Thursday, May 31, 2018

Wizara yakabidhiwa rasmi jukumu la kuisimamia Bodi ya Ushauri ya Masuala ya rushwa ya Umoja wa Afrika

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Adolf Mkenda akisaini hati ya kukubali rasmi kupokea jukumu la kuisimamia Bodi ya Ushauri kuhusu Masuala ya rushwa ya Umoja wa Afrika Mashariki. Kushoto ni Bw.Valentino Mlowola Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ambaye alikabidhi majukumu ya usimamizi wa Bodi hiyo kwa Wizara.

Makabidhiano hayo yalifanyika katika ofisi za Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa jijini Arusha .

Bodi hii yenye makao makuu yake jijini Arusha, Tanzania, tokea kuanzishwa kwake tarehe 30/01/2013 ilikuwa chini ya uangalizi wa TAKUKURU. 
 

Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Bw. Valentino Mlowola Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU wakifurahia jambo baada ya kuasaini hati za makabidhiano

Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akipokea nyaraka za Bodi ya Ushauri ya Masuala ya rushwa ya Umoja wa Afrika kutoka kwa  Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bw.Valentino Mlowola
Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Bw. Valentino Mlowola Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watendaji  na Watumishi wa Serikali, na Bodi ya Ushauri ya Masuala ya rushwa ya Umoja wa Afrika.

Mkutano wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji wafikiatamati


Mhe. Mhandisi Stella Manyanya Naibu Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji akifuatilia Mkutano wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji la Afrika Mashariki uliokuwa ukiendelea.

Mkutano huu ulilenga kujadili na kutolea ufumbuzi masuala mbalimbali yakiwemo ya kiforodha, ambayo yamekuwa kikwazo katika ufanyaji wa biashara za kuvuka mipaka katika Jumuiya.

Mkutano huu uliofanyika kuanzia tarehe 25 hadi 30 Mei, 2018 na ku
hudhuriwa na nchi zote wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki ulifikia tamati tarehe 30 Mei, 2018 jijini Arusha.
Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akizungumza kwenye Mkutano wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji uliofanyika jijini Arusha.
Kutoka kushoto ni Mhe. Dkt. Pindi Chana Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mhandisi Stella Manyanya (Mb) Naibu Waziri wa Biashara, Viwanda na Uwekezaji, na Bw. Benard Haule Kaimu Mkurugenzi wa Biashara, Uwekezaji, na Sekta za Uzalishaji wakifuatilia mkutano


Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akifuatilia Mkutano

Maza Kuu ikiongoza Mkutano wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji uliokuwa ukiendelea jijini Arusha
Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (kushoto) akisaini taarifa ya Mkutano wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara,Viwanda,Fedha na Uwekezaji. Kushoto Bw. Eliah Chilangazi Afisa Biashara kutoka Wizara ya Biashara, Viwanda, na Biashara



Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (kushoto), Mhe. Mhandisi Stella Manyanya (Mb) Naibu Waziri wa Biashara, Viwanda na Uwekezaji (Katikati), na Bw. Benard Haule Kaimu Mkurugenzi wa Biashara, Uwekezaji, na Sekta za Uzalishaji (kulia) wakishauriana jambo


Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mhe. Dkt. Pindi Chana Balozi wa Tanzania nchini Kenya wakifuatilia mkutano
Waheshimiwa Mawaziri, Mabalozi na Watendaji wa Serikali wa nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mkutano

Tuesday, May 29, 2018

Tanzania itaendelea kushiriki katika ulinzi wa amani duniani, Balozi Mahiga

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akihutubia katika maadhimisho ya miaka 70 ya Siku ya Walinda Amani Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Mashujaa vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam tarehe 29 Mei 2018.
 Siku ya Walinda Amani Duniani huadhimishwa tarehe 29 Mei ya kila mwaka ambapo kaulimbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu ni "Ulinzi wa Amani wa Umoja wa Mataifa: Miaka 70 ya huduma na kujitoa" (UN Peacekeeping: 70 Years of Service and Sacrifice).

