Sunday, December 20, 2020

JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI YAJIVUNIA MRADI WA UJENZI WA BWAWA LA KUZALISHA UMEME LA JULIUS NYERERE.


Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki imeeleza jinsi inavyojivunia na mradi wa ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme la Julius Nyerere ambalo baada ya kukamilika kwake hapo Juni 2022 linatarajiwa kuzalisha Migawati 2115 za umeme. 

Haya yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Mipango, Miundombinu, Fedha na Utawala Mhandisi Steven Mlote alipotembelea mradi huo ambao kwa ndio mradi pekee mkubwa wa umeme kwa sasa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Ameongeza kuwa mradi huu sio tu ni muhimu kwa Tanzania bali utazinufaisha pia nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki na nchi zingine jirani. Mhandisi Mlote pia ameeleza kuridhishwa kwake na ushiriki wa Watanzania katika katika ujenzi wa mradi huo, ambapo kati ya Wafanyakazi zaidi ya 5000, asilimia 90 ni Watanzania. 

Eng. Mlote ameonesha furaha yake baada ya kuelezwa kuwa mradi huo mkubwa Afrika Mashariki kwa sasa unafadhiliwa na Serikali ya Jumhuri ya Muungano wa Tanzania kwa asilimi 100, chini ya Uongozi wa Rais Dkt John Pombe Magufuli. Mhandisi Mlote ametoa wito kwa Watanzania hasa ambao wanazunguka eneo mradi wa kutunza mazingira ili kuufanya mradi huo kuendelea kuwa katika mazingira mazuri na salama wakati wote.

Awali ujumbe huo wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki umetembelea mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kwa lengo la kijionea maendeleo ya ujenzi wa maradi huo na kueleza kufurahishwa na kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, vilevile ametumia fursa hiyo kuwasihi vijana wa Kitanzania waliopata fursa ya ujenzi wa reli kuendelea kujifunza kwa moyo na kwa kujituma ili kupata maarifa na ujuzi wa kuendelea kutunza, kuendesha na kuendeleza miradi hata baada ya wataalmu kutoka makampuni yanayohusika na ujenzi kuondoka nchini. 

Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Mipango, Miundombinu, Fedha na Utawala Mhandisi Steven Mlote (Wapili kusho) akimsikiliza mtaalamu (hayupo pichani) aliyekuwa akielezea masuala mbalimbali kuhusu ujenzi wa mradi wa bwawa la umeme la Julius Nyerere alipotembelea mradi huo.

Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Mipango, Miundombinu, Fedha na Utawala Mhandisi Steven Mlote akifurahia jambo na wadau wengine walioenda kutembelea na kujifunza katika mradi huo.
Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Mipango, Miundombinu, Fedha na Utawala Mhandisi Steven Mlote kiwa katika picha ya pamoja na wadau wa sekta ya elimu walioenda kutembelea mradi huo

Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Mipango, Miundombinu, Fedha na Utawala Mhandisi Steven Mlote akifuatilia wasilisho (presentation) kuhusu mradi wa bwawa la kuzalisha umeme la Julius Nyerere kutoka kwa mtaalamu muda mfupi kabla ya kwenda kutembelea eno la mradi.




Saturday, December 19, 2020

Ujumbe wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki watembelea Mradi wa Ujenzi wa SGR


Ujumbe wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki umetembelea mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kwa lengo la kijionea maendeleo ya ujenzi wa maradi huo unaotekelezwa hapa nchi. Ujumbe huo ukiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya anayeshughulikia masuala ya Mipango, Miundombinu, Fedha na Utawala Eng. Steven Mlote ulianza safari ya kutembelea mradi huo kuanzi Makutopola hadi Dar es Salaam. Ujumbe ulipate fursa ya kujionea hatau ya maendeleo iliyofikiwa sambamba na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na katika utelezaji wa mradi, ikiwemo viwanda vya kuzalishia baadhi vifaa vinavyotumika katika ujenzi wa mradi.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo Eng. Mlote amesema amefurahishwa na kazi kubwa inayofanywa na Serikali katika kutekeleza mradi huo ambao unamanufaa makubwa kwa Taifa na kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki. “tuemona kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuteleza mradi huu mkubwa, tunampongeza Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli kwa kubuni mradi huu.” Eng.Mlote. Aidha, aliongezea kusema amefurahishwa na ushiriki wa idadi kubwa ya vijana wa Kitanzania katika sekta mbalimbali za ujenzi wa mradi huo ulioajiri takribani watu 13,796. Amewasihi vijana wa Kitanzania waliopata fursa ya ujenzi wa reli kuendelea kujifunza kwa moyo na kwa kujituma ili kupata maarifa na ujunzi wa kuendelea kutunza, kuendesha na kuendeleza mradi huo hata baada ya wataalmu kutoka kampuni inayohusika na ujenzi kuondoka nchi. 

