Mhe. Waziri Mahiga na Mhe. Naibu Waziri Kolimba wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Waheshimiwa Mabalozi na Watendaji wa Wizara waliohudhuria tukio la uwasilishwaji wa bajeti ya Wizara bungeni jijini Dodoma
HOTUBA YA MHESHIMIWA BALOZI DKT. AUGUSTINE PHILIP MAHIGA
(MB), WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI AKIWASILISHA
BUNGENI MAKADIRIO YA BAJETI YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA
2018/2019
AF
|
Adaptation
Fund
|
AfDB
|
African Development Bank
|
AfCFTA
|
African Continental Free Trade
Area
|
AGOA
|
African Growth and Opportunity
Act
|
AICC
|
Arusha
International Conference Centre
|
AMISOM
|
African Union Mission to Somalia
|
APRM
|
African Peer Review Mechanism
|
BBC
|
British Broadcasting Corporation
|
CGTN
|
China Global Television Network
|
COMESA
|
Common Market for Eastern and
|
|
Southern Africa
|
COP
|
Conference of Parties
|
DW
|
Deutsche Welle
|
EAC
|
East African Community
|
EPA
|
Economic Partnership Agreement
|
FAO
|
Food and Agriculture
Organization
|
|
FIB
|
Force Intervention Brigade
|
|
FOCAC
|
Forum on China-Africa
Cooperation
|
|
ii
|
|
Green Climate Fund
|
|
GEF
|
Global Environment Facility
|
|
GIZ
|
The Deutsche Gesellschaft für
|
|
Internationale Zusammenarbeit
GmbH
|
|
|
|
GPEDC
|
Global Partnership for Effective
|
|
|
Development Cooperation
|
|
IAEA
|
International Atomic Energy
Agency
|
|
IGAD
|
Intergovernmental Authority on
|
|
|
Development
|
|
ILO
|
International Labour
Organization
|
|
IMF
|
International Monetary Fund
|
|
IOM
|
International
Organization for Migration
|
|
IORA
|
Indian Ocean Rim Association
|
|
JNICC
|
Julius
Nyerere International Convention
|
|
|
Centre
|
|
KCB
|
Kenya Commercial Bank
|
|
KOICA
|
Korea International Cooperation
Agency
|
|
LDCF
|
Least Developed Countries Fund
|
|
MINUSCA United Nations Multidimensional
Integrated
Stabilisation
Mission in the Central African Republic
MK-ICC Mt. Kilimanjaro International
Convention
Centre
MONUSCO United Nations Organisation
Stabilisation
Mission
in the Democratic Republic of the Congo
NPT Non – Proliferation Treaty
PSPF Public Sector Pension Fund
RFI Radio France International
RMB Renminbi
SADC Southern African Development
Community
SDGs Sustainable Development
Goals
TAZARA Tanzania-Zambia Railway Authority
TBC Tanzania Broadcasting Corporation
TEHAMA Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano
TIC Tanzania Investment Centre
TMEA Trademark East Africa
UKIMWI Upungufu wa Kinga Mwilini
United
Nations African Union Mission in Darfur
UNDP
United Nations Development Progamme
UNDAP
United
Nations Development Assistance Plan
UNEP
United Nations Environment Progamme
UNESCO
United
Nations Educational Scientific and Cultural Organization
UNFPA
United Nations Population Fund
UN-HABITAT
United
Nations Human Settlement Programme
UNHCR
United
Nations High Commission for Refugees
UNICEF
United
Nations Children’s Emergency Fund
UN-ICTR
United
Nations International Criminal Tribunal for Rwanda
UNIDO
United
Nations Industrial Development Organization
UNIFIL
United Nations Interim Force in Lebanon
UNISFA
United
Nations Interim Security Force for Abyei
UNMISS United Nations Mission in the
Republic
of South Sudan
UTT Unit Trust of Tanzania
VoA Voice of America
WHO World Health Organization
WTO World Trade Organization
WWF World Wildlife Fund
1.
Mheshimiwa Spika, baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kuwasilisha Taarifa ya
Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara, naomba sasa kutoa hoja kwamba Bunge
lako Tukufu likubali kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa mpango na
bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa mwaka
wa fedha 2017/18. Aidha, naomba Bunge lako Tukufu lijadili na kupitisha Mpango
na Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2018/19.
2.
Mheshimiwa Spika, awali ya yote napenda kumshukuru
Mwenyezi Mungu, mwingi wa fadhila na rehema, kwa
kutujalia afya njema na kutuwezesha kukutana tena katika Bunge lako Tukufu, kujadili Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya
Wizara yangu.
3.
Mheshimiwa Spika, naungana na wenzangu walionitangulia
kuwashukuru na kuwapongeza watoa hoja waliozungumza kabla yangu, hususan Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mheshimiwa Dkt. Philip Isdory
Mpango (Mb), Waziri wa Fedha na Mipango ambao kwa hakika hotuba zao sio tu
zimezungumzia mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano, bali pia zimetoa dira
katika mustakabali wa taifa letu kwa kuainisha masuala muhimu ya kitaifa,
kikanda na kimataifa ambayo baadhi yake yanagusa majukumu ya Wizara yangu.
4.
Mheshimiwa Spika, naomba pia nitumie fursa hii kutoa
shukrani zangu kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama
chini ya uongozi wa Mhe. Mussa Azan Zungu (Mb) na Makamu wake Mhe. Salum Mwinyi
Rehani (Mb). Kamati hii imetoa mchango mkubwa na imekuwa muhimili muhimu katika
kuiwezesha Wizara yangu kutekeleza majukumu yake kwa kutoa ushauri kuhusu
masuala mbalimbali ya kiutendaji.
5.
Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee naomba nitumie
nafasi hii kuwashukuru Mheshimiwa Dkt. Susan Alphonce Kolimba (Mb), Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki; Prof. Adolf Faustine
Mkenda, Katibu Mkuu; Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi, Naibu Katibu Mkuu;
mabalozi wa Tanzania nje ya nchi; Wakuu wa Idara na Vitengo; watumishi wa
Wizara; na taasisi zilizo chini ya Wizara yangu kwa kujituma na kutekeleza
majukumu yao kwa weledi na kufanikisha kwa kiwango cha juu utekelezaji wa
bajeti ya mwaka wa fedha 2017/18, pamoja na kuandaa Bajeti ya Wizara ya mwaka
wa fedha 2018/19.
6.
Mheshimiwa Spika, kwa masikitiko makubwa, naungana
na Waheshimiwa Wabunge wenzangu kutoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki
na wananchi wa
Jimbo
la Songea Mjini kwa kifo cha Mhe. Leonidas Gama aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo
kilichotokea mwezi Novemba 2017. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala
pema peponi. Amina.
7.
Mheshimiwa Spika, nawapongeza wabunge wote waliochaguliwa
na kuteuliwa kisha kuapishwa katika kipindi cha mwaka huu wa fedha. Kuchaguliwa
na kuteuliwa kwao ni kielelezo cha kuaminiwa na wananchi ili kuwawakilisha
ipasavyo katika Bunge hili.
8.
Mheshimiwa Spika, nitakuwa mchoyo wa fadhila kama
sitamshukuru kwa dhati mke wangu mpendwa Elizabeth Mahiga pamoja na watoto kwa
kunivumilia, kuniunga mkono na kuniombea kwa Mwenyezi Mungu ili niweze
kutekeleza majukumu niliyopewa na Mheshimiwa Rais katika kujenga na kutetea
maslahi ya taifa letu.
HALI
YA MAHUSIANO NA NCHI NYINGINE
9.
Mheshimiwa Spika, mahusiano ya Tanzania na nchi na mashirika
mbalimbali ya kikanda na kimataifa yameendelea kushamiri kwa manufaa ya pande
zote zinazohusika. Tanzania tuna mahusiano mazuri na majirani zetu wote.
Kupitia Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika,
Tanzania ina makubaliano ya kuondoa vikwazo vya biashara na nchi zote jirani,
yaani Msumbiji, Malawi, Zambia, Kongo DRC, Burundi, Rwanda, Uganda na Kenya.
Kwa kuzingatia misingi ya Sera yetu ya Mambo ya Nje, tumeendelea kuchukua kila
hatua kudumisha ujirani mwema na nchi jirani. Tunazo ofisi za ubalozi katika
nchi zote ambazo ni majirani zetu kwenye nchi kavu na pia katika visiwa vya
Komoros. Tumeendelea na jitihada za kujenga ujirani mwema kwa jamii zinazoishi
mipakani na jamii za nchi jirani.
