Thursday, May 16, 2024

BALOZI MBAROUK AKUTANA NA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA ETHIOPIA JIJINI DODOMA


Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia Balozi Birtukan Ayano ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma.



Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia Balozi Birtukan Ayano ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma.

Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia Balozi Birtukan Ayano ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia Balozi Birtukan Ayano akizungumza na Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk alipomtembelea ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia Balozi Birtukan Ayano akizungumza na Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk alipomtembelea ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma.

 

Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia Balozi Birtukan Ayano ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma.

 

Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk katika picha ya pamoja na  Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia Balozi Birtukan Ayano alipomtembelea ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma.
Mkurugeni wa Idara ya Afrika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ali Sakila Mbarouk akimpokea Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia Balozi Birtukan Ayano alipowasili Wizarani  katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.

 

Mkurugeni wa Idara ya Afrika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ali Sakila akimkaribisha Balozi wa Ethiopia nchin Mhe. Shibru Mamo alipowasili Wizarani  katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.

 

 

Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk amekutana na kuzungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia Balozi Birtukan Ayano ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma.

Katika mazungumzo yao viongozi hao wamekubaliana kuendelea kuimarisha uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Ethiopia kwa manufaa ya pande zote mbili.

Akizungumza na mgeni wake Mhe. Balozi Mbarouk amesema Tanzania inajivunia kuwa na uhusiano na ushirikiano imara na Ethiopia hali ambayo inazifanya nchi hizo kuendelea kushirikiana katika sekta za usafiri wa anga, nishati, Kilimo, Mifugo, Utalii, Ulinzi na Uhamiaji

Balozi Mbarouk amesema Tanzania itatumia uhusiano wake na Ethiopia kukuza biashara na uwekezaji kwa manufaa ya pande zote mbili.

Balozi Mbarouk pia ameipongeza Ethiopia kwa kuwa nchi ya kwanza kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya Ujenzi wa Ofisi zake za Ubalozi na makazi ya Balozi katika eneo ambalo Serikali ya Ethiopia ilipewa na Serikali ya Tanzania.

Akizungumza katika kikao hicho Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia Balozi Ayano amesema Ethiopia inaiona Tanzania Kama mdau mühimu wa kushirikiana naye kwa lengo la kukuza biashara na uwekezaji  na kuendeleza uhusiano uliopo.

Amesema amekuja Tanzania kwa kazi ya kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya kujenga Ofisi ya Ubalozi  na makazi ya Balozi wao katika makao makuu ya Tanzania jijini Dodoma.

“Ethiopia ni makao makuu ya Umoja wa Afrika , sisi ni viongozi na tunataka kuendelea kuwa mfano kwa nchi za Afrika na nyingine kwa kuwa wakwanza kuwa na jengo letu hapa Mtumba,” alisema Balozi Ayano.

Ameongeza kuwa Ethiopia inaamini kuwa kitendo cha wao kuweka jiwe la msingi na kuanza Ujenzi wa majengo hayo kutaendelea kuimarisha uhusiano wake na Tanzania.

Mhe Balozi Ayano yuko nchini kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi katika kiwanja cha Ubalozi kilichopo katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.

Ethiopia inakuwa nchi ya kwanza kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya Ujenzi wa Ofisi za Ubalozi na makazi ya  Balozi tangu Serikali ya Tanzania ilipohamia jijini Dodoma Makao Makuu ya Serikali mwaka 2017.

China, Ujerumani, Ufaransa, Uingereza , Marekani na Umoja wa Mataifa na Mashirika yake yana Ofisi ndogo jijini Dodoma zilizofunguliwa baada ya Serikali kuhamia jijini Dodoma.

WAZIRI MAKAMBA AWASILI NCHINI CHINA KWA ZIARA YA KIKAZI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba (Mb.) leo tarehe 16 Mei 2024 amewasili nchini China kuanza ziara ya kikazi, kufauatia mwaliko wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Taifa hilo Mhe. WANG Yi. 