Kwa upande mwingine Eng. Mlote ametoa wito kwa Watanzania hasa ambao wanazunguka eneo la mrafi, wikuanza kujiandaa kikamilifu katika kunufaika na fursa zitakazotokana na mradi wa reli ya kisasa kwa kuanza kuongeza uzalisha wa mazao shambani na bidhaa za viwandani kwa kuwa mradi huo utarahisisha usafirishaji wa bidhaa na watu kwenda nchi jirani za Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Nchi za Afrika ya Kati. 

Ujumbe wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki pia unatarajia kutembelea mradi wa ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme la Mwalimu Nyerere, lililopo Wilayani Rufiji kwa lengo la kujionea hatua iliyofikiwa katika ujenzi.

Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Mipango, Miundombinu, Fedha na Utawala Eng. Steven Mlote akifualia mada iliyokuwa ikiwalishwa na mtalaamu wa ujenzi kuhusu hatua mbalimbali zilizofikiwa katika ujenzi wa mradi wa treni ya kisasa (SGR) mara baada ya kuwasili katika eneo la makutupola jijini Dodoma.

 


Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhandisi Steven Mlote akiwa na Mhandisi Ignas Lymo kutoka Shirika la Reli Tanzania wakitokea kwenye moja ya handaki (tunnel) la kupita treni.

Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhandisi Steven Mlote akisikiliza maelezo kutoka kwa mtaalamu alipotembelea moja ya handaki (tunnel) ya kupita treni ambalo lipo katika hatua za mwisho za ujenzi.

Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhandisi Steven Mlote  (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watalumu wa ujenzi na Watumishi wa Shirika la Reli Tanzania nje ya handaki (tunnel) la kupia treni.


Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhandisi Steven Mlote akifualia mada iliyokuwa ikiwalishwa na mtalaamu wa ujenzi kuhusu hatua mbalimbali zilizofikiwa katika ujenzi wa mradi wa treni ya kisasa (SGR) mara baada ya kuwasili katika eneo la kambi ya Soga, mkoani Pwani.

Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhandisi Steven Mlote akitembea pembezoni mwa reli ambayo ipo katika hatua za mwisho za ujenzi.


Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhandisi Steven Mlote akijadili jambo na watalamu wa ujenzi wa reli ya kisasa alipo tembelea ili kujionea maendeleo ya ujenzi wa mradi huo

Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhandisi Steven Mlote akisikiliza malezo kutoka kwa Mhandisi Ignas Lyimo kutoka Shirika la Reli Tanzania alipotembelea Stesheni ya Treni ya Morogoro mjini.


Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhandisi Steven Mlote akiendelea kusikiliza maelezo kutoka kwa Mhandisi Ignas Lyimo kutoka Shirika la Reli Tanzania alipotembelea Stesheni ya Treni ya Morogoro mjini.

 

Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhandisi Steven Mlote akisikiliza maelezo kutoka kwa mataalamu alipotembelea Stesheni ya Treni ya iliyopo eneo la Tazara jijini Dar es Salaam

Friday, December 18, 2020

TANZANIA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA IORA

 

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. William Ole Nasha akishiriki Mkutano wa 20 wa Baraza la Mawaziri wa Nchi zilizopo kwenye Mwambao wa Bahari ya Hindi (Indian Ocean Rim Association – IORA) uliofanyika tarehe 17 Disemba, 2020 kwa njia ya mtandao.