Katika
kuimarisha mahusiano hayo, viongozi wa nchi na mashirika mbalimbali wameendelea
kufanya ziara hapa nchini. Mathalan, kwa mwaka wa fedha 2017/18, Tanzania
ilipokea Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka Uganda, Misri, Burundi, Msumbiji na
Rwanda. Aidha, Mawaziri na Naibu Mawaziri kutoka nchi za Ujerumani, Israel,
Uingereza, Norway, Oman, Burundi, Misri, Poland, Shelisheli, Maldves, China na
Brazil walitembelea Tanzania katika kipindi hicho. Pia, Tanzania ilipokea wajumbe maalum wa wakuu wa nchi na
serikali kutoka nchi za Uganda, Rwanda,
Misri, Poland, Burundi, Morocco, Mjumbe Maalum wa Mwenyekiti wa
Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Umoja wa Mataifa na Palestina. Aidha, Ethiopia ipo katika hatua za mwisho za kufungua
ubalozi hapa nchini na Belarus nao wametuma timu ya uangalizi mwezi Desemba
2017 na kuahidi kufungua ubalozi wao mwezi Juni 2018.
10.
Mheshimiwa Spika, nchi yetu ilitembelewa pia na
Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa yakiwemo Shirika la Maendeleo ya Viwanda la
Umoja wa Mataifa (UNIDO); Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB); Shirika la Umoja
wa Mataifa linaloshughulikia Chakula na Kilimo (FAO); Shirika la Umoja wa
Mataifa linaloshughulikia masuala ya Ukimwi (UNAIDS); na Jumuiya ya Madola.
Aidha, viongozi wengine na wataalam kutoka katika mashirika na taasisi
mbalimbali za kimataifa ikiwemo Shirika la Maendeleo la Japan (JICA); Shirika
la Maendeleo la Korea (KOICA) na Aga Khan walitembelea Tanzania.
11.
Mheshimiwa Spika, Viongozi wetu Wakuu wa Kitaifa yaani
Mheshimiwa Rais, Mheshimiwa Makamu wa Rais, Mheshimiwa Rais wa Zanzibar,
Mheshimiwa Waziri Mkuu na Mheshimiwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar nao
walifanya ziara za kiserikali na kushiriki mikutano katika nchi mbalimbali.
12.
Mheshimiwa Spika, Tanzania imeendelea kuwa na mahusiano
mazuri ya kidiplomasia na nchi mbalimbali duniani. Hadi sasa jumla ya nchi 62
zina mabalozi wakaazi hapa nchini. Kati ya hizo, nchi
za China, Oman, Msumbiji na India zinaendesha pia ofisi ndogo za ubalozi
(konseli kuu) Zanzibar. Kadhalika, Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo, pamoja na kuwa na ubalozi Dar es Salaam, ina Konseli Kuu
mjini Kigoma. Aidha, nchi 39 zinawakilishwa nchini na mabalozi wasio wakaazi
ambao ofisi zao zipo nje ya Tanzania.
Vilevile, wapo makonseli wa heshima 24 wanaowakilisha nchi zao hapa nchini na
yapo mashirika 23 ya kimataifa yenye hadhi ya kidiplomasia yanayofanya kazi
nchini.
13.
Mheshimiwa Spika, Tanzania ina jumla ya balozi 41 zinazotuwakilisha
nje ya nchi. Pamoja na balozi hizo nchi yetu ina ofisi 3 za Konseli Kuu katika
miji ya Mombasa,
Jeddah
na Dubai. Kadhalika Tanzania ina jumla ya makonseli wa heshima 35
wanaotuwakilisha katika miji mbalimbali duniani.
14.
Mheshimiwa Spika, katika
hotuba yangu ya bajeti mwaka jana nilieleza kuhusu
Serikali kufungua balozi mpya sita katika nchi za Algeria, Israel, Uturuki,
Sudan, Qatar na Korea Kusini. Napenda kulijulisha Bunge lako Tukufu kwamba
tayari tumepeleka mabalozi kwenye vituo hivyo.
MISINGI
YA NCHI KATIKA MAHUSIANO YA KIMATAIFA
15.
Mheshimiwa Spika, taifa lolote duniani huongozwa na
misingi ambayo lengo lake kuu ni kudumisha amani, ulinzi, usalama na mshikamano
wa wananchi wake na taifa kwa ujumla. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
inaongozwa na misingi iliyowekwa na waasisi wa Taifa letu mara baada ya uhuru.
Misingi hiyo ni pamoja na kulinda uhuru wetu; kujiamulia mambo yetu wenyewe
bila kuingiliwa; kulinda mipaka ya nchi yetu; kulinda haki; kuimarisha ujirani
mwema; na kuunga mkono Sera ya Kutofungamana na Upande wowote kama dira na
msimamo wetu katika mahusiano na nchi nyingine katika Jumuiya ya Kimataifa.
16.
Mheshimiwa Spika, misingi hiyo ndiyo inayotufanya leo
tujivunie Taifa lenye amani, ulinzi imara na usalama duniani; taifa ambalo
limekuwa mstari wa mbele kutetea wanyonge, haki na uhuru; kutafuta amani na
kutatua migogoro ya nchi mbalimbali kwa gharama kubwa ya rasilimali watu na
fedha; Taifa linalojitolea wanajeshi wake kwenye ulinzi wa amani, na kuwa
tegemeo la mataifa katika misheni za kulinda amani; Taifa ambalo limekuwa
kimbilio
kubwa
kwa wananchi wa mataifa mengine yenye migogoro na ambao wanalazimika kukimbilia
nchi nyingine kuokoa maisha yao na kupewa hifadhi nchini mwetu.
17.
Mheshimiwa Spika, Tanzania inaheshimu misingi ya
mahusiano na mataifa mengine duniani ambayo tuna mahusiano ya kidiplomasia na
yale ambayo bado hatuna mahusiano ya kidiplomasia. Ni kwa misingi hiyo, mataifa
mengine nayo yanawajibika kuheshimu misingi ya Tanzania kama ilivyoainishwa
hapo juu. Nataka kulihakikishia Bunge lako Tukufu kuwa Tanzania italinda
misingi hiyo daima. Aidha, napenda ieleweke wazi kuwa Tanzania itaendelea
kushirikiana na mataifa yote duniani na kushiriki kikamilifu katika mijadala na
majukwaa ya kimataifa katika kutetea uhuru, haki za binadamu na usawa kwa
kuzingatia mahusiano yaliyopo kwa kila nchi kwa ajili ya maslahi mapana ya
uchumi, jamii na maendeleo ya nchi yetu.
Ni kwa
mantiki hiyo, Tanzania itaendelea kutekeleza Sera ya Kutofungamana na Upande
wowote kama ambavyo imekuwa ikifanya siku zote. Tanzania haitarajii nchi
nyingine yoyote kuiamulia mambo yake, kushinikizwa, kutishwa au kuingiliwa na
nchi yoyote katika mambo yetu ya ndani. Marafiki wetu ni lazima waheshimu
msimamo wetu kwamba hatutachaguliwa nani awe rafiki yetu na nani awe adui wetu.
Maslahi ya nchi yetu na imani yetu ya haki na usawa wa binadamu ndio dira ya
msimamo wetu kimataifa.
MSIMAMO WA TANZANIA KATIKA MASUALA MBALIMBALI YA KIMATAIFA
18.
Mheshimiwa Spika, napenda kutumia fursa hii kulieleza
Bunge lako Tukufu kuwa msimamo wa Tanzania kuhusu suala la Palestina na Israel
haujabadilika. Tanzania inaunga mkono msimamo wa Umoja wa Mataifa wa suluhu ya
kuwa na mataifa mawili yaani Palestina huru na Israel salama. Tunaendelea
kuunga mkono kufanyika kwa majadiliano yatakayosaidia kumalizika kwa mgogoro
huo uliodumu muda mrefu kati ya nchi hizi mbili. Ni kweli kwamba mahusiano yetu
na Israel yanaongezeka na tutahakikisha yanashamiri kwa manufaa na maendeleo ya
Taifa letu. Tanzania inatambua kuwa Israel ina haki ya kuishi kama Taifa huru
na salama na hivyo ndivyo iwe kwa Wapalestina ambao ni majirani zao.
Tutashiriki katika mijadala yote kimataifa katika kutafuta suluhu ya mashariki
ya kati.
19.
Mheshimiwa Spika, Tanzania pia inaendelea kuunga
mkono juhudi za usuluhishi wa mgogoro wa Sahara Magharibi, katika mchakato wa
maelewano unaosimamiwa na Umoja wa Mataifa na kuungwa mkono na Umoja wa Afrika.
