Thursday, May 2, 2024

BALOZI MBAROUK AFUNGUA MKUTANO WA NNE WA BARAZA LA WAFANYAKAZI LA WIZARA

Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk amefungua Mkutano wa Nne wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara uliofanyika jijini Arusha.



Akifungua Mkutano huo, Mhe. Balozi Mbarouk amewasihi  Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuendelea kubuni maeneo ya kimkakati ya ushirikiano ambayo yatakuza na kuendeleza ushawishi wa Tanzania katika majukwaa ya Kikanda na Kimataifa.



“Nichukue fursa hii kuwasihi kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia weledi na ubunifu, muendelee kubuni maeneo ya kimkakati ya ushirikiano ili kuimarisha uhusiano wa uwili, kikanda na Kimataifa kuendeleza ushawishi wa Tanzania katika majukwaa ya kimataifa,” alisisitiza Balozi Mbarouk.


Amesema Wizara inaandelea na kazi ya uandaaji wa Mkakati wa Kitaifa wa utekelezaji wa  Diplomasia ya Uchumi ambao kukamilika kwake kutachochea ufanisi na kuleta tija katika kukuza Ushirikiano wa kiuchumi na kijamii katika ngazi ya uwili, kikanda na kimataifa.

 


Amewataka wafanyakazi wa Wizara kuimarisha ushirikiano, uhusiano na maelewano miongoni mwao huku wakiendelea kufanya kazi kwa weledi, ujuzi wa hali ya juu ili kuleta tija na ufanisi kwa taifa.



Pia amewapongeza wajumbe wa Baraza kwa kazi nzuri ya kuwawakilisha wafanyakazi wengine katika Baraza hilo.



Awali akizungumza kwenye mkutano huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo amesema Wizara itaendelea kushughulikia changamoto mbalimbali za Wafanyakazi na kuboresha mazingira ya kazi ili kuhakikisha utekelezaji wa majukumu ya Wizara unakamilishwa kwa tija na ufanisi.

 


Naye Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Wizara, Bi Pili Sukwa ameawaasa Watumishi wa Wizara kuendelea kutii sheria, kanuni  taratibu na maelekezo mbalimbali yanayotolewa na Viongozi wa Wizara na Serikali kwa ujumla ili kwa pamoja kufikia malengo tarajiwa.



Mkutano huo, pamoja na mambo mengine umepokea taarifa mbalimbali za utekelezaji wa majukumu ya Wizara pamoja na kupokea na kujadili Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kabla ya kuwasilishwa kwenye Bunge la Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania.


Naibu Waziri wa Mambo na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) akifungua Mkutano wa Nne wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara lililofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) tarehe 02 Mei, 2024

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi na Mwenyekiti wa Baraza   Baraza la Wafanyakazi la Wizara, Dkt. Samwel Shelukindo  akizungumza wakati wa Mkutano wa Baraza hilo lililofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) tarehe 02 Mei, 2024

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anyeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi akizungumza wakati wa Mkutano wa Nne wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara uliofanyika jijini AICC jijini Arusha tarehe 02 Mei 2024


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaibu Mussa  akichangia jambo wakati wa Mkutano wa Nne wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara uliofanyika jijini Arusha tarehe 02 Mei 2024

Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Chiku Kiguhe akiwasilisha taarifa kuhusu masuala ya Utawala kwa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wakati wa Mkutano wa Nne wa Baraza hilo uliofanyika AICC jijini Arusha tarehe 02 Mei 2024

Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano wa Nne wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara wakifuatilia mkutano huo katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) tarehe 02 Mei, 2024

Mjumbe wa Mkutano wa Nne wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara Bw. Emmanuel Mwasabwite akichangia kitu wakati wa mkutano huo katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) tarehe 02 Mei, 2024


Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano wa Nne wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara wakifuatilia mkutano huo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) tarehe 02 Mei 2024
Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano wa Nne wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara wakifuatilia mkutano huo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) tarehe 02 Mei, 2024

Meza Kuu wakifuatilia Mkutano wa Nne wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara wakifuatilia mkutano huo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) tarehe 02 Mei, 2024

Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano wa Nne wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara wakifuatilia mkutano huo katika  Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) tarehe 02 Mei, 2024

Sekretarieti ya Mkutano wa Nne wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara wakinukuu masuala mbalimbali yaliyojadiliwa katika mkutano wa nne wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) tarehe 02 Mei, 2024

Mgeni rasmi ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (wa tano kushoto walioketi) pamoja na Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo (wa nne kushoto walioketi) wakiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Mkutano wa Nne wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara  baada ya ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) tarehe 02 Mei 2024  



 

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.