Ziara hii mbali na kudumisha ushirikiano wa kidiplomasia wa kihistoria uliopo baina ya mataifa haya mawili ni muendelezo wa utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi ikilenga kufuatilia utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa wakati wa ziara ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliyoifanya nchini humo Novemba 2 - 4, 2022.

Akiwa China, Waziri Makamba anatarajia kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Mhe. WANG Yi ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa China. 

Miongoni mwa masuala muhimu yanayotarajiwa kujadiliwa kwenye ziara hii ni pamoja na maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) unaotekelezwa na kampuni ya CCECC, maboresho ya reli ya TAZARA na uwekezaji kwenye mradi wa uchimbaji wa chuma wa Liganga na Mchuchuma. 

Aidha, Waziri Makamba na mwenyeji wake wanatarajia kujadili masula mbalimbali muhimu ya ushirikiano baina ya China na Afrika yanayoratibiwa kupitia Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) ikiwemo masuala ya ulinzi na usalama, kuelekea Mkutano wa Kilele wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwa hilo unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu 2024. 

Vilevile Makamba atafanya mazungumzo na viongozi wengine waandamizi wa Serikali na wakuu wa mashirika ya kimkakati wakiwemo Rais wa Shirika la Ushikiano wa Maendeleo ya Kimataifa (CIDCA), Rais wa Benki ya EXIM ya China na kampuni ya HUAWEI.

Kadhalika, Waziri Makamba atafanya mazungumzo na Mabalozi wa Nchi Wanachama wa SADC wanaziwakilisha nchi zao nchini China. 

Mwaka huu, Tanzania na China zimetimiza miaka 60 ya ushirikiano wa kidiplomasia ulioanzishwa na waasisi wa mataifa hayo mawili, Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Mao Zedong



Wednesday, May 15, 2024

TANZANIA NA UFARANSA KUIMARISHA DIPLOMASIA YA UCHUMI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba amekutana kwa mazungumzo na Waziri wa Biashara, Uchumi, Nchi zinazozungumza Kifaransa na Wafaransa waishio nje ya nchi, Mhe. Frank Reister katika ofisi za Wizara jijini Paris, Ufaransa tarehe 15 Mei, 2024.

Mawaziri hao wamejadili kuhusu namna bora ya kuimarisha ushirikiano kwenye masuala ya biashara na uwekezaji ambapo, Mhe. Makamba ametumia fursa hiyo kuukaribisha Ujumbe wa Wafanyabiashara utakaongozwa na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Ufaransa (MEDEF) unaotarajia kushiriki kwenye Jukwaa la Biashara linalotarajia kufanyika kuanzia tarehe 27 hadi 29 Mei, 2024 jijini Dar es Salaam na Zanzibar. 

Aidha, kuelekea mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika (CAN 2027), Mhe. Makamba amekaribisha makampuni ya Ufaransa kuja kuwekeza jijini Arusha kwenye nyanja mbalimbali ikiwemo nyumba za malazi na kumbi za mikutano. 

Tanzania inatarajia kuwa Mwenyeji mwenza wa Mashindano ya CAN 2027. Ufaransa kwa upande wao wameonesha nia ya kuwekeza ili kuwezesha Tanzania kuhudumia wageni watakaokuja wakati wa mashindano hayo.

Mhe. Riester pia amewakaribisha wafanyabiasha na wawekezaji wa Tanzania kuwekeza nchini Ufaransa kwa kuwa nchi hiyo imeweka mazingira mazuri ya uwekezaji.

Mhe. Waziri Makamba ameishukuru Serikali ya Ufaransa kwa kuendelea kuwa mshirika mzuri wa maendeleo nchini Tanzania kwa kufadhiri miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo nishati, miundombinu ya usafirishaji, maji safi, kilimo na afya.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba akizungumza na Waziri wa Biashara za Nje, Uwekezaji, Nchi zinazozungumza Kifaransa na Wafaransa Waishio Nje ya Nchi, Mhe. Franck Riester katika ofisi za Wizara hiyo jijini Paris, Ufaransa tarehe 15 Mei, 2024. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Noel Kaganda. 

