Friday, June 29, 2018

Mkutano wa 15 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Uchukuzi, Mawasiliano na Hali ya Hewa wafikia tamati


Mhe. Prof. Makame Mbarawa  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, akizungumza kwenye Mkutano wa 15 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Uchukuzi, Mawasiliano na Hali ya Hewa la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha katika ukumbi wa mikutano wa Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mhe. Prof.Mbarawa akizungumza katika mkutano huo amezisihi nchi wananchama za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuongeza kasi ya kutekeleza miradi inayopangwa katika ngazi ya Jumuiya kwa kuzingatia ukomo wa tarehe.


Mhe. Prof. Makame Mbarawa  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano akisaini taarifa ya mkutano mara baada ya  majadiliano

Kutoka kushoto  Bibi. Zaina Ibrahim Mwalukuta Mkurugenzi wa Viwanja vya Ndege Zanzibar (ZAA), Dkt. Leonard Chamuriho Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Sekta ya Uchukuzi, Dkt. Maria Sassabo Katibu Mkuu Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na Mhandisi Happiness Mgalula Mkurugenzi wa barabara, Wizara ya Ujuenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Sekta ya Ujenzi wakifuatilia mkutano

Meza kuu ikiongoza mjadala wakati wa mkutano

Sehemu ya wajumbe wakifuatilia mkutano


Mhe. Prof. Mbarawa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano akizungumza wakati wa mkutano

JAJI IMANI ABOUD ASHINDA UCHAGUZI WA MAJAJI WA MAHAKAMA YA AFRIKA YA HAKI ZA BINADAMU NA WATU


Jaji Imani Aboud wa Tanzania


JAJI IMANI ABOUD WA TANZANIA ASHINDA UCHAGUZI WA MAJAJI WA MAHAKAMA YA AFRIKA YA HAKI ZA BINADAMU NA WATU


Mkutano wa 33 wa Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Afrika unaoendelea Jijini Nouakchott, Mauritania kwa siku mbili, leo tarehe 29 Juni, 2018 umefanya uchaguzi wa Majaji wanne wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu.
Mgombea wa Tanzania Mhe. Jaji Imani D. Aboud ameshinda uchaguzi huo kwa kura 47 kati ya kura 50 zilizopigwa na kufanikiwa kuchukua nafasi ya Jaji Solomy Balungi Bossa wa Uganda aliyejiuzulu nafasi hiyo kabla ya kumaliza kipindi chake.
Kwa ushindi huo, Mhe. Jaji Aboud atakuwa Jaji wa Mahakama hiyo akiwakilisha Kanda ya Afrika Mashariki kwa kipindi cha miaka miwili.
Majaji wengine walioshinda kwenye uchaguzi huo ni pamoja na Jaji Kioko Ben (Kenya), Jaji Tchikaye Balise (Jamhuri ya Congo), na Jaji Anukam Stella Isibhkhomen (Nigeria).
Ushindi huu unadhihirisha uwezo mkubwa alionao Mhe. Jaji Aboud na heshima kubwa iliyonayo nchi yetu katika Bara la Afrika.
-Mwisho-