Tuna imani kuwa kurejea kwa Morocco katika Umoja wa Afrika kutatoa fursa kwa
Umoja huo kutoa mchango wake katika kutafuta suluhu ya mgogoro huo ambao kwa
muda mrefu umekuwa ukishughulikiwa na Umoja wa Mataifa. POLISARIO ni chama cha
ukombozi ambacho kilipewa hadhi ya Serikali na uanachama wa
Umoja
wa Afrika tangu mwaka 1982. Suala hili limeanza kuleta utata wa kisheria katika
Umoja wa Afrika na katika duru za kimataifa. Morocco imeanzisha Ubalozi hapa
nchini. Mfalme Mohamed VI alitembelea hapa nchini mwishoni mwa mwaka 2016 na
kutiliana saini mikataba 21 ya ushirikiano katika sekta mbalimbali. Tanzania
iliunga mkono Morocco kurudi katika Umoja wa Afrika na kuingia katika Baraza la
Usalama na Amani la Umoja wa Afrika. Tanzania itaendelea kushiriki katika vikao
mbalimbali vya kutafuta suluhu ya mgogoro huo. Tunatarajia uhusiano wetu na
nchi ya Morocco utaendelea kukua hasa katika sekta mbalimbali.
UTEKELEZAJI WA SERA YA MAMBO YA
NJE Kulinda Amani
20.
Mheshimiwa Spika, hali ya usalama duniani imeendelea
kuimarika pamoja na kwamba changamoto kadhaa zimeendelea kuwepo katika baadhi
ya maeneo. Changamoto hizo ni pamoja na migogoro ya kisiasa inayoendelea katika
nchi mbalimbali duniani, matukio ya kigaidi na kuongezeka makundi yenye itikadi
kali pamoja na athari za kiusalama zinazosababishwa na mabadiliko ya tabianchi.
Tishio jingine kimataifa ni biashara haramu kama vile za madawa ya kulevya,
usafirishaji wa binadamu na utakatishaji wa fedha ambayo haina mipaka. Katika
kukabiliana na changamoto hizo, Tanzania imeendelea kuunga mkono jitihada za
kikanda na za Umoja wa Mataifa za kuimarisha amani na usalama duniani.
21.
Mheshimiwa Spika, katika kuunga mkono jitihada za Umoja wa
Mataifa zinazolenga kuimarisha amani na usalama duniani, nchi yetu imeendelea
kutoa mchango wa askari wake kwenye misheni za kulinda amani za Umoja wa
Mataifa. Mchango huu ni muhimu na umeiletea nchi yetu sifa kubwa kimataifa kwa
askari kuwa na nidhamu na kujitoa katika kuifanya dunia kuwa salama. Ushiriki
wa askari wetu katika misheni hizo umewaongezea weledi na ujuzi katika masuala ya
medani za kijeshi na usalama wa kimataifa.
22.
Mheshimiwa Spika, pamoja na mafanikio yaliyopatikana,
tumekuwa tukipata changamoto za kupoteza baadhi ya askari wetu katika misheni
hizo. Kwa mfano, shambulio la tarehe 8 Desemba 2017 lililosababisha askari wetu
15 kupoteza maisha na wengine 43 kujeruhiwa nchini DRC, linabaki kuwa moja ya
shambulizi baya zaidi kuwahi kutokea kwenye misheni za kulinda amani duniani
kwa takribani miaka 25 iliyopita.
23.
Mheshimiwa Spika, tunaushukuru Umoja wa Mataifa
kwa kuunda timu ya kuchunguza chanzo cha tukio hilo iliyojumuisha maafisa
wawili wa ngazi ya juu kutoka
Jeshi
la Wananchi wa Tanzania. Timu hiyo imeshakamilisha uchunguzi wake kuhusu chanzo
cha tukio hilo na kutoa mapendekezo ya hatua za kuchukua ili kuzuia matukio kama
hayo yasitokee tena. Serikali inaendelea kuwasiliana na Umoja wa Mataifa kwa
ajili ya utekelezaji wa taarifa hiyo ambayo itasaidia pia Umoja wa Mataifa
kuboresha utendaji wake na ulinzi wa askari kwenye misheni za kulinda amani.
24.
Mheshimiwa Spika, naomba ifahamike kwamba, pamoja
na shambulio hilo kubwa na la kusikitisha, kamwe hatutarudi nyuma wala
kukatishwa tamaa. Tunaamini kwenye misingi yetu ya kusimamia haki na kulinda
amani kwa ajili ya kuokoa maisha ya watu na kuweka mazingira mazuri ya ustawi
wa jamii. Tanzania itaendelea kusimamia misingi hiyo na kuimarisha ushiriki
wetu katika misheni za kulinda amani duniani.
MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA WIZARA KWA MWAKA WA
FEDHA 2017/18
25.
Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza majukumu ya
Wizara kwa mwaka 2017/18, Wizara yangu ilitengewa kiasi cha Shilingi 157,980,248,704. Kati ya fedha
hizo, Shilingi 149,980,248,704 ilikuwa
kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Shilingi 8,000,000,000 ilikuwa kwa
ajili ya bajeti ya maendeleo. Katika fedha zilizotengwa kwa Matumizi ya
Kawaida, Shilingi 140,496,296,704
ilikuwa kwa ajili ya Matumizi Mengineyo na Shilingi
9,483,952,000 ilikuwa kwa ajili ya mishahara.
26.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2017/18,
Wizara ilitarajia kukusanya maduhuli kiasi cha Shilingi 25,773,882,820. Hadi kufikia tarehe 30 Aprili
2018,
Wizara imefanikiwa kukusanya kiasi cha Shilingi
22,198,966,840, sawa na asilimia 86
ya makisio ya
makusanyo
yote ya maduhuli. Hadi kufikia tarehe 30 Aprili 2018, balozi zetu nje
zimerejesha katika Mfuko Mkuu wa Serikali kiasi cha Shilingi 13,025,539,374. Wizara yangu itaendelea kusimamia na
kuhakikisha kuwa kiasi chote cha maduhuli kitakachokusanywa kwa mwaka wa fedha
2017/18 kinarejeshwa katika Mfuko Mkuu kama ilivyoelekezwa na Serikali.
27.
Mheshimiwa
Spika, hadi
kufikia tarehe 30 Aprili
2018,
Wizara ilipokea jumla ya Shilingi
114,185,986,274, sawa na asilimia 72 ya bajeti iliyopitishwa na Bunge. Kati
ya fedha hizo, Shilingi 104,538,835,394
ilikuwa kwa ajili ya bajeti ya Matumizi Mengineyo; Shilingi 6,226,955,225 ilikuwa kwa ajili ya mishahara; na Shilingi 3,420,195,655 ilikuwa kwa
ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo.
Miradi
ya Maendeleo ya Wizara
28.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2017/18,
Wizara ilipangiwa bajeti ya maendeleo kiasi cha Shilingi 8,000,000,000. Hadi kufikia mwanzoni mwa mwezi Mei 2018,
Wizara ilipokea kutoka Hazina mgao wa fedha za bajeti ya maendeleo kiasi cha Shilingi 3,420,195,655, sawa na asilimia 42.7 ya fedha za bajeti ya maendeleo iliyoidhinishwa. Kati ya
fedha hizo, Shilingi 1,815,527,215 zimepangwa kutumika
kufanya ukarabati wa jengo la ofisi
na makazi ya watumishi kwenye ubalozi wa Tanzania Kampala; Shilingi 315,425,000 ni kwa ajili ya ukarabati wa makazi ya balozi
Kinshasa; Shilingi
12
593,300,000
kutumika kukarabati nyumba za ubalozi wa Tanzania Lilongwe; Shilingi 195,943,440 kukarabati makazi
ya balozi wa Tanzania Brussels; na shilingi
500,000,000 kwa ajili ya kukarabati
miundombinu ya Chuo cha Diplomasia.
29.
Mheshimiwa Spika, Wizara inaendelea kufuatilia Wizara
ya Fedha na Mipango upatikanaji wa fedha za maendeleo kiasi cha Shilingi 4,579,804,345 sawa na asilimia
57.3 ambazo hazijatolewa ili
kutekeleza miradi ya maendeleo iliyopangwa kwa mwaka wa fedha 2017/18.
30.
Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuzingatia sheria,
kanuni, taratibu na miongozo ya fedha za umma katika kudhibiti mapato na
matumizi ya Serikali. Kwa kudhihirisha hilo, Wizara pamoja na balozi zake 39
zimepata hati safi isipokuwa balozi mbili zimepata hati zenye shaka katika
ukaguzi kwa mwaka wa fedha 2016/17. Nachukua fursa hii kuwashukuru watendaji wa
Wizara na kuwahimiza waendelee kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo
ya matumizi ya fedha za umma na ununuzi wakati wote wanapotekeleza majukumu
yao.
31.
Mheshimiwa Spika, baada ya kutoa taarifa ya mapato
na matumizi ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2017/18, naomba sasa nitumie fursa hii
kueleza kwa kifupi baadhi ya mafanikio ya Wizara katika kipindi hicho.
DIPLOMASIA YA UCHUMI NA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA WIZARA
32.
