Friday, May 24, 2024

MIAKA 20 YA BARAZA LA AMANI NA USALAMA AFRİKA RAIS MSTAAFU WA NIGERIA MHE. OBASANJO AWASILI NCHINI

Rais Mstaafu wa Nigeria Mhe. Olusegun Obasanjo akiwa katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam alipowasili nchini tarehe 24 Mei 24 kwa ajili ya kushiriki maadhimisho ya miaka 20 ya Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika.

 

Rais Mstaafu wa Nigeria Mhe. Olusegun Obasanjo akiwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Said Shaibu Mussa katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam alipowasili nchini tarehe 24 Mei 24 kwa ajili ya kushiriki maadhimisho ya miaka 20 ya Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika.

Rais Mstaafu wa Nigeria Mhe. Olusegun Obasanjo akiwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Said Shaibu Mussa katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam alipowasili nchini tarehe 24 Mei 24 kwa ajili ya kushiriki maadhimisho ya miaka 20 ya Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika

 


 

Rais Mstaafu wa Nigeria Mhe. Olusegun Obasanjo amewasili nchini leo tarehe 24 Mei 24 kwa ajili ya kushiriki maadhimisho ya miaka 20 ya Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini  Dar es Salaam Mhe. Obasanjo alilakiwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afrika Mashariki Balozi Said Shaib Mussa.

Mhe. Obasanjo ni miongoni mwa Marais Wastaafu na viongozi wengine wa Nchi za Afrika, Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa ambao watashiriki maadhimisho hayo yatakayofanyika nchini tarehe 25 Mei,2024.

Maadhimisho ya Miaka 20 ya Baraza hilo yataongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC)

 
Uenyeji wa Tanzania katika maadhimisho hayo unatokana na maamuzi ya Mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika uliofanyika mwezi Februari 2024 jijini Addis Ababa, Ethiopia ambapo Tanzania ilichaguliwa tena kuhudumu kwenye Baraza hilo kwa muhula mwingine wa miaka miwili hadi mwaka 2026.
 
Baraza la Amani na Usalama ni chombo cha juu cha maamuzi kuhusu masuala ya amani na usalama kwenye Umoja wa Afrika likiwa na jukumu la kuzuia kutokea kwa migogoro, kusuluhisha au kukabiliana nayo pale inapojitokeza.
 
Nchi 15 tu kati ya nchi 55 wanachama wa Umoja wa Afrika ndio wajumbe wa Baraza hilo na  wajumbe wa sasa ni; Tanzania, Uganda , Djibout, Cameroon, DRC,  Equatorial Guinea ,Afrika Kusini, Angola, Botswana, Cote d’Ivoire , Gambia, Nigeria,  Sierra Leone,  Misri na Morocco.
 
Kwa mwezi huu wa Mei, Tanzania ni Mwenyekiti wa Baraza hilo na kuwa Mjumbe kwenye Baraza hili ni ishara ya kuheshimika na kuaminika kwa nchi na Katika nafasi ya Uenyekiti Tanzania inajukumu la kusimamia shughuli zote zinazohusu Baraza, ikiwemo kufuatilia kwa karibu hali ya ulinzi na usalama kwenye Bara la Afrika, kutoa miongozo ya kushughulikia na masuala ya kiusalama pale inapobidi na pia kuandaa ratiba na kuongoza vikao vya Baraza.
 
Katika maadhimisho hayo Tanzania kwa kushirikiana na Sekretarieti ya Baraza iliaandaa shughuli mbalimbali zilizofanyika  kila wiki katika mwezi Mei ambazo zilibeba dhima mahsusi za: Usuluhishi na majadiliano; masuala ya mahitaji ya kibinadamu,amani na usalama; ulinzi kwa Watoto na kusaidia misheni za amani.
 
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ya Miaka 20 ya Baraza la Usalama la Umoja wa Afrika ni; ‘’Miaka 20 ya Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika ikiwa chombo cha Maamuzi: Miongo miwili ya Afrika ya tuitakayo.
 
Maadhimisho haya, yanatoa fursa kwa Waafrika wote wenye kuitakia mema Afrika kutoa maoni yao ya kuliimarisha Baraza ili liweze kushughulikia changamoto za kiusalama barani Afrika ambapo wageni takriban 120 kutoka nchi mbalimbali wanatarajiwa kuhudhuria maadhimisho hayo
 
Mbali na Mhe. Obasanjo, Rais Rais Mstaafu wa Burundi, Mhe. Domitien Ndayizeye, Rais Mstaafu wa Msumbiji, Mhe. Joachim Chissano na Rais Mstaafu wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete pia watahudhuria maadhimisho hayo ambayo yatahitimishwa kwa kutolewa kwa Tamko la Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.