Katika hotuba yake, Mhe. Waziri Mahiga alieleza kuwa yapata miaka 12 tangu Tanzania ianze kushiriki katika ulinzi wa amani chini ya bendera ya Umoja wa Mataifa. 

Pia akasisitiza Tanzania itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha inasaidia kupatikana kwa amani katika mataifa mengine kwakuwa hakuna taifa linaloweza kufanikiwa katika maendeleo pasipo kuwepo na amani ya uhakika. " Sio jambo rahisi kukubali kutoa uhai wako kwa ajili ya mtu mwingine lakini Tanzania itaendelea kuungana na mataifa mengine duniani katika kusaidia kupatikana kwa amani ya mataifa hayo" alisema Mhe. Mahiga.

Aidha, Katika kuwakumbuka Walinda Amani wote Duniani waliopoteza maisha wakati wakitekeleza majukumu yao, pamoja na kutoa heshima kwa wale ambao bado wanaendelea na jukumu la kulinda amani, Tanzania imepoteza jumla ya askari wapatao 30 ndani ya miaka 10, pia dunia imepoteza zaidi ya askari 3500 na kwa sasa Tanzania inajivunia kuwa na jumla ya askari wapatao 2,600 wanaohudumu katika misheni sita (6) za ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez akihutubia katika maadhimisho ya siku ya Walinda Amani Duniani ambapo alieleza pamoja na kuendelea kusimamia utekelezaji wa shughuli za maendeleo, Umoja wa Mataifa utaendelea kuhakikisha Dunia inakuwa mahali salama pa kuishi ili kuweza kuyafikia malengo ya maendeleo endelevu.

Mhe. Waziri Mahiga akiweka shada la maua katika Mnara wa Mashujaa uliopo Viwanja vya Mnazi Mmoja ikiwa ni sehemu ya kuenzi mchango wa Walinda Amani Duniani.
Wakitoa heshima kwa ajili ya kuwakumbuka Walinda Amani Duniani, waliosimama mbele kutoka kushoto ni Mhe. Waziri Mahiga akiwa na Mwakilishi kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Maj. Gen. Henry Kamunde, Bw. Alvaro Rodriguez na Mwakilishi kutoka Jeshi la Polisi Tanzania, Kamishna Nsato Marijani.
Mhe.Waziri Mahiga  akisalimiana na Askari walioshiriki katika Misheni za Ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa.

Mhe. Waziri Mahiga akisalimiana na sehemu nyingine ya Askari walioshiriki katika Misheni za Ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa.
Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Deusdedit Kaganda pamoja na askari kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Polisi Tanzania wakifuatilia hotuba ya Mgeni Rasmi.

Sehemu nyingine ya Askari na wageni waalikwa wakifuatilia hotuba ya Mgeni Rasmi.
Waheshimiwa Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa nchini wakifuatilia matukio mbalimbali katika maadhimisho hayo.
Sehemu nyingine ya Waheshimiwa  Mabalozi, Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa nchini na wageni waalikwa wakifuatilia matukio mbalimbali katika maadhimisho hayo.
Waheshimiwa Mabalozi na Wageni waalikwa wakifuatilia maadhimisho ya Siku ya Walinda Amani Duniani.
Gwaride la heshima kwa Mgeni Rasmi.
Askari wa JWTZ wakiingia viwanja vya Mnazi Mmoja.

Monday, May 28, 2018

Waziri Mahiga atembelea Ubalozi wa Palestina nchini

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Augustine Mahiga akisaini kitabu cha maombolezo ya Wapelestina waliouwa kwenye Ukanda wa Gaza hivi karibuni, Mhe.Waziri Mahiga alisaini kitabu hicho alipotembelea katika Ubalozi huo tarehe 28 Mei,2018, anayeshuhudia ni Balozi wa Palestina hapa nchini Mhe. Balozi Hazem Shabat.

 Mhe. Waziri Mahiga akipata maelezo kutoka kwa Mhe. Balozi Shabat kuhusu sanaa ya picha inayoelezea utamaduni wa Wapalestina, aliyesimama kushoto ni Naibu Balozi wa Palestina hapa nchini Bw.Derar Ghannam.