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. William Ole Nasha akifuatilia Mkutano wa 20 wa Baraza la Mawaziri wa Nchi zilizopo kwenye Mwambao wa Bahari  ya Hindi (Indian Ocean Rim Association – IORA) uliofanyika     tarehe 17 Disemba, 2020 kwa njia ya mtandao. Kulia akifuatilia mkutano huo ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kikanda Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano     wa Afrika Mashariki Bi. Agness Kayola

      

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. William Ole Nasha akifuatilia Mkutano wa 20 wa Baraza la Mawaziri wa Nchi zilizopo kwenye Mwambao wa Bahari ya Hindi (Indian Ocean Rim Association – IORA) 


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. William Ole Nasha akifuatilia Mkutano wa 20 wa Baraza la Mawaziri wa Nchi zilizopo kwenye Mwambao wa Bahari ya Hindi (Indian Ocean Rim Association – IORA) 


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. William Ole Nasha akiongoza ujumbe wa Tanzania ulioshiriki Mkutano wa 20 wa Baraza la Mawaziri wa Nchi zilizopo kwenye Mwambao wa Bahari ya Hindi (Indian Ocean Rim Association – IORA) uliofanyika tarehe 17 Disemba, 2020 kwa njia ya mtandao. 


TANZANIA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA IORA

Tanzania imedhamiria kuimarisha ushirikiano na Jumuiya ya Nchi zilizo kwenye Mwambao wa Bahari ya Hindi (Indian Ocean Rim Association – IORA) katika kutekeleza mikakati ya uchumi wa bluu ambao unalenga kuimarisha sekta ya uvuvi hususan uvuvi wa bahari kuu.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. William Ole Nasha amesema hayo aliposhiriki Mkutano wa 20 wa Baraza la Mawaziri wa Nchi zilizopo kwenye Mwambao wa Bahari ya Hindi (Indian Ocean Rim Association – IORA) uliofanyika tarehe 17 Disemba, 2020 kwa njia ya mtandao.

Amesema Tanzania itaboresha Sekta ya Uvuvi kwa kuimarisha kilimo cha mwani, utalii wa meli (cruise tourism), michezo ya baharini, utafutaji wa rasilimali za mafuta na gesi kwenye eneo la bahari, ujenzi wa bandari maalum za uvuvi, mafuta na gesi na masuala mengine muhimu ya kuimarisha uchumi na ustawi wa wananchi.

Mhe. Ole Nasha ametumia mkutano huo kuwakaribisha wenye nia ya kuwekeza nchini kuja kwa wingi ili kutumia rasilimali zilizopo kwa pamoja na kwa faida ya pande zote mbili.

Amesema Serikali ya Tanzania imejipanga kutumia rasilimali zilizopo katika bahari ya Hindi na kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji ili kuwavutia na kuimarisha Ushirikiano kati ya Serikali na Sekta binafsi.

Mkutano wa 20 wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya hiyo ya IORA umejadili masuala ya maendeleo katika eneo la Bahari ya Hindi ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa mpango kazi wa Jumuiya ya IORA wa mwaka 2017 – 2021. maandalizi ya mpango kazi mpya wa IORA wa mwaka 2022 – 2026; ushiriki na ushirikishwaji wa washirika wa mazungumzo katika masuala ya miradi na program za Jumuiya; masuala ya ulinzi na usalama wa bahari ya Hindi, mkakati wa kupambana na uhalifu, uharamia na biashara haramu ya binadamu katika eneo hilo la bahari.

Mkutano huo wa Baraza la Mawaziri ulitanguliwa na Mkutano wa 22 wa Kamati ya Makatibu Wakuu/ Maafisa waandamizi wa Jumuiya ya IORA uliofanyika tarehe 15 – 17 Desemba, 2020.

 

 


Thursday, December 17, 2020

HABARI KTK PICHA ZIARA YA WAWEKEZAJI KUTOKA UTURUKI NCHINI TANZANIA


Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo akielezea juu ya ziara ya wawekezaji na wafanyabiashara kutoka Uturuki katika studio za Radio Uhuru (Uhuru FM) Leo Jijini Dar es Salaam

 

Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo akiwa na wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Uturuki pamoja na wadau kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), Shirika la Viwanda Vidogo nchini (SIDO) na Mamlaka ya Kanda za Kusindika Usafirishaji Tanzania (EPZA) wakiwa tayari kwa kikao kazi. Wadau hao wamekutana kwa pamoja katika ofisi za TIC Jijini Dar es Salaam kuwaelezea wawekezaji kuhusu fursa mbalimbali za biashara zilizopo nchini. 


Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo (wa kwanza kushoto) pamoja na wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Uturuki wakifuatilia mada iliyokuwa inawasilishwa katika Ofisi za TIC, leo jijini Dar es Salaam


Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo (wa kwanza kushoto), wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Uturuki pamoja na wadau kutoka TIC, EPZA, TCCIA, TPSF na SIDO wakisikiliza mada iliyokuwa inahusu fursa mbalimbali za uwekezaji hapa nchini leo jijini Dar es Salaam


Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo akiongea na wanahabari (hawapo pichani) mara baada ya kumalizika kwa kikao baina ya Wawekezaji na Wafanyabiashara kutoka Uturuki pamoja na wadau kutoka TIC, EPZA, SIDO, TCCIA na TPSF Jijini Dar es Salaam 


Mwenyekiti wa Bodi wa Kampuni ya Kardag kutoka Uturuki ambae pia ni mmoja kati ya wawekezaji akiongea na wanahabari (hawapo pichani) mara baada ya kumalizika kwa kikao baina yao na wadau kutoka TIC, EPZA, SIDO, TCCIA na TPSF Jijini Dar es Salaam 












Tuesday, December 15, 2020

WAWEKEZAJI KUTOKA UTURUKI WAWASILI TANZANIA KUWEKEZA

Wawekezaji kutoka nchini Uturuki wamewasili nchini Tanzania kwa ajili ya kujionea fursa za uwekezaji na biashara zilizopo nchini ili waweze kuwekeza na kukuza Diplomasia ya Uchumi baina ya mataifa hayo.

Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo amethibisha kuwasili kwa wawekezaji hao wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya Waturiki "Compass Partners" leo jijini Dar es Salaam, na kuongeza kuwa wawekezaji watano kati ya kumi wamefika nchini na kujumika na waturuki wengine wanaofanya biashara zao hapa nchini.

"Wawekezaji hawa kutoka Uturuki wamekuja na wamefungua taasisi yao inayojulikana kwa jina la "Compass Partners" ili kuendeleza biashara na tunaamini kwa kutekeleza biashara hii tunaenda kuendeleza uchumi wa Tanzania na kutengeneza ajira kwa watanzania," Amesema Prof. Kiondo

Prof. Kiondo ameongeza kuwa, hatua ya kwanza wawekezaji hao wameleta bidhaa mbalimbali ili watanzania wazione, hatua ya pili itakuwa ni uwekezaji wa kiwanda hapa nchini kwa ajili ya kuanza uzalishaji wa bidhaa ambazo zitauzwa hapa nchini.

Aidha, kwa upande wa bidha zinazozalishwa hapa nchini ambazo zina fursa ya kuuzwa Uturuki ni pamoja na chai, pamba, tumbaku na kahawa bidhaa hizi zote zina soko kubwa sana nchini Uturuki.

Tunazalisha tani 350,000 za pamba lakini tunaweza kuchakata asilimia 15 tu, hivyo tumepata tayari mwekezaji ambaye atawekeza katika kiwanda cha nguo mkonani simiyu ili kuongeza thamani ya bidhaa ya pamba hapa nchini.

Balozi, Prof. Kiondo ametoa wito kwa Watanzania kuanza kuchangamkia fursa hizo za biashara ili waweze kuongeza kipato na kuongeza biashara zao.

Kwa upande wake, Kaimu Balozi wa Uturiki hapa Nchini, Mhe. Onur Yah amesema kuwa biashara kati ya Tanzania na Uturiki imekuwa ikiimarika kila wakati kwani Tanzania ni sehemu salama ya kuwekeza na kufanya biashara.

"Kupitia uwekezaji katika sekta mbalimbali ni imani yangu kuwa tutaendelea kukuza na kuimarisha uhusiano wetu wa kidiplomasia," Amesema Mhe. Yah

Aidha, amewataka Waturuki na Watanzania kutumia fursa za biashara zinazopatikana baina ya mataifa hayo ili kufanya biashara na kukuza uchumi wao.