Kulia ni wa Waziri wa Biashara za Nje, Uwekezaji, Nchi zinazozungumza Kifaransa na Wafaransa Waishio Nje ya Nchi, Mhe. Franck Riester akizungumzia utekelezaji wa masuala mbalimbali ya biashara na uwekezaji ambayo kampuni za kifaransa zimewekeza nchini Tanzania.

Kutoka kulia, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba, Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Mhe. Ali Mwadini na Afisa Mambo ya Nje, Bw, Athuman Kikwete wakifatilia mazungumzo.

Mheshimiwa Waziri Makamba akisalimiana na Mheshimiwa Waziri Riester baada ya kuwasili ofisini kwake kwa mazungumzo.

Mheshimiwa Waziri Makamba akiteta jambo na Mheshimiwa Waziri Riester baada ya kuwasili ofisini za Wizara jijini Paris, Ufaransa.

Mheshimiwa Waziri Makamba akikaribishwa na Mheshimiwa Waziri Riester baada ya kuwasili ofisini za Wizara hiyo jijini Paris, Ufaransa

Mheshimiwa Waziri Makamba akisalimiana na maafisa walioambatana na  Mheshimiwa Waziri Riester katika mazungumzo.

Mazungumzo yakiendelea.

Picha ya pamoja.



WAZIRI MAKAMBA AONGOZA MJADALA KUHUSU "NISHATI SAFI YA KUPIKIA KUWA SERA YA KIPAUMBELE BARANI AFRIKA"

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) ameongoza majadiliano kuhusu "Nishati Safi ya Kupikia kuwa Suala la Kipaumbele barani Afrika" uliofanyika katika Makao Makuu ya UNESCO jijini Paris, Ufaransa leo tarehe 14 Mei, 2024.

Aliongoza majadiliano hayo na mwenyekiti mwenza Mhe. Mary Robinson, Mwenyekiti wa Wazee na Rais Mstaafu wa Ireland.

Mjadala huo pamoja na masuala mengine ulijadili kwa kina umuhimu wa kila Nchi kuweka mikakati ya kisera ili kuhakikisha nishati safi ya kupikia inapatikana kwa uhakika na kwa gharama nafuu ili kuwafikia wananchi wote.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) akiongoza majadililiano kuhusu "Nishati Safi ya Kupikia kuwa Suala ya Kipaumbele Barani Afrika" uliofanyika jijini Paris, Ufarasa tarehe 14 Mei, 2024.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Januari Makamba pamoja na Mwenyekiti mwenza na Rais Mstaafu wa Ireland Mhe. Mary Robinson wakifatilia majadiliano.

Wakipongezana kwa kuongoza mjadala.

Majadiliano yakiendelea.


TANZANIA NA UFARANSA ZASAINI TAMKO LA PARIS

Tanzania na Ufaransa zimesaini Tamko la Paris (Paris Declaration) katika kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia na kiuchumi uliopo baina ya nchi hizo mbili.

Tamko hilo limesainiwa leo tarehe 14 Mei, 2024 jijini Paris Ufaransa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba na Waziri wa Ufaransa anayeshughulikia Maendeleo ya Kimataifa, Mhe. Chrysoula Zacharopoulou.

Maeneo ya ushirikiano yaliyosainiwa ni pamoja na Nishati na mabadiliko ya tabianchi, usafirishaji na maendeleo ya miundombinu, usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawake.

Hafla ya utiaji saini imeshuhudiwa na Mabalozi wanaowakilisha katika hizo, Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Mhe. Ali Jabir Mwadini, Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Nabil Hajlaoui, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Noel Kaganda na Maafisa wengine Waandamizi walioambatana na Viongozi hao wawili.



