Tuesday, May 28, 2024

MABALOZI KUPIMWA UTENDAJI KAZI KWA KUTUMIA VIGEZO/VIASHIRIA MAHSUSI (KPIs)



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) ameeleza kuwa Wizara  imeanzisha utaratibu maalum wa kupima utendaji kazi wa Balozi na Konseli Kuu kwa kutumia vigezo/viashiriki wakati akiwasilisha makadirio ya bajeti ya Wizara Bungeni jijini Dodoma tarehe 28 Mei, 2024.

Mhe. Makamba ameeleza kuwa ili kuhakikisha Wizara inakwenda sambamba na maono na matarajio ya Mheshimiwa Rais katika utekelezaji wa majukumu yake, mnamo mwezi Aprili mwaka huu Wizara ilifanya kikao na Mabalozi wote, Makonseli Wakuu, Wakuu wa Utawala na Fedha katika Balozi zetu zote duniani pamoja na viongozi na Menejimenti ya Wizara mjini Kibaha, Mkoani Pwani.


Kikao hicho kilikuwa na azma kuu ya kujitathmini na kuweka mikakati ya pamoja ya kuboresha utendaji wetu na wajumbe wa mkutano huo walipata heshima ya kumsikiliza Mheshimiwa Rais na viongozi wengine Serikalini.


Kufuatia kikao hicho, Wizara imeanzisha utaratibu mpya wa kupima utendaji kazi wa Mabalozi wetu nje ya nchi ili kuhakikisha kuwa uwakilishi wetu kupitia Balozi zetu unaleta mchango unaopimika kwenye malengo ya wizara na nchi kwa ujumla.  
 
Mfumo huu utaanza kutumika kwenye mwaka ujao wa fedha 2024/2024.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.