ya hapo Bwana Saleh alikuwa Balozi Mdogo (Consul General) nchini Dubai.

Uteuzi huu unaanzia tarehe 12 Oktoba, 2011. Wataapishwa tarehe 19 Desemba, 2011 saa 03.00 Asubuhi.

……………………………… MWISHO …………………………………….

(Phillemon L. Luhanjo)

KATIBU MKUU KIONGOZI IKULU,
DAR ES SALAM.
16 Desemba, 2011

Wednesday, December 14, 2011

Hon. Bernard Membe to attend Africa/Turkey Ministerial Review Conference


Istanbul to host the Africa/Turkey Ministerial Review Conference


Addis Ababa - On 16 December 2011, the Africa/Turkey Ministerial Review Conference will be held in Istanbul,Turkey, in linewith the Follow-up Mechanism of the Istanbul Declaration on “Africa– Turkey Partnership”. The Minister of Foreign Affairs of the Republic of Turkey, Mr. Ahmet Davutoğlu, the Minister of Foreign Affairs,International Cooperation and Francophonie of the Republic of Equatorial Guineaand Chairperson of the Executive Council of the African Union, Mr. Pastor MicheOndo Bile (Equatorial Guinea) and the Chairperson of the African UnionCommission, Dr. Jean Ping will co-chair the Conference.

Theconference that will be attended by representative of African countries and Turkey, the Chairperson of the African Union Commission (AUC), Representativesof the African Union Commission, the New Partnership for Africa’sDevelopment (NEPAD) Planning and Coordination Agency, and Regional EconomicCommunities (RECs) as well as observers from various international and regionalorganizations, will enable the two sides to review and discuss theAfrica-Turkish Partnership and the future perspectives. This will include thereview of the implementation of the Joint Plan of Action – Turkey-Africaapproved in November 2010.

The conference will, as well deliberate on the preparation of the 2ndTurkey-Africa Cooperation Summit. The First Africa – Turkey Cooperation Summit, held in Istanbul in August 2008, confirmed the commitment of Heads ofState and Government from both sides to work towards strengthening the variousdimensions of the strategic partnership.

AHigh Level Preparatory Meeting that will take place on 15 December will precedethe ministerial conference to consider the identified priority projects, thedraft Joint Communiqué and the agenda of the Ministerial Review Conference.

TheDeputy Undersecretary of Turkish Ministry of Foreign Affairs, the Chairpersonof the Permanent Representatives Committee and a Representative of the AfricanUnion Commission will address the preparatory meeting.


AJoint Press Conference chaired by the Minister of Foreign Affairs of Turkey, the Chairperson of AU Executive Council of the African Union and theChairperson of the African Union Commission, will be held at the end of theConference (16 December 2011 at 18:45 – 19:15 hours at theÇırağan Palace Kempinski Hotel on.


Theaccreditation of the international press members will be made through theTurkish General Directorate of Press and Information. The announcementconcerning the accreditation will be made by the aforementioned GeneralDirectorate and through the Press Accreditations Desk, which will be opened atthe Çırağan Palace Hotel on 16 December 2011.

The accredited members of the press will have access to theevent. A Press Center will be available during the meeting at the“Çırağan Palace Hotel” giving communication,documentation and services to the representative of the media. A Yellow Badge will be given to Members of thePress selected by Turkish Directorate of Press and Information.


For further information, pleasecontact: Habiba Mejri-Cheikh, Director of Information and Communication African Union Commission; Email: habibam@african-union.orgor Mejri-cheikh.habiba@hotmail.com

Tuesday, December 13, 2011

Balozi Mpya wa Umoja wa Ulaya awasili nchini

Balozi Mteule Filiberto C. Sebregondi akikabidhi nakala za hati za utambulisho kwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe leo mjini Dar es salaam.  

Thursday, December 8, 2011

Leaders arriving for the 50 years of Independence celebrations: Mozambique

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (kulia)akimtambulisha Rais wa Msumbiji Mhe. Armando Guebuza kwa Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi Mhe. Mathayo David Mathayo mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere kuhudhuria sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Katikati ni Balozi wa Msumbiji nchini Tanzania.


Leaders arriving for the 50 years of Independence celebrations: Malawi

Waziri Membe, akimtambulisha Rais wa Malawi Mhe. Bingu wa Mutharika, kwa viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili mjini Dar es salaam leo. Rais Mutharika amepokelewa pia na Mhe. Profesa Jumanne Maghembe, Waziri wa Kilimo wa Tanzania. Rais Bingu wa Mutharika amefuatana na ujumbe wa watu 15 kuhudhuria sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara hapo kesho tarehe 9.12.2011.Leaders arriving for the 50 years of Independence celebrations: Democratic Peoples Republic of Korea

Rais wa Bunge la Korea Mhe. Kim Jong Nam akiwasili nchini na kupita kwenye gwaride la heshima kwenye Kiwanja cha Ndege cha Mwalimu Julius Nyerere mjini Dar es salaam leo. Mhe. Kim Jong Nam ameambatana na ujumbe wa watu 17 akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea, kuhudhuria sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
 


H.E. Kim Jong Nam, President of The Presidium of the Supreme People's Assembly of DPRK arriving at the airport in Dar es salaam on the 8.12.2011 for the celebration of the 50th anniversary of Tanzania's Independence.   
Hon. Bernard MembeMinister for Foreign Affairs and International Cooperation, H.E. Kim Jong Nam and Hon. Selina Kombani, Minister of Justice and Constitutional Affairs watching entertainment at the aiport immedietely after arriving in Dar es salaam on 8.12.2011.
 Mhe. Bernard Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa na Mhe. Kim Jong Nam, Rais wa Bunge la Korea wakiangalia vikundi vya Burudani mara baada ya kuwasili nchini. Mhe. Nam amepokelewa pia na Mhe. Selina Kombani, Waziri wa Katiba na Sheria (kulia).
 H.E. Kim Jong Nam is in the country for Uhuru celebrations and he is leading the delegation of 17 people from his country including Foreign Minister.