 Mhe. Waziri Mahiga akisisitiza jambo katika mazungumzo yaliyofanyika Ubalozini hapo, lengo la mazungumzo hayo pamoja na mambo mengine ni kuzidi kuboresha mahusiano yaliyopo kati ya Tanzania na Palestina.
 Mhe. Waziri Mahiga akiwa ameshikilia moja ya picha yenye maelezo ya kuhimiza haki ya Wapalestina  ya kuishi.
 Mhe. Balozi Shabat akimfafanulia jambo kwenye Kitabu alichomkabidhi Mhe. Waziri Mahiga kama zawadi, Kitabu hicho kinaelezea Historia ya Mji wa Yerusalem.



Mhe. Waziri Mahiga akiagana na mwenyeji wake baada ya mazungumzo.

Sehemu ya maelezo ya sanaa ya picha zilizopo Ubalozini hapo, picha hizi zinaelezea kuhusu Amani katika Palestina na Haki ya Kuishi ya Wapalestina.

Sunday, May 27, 2018

Naibu Katibu Mkuu Mambo ya Nje akutana na Balozi wa Argentina nchini



Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi akizungumza na Balozi wa Argentina nchini Mhe. Gomez Bustillo alipomtembelea Wizarani Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei 2018.

Balozi Mwinyi na Mhe. Bustillo wakijadili namna ya kuendeleza miradi ya maendeleo na kuongeza maeneo mapya ya ushirikiano baina ya mataifa hayo mawili.
Balozi Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Bustillo, kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Amerika na Ulaya, Bw. Jestas Nyamanga.




Saturday, May 26, 2018

Waziri Mahiga afanya mazungumzo na Balozi wa Denmark nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) akimkaribisha Balozi wa Denmark nchini Mhe. Einar Hebogard Jensen walipokutana katika ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei 2018.
 Mazungumzo yakiendelea. 

Mkutano wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji waendelea jijini Arusha

 Bw.Benard Haule Kaimu Mkurugenzi wa Biashara, Uwekezaji na
Sekta za Uzalishaji, akizungumza kwenye mkutano wa Baraza la
Kisekta la Mawaziri wa  Biashara, Viwanda,Fedha na Uwekezaji 

unaoendelea kufanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo katika

majengo ya ofisi za Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
jijini Arusha










     
Mkutano wa Kisekta wa Baraza la Mawaziri wa Biashara,Viwanda, Fedha na Uwekezaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unaendelea kufanyika jijini Arusha. Mkutano huu unafanyika kwa kipindi cha siku saba (7) kuanzia tarehe 25 hadi 30 Mei, 2018. Pamoja na mambo mengine yatakayojili, Mkutano huu unatarajia kufanya yafuatayo:-
  • Kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa maagizo  na maamuzi yaliyofanywa na mkutano uliopita wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji;
  • Kupokea na kajadili taarifa ya majadiliano ya awali ya bajeti ya Baraza la Mawaziri wa Fedha la Jumuiya ya Afrika Mashariki;
  • Kupokea na kujadili taarifa ya Kamati ya Forodha
  • Kupokea na kujadili taarifa ya Kamati ya Kisekta ya Biashara;
  • Kupokea na kujadili taarifa ya Kamati ya Mamlaka ya Ushindani;
  • Kupokea na kujadili taarifa ya Kamati ya Viwango ya Jumuiya ya Afrika Mashariki; na
  • Kupokea na kujadili taarifa kutoka Kamati ya Kisekta ya Viwanda.

Mkutano huu anafanyika katika ngazi tatu ambazo ni ngazi ya waalam, ngazi Makatibu Wakuu, na ngazi ya Mawaziri.

Mkutano huu umehudhuriwa na wajumbe kutoka nchi zote  wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki. 