Mheshimiwa Spika, katika malengo ya Sera ya
Mambo ya Nje kuna malengo ambayo ni ya kudumu yanayoiwezesha nchi kuwa katika
nafasi ya jumuiya ya mataifa kama Taifa huru lenye umoja, usalama na lenye
hadhi na siha nzuri. Hii hasa ni diplomasia ya siasa. Pia kuna malengo ambayo
yanaendana na wakati huo wa uongozi na vipaumbele vya Serikali na Taifa kwa
ujumla. Katika miaka ya sitini hadi themanini malengo ya ziada katika Sera ya
Tanzania yalikuwa ukombozi wa Bara la Afrika kutoka kwa ukoloni na ubaguzi wa
rangi. Baada ya kukamilisha hayo Tanzania iliona umuhimu wa kuwa na Sera ya
Mambo ya Nje yenye msisitizo wa diplomasia ya uchumi ili kusukuma maendeleo ya
Taifa letu.
33.
Mheshimiwa
Spika, Diplomasia ya uchumi ni msisitizo wa Sera ya Mambo ya Nje yenye mikakati, malengo, mbinu
na maarifa yanayoelekeza taifa kupata na kuvuna rasilimali na utaalam kutoka
jumuiya ya mataifa ili kuleta na kuchochea maendeleo ya taifa husika. Mwaka
2001 Tanzania ilipitisha sera inayosisitiza diplomasia ya uchumi ili kuendeleza
maendeleo hasa katika sekta ya uchumi. Katika Awamu hii ya tano, Mheshimiwa
Rais John Pombe Magufuli alitangaza mapema kuwa Tanzania iwe ni nchi ya viwanda
ili kusukuma zaidi maendeleo ya uchumi na ajira kufikia uchumi wa kati ifikapo
mwaka
2025. Azma hii inamaanisha kuwa diplomasia ya uchumi
lazima
iongeze mkakati wa Diplomasia wa Viwanda ili kutekeleza maono na mawazo ya
Mheshimiwa Rais kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda vilivyojikita kwenye
kilimo. Diplomasia ya uchumi wa viwanda lazima itoe vipaumbele katika
uwekezaji, miundombinu ikiwa ni pamoja na nishati, biashara na masoko ya bidhaa
kutoka viwandani. Sambamba na mkakati huo, dhana ya diplomasia ya uchumi lazima
iendelee kulenga sekta nyingine kama kilimo, utalii na madini ambayo kwa namna
moja au nyingine zinashabihiana na viwanda.
Viwanda,
Biashara na Uwekezaji
34.
Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza diplomasia ya
uchumi, Wizara yangu kwa kushirikiana na wadau wengine ndani ya Serikali na
kutoka sekta binafsi inaratibu upatikanaji wa masoko, mitaji, na teknolojia kwa
ajili ya kukuza biashara na uwekezaji nchini. Miongoni mwa juhudi zilizofanywa
na Wizara yangu ni kushawishi wawekezaji kupitia ziara za viongozi, balozi zetu
nje ya nchi, na makongamano ya biashara na uwekezaji yaliyofanyika ndani na nje
ya nchi. Kupitia juhudi hizo, tumeweza kufanikisha kuleta ujumbe wa wawekezaji
na wafanyabiashara kutoka nchi kadhaa zikiwemo Ujerumani, Ufaransa, Hispania,
Misri, China, India, Falme za Kiarabu, Oman na Israel. Baadhi ya wawekezaji hao
tayari wameingia ubia na kampuni za Tanzania na wengine wameanza hatua
mbalimbali za uwekezaji nchini.
Moja
ya hatua hizo ni uamuzi uliofanywa na jumuiya ya wafanyabiashara wa Ujerumani
mwezi Aprili 2018 wa kufungua ofisi maalum ya biashara ya nchi hiyo inayoitwa
AHK kwa lengo la kuratibu kwa ukaribu zaidi uwekezaji na biashara zinazofanywa
na zitakazofanywa na Ujerumani hapa nchini. Aidha, Ufaransa imefungua ofisi ya
biashara kupitia kampuni ya BASF kwa lengo la kuratibu shughuli za kibiashara
zitakazokuwa zikifanywa na kampuni hiyo na wabia wake hususan katika masuala ya
uzalishaji wa kemikali za viwandani.
35.
Mheshimiwa Spika, Wizara yangu pia iliratibu ushiriki
wa Tanzania kwenye makongamano mbalimbali ya biashara na uwekezaji
yaliyoandaliwa nje ya nchi. Makongamano hayo ni pamoja na yale yaliyofanyika
nchini Kenya, Hispania, Uturuki, Uholanzi, Indonesia, Korea Kusini, China,
Vietnam, Ujerumani na Umoja wa Falme za Kiarabu. Aidha, viongozi wetu
wanapopata fursa ya kufanya ziara mbalimbali nje ya nchi wamekuwa wakitumia
fursa hiyo kuzungumza na kuwashawishi wawekezaji kuwekeza nchini, binafsi
nimekuwa nikifanya hivyo na viongozi wenzangu pia wamekuwa wakifanya hivyo. Kwa
mfano, mwezi Aprili 2018 Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein
alitembelea Falme za Kiarabu na Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko wa
Zanzibar, Mhe. Balozi Amina Salum Ali, alipofanya ziara ya kikazi nchini China
walitumia fursa hiyo kushawishi wawekezaji katika sekta za uvuvi, viwanda,
kilimo na utalii na hatimaye kuingia nao makubaliano ya kuanza hatua za uwekezaji
kwenye
36.
Mheshimiwa Spika, mwezi Aprili 2018, Wizara ikishirikiana
na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji; Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara
Tanzania; na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania kupitia ubalozi wetu nchini
Kenya iliandaa maonesho ya bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya Tanzania,
yaliyofanyika Nairobi. Haya yalikuwa ni maonesho ya kipekee kuwahi kufanywa na
nchi yetu. Jumla ya kampuni 27 zinazozalisha bidhaa za viwandani kutoka
Tanzania zilishiriki ili kutangaza bidhaa zao na kuvutia utalii. Maonesho hayo
yalitoa fursa kwa wafanyabiashara wa Tanzania kutafuta masoko ya bidhaa zetu
nchini Kenya.
37.
Mheshimiwa Spika, napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu
kuwa maonesho hayo yamefungua soko zaidi kwa bidhaa za Tanzania nchini Kenya na
kuimarisha mahusiano kati ya nchi zetu mbili na wafanyabiashara. Natoa wito kwa
wafanyabiashara kuchangamkia fursa ya masoko ya bidhaa za Tanzania ndani ya
Jumuiya ya Afrika Mashariki. Balozi zetu nyingine pia zimekuwa zikiendesha
makongamano na shughuli nyingine mbalimbali za kukuza utalii, kuvutia
wawekezaji na kutafuta masoko.
38.
Mheshimiwa Spika, juhudi hizi zinazofanywa na Wizara
yangu pamoja na wadau wengine ndani na nje ya Serikali zinatoa nafasi kwa
wafanyabiashara na wawekezaji kujionea fursa mbalimbali za uwekezaji, biashara,
masoko, teknolojia na upatikanaji wa mitaji. Hivyo, ninatoa rai
17
kwa
wadau wote wanaosimamia masuala ya biashara na uwekezaji kuendelea kutoa
ushirikiano wa kutosha kwa wawekezaji walioonesha nia ya kuwekeza nchini. Nitumie
fursa hii kutoa wito kwa wafanyabiashara wetu kutumia fursa hizo kikamilifu.
39.
Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha biashara kati
ya Tanzania na Misri, Wizara yangu kwa kushirikiana na wadau husika iliratibu
majadiliano ya kuondoleana ushuru wa forodha na Misri. Majadiliano hayo
yamekamilika mwezi Machi 2018 kwa pande zote kukubaliana kuwa, Misri iondoe
ushuru kwa kiwango cha asilimia 100, na Tanzania iondoe kwa kiwango cha
asilimia 96.89. Kiwango kilichosalia kwa Tanzania kitaondolewa katika kipindi cha
miaka mitano ijayo.
40.
Mheshimiwa Spika, mwezi Febuari, 2018 nilifanya ziara
ya kikazi nchini Korea Kusini ambapo nilifungua kongamano la biashara na
uwekezaji kati ya Tanzania na nchi hiyo. Kufuatia kongamano hilo viongozi wa
kampuni ya Hyundai walifika nchini kufanya mazungumzo na Kituo cha Uwekezaji
nchini (TIC) kwa lengo kuanzisha kiwanda cha kutengeneza vipuli vya magari.
Wizara yangu kwa kushirikiana na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
itaendelea kufuatilia mazungumzo hayo.Halikadhalika, nilipotembelea China
mwishoni mwa mwaka jana nilikutana na wawekezaji katika viwanda vya magari
ambao wameahidi kuja kuona uwezekano wa kuwekeza hapa nchini.