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (kushoto) pamoja na Waziri wa Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa ufaransa, Mhe. Chrysoula Zacharopoulou wakisaini Tamko la Paris tarehe 14 Mei, 2024.

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ufaransa, Mhe. Ali Jabir Mwadini (kati), Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Noel Kaganda na Afisa Mambo ya Nje, Bw. Athuman Kikwete wakishuhudia utiaji saini wa Tamko la Paris.

Hafla ya utiaji saini Tamko la Paris.

Picha ya Pamoja 

Waheshimiwa Mawaziri wakibadilisha Hati za Tamko baada ya kutia saini.

Picha ya pamoja waheshimiwa Mawaziri na Waheshimiwa Mabalozi waoawakilisha nchini Ufaransa na Tanzania.

Mhe. Waziri Makamba na Mhe. Chrysoula Zacharopoulou wakiteta baada ya kukamilisha zoezi la utiaji saini.


Tuesday, May 14, 2024

RAIS SAMIA "BAJETI KUU YA SERIKALI KUWEZESHA NISHATI SAFI YA KUPIKIA NA WANAWAKE"

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefungua Mkutano wa Nishati Safi ya Kupikia Barani Afrika unaofanyika katika Makao Makuu ya UNESCO jijini Paris, Ufaransa tarehe 14 Mei, 2024.

Katika hotuba yake ya ufunguzi Mheshimiwa Rais Samia amesisitiza umuhimu wa nishati safi kwa Nchi za Afrika ili kudhibiti madhara yatokanayo na kadhia za kukosa nishati hiyo kama vile, uharibifu wa mazingira unaosababishwa na ukataji wa miti na uchomaji wa mkaa, unyanyasaji wa kijinsia na vifo kwa wanawake na watoto.

Aidha, amesema Tanzania imelipa kipaumbele suala la nishati safi ya kupikia ambapo imeongeza bajeti ya Serikali ili kuwezesha upatikanaji wa nishati safi kwa urahisi, gharama nafuu pamoja na uwekezaji katika teknolojia. Vilevile  itasimamia utekelezaji wa sera, mikakati na miongozo ya matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa ustawi wa jamii.

"Serikali imelipa umuhimu suala la nishati safi ya kupikia ambapo katika kuyafikia malengo hayo bajeti kuu ya Serikali imeweka kipaumbele katika kuwezesha upatikanaji wa nishati hiyo sambamba na kuwainua wanawake." Rais Samia

Rais Samia ameongoza mkutano huo akiwa pamoja na wenyeviti wenza: Waziri Mkuu wa Norway, Mhe. Jonas Gahr Støre; Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kimataifa ya Nishati, Dkt. Fatih Birol; na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dkt. Akinwumi Adesina.

Pamoja na masuala mengine, mkutano huo una lengo la kufanya matumizi ya nishati safi ya kupikia kuwa suala la kipaumbele katika agenda ya kimataifa; kuainisha hatua madhubuti za kisera zitakazoharakisha matumizi ya nishati safi ya kupikia; na kutoa fursa kwa washiriki kutoa ahadi za kifedha, sera, na ubia ili kufikia azma ya kukuza matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Kupitia mkutano huo, jumla ya ahadi za kiasi cha USD 2.2 bilioni zimekusanywa  ili kusaidia katika usimamizi wa sera na miongozo mbalimbali na uwekaji wa miundombinu itakayowezesha upatikanaji wa nishati safi.

Ikumbukwe  kuwa, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeshapiga hatua katika jitihadi za kitaifa za kuhakikisha nishati safi ya kupikia inapatikana nchini kupitia Mkakati wa Taifa wa Nishati Safi ya Kupikia ulizozinduliwa tarehe 8 Mei, 2024 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akitambulika kama Kimara wa Nishati Safi ya Kupikia Ulimwenguni.