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam, 29 Juni, 2018

Ziara ya Rais Mnangagwa katika picha

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Edmund Mndolwa mara baada ya kuwasili katika Chuo cha Kilimo na Mifugo cha Kaole Bagamoyo mkoani Pwani. Rais huyo wa Zimbabwe alisoma Shuleni hapo mwaka 1963 pamoja na wapigania Uhuru wa Chama cha FRELIMO na ilijulikana kama Shule ya Mafunzo ya Ufundi ya  Wapigania Uhuru wa Chama cha FRELIMO.
Rais wa Zimbabwe Mhe. Emmerson Mnangagwa akizungumza na wafanyakazi pamoja na wanafunzi wanaosoma katika Chuo cha Kilimo na Mifugo cha Kaole (hawapo pichani).
 Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akiangalia moja ya sufuria waliokuwa wakiitumia kila siku miaka ya sitini, wakati wakisoma katika Shule ya Mafunzo ya Ufundi ya wapigani Uhuru ya Chama cha FRELIMO.
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akitoka katika moja ya mabweni yaliyotumika katika mwaka 1963 wakati wakiwa katika Shule ya Mafunzo ya Ufundi ya wapigani Uhuru ya Chama cha FRELIMO ambacho sasa kinajulikana kama Chuo cha Kilimo na Mifugo cha Kaole Bagamoyo mkoani Pwani.
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akimsikiliza Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi mara baada ya kumaliza kukagua baadhi ya madarasa na mabweni waliyokuwa wakiyatumia katika Shule ya Mafunzo ya Ufundi ya wapigani Uhuru ya Chama cha FRELIMO ambacho sasa kinajulikana kama Chuo cha Kilimo na Mifugo cha Kaole Bagamoyo mkoani Pwani.
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akiwa katika picha na Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Edmund Mndolwa, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Susan Kolimba (Mb.) (wa nne kutoka kushoto mstari wa pili), viongozi wengine wa Tanzania na Zimbabwe pamoja na wanafunzi wanaosoma katika Chuo cha Kilimo na Mifugo cha Kaole Bagamoyo mkoani Pwani

Thursday, June 28, 2018

Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe Mh. Emmerson Mnangagwa afanya ziara nchini.

Ndege iliyombeba Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe Mhe. Emmerson Dambudzo Mnangagwa ikiwasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es salaam, tarehe 28 Juni 2018. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akimkaribisha mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe Mhe. Emmerson Dambudzo Mnangagwa mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.


Mhe. Rais Mnangagwa akiwapungia mkono wananchi waliofurika kumlaki katika uwanja wa ndege Dar es salaam.
Mhe. Rais Magufuli akiwa na mgeni wake Mhe. Rais Mnangagwa mara baada ya kukagua vikundi vya ngoma vilivyokuwa vikitumbuiza  uwanjani hapo.

Wednesday, June 27, 2018

Katika picha; Taswira ya jengo la Kituo cha Kutoa Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) cha Tunduma


Mwonekano wa jengo la Tunduma OSBP kwa upande mbele (upande wa kuingilia)
Mwonekano wa jengo la Tunduma OSBP kwa upande wa kuingilia
Mwonekano wa jengo la Tunduma OSBP kwa upande wa kutokea (kuelekea Nakonde, Zambia)

Mwonekano wa jengo la Tunduma OSBP kwa ndani

Baadhi ya vifaa vya ujenzi vikiwa kazini.

Kamati ya ujenzi wa Tunduma OSBP ikiwa kwenye kikao cha kutathimini maendeleo ya ujenzi kilichofanyika katika moja ya ukumbi wa mikutano uliopo kwenye jengo hilo hivi karibuni.

Kamati ya ujenzi ikitembelea sehemu ya eneo la kuegesha magari ambalo ujenzi wake bado unaendelea
Kamati ya ujenzi ikiangalia maendeleo ya ujenzi wa ghala la kuhifadhia bidhaa katika kituo hicho.
Mradi wa ujenzi wa Kituo cha Kutoa Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) cha Tunduma, mpaka kati ya Tanzania na Zambia umekamilika kwa takribani 95%. 

Ujenzi wa Kituo hiki unatarajiwa kuboresha mazingira ya biashara baina ya nchi hizi mbili (Tanzania/Zambia). 

Ujenzi wa mradi huu ulioanza mwaka 2016 umechukua ukubwa wa eneo linalokadiriwa kuwa na takriban kilomita za mraba 43,000.

Ujenzi wa mradi huu unafadhiliwa na shirika la TradeMark  East Afrika.

Mkutano wa 16 wa Majadiliano ya Kisiasa kati ya Tanzania na Korea Kusini wafanyika jijini Dar

 Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Astralasia Bibi Yusta Nyange (wa pili kutoka kushoto) akifurahia jambo kwenye majadiliano ya 16 ya Kisiasa kati ya Tanzania na Jamhuri ya Korea, yaliyofanyika tarehe 27 Juni 2018 , katika ukumbi wa mikutano wa Julius Nyerere(JNICC), Dar es salaam.
Wengine katika picha ni Maafisa kutoka Wizarani  Emmanuel Luangisa(wa mwisho kulia), Ramla Hamisi(wa kwanza kulia) na anayefuata ni Bi Blandina Kasagama wakifuatilia majadiliano hayo.
Pamoja na mambo mengine majadiliano hayo yalijikita katika kuzungumzia namna ya kuimarisha mahusiano yaliyopo kati ya Tanzania na Korea katika maeneo mbalimbali.
 Mkutano ukiendelea
Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika na Mashariki ya Kati, Bw. KOH Kyung-sok(wa pili kushoto), akiwa na ujumbe wake kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea na Ubalozi wa Korea nchini wakiwa katika majadiliano hayo.
 Bibi Yusta Nyange(kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Bw.
KOH Kyung-sok baada ya Mkutano.
Bibi Yusta Nyange(kulia) akimkabidhi zawadi Bw. KOH Kyung-sok baada ya Mkutano.
Picha ya Pamoja baada ya Mkutano

RAIS WA ZIMBABWE ZIARANI NCHINITAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Taarifa kuhusu ziara ya Rais wa Zimbabwe nchini

Mheshimiwa Emmerson Dambudzo Mnangagwa, Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe atafanya ziara ya kitaifa nchini Tanzania tarehe 28 hadi 29 Juni, 2018. Hii itakuwa ziara ya kwanza ya Mheshimiwa Rais Mnangagwa nchini Tanzania tangu aingie madarakani mwezi Novemba, 2017.

Lengo la ziara hii ya Rais wa Zimbabwe ni kujitambulisha kwa Rais na wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tangu aingie madarakani, Mheshimiwa Rais Mnangagwa ameshafanya ziara katika nchi za Namibia, Zambia, Msumbiji, Angola, Afrika Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Botswana.

Ziara hii ni muhimu kwa Tanzania kwani itatoa fursa ya kuimarisha na kukuza zaidi mahusiano mazuri yaliyopo ya kidiplomasia, kihistoria, kiuchumi na kijamii kati ya nchi hizi mbili. Ziara hii pia itatoa fursa kwa viongozi wetu kujadili masuala mbalimbali yanayohusu nchi hizi mbili ya kikanda na kimataifa.

Wakati wa ziara hiyo,  Mhe. Rais Mnangagwa atafanya  mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. 

Rais Mnangagwa anatarajiwa pia kutembelea Chuo cha Kilimo cha Wazazi Kaole Bagamoyo ambacho awali kilitumika kutoa mafunzo kwa wapigania uhuru kutoka nchi za Kusini mwa Bara la Afrika na Mhe. Rais Mnangagwa ni miongoni mwa waliopata mafunzo katika chuo hicho. 

Mhe. Rais Mnangagwa anatarajiwa kuondoka tarehe 29 Juni 2018 kurejea chini Zimbabwe.
-Mwisho-


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam, 27 Juni, 2018

Tuesday, June 26, 2018

Balozi Migiro azindua rasmi Jumuiya ya Watanzania waishio Uingereza-ATUK

Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Dkt. Asha-Rose Migiro akiitazama keki iliyoandaliwa wakati wa uzinduzi rasmi wa Jumuiya ya Watanzania waishio Uingereza (Association of Tanzanians in the UK-ATUK)
Mhe. Balozi Migiro akifurahia jambo na sehemu ya Watanzania walioshiriki uzinduzi huo

Sehemu ya Watanzania na wageni waalikwa waliohudhuria tukio hilo la kihistoria 

===================================================UZINDUZI WA  ASSOCIATION OF TANZANIANS IN THE UK – ATUK 

Mhe. Dkt. Asha-Rose Migiro, Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za uzinduzi wa Jumuiya Mwamvuli ya Watanzania waishio nchini Uingereza na Ireland ya Kaskazini iitwayo ATUK –Association of Tanzanians in the UK zilizofanyika mjini Reading tarehe 23 Juni, 2018. Jumuiya hii inatokana na muungano wa jumuiya za diaspora kutoka mikoa mbalimbali ya hapa Uingereza na wanachama wa kujitegemea.