Kilimo,
Ufugaji, Uvuvi na Umwagiliaji
41.
Mheshimiwa Spika, Wizara yangu iliratibu upatikanaji
wa mkopo nafuu wa Dola za Marekani milioni 55 kutoka Serikali ya Poland ambazo
zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa maghala na vihenge vya kuhifadhia
nafaka katika mikoa ya Ruvuma, Njombe, Rukwa, Songwe, Dodoma, Shinyanga,
Manyara, na Katavi. Kukamilika kwa mradi huo kutapunguza upotevu wa mazao baada
ya mavuno (post-harvest loss). Wizara yangu pia imeratibu upatikanaji wa
ufadhili wa mradi wa kituo kikubwa cha ujenzi wa kuzalisha samaki cha Zanzibar
unaodhaminiwa kwa ushirika kati ya Korea Kusini kupitia Shirika lake la
maendeleo la KOICA pamoja na Shirika la Chakula Duniani (FAO) wenye thamani ya
Dola za Marekani milioni 3.2.
42.
Mheshimiwa Spika, Wizara yangu kwa kushirikiana na
wadau wengine imefanikisha kupatikana ufadhili wa miradi ya umwagiliaji ya Muhongo-Kagera
na bonde la Luiche-Kigoma kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait. Baada ya
kukamilika kwa tathmini ya miradi hiyo mwezi Machi 2018, rasimu ya mkataba wa
kuipatia Tanzania mkopo wa masharti nafuu wenye thamani ya Dola za Marekani
milioni 15.3 ilisainiwa. Aidha, ushirikiano wa Tanzania na China kupitia jukwaa
la FOCAC umeendelea kuchangia sekta ya maji ambapo katika kipindi hiki,
Zanzibar imefadhiliwa mradi wa kujenga kituo kipya cha kutibu maji katika eneo
la Donge Mbiji, wilaya ya Kaskazini Unguja wenye thamani ya Dola za Marekani
milioni 5.5.
43.
Mheshimiwa Spika, Wizara yangu imeendelea kujenga
mahusiano mazuri na nchi marafiki na mashirika ya kimataifa ambao ni washirika
wetu wa maendeleo. Uhusiano huo mzuri umewezesha Serikali kupata ufadhili wa
miradi mbalimbali ya maendeleo. Miongoni mwa ufadhili huo ni ule uliotoka Umoja
wa Ulaya, Serikali ya Marekani kupitia shirika lake la maendeleo la USAID,
Serikali ya Uingereza kupitia shirika lake la maendeleo la DFID, Serikali ya
Japan kupitia shirika lake la maendeleo la JICA, Serikali ya Korea Kusini
kupitia shirika lake la maendeleo la KOICA, Serikali ya Ujerumani kupitia GIZ,
Serikali ya Denmark kupitia DANIDA, Serikali ya Canada kupitia CIDA, Serikali
ya Ufaransa kupitia shirika lake la AFD, Umoja wa Falme za Kiarabu kupitia
Mfuko wa Maendeleo wa Abudhabi, Serikali ya Saudi Arabia kupitia Mfuko wake wa
Maendeleo wa Saudia, pamoja na Serikali ya Kuwait kupitia Mfuko wake wa
maendeleo wa Kuwait. Serikali ya Oman pia imekubali kusaidia kufadhili
uboreshaji wa baadhi ya miundombinu katika mikoa mbalimbali ikiwa ni pamoja na
Jiji la Dodoma.
44.
Mheshimiwa Spika, halikadhalika, China imezikaribisha
nchi za Afrika kujiunga na mpango wake wa One Belt One Road Initiative ambao
unatoa manufaa mapana katika uwekezaji wa miundombinu ya nishati, reli,
barabara, bandari na viwanja vya ndege. Kutokana na hatua hiyo, nilipofanya
ziara yangu nchini China, niliwasilisha
maombi
ya Tanzania kujiunga na mpango huo. Napenda kulifahamisha Bunge lako kuwa,
mwezi Aprili 2018 Serikali ya China ilikubali ombi hilo na taratibu za kujiunga
na mpango huo zinaendelea.
Afya
na Ustawi wa Jamii
45.
Mheshimiwa Spika, sekta ya afya ni miongoni mwa sekta
zinazonufaika na ufadhili wa miradi ya maendeleo kutoka nchi wahisani pamoja na
washirika wetu wa maendeleo. Serikali ya Marekani mwezi Mei 2018 iliahidi kutoa
Dola za Marekani milioni 512 kufadhili Mpango wa Kupambana na Virusi vya Ukimwi
nchini chini ya program yake ijulikanayo kama President’s Emergency Plan for AIDS
Relief (PEPFAR). Serikali ya Kuwait pia imezindua mpango maalum wa kusaidia sekta ya afya hapa nchini wenye thamani
ya Dola za Marekani 500,000. Mpango huo ujulikanao kama Half-Million Dollar
Program umewezesha upatikanaji wa vifaatiba kwa watu wenye mahitaji maalum
katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Taasisi ya Mifupa ya MOI, pamoja na
Hospitali ya Benjamin Mkapa ya Dodoma. Aidha, Kuwait imetoa Dola za Marekani
milioni 13.6 kwa ajili ya kufanya ukarabati mkubwa katika Hospitali ya Rufaa ya
Mnazi Mmoja, Zanzibar; na Serikali ya China pia imesaidia ukarabati wa
Hospitali ya Abdulla Mzee, Pemba kama moja ya miradi yake ya afya hapa nchini.
Serikali ya Israel itaongeza misaada yake ya wataalam, mafunzo na vifaa kwa
Taasisi ya Moyo ya Jakaya Mrisho Kikwete.
46.
Mheshimiwa Spika, Tanzania pia imenufaika na Mfuko
wa Afya duniani ujulikanao kama Global Fund unaotoa ufadhili wa programu
mbalimbali za kukabiliana na maradhi ya Malaria, Kifua Kikuu na Ukimwi. Tangu
mfuko huo uanzishwe hapa nchini mwaka 2013, tayari Tanzania imenufaika na Dola
za Marekani takriban bilioni 2 na hivyo kuifanya Tanzania kuwa miongoni mwa
nchi zinazonufaika zaidi na ufadhili wa mfuko huo barani Afrika. Aidha, mwezi
Aprili 2018 Serikali ilisaini makubaliano na mfuko huo ya kiasi kingine cha
Dola za Marekani milioni 700 kwa ajili ya ufadhili wa miradi ya afya katika
kipindi cha miaka mitatu ijayo. Wadau wengine wanaosaidia sekta ya afya ni
mashirika ya maendeleo ya kimataifa pamoja na nchi marafiki kama vile
Uingereza, Denmark, Canada,
Ireland, Palestina, Umoja wa Falme
za Kiarabu, Cuba, Misri, Israel, Ujerumani, na Brazil.
Nishati
na Madini
47.
Mheshimiwa Spika, Wizara yangu kwa kutambua umuhimu
wa sekta hii katika maendeleo ya uchumi wa nchi imeendelea kuitafutia washirika
kutoka nchi marafiki na mashirika ya kimataifa katika miradi yake mbalimbali.
Miongoni mwa wafadhili wakubwa ni Benki ya Maendeleo ya Afrika na Benki ya
Dunia. Aidha, kupitia ziara iliyofanywa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway
hapa nchini mwezi Juni 2017, Serikali ya nchi hiyo imezindua awamu ya pili ya
program itakayodumu hadi mwaka 2020, kwa ajili ya kuendeleza sekta ya mafuta
nchini. Kupitia programu hiyo, Norway itatoa kiasi cha Dola za Marekani milioni
5.9
22
kwa
ajili ya kuendeleza sekta ya mafuta hapa nchini, na kiasi kingine cha Dola za
Marekani milioni 10.5 kwa ajili ya kuendeleza mfumo wa ukusanyaji kodi. Nchi
nyingine zinazofadhili miradi kwenye sekta hii kwa kupitia Wizara yangu ni
pamoja na Ujerumani, Sweden, Finland na India.
Elimu
na Mafunzo ya Ufundi
48.
Mheshimiwa Spika, Wizara yangu imeendelea kuratibu
upatikanaji wa fursa za masomo na mafunzo ya ufundi kutoka nchi marafiki.
