Thursday, December 3, 2020

RAIS WA UFARANSA AMTUMIA BARUA YA PONGEZI RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT JOHN POMBE MAGUFULI KWA KUIWEZESHA TANZANIA KUINGIA KATIKA ORODHA YA NCHI ZA UCHUMI WA KATI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akipokea barua ya kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kuiongoza Tanzania kuingia katika orodha ya  Nchi za kipato cha kati iliyoandikva na Rais wa Ufaransa Mhe. Emmanuel Macron. Anayemkabidhi barua hiyo Prof. Kabudi ni Balozi wa Ufaransa hapa Nchini Mhe. Frederic Clavier 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Ufaransa hapa Nchini Mhe Frederic Clavier. Mazungumzo halo yamefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar Es Salaam ambapo Mhe. Kabudi amemueleza Balozi huyo kuwa katika kipindi cha pili cha Seriali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli Serikali itajikita zaidi katika kuimarisha sekta binafsi na kuvutia wawekezaji hususan baada ya kipindi cha kwanza cha awamu ya tano kujikita katika uboreshaji wa miundombinu,nishati na kuwekeza katika maendeleo ya jamii
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika mazungumzo na Msajili wa Mahakama ya Kimataifa ya Kesi Masalia za Mauaji ya Kimbari (International Residual Mechanism for Criminal Tribunals -IRMCT) Bwana Abubacar Tambadou aliyefika kujitambulisha baada ya kupata uteuzi huo pia kuishukuru Tanzania kwa ushirikiano unaoutoa kwa Mahakama hiyo na kuomba kuendelea kutoa ushirikiano ili kuiwezesha kutimiza majukumu yake.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Msajili wa Mahakama ya Kimataifa ya Kesi Masalia za Mauaji ya Kimbari (International Residual Mechanism for Criminal Tribunals -IRMCT) Bwana Abubacar Tambadou mara baada ya kumaliza mazungumzo yao 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akimkabidhi zawadi yenye picha ya Mlima Kilimanjaro Balozi wa Italia hapa Nchini Mhe Mhe. Roberto Mengoni. Balozi Mengoni alikuwa akiagana na Prof. Kabudi mara baada ya kumaliza kipindi chake cha Ubalozi hapa Nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akimkabidhi zawadi yenye picha ya Mlima Kilimanjaro Balozi wa Italia hapa Nchini Mhe 
Mhe. Theresia Samaria
  Balozi Samaria alikuwa akiagana na Prof. Kabudi mara baada ya kumaliza kipindi chake cha Ubalozi hapa Nchini
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) hapa Nchini Balozi Manfred Fanti. katika mazungumzo yao yaliyofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Fanti ameweleza Prof. Kabudi kuwa  pamoja na kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Umoja wa Ulaya kujadili masuala mbalimbali yanayoihusu Tanzania bado hakuna maazimio yeyote yaliyofikiwa na Umoja huo kuhusu Tanzania na kwamba Umoja wa Ulaya utaendelea kuimarisha mahusiano mazuri na ya kihistoria yaliopo kati ya Tanzania na Umoja huo.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.