Ushirikiano wa Tanzania na Uturuki ni wa muda mrefu, pamoja na mambo mengine uhusiano huo umekuwa ukijikita zaidi katika kuendeleza uwekezaji wa viwanda, elimu na utalii hasa katika kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania nchini Uturuki.

Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo akiongea na wanahabari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya Waturiki "Compass Partners" leo jijini Dar es Salaam


Kaimu Balozi wa Uturiki hapa Nchini, Mhe. Onur Yah akiongea na wanahabari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya Waturiki "Compass Partners" leo jijini Dar es Salaam


Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo pamoja na Kaimu Balozi wa Uturiki hapa Nchini, Mhe. Onur Yah wakikata utepe wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya Waturiki "Compass Partners" leo jijini Dar es Salaam



 

 

WAZIRI KABUDI AHIMIZA USHIRIKIANO MIONGONI MWA NCHI ZA OACPS


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palagamba John Kabudi (Mb) akiongoza Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Nchi za Afrika, Caribbean na Pacific (OACPS) uliokuwa ukiendelea kwa njia ya mtandao (Video Conference). Prof. Kabudi ni Rais wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya hiyo hadi Januari 31, 2021

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palagamba John Kabudi (Mb) akiwa na ujumbe wa Tanzania alipokuwa akiongoza Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Nchi za Afrika, Caribbean na Pacific (OACPS). Kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mshariki Mhe. William Tate Ole Nasha, Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Mhe. Jestas Abouk Nyamanga, Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Mwanaid Ali Hamis

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palagamba John Kabudi (Mb) akiwa na ujumbe wa Tanzania akiongoza Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Nchi za Afrika, Caribbean na Pacific (OACPS).


Sehemu ya Ujumbe wa Tanzania wakifuatilia Makutano wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Nchi za Afrika, Caribbean na Pacific (OACPS).

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palagamba John Kabudi (Mb)akisisitiza jambo wakati akiongoza Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Nchi za Afrika, Caribbean na Pacific (OACPS) uliokuwa ukiendelea kwa njia ya mtandao (Video Conference). Prof. Kabudi ni Rais wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya hiyo hadi Januari 31, 2021.


Monday, December 14, 2020

UBALOZI WA TANZANIA NCHINI QATAR WAANZISHA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WATANZANIA WANAOAJIRIWA NCHINI HUMO

Ubalozi wa Tanzania nchini Qatar umeanzisha rasmi programu ya  mafunzo  kwa waajiriwa wapya kutoka Tanzania wanaokwenda kufanya kazi nchini humo.

Mafunzo hayo yameanzishwa kwa makubaliano kati ya Ubalozi na  Kampuni zote zinazoajiri wafanyakazi kutoka Tanzania ambao  Ubalozi huwapatia barua kwa ajili ya kuthibitisha uhalali wao ili kupata kibali cha kuingia nchini humo. Mafunzo hayo ambayo hutolewa mara tu wanapowasili nchini humo, yanalenga kuwajengea uwezo wa kazi pamoja na kuwaelewesha sheria na taratibu za ajira za Qatar pamoja na haki zao za msingi.

Kadhalika, mafunzo hayo  yameanzishwa ili kuwajulisha maadili, mila na utamaduni za Qatar pamoja na kuwahimiza kujua wajibu wao ili kudumisha heshima ya Tanzania kimataifa na kuitangaza vyema nchi. 

Mafunzo ya awali yametolewa tarehe 12 Desemba, 2020 kwa Mabinti 9 kutoka Tanzania ambao wameajiriwa na Kampuni ya Qatar Manpower Solutions (WISA) inayomilikiwa na Serikali kwa ajili kufanya usafi na huduma za ndani. 

Mafunzo hayo ambayo yamesimamiwa na Bw. Volka Gowele, Afisa wa Ubalozi yameendeshwa na Bw. Sahim Ayoub Khatib, Diaspora wa Tanzania na Mwajiriwa kwenye Kampuni ya HBK ya Qatar kwenye Kitengo cha Utawala na Rasilimali Watu. Bw. Khatib amejitolea kusaidia kuendesha mafunzo hayo kwa Watanzania.