Ufadhili huo ni katika mafunzo ya muda mfupi, shahada ya kwanza, uzamili,
uzamivu, uboreshaji mafunzo ya ualimu, uboreshaji mitaala na miundombinu ya
kufundishia katika vyuo vyetu vya ufundi na teknolojia; vitabu; pamoja na
ujenzi wa maktaba ya kisasa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Nachukua fursa
hii kuzishukuru nchi zote zinazofadhili miradi katika sekta ya elimu na mafunzo
ikiwa ni pamoja na China, Italia, Hungary, Poland, Uholanzi, Australia, India,
Malta, Misri, Korea, Malaysia, Indonesia, Vietnam, Japan, New Zealand, Algeria,
Uingereza, Ujerumani, Uswisi, Brunei, Oman, Cuba, Israel, Palestina na Saudi
Arabia. Natoa wito kwa Watanzania watumie fursa hizi ipasavyo.
Utalii
49.
Mheshimiwa Spika, Wizara yangu kupitia Balozi zetu
nje imeendelea kushirikiana na wadau wengine wa Serikali kutangaza vivutio vya
utalii na kuratibu ujio wa watalii nchini. Nafurahi kutambua ripoti iliyotolewa
mwezi
Mei
2018 na Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na ripoti za balozi zetu
zikiainisha kwamba idadi ya watalii nchini sio tu imeongezeka lakini pia pato
litokanalo na sekta hiyo limeongezeka. Aidha, ripoti hizo zimebainisha kwamba
tofauti na ilivyozoeleka huko nyuma kwa watalii wengi walikuwa wakitoka nchi za
Marekani, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Italia na Hispania, hivi sasa kuna
ongezeko kubwa pia la watalii kutoka nchi za China, Australia, Uholanzi,
Uswisi, India na Israel. Ongezeko hilo la idadi ya watalii ni matokeo ya kasi
ya kuvitangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini inayofanywa na mamlaka za
ndani pamoja na balozi zetu nje ya nchi. Wizara yangu kupitia balozi zetu
itaendeleza juhudi hizi kwa kasi zaidi hasa katika Balozi zetu mpya za Korea
Kusini, Uturuki, Qatar na Israel.
50.
Mheshimiwa Spika, katika kutangaza vivutio vya utalii
vya Tanzania katika nchi zenye watalii wengi, ubalozi wa Tanzania Beijing
umeendelea kutumia nafasi yake ya kimkakati kwa kutangaza utalii wetu kupitia
mitandao ya kijamii ya China kama QQ na WeChat kwa kuweka matangazo ya vivutio
kwa lugha za kichina. Aidha, ubalozi kwa kushirikiana na mamlaka za utalii
nchini ziliandaa ziara za waigizaji mashuhuri kutoka China ambapo waliandaa
makala za kutangaza utalii wa Kisiwapanza -Pemba, Hifadhi ya Taifa ya
Serengeti, Mbuga ya Selou na Ziwa Eyasi. Makala hizo zilizoandaliwa zimelenga
kutangazwa katika runinga zinazoangaliwa na watu wengi zaidi nchini China. Soko
la watalii kutoka China ni kubwa kuliko yote kama tukijitangaza vizuri
51.
Mheshimiwa Spika, kufuatia ziara ya meli ya Sultan wa
Oman mwezi Oktoba 2017, Serikali ya Oman imeahidi kukarabati na kuhifadhi Jumba
la Maajabu (Beit el Ajab) Zanzibar. Aidha, mwezi Aprili 2018 Tanzania na Oman
zilisaini makubaliano ya Ushirikiano katika masuala ya kumbukumbu na nyaraka
ili kukuza utalii unaotokana na historia kati ya Oman na Zanzibar.
Msamaha
wa madeni ya nje
52.
Mheshimiwa Spika, moja ya hatua inayofanywa na
Wizara yangu kwa kushirikiana na wizara nyingine ni kushawishi nchi marafiki
kutufutia madeni, kuyapunguza au kuweka masharti nafuu ya kuyalipa. Napenda
kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa nilipofanya ziara nchini Iran mwezi Oktoba
2017, Serikali ya nchi hiyo iliridhia na kutangaza kusamehe riba ya deni lililokopwa
mwaka 1984 ambayo kwa sasa imefikia kiasi cha Dola za Marekani milioni 150.
Aidha,
mwezi Septemba 2017, Serikali ya Brazil pia ilitoa msamaha wa thamani ya Dola
za Marekani milioni 203.6 ambayo ni asilimia 86 ya deni lote tunalodaiwa na
nchi hiyo. Misamaha hiyo ni wazi itaipa nafuu nchi yetu katika kulipa madeni.
Naomba kutumia nafasi hii kuzishukuru Serikali za Iran na Brazil kwa misamaha
hiyo.
53.
Mheshimiwa Spika, pamoja na wajibu wa Serikali kulipa
madeni yake nje, Wizara yangu kwa kushirikiana na wadau wengine ndani ya
Serikali itaendelea na juhudi za kuomba kusamehewa au kupata nafuu ya aina
yoyote
katika kulipa madeni ya Serikali. 25
MIKUTANO YA TUME ZA PAMOJA ZA KUDUMU ZA USHIRIKIANO
54.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka huu wa fedha, Wizara
kwa kushirikiana na wadau mbalimbali iliratibu na kushiriki katika mkutano wa
Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Misri uliofanyika
Cairo, mwezi Januari 2018. Mimi binafsi niliongoza ujumbe wa Tanzania katika
mkutano huo ambapo nchi zetu mbili zilikubaliana kushirikiana katika sekta za
viwanda, biashara na uwekezaji; maji; kilimo, mifugo na uvuvi; ujenzi, uchukuzi
na mawasiliano; afya, nishati, maliasili na utalii; elimu, mambo ya ndani ya
nchi na habari. Majadiliano ya utekelezaji wa maazimio mbalimbali yameshaanza
na tayari uongozi wa Shirika la ndege la Misri umeshatembelea nchini na
kukutana na wataalam wa Idara na Taasisi za Serikali.
USHIRIKI WA TANZANIA KATIKA JUMUIYA ZA KIKANDA NA
KIMATAIFA
Jumuiya za Kikanda Jumuiya
ya Afrika Mashariki
Uondoaji
wa Vikwazo Visivyo vya Forodha
55.
Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuratibu kamati
ya kitaifa ya kufuatilia uondoaji wa vikwazo vya kibiashara visivyo vya forodha
pamoja na mikutano
ya
kikanda kwa ajili ya kujadili vikwazo mbalimbali vinavyojitokeza. Kwa kipindi
cha mwezi Julai 2017 hadi Machi 2018, jumla ya vikwazo sita vilivyodumu kwa
muda mrefu vimeondolewa na hivyo kufikia jumla ya vikwazo 122 vilivyoondolewa
tangu mwaka 2009. Majadiliano ya kuviondoa vikwazo vingine 33 bado yanaendelea.
Miongoni mwa vikwazo vilivyoondolewa vinavyoihusu Tanzania ni kupunguzwa kwa
vizuizi barabarani katika njia kuu ya kati na kaskazini; kuwianisha muda wa
kufanya kazi baina ya mamlaka za mapato za Tanzania na Kenya kwenye ukaguzi wa
mizigo katika bandari kavu mjini Nairobi; kuondoa kodi ya ongezeko la thamani
katika huduma za bandari kwa mizigo inayosafirishwa kwenda nje ya nchi; tozo ya
Dola za Marekani 152 kwa mabasi yanayotoka Rwanda na zuio la kuuza bidhaa za
chakula kwenda Uganda, pamoja na kurekebisha sheria na kuainisha ubora wa
bidhaa mbalimbali tunazouziana.
Mapitio
ya Wigo wa Pamoja wa Ushuru wa Forodha
56.
Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na wadau
wengine imeendelea kuratibu na kusimamia mapitio ya Wigo wa Pamoja wa Ushuru wa
Forodha. Kwa sasa nchi za Jumuiya zimeendelea kufanya tafiti katika ngazi ya
nchi na kanda kwa lengo la kuwa na taarifa sahihi ya namna ya kupanga viwango
vya ushuru wa forodha katika Wigo wa Pamoja wa Ushuru wa Forodha wa Jumuiya.
Majumuisho ya awali ya matokeo ya tafiti kutoka kila nchi mwanachama wa Jumuiya
yanapendekeza mabadiliko ya viwango vya
ushuru
wa forodha yazingatie ukuzaji wa viwanda kwa nchi wanachama; kupunguza gharama
za uzalishaji; kuongeza biashara miongoni mwa nchi wanachama; na kuwalinda
walaji.
Utekelezaji wa Itifaki ya Soko la Pamoja la Afrika
Mashariki
57.
Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka wa fedha
2017/18, Wizara iliratibu majadiliano ya mapitio ya Jedwali la Biashara ya
Huduma katika Itifaki ya Soko la Pamoja. Lengo la kufanya mapitio hayo ni
kuondoa changamoto zilizokuwa zikikwaza utekelezaji wa Itifaki hiyo katika eneo
la huduma. Tayari nchi zote wanachama zimewasilisha maboresho ya jedwali la
huduma katika Itifaki ya Soko la Pamoja ambapo changamoto zilizoainishwa zimepatiwa
ufumbuzi.
