Thursday, March 31, 2016

Ubalozi wa Pakstan nchini waadhimisha miaka 76 ya uhuru

 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi akitoa hotuba kama mgeni rasmi katika hafla ya maadhimisho ya miaka 76 ya Taifa la Jamhuri ya Kiislamu ya Pakistan. Katika hotuba yake Balozi Mwinyi alielezea historia ya uhusiano wa kidiplomasia baina ya mataifa hayo ulioanza tangu mwaka 1967 chini ya usimamizi wa Waasisi wa nchi hizo. Hafla hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Golden Tulip,Jijini Dar es Salaam.  
Kaimu Balozi wa Pakistan, Bw. Amir Muhammad Khan  pia alipata fursa ya kuhutubia wageni waalikwa ambapo alieleza nia ya wazi ya Serikali ya Pakistan kuzidi kukuza ushirikiano wa kiplomasia na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwamba Pakistan imekuwa ikishiriana na Tanzania katika  sekta ya usafiri  upande wa reli, taasisi za kifedha na ushirikiano katika masuala ya ulizi na usalama. 
 Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Balozi Mbelwa Kairuki (kushoto) na Balozi wa India nchini Mhe. Sandeep Arya wakifuatilia hotuba ya Kiamu Balozi wa Pakistan nchini (hayupo pichani)
Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salim kushoto akiwa na sehemu ya mabalozi na wageni waalikwa waliohudhuria maadhimisho hayo.
Sehemu nyingine ya mabalozi na wageni wakifuatilia hotuba.
Jumuiya ya watu wa Jamhuri ya kiislam ya Pakistan wanaoishi nchini Tanzania pia walishiriki katika hafla hiyo.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Mhe. Alhaji Ally Hassan Mwinyi akishiriki katika kusherehekea hafla hiyo pamoja na Naibu Katibu Mkuu, Balozi  Mwinyi na Kaimu Balozi wa Pakistan nchini, Bw. Khan
Wakikata keki kusherekea maadhimisho hayo

Kaimu Balozi wa Pakistan,Bw. Khan alipokuwa akikaribisha wageni walioshiriki katika hafla ya maadhimisho ya miaka 76 ya Jamhuri ya Kiislamu ya Pakistan

Wageni waalikwa waliohudhuria maadhimisho hayo

MWANADIASPORA MBAROUK RASHID AKABIDHI MSAADA WA VIFAA KWA AJILI YA WATANZANIA WALEMAVU KWA NAIBU BALOZI WA TANZANIA NCHINI SWEDEN

Naibu Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Bw. Andy Mwandembwa amepokea msaada wa vifaa mbali mbali kwa ajili ya watanzania wenye ulemavu wa ngozi wanaofanya shughuli za ujasiriamali kutoka kwa Mwanadiaspora mkereketwa anayeishi Sweden, Bw. Mbarouk Rashidi. Msaada huo unajumisha vifaa vya ufundi wa karakana, nguo, vitabu na vitendea kazi vingine.

Tanzania yapokea msaada wa shilingi bilioni 116.4 kutoka Japan.


Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) akibadilishana hati ya makubaliano walizosaini na Serikali ya Japan utakaoitakayoiwezesha Tanzania kupata kiasi Yen Bilioni 6 ambazo ni sawa na Sh. Bilioni 116.4 za Kitanzania. Kulia ni Balozi wa Japan nchini Tanzania Bw. Masaharu Yoshida.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) akisaini hati ya makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Japan leo jijini Dar es salaam ambao utaiwezesha Tanzania kupata kiasi Yen Bilioni 6 ambazo ni sawa na Sh. Bilioni 116.4 za Kitanzania. Kulia ni Balozi wa Japan nchini Tanzania Bw. Masaharu Yoshida.


Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kusaini hati ya makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Japan leo jijini Dar es salaam ambao utaiwezesha Tanzania kupata kiasi Yen Bilioni 6 ambazo ni sawa na Sh. Bilioni 116.4 za Kitanzania.
Balozi wa Japan nchini Tanzania Bw. Masaharu Yoshida akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kusaini hati ya makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Japan leo jijini Dar es salaam ambao utaiwezesha Tanzania kupata kiasi Yen Bilioni 6 ambazo ni sawa na Sh. Bilioni 116.4 za Kitanzania. 


===========================================

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesaini hati mbili za makubaliano na Serikali ya Japan itakayoiwezesha Tanzania kupata kiasi Yen Bilioni 6 ambazo ni sawa na Sh. Bilioni 116.4 za Kitanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusaini hati hizo, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile alisema mkataba wa kwanza utasaidia katika kukamilisha bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/17.

Dkt. Likwelile alisema kuwa msaada huo unalenga kuweka mazingira rafiki ya kwa wafanyabiashara, kuboresha masoko na kuwezesha mazingira ya ushindani katika utengenezaji wa ajira nchini.

Mkataba wa pili  unahusu masuala ya kiufundi  yatakayotumika katika kufanya marekebisho ya mkataba uliosainiwa  Octoba 20, 1966, kwa
kuzingatia sheria nyingi zimebadilika, kusainiwa kwa hati hiyo ya makubaliano itasaidia kutabadilisha baadhi ya vifungu vyenye jina Tanzania na kuweka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kujumuisha pande zote mbili za Muungano katika kutekeleza miradi ya maendeleo nchini.

Aidha, makubaliano hayo yatasaidia kubadilisha baadhi ya vipengele vya mkataba uliopita ikiwemo kipengele cha usambazaji wa madawa ili kuweza kukidhi mahitaji ya sasa ya wataalamu kutoka nchini Japan kuweza kuja kufanya kazi za kujitolea hapa nchini Tanzania.
Katibu Mkuu Dkt. Likwelile ameishukuru Serikali ya Japan na kusisitiza kuwa fedha hizo zitatumika kama ilivyopangwa ili kuweza kuwa na tija na kuwaletea maendeleo Watanzania.

Naye Balozi wa Japan nchini Tanzania Bw. Masaharu Yoshida amesema kuwa Serikali ya Japan ina imani kuwa ushirikiano uliopo baina ya nchi hizi mbili utasaidia kukuza maendeleo ya uchumi na kijamii.

Balozi Yoshida amesema kuwa Serikali ya Japani inaunga mkono juhudi za Serikali inayo ongozwa na Rais Dkt. John Magufuli katika masuala ya viwanda na mazingira mazuri yanayovutia wawekezaji kuwekeza nchini Tanzania.


Adha amesema kuwa Japan itaendelea kuwaleta vijana wanaojitolea katika sekta ya uchumii na ya kijamii jambo limekuwa likitekelezwa tangu mwaka 1969 ambapo hadi sasa idadi ya vijana hao wa kujitolea imefikia zaidi ya 1500.