Matarajio ya kitaifa ni kuwa ifikapo mwaka 2034, Tanzania itakuwa imepiga hatua katika kukuza kiwango cha matumizi ya nishati safi ya kupikia, hali itakayowezesha utunzaji wa mazingira, kuboresha afya na ustawi wa jamii, kukuza uchumi na kusaidia kutimiza Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa ya Mwaka 2030.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan,akihutubia wakati wa hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi Kuhusu Nishati Safi ya Kupikia barani Afrika unaofanyika katika Makao Makuu ya UNESCI jijini Paris, Ufaransa tarehe 14 Mei, 2024.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) akifuatilia majadiliano katika  Mkutano wa Nishati Safi ya Kupikia barani Afrika uliofanyika Makao Makuu ya UNESCO jijini Paris, Ufaransa tarehe 14 Mei, 2024.

Mkutano ukiendelea

Ujumbe kutoka sekta binafsi ukifatilia mkutano huo.

Picha ya pamoja ya meza kuu baada ya ufunguzi wa mkutano huo.




Monday, May 13, 2024

RAIS SAMIA AWASILI PARIS, UFARANSA KWA ZIARA YA KIKAZI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili jijini Paris, Ufaransa tarehe 12 Mei, 2024 na kupokelewa na Viongozi Waandamizi wa Serikali, Watumishi wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ufaransa na Watanzania wanaoishi nchini humo.


Rais Samia ataongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi kuhusu Nishati Safi ya kupikia barani Afrika utakaofanyika Makao Makuu ya UNESCO na kuhudhuriwa na Marais wengine wa Afrika akiwemo Rais wa Jamhuri ya Sierra Leone, Mhe. Julius Maada Bio na Rais wa Ghana, Mhe. Nana Akufo-Addo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea maua kutoka kwa mtoto Khaira Ali Jabiri mara baada ya kuwasili jijini Paris, Ufaransa kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi Kuhusu Nishati Safi ya Kupikia utakaofanyika tarehe 14 Mei, 2024

Mhe. Rais Samia akisalimiana na Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. Suleiman Jaffo (Mb.) mara baada ya kuwasili jijini Paris, Ufaransa tarehe 12 Mei, 2024.

Mhe, Rais Samia akisalimia na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga (Mb.) mara baada ya kuwasili jijini Paris, Ufaransa tarehe 12 Mei, 2024.

Sehemu ya watumishi wa ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ufaransa wakisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan mara baada ya kuwasili jijini Paris, Ufaransa tarehe 12 Mei, 2024.






 

Sunday, May 12, 2024

WAZIRI MAKAMBA AONGOZA KIKAO CHA MAANDALIZI YA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI KUHUSU NISHATI SAFI YA KUPIKIA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba akiongoza kikao cha maandalizi cha ujumbe wa Tanzania uliopo jijini Paris, Ufaransa kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi kuhusu Nishati Safi ya Kupikia utakaofanyika tarehe 14 Mei, 2024 katika Makao Makuu ya UNESCO.

Lengo la mkutano huo ni kulifanya suala zima la nishati safi ya kupikia kuwa la kipaumbele katika agenda ya kimataifa; kuanisha hatua madhubuti za kisera zitakazoharakisha matumizi ya nisahti safi ya kupikia na kutoa fursa ya washirika kutoa ahadi za kifedha, sera na ubia ili kufikia azma ya kukuza matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Kikao hicho cha maandalizi kimefanyika katika ofisi za ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ufaransa tarehe 12 Mei, 2024.

Kutoka kushoto ni Mshauri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania- Diplomasia, Balozi Maulida Hassan, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Noel Kaganda na Mkuu wa Utawala na Fedha katika Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ufaransa, Bw. Amos Tengu wakifatilia kikao kilichofanyika katika ofisi za ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ufaransa tarehe 12 Mei, 2024. 


Wajumbe wa kikao hicho wakifatilia majadiliano.
Kikao kikiendelea. 

Kikao kikiendelea.