Bw. Benard Haule Kaimu Mkurugenzi wa Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji akichangia wakati wa Mkutano wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda,Fedha na Uwekezaji unaondelea jijini Arusha

Bw. Raymond Agaba Kamishna wa Biashara za Ndani (kushoto) kutoka Jamhuri ya Uganda akiongoza mkutano. Kulia ni Bibi Flavia Busingye Afisa Mkuu wa Forodha,ufuatiliaji na utekelezaji kutoka Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki

Mkutano ukiendelea

Wednesday, May 23, 2018

Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki yapitishwa na Bunge


   
Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akisoma hotuba ya bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2018/2019 bungeni jijini Dodoma. 

Mapema leo Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepisha kiasi cha Shilingi Bilioni Mia Moja Sabini na Saba, Milioni Sita na Mia Mbili Thelathini na Mbili Elfu.

 Kati ya fedha hizo Shilingi Bilioni Mia Moja Sitini na Sita, Milioni Mia Sita na Sita, na Mia Mbili Thelathini na Mbili Elfu ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida, na Shilingi Bilioni Kumi na Milioni Mia Nne ni kwa ajili ya bajeti ya maendeleo.
Pro. Adolf F. Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,(wa kwanza kushoto) akifuatilia uwasilishwaji wa hotuba ya bajeti ya Wizara. Wa pili kutoka kushoto, ni Naibu Katibu Mkuu Balozi Ramadhani Mwinyi akifuatilia hotuba.

Sehemu ya Watendaji wa Wizara wakifuatilia hotuba ya bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2018/2019 iliyowasilishwa na kupishwa bungeni jijini Dodoma

Mhe.Balozi Dkt. Augustine Mahiga akijibu maswali bungeni mara baada ya kuwasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2018/2019

Mhe. Dkt. Susan Kolimba Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (kushoto), akifuatilia hotuba ya bajeti bungeni jijini Dodoma

Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akifafanua jambo mara baada ya kuwasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara.

Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akisalimiana na Dkt. Stergomena Tax Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) walipokutana katika viunga vya Bunge jijini Dodoma mara baada kuwasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara.

Mhe. Waziri Mahiga akijadili jambo na Mhe. Zitto Kabwe Mbunge wa Kigoma Mjini katika viunga vya Bunge jijini Dodoma mara baada ya kupitishwa kwa hotuba ya bajeti ya Wizara

Mhe. Waziri  Mahiga na Mhe. Naibu Waziri Kolimba wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Waheshimiwa Mabalozi na Watendaji wa Wizara waliohudhuria tukio la uwasilishwaji wa bajeti ya Wizara bungeni jijini Dodoma






HOTUBA YA MHESHIMIWA BALOZI DKT. AUGUSTINE PHILIP MAHIGA (MB), WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA BAJETI YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019



ORODHA YA VIFUPISHO
AF
Adaptation Fund
AfDB
African Development Bank
AfCFTA
African Continental Free Trade Area
AGOA
African Growth and Opportunity Act
AICC
Arusha International Conference Centre
AMISOM
African Union Mission to Somalia
APRM
African Peer Review Mechanism
BBC
British Broadcasting Corporation
CGTN
China Global Television Network
COMESA
Common Market for Eastern and

Southern Africa
COP
Conference of Parties
DW
Deutsche Welle
EAC
East African Community
EPA
Economic Partnership Agreement
FAO
Food and Agriculture Organization

FIB
Force Intervention Brigade

FOCAC
Forum on China-Africa Cooperation

ii



GCF
Green Climate Fund
GEF
Global Environment Facility
GIZ
The Deutsche Gesellschaft für
Internationale Zusammenarbeit GmbH

GPEDC
Global Partnership for Effective

Development Cooperation
IAEA
International Atomic Energy Agency
IGAD
Intergovernmental Authority on

Development
ILO
International Labour Organization
IMF
International Monetary Fund
IOM
International Organization for Migration
IORA
Indian Ocean Rim Association
JNICC
Julius Nyerere International Convention