Bw. Sahim Ayoub Khatib (mwenye karatasi), Diaspora wa Tanzania nchini Qatar ambaye pia ni Mwajiriwa wa Kampuni ya HBK ya nchini humo akitoa mafunzo kwa Mabinti 9 kutoka Tanzania ambao wameaajiriwa na Kampuni ya Manpower Solutions (WISA) inayomilikiwa na Serikali kwa ajili ya kufanya kazi za usafi na huduma za ndani. Mafunzo hayo ambayo yanalenga kuwajengea uwezo  pamoja na kuwaelewesha sheria na taratibu za ajira za Qatar, yameandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini humo. Mafunzo hayo yalifanyika kwenye Ofisi za Ubalozi hivi karibuni na kusimamiwa na Bw. Volka Gowele (mwenye barakoa), Afisa wa Ubalozi.


Mafunzo yakiendelea kwa Mabinti hao
Mabinti tisa kutoka Tanzania walioshirki mafunzo ya kuwajengea uwezo yaliyoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Qatar


Picha ya pamoja kati ya Bw. Khatib (kushoto), Bw. Gowele (wa pili kushoto) pamoja na Mabinti tisa kutoka Tanzania walioshiriki mafunzo ya kuwajengea uwezo yaliyoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Qatar.

 

Saturday, December 12, 2020

TANZANIA, PAKISTAN ZASAINI MIKATABA YA MAKUBALIANO YA KIDIPLOMASIA

Tanzania na Pakistan zimetiliana saini mikataba miwili ya makubaliano ambayo ni mkataba wa mashaurino ya kidiplomasia pamoja na mkataba wa kuanzisha tume ya pamoja ya ushirikiano wa kiuchumi.

Mikataba hiyo imesainiwa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi pamoja na Balozi wa Pakistani hapa nchini, Mhe. Mohammad Saleem.

Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) amesema kuwa makubaliano hayo yanatoa fursa nyingi zilizopo za kuongeza na kukuza biashara kati ya Tanzania na Pakistan hasa katika sekta ya kilimo ikiwemo chai, pamba, korosho, mbegu za mafuta, Madini ya Tanzanite, pamoja na uwekezaji.

"Tanzania na Pakistan zina uhusiano wa muda mrefu na katika mazungumzo yetu ya leo, Balozi wa Pakistan ameeleza fursa zilizopo Pakistan ambapo fursa hizo zikitumiwa vizuri zitanufaisha mataifa yote mawili," Amesema Prof. Kabudi 

Prof. Kabudi ameongeza kuwa makubaliano hayo ni kielelezo kingine cha uhusiano mzuri uliopo baina ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Pakistan na kwamba fursa hizo zitaendelea kuongeze ushirikiano wa diplomasia ya uchumi baina ya Tanzania na Pakistan.

Kwa Upande wake Balozi wa Pakistani hapa nchini, Mhe. Mohammad Saleem amesema kuwa kusainiwa kwa mikataba hiyo muhimu itasaidia kukuza na kuendeleza diplomasia ya Uchumi baina ya Tanzania na Pakistan.

"Ni imani yangu kuwa kusainiwa kwa mikataba hii miwili ya makubaliano baina ya Serikali ya Tanzania na Pakistan kutasaidia kudumisha na kukuza uchumi kati ya mataifa yetu," Amesema Balozi Saleem

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi akiangalia baadhi ya nyaraka alizokabidhiwa na Balozi wa Pakistani nchini, Mhe. Mohammad Saleem katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam


Balozi wa Pakistani nchini, Mhe. Mohammad Saleem akimuelezea jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi kabla ya kusainiwa kwa mikataba ya makubaliano Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi akimueleza jambo Balozi wa Pakistani nchini, Mhe. Mohammad Saleem katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi pamoja na Balozi wa Pakistani nchini, Mhe. Mohammad Saleem wakisaini mikataba ya makubaliano katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam




Friday, December 11, 2020

TZ YAHIMIZA MATAIFA MAKUBWA KUENDELEA KUZIFUTIA MADENI NCHI ZA OACPS

Tanzania imeendelea kuhimiza umuhimu wa mataifa makubwa kuzifutia madeni nchi za Jumuiya ya nchi za Afrika, Caribbean na Pasifiki (OACPS) zilizoathiri na janga la COVID-19 pamoja na kuyataka mataifa hayo kuhakikisha kwamba chanjo ya COVID-19 itakayopatikana inazifikia nchi zote za Jumuiya hiyo.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) ambaye pia ni Rais wa Baraza la Mawaziri la OACPS wakati alipokuwa anawasilisha hotuba yake katika Mkutano wa 39 wa Bunge la pamoja baina ya nchi za ACP na EU na Mkutano wa 111 wa Baraza la Mawaziri kutoka nchi za Jumuiya ya OACPS uliofanyika jana kwa njia ya Mtandao (Video Conference) jijini Dar es Salaam.

"Kutokana na jukumu langu kama Rais wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya OACPS nimehutubia kwa njia ya video Bunge la pamoja la Ulaya na ACP (ACP-EU Joint Parliamentary Assembly). Katika hotuba yangu nimehimiza umuhimu wa mataifa makubwa kuendelea kuzifutia madeni nchi za OACPS zilizoathiri na janga la COVID-19, pamoja na kuyataka mataifa hayo kuhakikisha kwamba chanjo ya COVID-19 itakayopatikana inazifikia nchi zote za Jumuiya yetu ya OACPS," Amesema Prof. Kabudi

Halikadhalika, Prof. Kabudi ameelezea hatua iliyofikiwa na nchi za OACPS ikiwemo Tanzania katika kujenga democrasia, uchumi, biashara na maendeleo ya watu ikiwemo suala la kulinda na kuheshimu haki za binadamu. Aidha, aliwajulisha juu ya  changamoto zinazozikabili nchi za OACPS katika kutimiza adhma yao ya maendeleo, ikiwemo janga la ugonjwa wa COVID -19, mabadiliko ya tabia nchi, ugumu wa kuyafikia masoko ya ulaya, masuala ya amani na usalama ikiwemo suala la wakimbizi. 

Kwa upande wake Waziri wa Uchumi na Maendeleo wa Ujerumani, Dkt. Gerd Muller, ambaye pia ni Raisi wa Baraza la  Mawaziri la Umoja wa Ulaya alimhakikishia Prof. Kabudi kuwa Umoja wa Ulaya (EU) utaendeleza ushirikiano wake na nchi za OACPS katika kuhakikisha kuwa uchumi wa Jumuiya hiyo unazidi kuimarika.

"Naomba kutumia fursa hii kukuhakikishia kuwa sisi ka EU tupo tayari kushikamana na Jumuiya ya OACPS kuimarisha uhusiano wetu kiuchumi, kisiasa, kidiplomasia lakini pia kulinda na kuapa kipaumbele masuala yote yanayohusu haki za binadamu," Amesema Dkt. Muller.

Mbali na Dkt. Muller wengine waliohutubia katika mkutano huo ni pamoja na Jutta Urpilanen, Kamishna wa Ubia wa Kimataifa kutoka EU ambaye nae pia alisisitiza kuendeleza mshikamano baina ya nchi za EU na OACPS.

Katika hatua nyigine, Prof. Kabudi ameeleza kuwa kumalizika kwa mkutano wa 39 wa Bunge la pamoja baina ya nchi za ACP na EU kumetoa fursa ya kufanyika kwa mkutano wa wa Baraza la Mawaziri wa nchi za OACPS unaotegemewa kuanza kufanyika kwa njia ya mtandao (Video Conference) kuanzia tarehe 13 hadi 17.

Prof. Kabudi ameongeza kuwa katika mkutano huo, masuala muhimu yatakayo jadiliwa ni pamoja na Mapambano dhidi ya ugonjwa Corona, majadiliano ya mkataba mpya wa ubia mpya baina ya nchi za OACPS na Umoja wa Ulaya, Mageuzi (reforms) ndani ya Sekretariati ya OACPS, kusimamia kusainiwa kwa Mkataba ulioboreshwa wa Georgetown (the Revised Georgetown Agreement) na nchi za OACPS pamoja na Mikakati ya kufanya shughuli za Jumuiya ziguse zaidi Maisha ya wananchi.