58.
Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuratibu utoaji
wa elimu kwa umma mijini na vijijini ili kuwawezesha wananchi na hasa vijana
kushiriki katika kuchangamkia fursa zilizoko kwenye soko la Jumuiya ya Afrika
Mashariki. Wizara kwa kushirikiana na asasi za kiraia pamoja na vyombo vya
habari kupitia makongamano mbalimbali iliendesha programu maalum ya kuhamasisha
vijana wa Kitanzania kuzitambua na kuzitumia ipasavyo fursa zitokanazo na
Mtangamano wa Afrika Mashariki. Programu hiyo ilipewa jina la Kampeni ya
Msafara wa Vijana ya Biashara ya Kuvuka Mpaka. Kampeni hiyo ilifanyika katika
28
mikoa
ya Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, Manyara na Arusha. Wizara pia kwa
kushirikiana na Benki ya Dunia ilitoa elimu kwa umma kwa vijana wa vyuo vikuu
juu ya kuchangamkia fursa katika mtangamano.
Utekelezaji wa Itifaki ya Umoja wa Fedha ya Afrika
Mashariki
59.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2017/18
Wizara yangu imeendelea kuratibu na kushiriki katika uandaaji wa sera, sheria,
kanuni na taratibu za kuendeleza sekta ya fedha katika eneo la usimamizi wa
bima, huduma ndogo za kifedha (microfinance), pensheni na benki. Aidha, Wizara
yangu kwa mwaka wa fedha 2018/19 itaendelea kuratibu na kushiriki majadiliano
ya maeneo tajwa hapo juu hadi yatakapokamilika.
60.
Mheshimiwa Spika, ninapenda kuliarifu Bunge lako
Tukufu kuwa, Bunge la Afrika Mashariki lililokaa Dodoma mwezi Aprili 2018,
lilipokea na kujadili miswada miwili inayohusiana na utekelezaji wa Itifaki ya
Umoja wa Fedha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Miswada hiyo ni ya kuanzisha
Taasisi ya Fedha na Taasisi ya Takwimu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Muswada
wa Kuanzisha Taasisi ya Fedha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ulipitishwa na
Bunge hilo na hatua inayofuata ni kuidhinishwa na Wakuu wa Nchi Wanachama.
Ushirikiano Baina ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Kanda
Nyingine
61.
Mheshimiwa Spika, Viongozi Wakuu wa Nchi za Jumuiya
ya Afrika Mashariki katika mkutano wao wa 18 uliofanyika Dar es Salaam mwezi
Mei 2017 pamoja na mambo mengine, walikubaliana kuwa Mheshimiwa Yoweri Kaguta
Museveni, Rais wa Uganda na mwenyekiti wa Jumuiya, akutane na Rais wa Umoja wa
Ulaya, Mhe. Jean-Claude Juncker ili kujadili changamoto za Mkataba wa Ubia wa
Kiuchumi (EPA) baina ya Jumuiya hizo. Kufuatia maamuzi hayo, Wizara iliratibu
ushiriki wa Tanzania katika ziara hiyo iliyofanyika Brussels, Ubelgiji mwezi
Septemba 2017. Mwenyekiti aliwasilisha rasmi hoja za Jumuiya ya Afrika
Mashariki kuhusu changamoto za EPA na mwezi Desemba 2017, Rais wa Umoja wa
Ulaya, Mhe. Jean-Claude Juncker aliwasilisha majibu ya hoja hizo.
62.
Mheshimiwa Spika, katika Mkutano wa 19 wa Viongozi
Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Kampala mwezi Februari
2018 Rais wa Uganda na Mwenyekiti wa Jumuiya aliwasilisha majibu ya Umoja wa
Ulaya kwa Viongozi Wakuu wa Nchi za Jumuiya. Viongozi Wakuu hao hawakuridhishwa
na majibu yaliyotolewa na Umoja wa Ulaya hivyo, walimpa mamlaka Mwenyekiti wa
Jumuiya kuendelea kuwasiliana na Umoja wa Ulaya kwa lengo la kupata majibu
yanayoendana na hoja zilizowasilishwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki.
63.
Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2017/18,
Wizara iliendelea kuratibu majadiliano ya maeneo yaliyosalia katika kuanzisha
Eneo Huru la Biashara la Utatu wa COMESA-EAC-SADC pamoja na kuweka katika lugha
ya kiuandishi viambatisho vya Mkataba huo. Majadiliano yamekamilika katika
Kiambatisho Na. II kinachohusu Usuluhishi wa Migogoro ya Biashara, Kiambatisho
Na. IV kinachohusu Sheria ya Utambuzi wa Uasilia wa Bidhaa na Kiambatisho Na. X
kinachohusu Utatuzi wa Migogoro. Majadiliano yanaendelea baina ya nchi
wanachama kwenye kanuni za utambuzi wa uasilia wa bidhaa pamoja na uondoaji wa
ushuru wa forodha.
Sekta
za Uzalishaji
64.
Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na Wizara
ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji imeratibu maandalizi na ushiriki wa Tanzania
katika mikutano ya kuandaa sera na mikakati ya kukuza viwanda katika Jumuiya ya
Afrika Mashariki hususan katika maeneo yaliyoainishwa na Wakuu wa Nchi kuwa ya
vipaumbele hasa utengenezaji wa magari, uzalishaji wa dawa na bidhaa za nguo na
ngozi. Wizara ilihakikisha vipaumbele vya nchi vinajumuishwa katika sera na
mikakati iliyoandaliwa ikiwemo Mkakati wa Tano wa Maendeleo ya Jumuiya ya
Afrika Mashariki 2016/17-2020/21. Ni mategemeo yetu kuwa sera hizi za mtangamano
zitasaidia kukuza viwanda na hivyo kuchangia kuifikisha Tanzania katika uchumi
wa kati ifikapo mwaka 2025.
Uendelezaji wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii
65.
Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuratibu utekelezaji
wa programu na miradi ya kikanda ya uendelezaji wa miundombinu ya uchumi na
huduma za jamii kama ifuatavyo:
Maendeleo ya Miundombinu ya Uchukuzi, Nishati na Uwekezaji
katika Sekta ya Afya
66.
Mheshimiwa Spika, Wizara iliratibu na kushiriki katika
Mkutano wa Kazi wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
uliojadili maendeleo ya sekta ya miundombinu ya uchukuzi, nishati, na uwekezaji
katika sekta ya afya uliofanyika Kampala mwezi Februari 2018. Lengo la mkutano
huo lilikuwa ni kubaini kiasi cha fedha kinachohitajika kutekeleza miradi hiyo
ambapo imeelezwa kuwa katika miaka 10 ijayo kiasi cha Dola za Marekani bilioni
78 zitahitajika kutekeleza miradi ya miundombinu ya uchukuzi na nishati. Hivyo,
miradi 17 ya kipaumbele cha juu ilipitishwa ambapo miradi 10 kati ya hiyo
itatekelezwa Tanzania.
67.
Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha sekta ya afya,
Wakuu wa Nchi walipitisha vipaumbele tisa. Miongoni mwa vipaumbele hivyo ni
kupanua wigo wa huduma za tiba za ubingwa kwa kuimarisha miundombinu, vifaatiba
na
wataalam; na kupambana na magonjwa ya mlipuko 32
na
dharura za kiafya zinazotokana na mwingiliano wa kimataifa. Vilevile,
vipaumbele hivyo vimeelekezwa katika kujenga uwezo wa taasisi na vyuo
vinavyotoa mafunzo ya afya kwa kuwianisha mitaala ya mafunzo, viwango na
miongozo katika sekta ya afya ili kuwa na wataalam wa kutosha na wenye weledi;
kupanua wigo wa matumizi na huduma za bima ya afya na hifadhi ya afya ya jamii;
na kuendeleza utafiti katika sekta ya afya.
68.
Mheshimiwa Spika, ni matumaini yangu kuwa Wizara
za kisekta kwa kadri hali ya bajeti itakavyoruhusu, zitaendelea kutenga fedha
kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya kipaumbele.
Usimamizi
wa Mazingira Bonde la Ziwa Victoria
69.
Mheshimiwa Spika, wakati wa kikao kilichopita cha bajeti
cha 2017/18, nililiarifu Bunge lako Tukufu kuhusu Awamu ya Pili ya Mradi wa
Usimamizi wa Mazingira katika Ziwa Victoria. Naomba kuliarifu Bunge lako kuwa
mradi huo umekamilika mwezi Desemba 2017 ambapo faida zilizopatikana ni pamoja
na kupunguza magugu maji na kuwapatia maji safi na salama wananchi wanaoishi
maeneo ya mradi. Wizara yangu kwa kushirikiana na wadau wengine inaratibu
majadiliano ya Awamu ya Tatu ya Mradi huo.