Centre
KCB
Kenya Commercial Bank
KOICA
Korea International Cooperation Agency
LDCF
Least Developed Countries Fund









iii


MINUSCA                   United Nations Multidimensional Integrated

Stabilisation Mission in the Central African Republic

MK-ICC                       Mt. Kilimanjaro International Convention

Centre

MONUSCO               United Nations Organisation Stabilisation

Mission in the Democratic Republic of the Congo

NPT                                 Non – Proliferation Treaty

PSPF                             Public Sector Pension Fund

RFI                                  Radio France International

RMB                               Renminbi

SADC                            Southern African Development

Community

SDGs                             Sustainable Development

Goals

TAZARA                     Tanzania-Zambia Railway Authority

TBC                                Tanzania Broadcasting Corporation

TEHAMA                   Teknolojia ya Habari na Mawasiliano

TIC                                  Tanzania Investment Centre

TMEA                           Trademark East Africa

UKIMWI                      Upungufu wa Kinga Mwilini





iv


UNAMID


United Nations African Union Mission in Darfur



UNDP


United Nations Development Progamme




UNDAP



United Nations Development Assistance Plan



UNEP


United Nations Environment Progamme





UNESCO


United Nations Educational Scientific and Cultural Organization



UNFPA


United Nations Population Fund



UN-HABITAT


United Nations Human Settlement Programme



UNHCR


United Nations High Commission for Refugees



UNICEF


United Nations Children’s Emergency Fund



UN-ICTR


United Nations International Criminal Tribunal for Rwanda



UNIDO


United Nations Industrial Development Organization



UNIFIL


United Nations Interim Force in Lebanon



UNISFA


United Nations Interim Security Force for Abyei




v


UNMISS                       United Nations Mission in the Republic

of South Sudan

UTT                                 Unit Trust of Tanzania

VoA                                 Voice of America

WHO                              World Health Organization


WTO                               World Trade Organization

WWF                              World Wildlife Fund






vi


UTANGULIZI

1.   Mheshimiwa Spika, baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kuwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara, naomba sasa kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu likubali kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa mpango na bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa mwaka wa fedha 2017/18. Aidha, naomba Bunge lako Tukufu lijadili na kupitisha Mpango na Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2018/19.

2.   Mheshimiwa Spika, awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa fadhila na rehema, kwa kutujalia afya njema na kutuwezesha kukutana tena katika Bunge lako Tukufu, kujadili Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yangu.

3.   Mheshimiwa Spika, naungana na wenzangu walionitangulia kuwashukuru na kuwapongeza watoa hoja waliozungumza kabla yangu, hususan Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mheshimiwa Dkt. Philip Isdory Mpango (Mb), Waziri wa Fedha na Mipango ambao kwa hakika hotuba zao sio tu zimezungumzia mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano, bali pia zimetoa dira katika mustakabali wa taifa letu kwa kuainisha masuala muhimu ya kitaifa, kikanda na kimataifa ambayo baadhi yake yanagusa majukumu ya Wizara yangu.



1


4.   Mheshimiwa Spika, naomba pia nitumie fursa hii kutoa shukrani zangu kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama chini ya uongozi wa Mhe. Mussa Azan Zungu (Mb) na Makamu wake Mhe. Salum Mwinyi Rehani (Mb). Kamati hii imetoa mchango mkubwa na imekuwa muhimili muhimu katika kuiwezesha Wizara yangu kutekeleza majukumu yake kwa kutoa ushauri kuhusu masuala mbalimbali ya kiutendaji.

5.   Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee naomba nitumie nafasi hii kuwashukuru Mheshimiwa Dkt. Susan Alphonce Kolimba (Mb), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki; Prof. Adolf Faustine Mkenda, Katibu Mkuu; Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi, Naibu Katibu Mkuu; mabalozi wa Tanzania nje ya nchi; Wakuu wa Idara na Vitengo; watumishi wa Wizara; na taasisi zilizo chini ya Wizara yangu kwa kujituma na kutekeleza majukumu yao kwa weledi na kufanikisha kwa kiwango cha juu utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2017/18, pamoja na kuandaa Bajeti ya Wizara ya mwaka wa fedha 2018/19.