Thursday, March 31, 2016

Ubalozi wa Pakstan nchini waadhimisha miaka 76 ya uhuru

 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi akitoa hotuba kama mgeni rasmi katika hafla ya maadhimisho ya miaka 76 ya Taifa la Jamhuri ya Kiislamu ya Pakistan. Katika hotuba yake Balozi Mwinyi alielezea historia ya uhusiano wa kidiplomasia baina ya mataifa hayo ulioanza tangu mwaka 1967 chini ya usimamizi wa Waasisi wa nchi hizo. Hafla hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Golden Tulip,Jijini Dar es Salaam.  
Kaimu Balozi wa Pakistan, Bw. Amir Muhammad Khan  pia alipata fursa ya kuhutubia wageni waalikwa ambapo alieleza nia ya wazi ya Serikali ya Pakistan kuzidi kukuza ushirikiano wa kiplomasia na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwamba Pakistan imekuwa ikishiriana na Tanzania katika  sekta ya usafiri  upande wa reli, taasisi za kifedha na ushirikiano katika masuala ya ulizi na usalama. 
 Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Balozi Mbelwa Kairuki (kushoto) na Balozi wa India nchini Mhe. Sandeep Arya wakifuatilia hotuba ya Kiamu Balozi wa Pakistan nchini (hayupo pichani)
Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salim kushoto akiwa na sehemu ya mabalozi na wageni waalikwa waliohudhuria maadhimisho hayo.
Sehemu nyingine ya mabalozi na wageni wakifuatilia hotuba.
Jumuiya ya watu wa Jamhuri ya kiislam ya Pakistan wanaoishi nchini Tanzania pia walishiriki katika hafla hiyo.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Mhe. Alhaji Ally Hassan Mwinyi akishiriki katika kusherehekea hafla hiyo pamoja na Naibu Katibu Mkuu, Balozi  Mwinyi na Kaimu Balozi wa Pakistan nchini, Bw. Khan
Wakikata keki kusherekea maadhimisho hayo

Kaimu Balozi wa Pakistan,Bw. Khan alipokuwa akikaribisha wageni walioshiriki katika hafla ya maadhimisho ya miaka 76 ya Jamhuri ya Kiislamu ya Pakistan

Wageni waalikwa waliohudhuria maadhimisho hayo

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.