Tuesday, May 28, 2024

DIPLOMASIA YA UCHUMI YAPEWA MSUKUMO MPYA- WAZIRI MAKAMBA


 


TODAY
MIRADI MIKUBWA YA VITEGA UCHUMI KATIKA BALOZI YAJA Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeeleza kuwa inaratibu na kusimamia Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo katika viwanja vya Balozi za Tanzania nje wakati wa uwasilishaji wa makadirio ya bajeti yake bungeni jijini Dodoma tarehe 28 Mei, 2024. Ufafanuzi huo umetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) ambapo ameeleza kuwa katika mwaka wa fedha 2023/2024, Wizara iliidhinishiwa jumla ya shilingi 17,887,608,000 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo. Kati ya fedha hizo, shilingi 8,400,000,000 ni kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa majengo kwenye balozi zetu. Hadi kufikia mwezi Aprili, 2024 Wizara imepokea na kutumia fedha kutoka…
Read more
16:44
16:45
MUUNDO WA WIZARA KUBORESHWA ILI KUAKISI MAHITAJI YA SASA Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) amelieleza Bunge kuhusu jitihada mbalimbali zinazofanywa na Wizara hiyo katika kuboresha utendaji wake. Ufafanuzi huo umetolewa wakati wa uwasilishaji wa makadirio ya bajeti ya wizara uliofanyika bungeni jijini Dodoma tarehe 28 Mei, 2024. Aidha, Waziri Makamba ameeleza kuwa katika kufanikisha hilo Wizara iliunda timu ya ndani ya kujitathmini ambayo ripoti yake iliwasilishwa kwa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na baadae katika Baraza la Mawaziri. Pia, Wizara inafanya maboresho ya muundo kwa lengo la kuongeza ufanisi wenye tija ili kuendana na mahitaji halisi ya wakati wa sas…
Read more
16:46

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) ameeleza kuwa msisitizo wa Sera ya Mambo ya Nje ni Diplomasia ya Uchumi wakati akiwasilisha makadirio ya Hotuba ya Bajeti ya Wizara Bungeni jijini Dodoma. 
 
Katika hotuba hiyo amelifahamisha Bunge kuwa, Wizara imekamilisha rasimu ya awali ya Mkakati wa Kitaifa wa Utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi itakayotoa mwongozo wa utekelezaji wa majukumu yake. 
 
"Mkakati huo umeainisha maeneo saba ya kipaumbele ambayo Wizara itayatilia mkazo katika utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi”, alisema Waziri Makamba. 
 
Maeneo hayo ni pamoja na kuvutia uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje, kutafuta masoko ya bidhaa za Tanzania nje ya nchi, kuvutia watalii kuja Tanzania, kutafuta misaada na mikopo ya masharti nafuu kutoka nje, kutafuta fursa za ajira na masomo kwa Watanzania nje ya nchi, kujenga taswira nzuri ya nchi yetu kimataifa, kujenga wezo wa kitaasisi wa Wizara, na Wizara na Taasisi nyingine kusimamia vizuri utekelezaji wa Mkakati wa Diplomasia ya Uchumi. 
 
Aidha, kukamilika kwa mkakati huo kutaiwezesha Serikali na wadau wote kutambua majukumu yao katika mnyororo wa hatua za kutekeleza diplomasia ya uchumi kwa kuzingatia vipaumbele vya taifa. 
 
Utekelezaji wa diplomasia ya uchumi umeiwezesha nchi kuingia makubaliano mbalimbali yenye tija kwa Taifa. Makubaliano hayo yamewezesha kupata mikopo nafuu na misaada, kuvutia watalii, kupata masoko ya bidhaa zetu, kuvutia wawekezaji na wabia wa aina mbalimbali wa maendeleo yetu. Mafanikio mengine yaliyopatikana ni; kupata masoko ya bidhaa na huduma nje ya nchi, kuwezesha uagizaji bidhaa na huduma muhimu kutoka nje ya nchi ili kukidhi mahitaji ya ndani; na kuvutia uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje. 
 
Wizara imefanikisha jukumu hilo kwa kushirikiana na Wizara za kisekta, Taasisi za Umma na Sekta Binafsi ambapo zimekuwa zikiratibu makongamano mbalimbali ya biashara na uwekezaji yanayofanyika pamoja na ziara za Mheshimiwa Rais nchi za nje. 
 
Vilevile, kuratibu ziara za watendaji wa serikali katika nchi na kuzungumzia masuala ya kiuchumi, biashara na uwekezaji kwa wadau mbalimbali wa maendeleo.



No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.