Tuesday, December 8, 2020

HABARI KATIKA PICHA MAHAFALI YA 50 YA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akimkabidhi zawadi ya vitabu Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Namibia ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia, Mhe. Netumbo Ndaitwah


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwasilisha salamu za Serikali kwenye mahafali ya 50 ya chuo hicho yaliyofanyika jijini Dar es Salaam


Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi moja kati ya zawadi Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Namibia ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia, Mhe. Netumbo Ndaitwah


Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku shahada ya heshima Naibu Waziri Mkuu Wa Jamhuri ya Namibia ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia, Mhe. Netumbo Ndaitwah


Baadhi ya wahitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakiwa ukumbini tayari kwa ajili ya kutunukiwa shahada  


Baadhi ya Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa Nchini wakifuatilia sherehe za mahafali ya 50 ya chuo hicho yaliyofanyika jijini Dar es Salaam


Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) katika mahafali ya 50 ya chuo hicho yaliyofanyika jijini Dar es Salaam


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.