Wajumbe wa Kamati ya Muda iliyoratibu kuanzishwa kwa ATUK walipongeza na kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli za kupambana na ufisadi, kusimamia uwazi na uwajibikaji katika utumishi wa umma na kuongeza kasi ya kujenga uchumi wa viwanda. Kauli mbiu ya hafla hii ilikuwa “UMOJA NI NGUVU, TANZANIA YA VIWANDA INAWEZEKANA”. Hivyo mojawapo ya malengo ya kuanzishwa kwa ATUK ni kujenga umoja na kukusanya nguvu za kuchangia jitihada za kujenga uchumi wa viwanda nchini mwetu.

Akihutubia hadhara hiyo Balozi Migiro aliwapongeza ATUK na alihimiza umoja na kukumbusha kwamba wakati wote Mhe. Rais amekuwa akisisitiza umoja wa Watanzania bila kujali tofauti zao kwani umoja ni nyenzo muhimu ya kujiteletea maendeleo. Hivyo Balozi Migiro aliwashukuru kwa Muungano huo na kueleza kwamba wakiendeleza mshikamano wataweza kuchangia  kwa ufanisi jitihada kubwa za Mhe. Rais  Magufuli na Serikali ya Awamu ya Tano katika kuwaletea maendeleo Watanzania wote.


Katibu Mkuu akutana na wadau mbalimbali kutoka Serikalini na Taasisi za Umoja wa Mataifa kujadili SDGs.


   

 Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Aldof Mkenda akisistiza jambo wakati wa ufunguzi wa Mkutano kati ya Serikali na Umoja wa Mataifa na Taasisi zake kujadili utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo  Endelevu. Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC), Dar es Salaam, Tarehe 26 Juni2018.
Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Dunia(SDGs) yako 17 yenye shabaha 169 na  Viashiria 232, malengo hayo yanatekelezwa kwa pamoja na Jumuiya ya Kimataifa kwa kushirikisha kila sekta na utekelezaji wake unahimiza ushiriki wa kila kundi kwenye jamii.
 Katibu Mkuu Prof. Mkenda( wa pili kushoto), Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Prof. Faustine Kamuzora, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (mwisho kulia) na wa mwisho kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Bw. Alvaro Rodriguez, wakifuatilia majadiliano ya Mkutano huo.
 Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akielezea malengo ya Mkutano huo.
 Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Bw. Alvaro Rodriguez, akitoa taarifa ya ufunguzi kwa upande wa Umoja wa Mataifa.
 Sehemu ya washiriki wakifuatilia mkutano huo.
 Wa pili kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar na washiriki wengine kutoka Serikalini walioshiriki katika mkutano huo.
 Sehemu ya Maafisa kutoka Wizarani wakifuatilia mkutano huo.
 Katibu Mkuu Prof. Mkenda akiwaelezea wanahabari kuhusu mpira uliondikwa Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu ya Dunia, aliokabidhiwa na Bw. Rodriguez kuashiria  utekelezaji wa malengo hayo kwa kasi na kuzingatia Muktadha wa mazingira ya Tanzania.
Picha ya pamoja baada ya mkutano.

Waziri Mahiga akutana kwa pamoja na Balozi wa Uingereza na Kaimu Balozi wa Marekani nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga (Mb.), akisalimiana na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania  Dkt. Inmi Patterson akiwa amefuatana na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. Sarah Cooke mara walipomtembelea na kufanya nae mazungumzo kwenye Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje zilizopo Jijini Dar es Salaam 
Dkt. Mahiga akisalimiana na Mhe. Balozi Cooke.
Dkt. Mahiga akimsikiliza Mhe. Balozi Cooke alipokuwa akimweleza jambo wakati wa mazungumzo yao
Sehemu ya ujumbe wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia mazungumzo kati ya Mhe Waziri Mahiga na Balozi Cooke (hawapo pichani). Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya  Ulaya na Amerika, Bw. Jestas Nyamanga, Katibu wa Waziri, Bw. Gerald Mbwafu ( kulia) pamoja na Anthony Mtafya, Afisa Mambo ya Nje
Kaimu Balozi wa Marekani nchini Dkt. Patterson ( kulia) pamoja na Maafisa Waandamizi kutoka Ubalozi wa Marekani na Uingereza nchini wakisikiliza kwa makini mazungumzo kati ya Dkt. Mahiga na Balozi Cooke (hawapo pichani).
Mkutano ukiendelea.