Itakumbukwa kuwa Agosti 1, 2020 Tanzania ilikabidhiwa jukumu la kuongoza Jumuiya ya nchi za Afrika, Caribbean na Pasifiki (OACPS) kwa ngazi ya Mawaziri na kwa ngazi ya balozi Brussels.

Jukumu hilo ni heshima kubwa kwa Tanzania na ni ishara ya wazi ya jumuiya ya kimataifa kutambua kazi kubwa anayofanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ndani ya nchi na hivyo kutamani pia ushawishi wake huo uwe katika ngazi ya kimataifa hususan katika jumuiyan hii ya OACPS.

Hii ni mara ya tatu Tanzania kuchaguliwa kuwa  Mwenyekiti wa Jumuiya hii tangu ilipoanzishwa mwaka 1975. Tanzania ilikuwa Mwenyekiti mwaka 1992 na mwaka 2014. Chini ya Uongozi wa Tanzania vipaumbele vikuu ni pamoja na kupambana na ugonjwa wa corona na athari zake, kusimamia kukamilishaji wa majadiliano ya mkataba mpya wa ubia kati yan chi za OACPS na Umoja wa Ulaya,  kusimamia mageuzi makubwa ndani ya Jumuiya ya OACPS ili iendane na wakati na kuelekeza rasilimali zake kwenye maeneo  muhimu yenye tija  kwa wanachama.

 Aidha, Tanzania pia imelenga kuimarishaji ushiriano miaongoni mwa nchi za OACPS (Connectivity) na kufanya mashauriano na wabia wetu wengine wa maendeleo ukiwemo Umoja wa Ulaya katika kuweka mifumo mizuri zaidi ya kuimarisha biashara, ongezeko la thamani ya mazao ya kilimo, matumizi ya digitali na fursa zaidi za masoko.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) na Rais wa Baraza la Mawaziri la OACPS akisisitiza jambo wakati alipokuwa anawasilisha hotuba yake katika Mkutano wa 39 wa Bunge la pamoja baina ya nchi za ACP na EU jana jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ulifanyika kwa njia ya Mtandao (Video Conference). Picha na Nelson Kessy


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) na Rais wa Baraza la Mawaziri la OACPS akichangia mada katika Mkutano wa 39 wa Bunge la pamoja baina ya nchi za ACP na EU jana jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ulifanyika kwa njia ya Mtandao (Video Conference). Picha na Nelson Kessy









Thursday, December 10, 2020

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE ALA KIAPO CHA UTII BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. William Tate Olenasha, ameapa kiapo cha Utii cha Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki

Mhe. Olenasha ameapa kiapo hicho na kushuhudiwa na Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Martin Ngoga pamoja na wabunge wengine wanaounda Bunge hilo ili kumwezesha kushiriki kwenye Bunge hilo kama Naibu Waziri anayeshughulikia masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mhe. Olenasha ameapa kiapo hicho akiwa katika Ofisi za Wizara zilizopo kwenye Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma wakati wa kikao kilichofanyika kwa njia ya mtandao tarehe 10 Desemba 2020.

Aidha, kikao hicho kimehudhuriwa na Wabunge wa Bunge hilo ambao wengi wameshiriki kutokea kwenye nchi zao wakati Mhe. Spika akiwa Makao Makuu ya Bunge hilo jijini Arusha.

Kikao hicho, pamoja na mambo mengine kimejadili Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge la Afrika Mashariki ya Masuala Mtambuka

 



Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. William Tate Olenasha akiapa kiapo cha utii na uadilifu mbele ya Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Ngoga Martin   


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. William Tate Olenasha akiapa kiapo cha utii na uadilifu mbele ya Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Ngoga Martin   

Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Tanzania, Mhe. Josephine Sebastian Lemoyan akimtambulisha Mhe. Olenasha kwenye Bunge hilo kama Mjumbe mpya

Mhe. Olenasha akisaini Hati ya Kiapo baada ya kula kiapo cha utaii cha kushiriki Bunge la Afrika Mashariki


Mhe. Olenasha kwa pamoja na Mhe. Josephine wakifuatilia mjadala uliokuwa ukiendelea wakati wa kikao cha Bunge la EALA


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Olenasha akichangia jambo wakati wa kikao  


Mhe. Olenasha na Mhe. Josephine wakifuatilia mjadala wakati wa kikao hicho