70.
Mheshimiwa Spika, Wizara iliratibu upatikanaji wa
kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Kikanda
33
cha
Uratibu wa Usalama na Uokozi (Maritime Rescue Coordination Centre - MRCC)
katika Ziwa Victoria jijini Mwanza. Tanzania imewasilisha Hati ya Umiliki wa
Kiwanja chenye ukubwa wa mita za mraba 13,287 kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Ujenzi wa kituo hicho utakuwa na manufaa ya kurahisisha usafirishaji katika
Ziwa Victoria na udhibiti, uokozi na usalama.
Masuala
ya Siasa
71.
Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kuimarisha demokrasia,
utawala bora, na kulinda haki za binadamu kwa kushirikiana na nchi wanachama wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kwa kuzingatia hilo, Wizara iliratibu na kushiriki
kwenye kongamano la Utawala Bora la Jumuiya ya Afrika Mashariki lililofanyika
Arusha mwezi Oktoba 2017. Pamoja na mambo mengine, kongamano hilo liliazimia
kwamba Tume za Haki za Binadamu za nchi wanachama zitoe mafunzo kwa vyombo vya
usalama. Aidha, nchi wanachama zilitakiwa kuimarisha uwezo wa Tume za Uchaguzi
ili ziweze kutekeleza majukumu yake kwa usawa na kwa kuzingatia maadili.
Uchaguzi
Mkuu Nchini Kenya na Rwanda
72.
Mheshimiwa Spika, katika kuendeleza demokrasia na
kulinda amani katika Jumuiya, Tanzania ilikuwa sehemu ya timu ya waangalizi wa
uchaguzi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika chaguzi zilizofanyika nchini
Rwanda
34
na
Kenya mwaka 2017. Katika chaguzi hizo, Mheshimiwa Uhuru Kenyatta kutoka
muungano wa Jubilee alichaguliwa kuwa Rais Kenya na Mheshimiwa Paul Kagame
kutoka chama cha RPF alichaguliwa kuwa Rais Rwanda. Ripoti za usimamizi katika
chaguzi hizo zimeeleza kuwa chaguzi zilikuwa huru na haki. Nachukua nafasi hii kutoa
pongezi za dhati kwa wananchi wa Kenya na Rwanda kwa kufanya chaguzi kwa amani.
Fungamano
la Kisiasa la Afrika Mashariki
73.
Mheshimiwa Spika, Mkutano wa 35 wa dharura wa Baraza
la Mawaziri wa Jumuiya uliofanyika Kampala, mwezi Februari 2018 ulipitisha
Rasimu ya Andiko, Hadidu za Rejea, na Mpangokazi wa kuanzisha Fungamano la
Kisiasa la Afrika Mashariki. Aidha, maandalizi ya rasimu ya Katiba ya Fungamano
yanaendelea kwa mujibu wa mpangokazi ulioidhinishwa na zoezi hili linatarajiwa
kukamilika mwaka 2022.
Hati Mpya ya Kusafiria ya Kielektroniki ya Afrika
Mashariki
74.
Mheshimiwa Spika, Wakuu wa Nchi Wanachama wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki katika Mkutano wao wa 17 uliofanyika Arusha mwezi
Februari 2016 walizindua rasmi hati ya kusafiria ya kielektroniki ya Jumuiya ya
Afrika
Mashariki na kukubaliana kuwa kila
nchi mwanachama ianze kuzitumia ifikapo mwezi Januari 2018.
75.
Mheshimiwa Spika, napenda kulieleza Bunge lako Tukufu
kuwa mwezi Januari 2018, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Mugufuli, Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania alizindua rasmi hati hiyo kwa wananchi wa Tanzania.
Wananchi wa Tanzania wataruhusiwa kuendelea kutumia hati walizonazo kwa kipindi
cha miaka miwili hadi ifikapo mwezi Desemba 2019. Utoaji wa hati hizi
unasimamiwa na mamlaka husika katika kila nchi mwanachama kulingana na sheria
za nchi yake.
Mapambano
Dhidi ya Ugaidi na Uharamia
76.
Mheshimiwa Spika, Jumuiya ya Afrika Mashariki inaandaa
mpango wa utekelezaji wa mkakati wa kupambana na ugaidi. Mkutano wa wadau
uliofanyika Mwanza, mwezi Oktoba 2017 uliandaa mfumo utakaowezesha vyombo
vinavyohusika na mapambano dhidi ya ugaidi kufanya kazi kwa pamoja katika
kutekeleza mkakati huo.
77.
Mheshimiwa Spika, katika kupambana na uharamia kwenye
Bahari ya Hindi, Wizara kwa kushirikiana na wadau wengine imeendelea kuratibu
utekelezaji wa Mkakati wa Kikanda wa kupambana na uharamia kwa kuratibu
makubaliano maalum ya namna ya kubadilishana taarifa za wahalifu. Kufikiwa kwa
makubaliano hayo kutasaidia nchi wanachama kubadilishana uzoefu na kubaini
mbinu zinazotumiwa na maharamia ili kuimarisha mapambano dhidi ya uharamia
katika Bahari ya Hindi. Vilevile, Wizara kwa kushirikiana na Wizara ya Ulinzi
na Jeshi la Kujenga
Taifa
iliratibu zoezi la pamoja la kijeshi la kamandi za kijeshi ya nchi wanachama wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki lijulikanalo kama ‘EAC CPX USHIRIKIANO IMARA 2017’
lililofanyika Dar es Salaam mwezi Desemba 2017. Lengo la zoezi hilo lilikuwa ni
kujenga uwezo wa majeshi ya nchi wanachama katika kuendesha operesheni za
kulinda amani; kupambana na ugaidi; kupambana na uharamia; na kukabiliana na
majanga.
Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)
78.
Mheshimiwa Spika, Mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi
na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika ulifanyika Pretoria mwezi
Agosti 2017. Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo uliongozwa na Mheshimiwa
Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
akimwakilisha Mheshimiwa Rais.
79.
Mheshimiwa Spika, naomba kuliarifu Bunge lako
Tukufu kuwa Mheshimiwa Makamu wa Rais, kama Mwenyekiti wa Asasi hiyo,
aliwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Asasi ya SADC ya ushirikiano
katika siasa, ulinzi na usalama kwa kipindi cha Agosti 2016 hadi Agosti 2017.
Taarifa hiyo ilieleza kwa kina tathmini ya hali ya siasa, ulinzi na usalama
katika kanda hususan katika Nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jamhuri
ya Madagascar na Falme ya Lesotho. Tanzania ilipongezwa kwa kusimamia vizuri
majukumu ya Asasi hiyo.
80.
Mheshimiwa Spika, Mkutano huo, pamoja na mambo
mengine, ulimteua Dkt Stergomena L. Tax, kuendelea na wadhifa wa Katibu
Mtendaji wa SADC kwa kipindi cha pili na cha mwisho; uliazimia kuisaidia
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kufanya uchaguzi tarehe 23 Desemba
2018; na kuridhia ombi la Serikali ya Visiwa vya Comoro kuwa mwanachama wa 16
wa Jumuiya hiyo.
81.
Mheshimiwa Spika, napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu
kuwa Tanzania ilikabidhi rasmi uenyekiti wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano katika
Siasa, Ulinzi na Usalama kwa Jamhuri ya Angola.
Ushirikiano
kati ya SADC na Umoja wa Ulaya
82.
Mheshimiwa Spika, Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa
Afrika na Umoja wa Ulaya ziliingia makubaliano ya mpango wa ushirikiano wa
miaka mitano kuanzia mwaka 2015 hadi 2020. Katika Mpango huo, Umoja wa Ulaya,
pamoja na mambo mengine, uliridhia kutoa kiasi cha Euro milioni 31.6 kupitia
Awamu ya 11 ya Mfuko wa Maendeleo wa Umoja wa Ulaya, kuzisaidia nchi wanachama
wa SADC kutekeleza Itifaki ya Biashara. Tayari Tanzania imenufaika na mpango
huo kwa kupokea kiasi cha Euro 420,000 kati ya Euro milioni 1.4 zilizoahidiwa.
Kiasi hicho cha fedha kitatumika kufanya mapitio ya Sera ya viwanda ya
Tanzania, kuhamasisha biashara na kuondoa vikwazo vya
kibiashara visivyo vya kiushuru. 38
Jumuiya
ya Nchi Zinazopakana na Bahari ya Hindi
83.
Mheshimiwa Spika, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa
kushirikiana na IORA ilifanya warsha ya kuandaa Mkakati wa Kikanda wa Usimamizi
Endelevu wa Rasilimali za Uvuvi katika Ukanda wa Bahari ya Hindi mwezi Oktoba
2017.
84.
Mheshimiwa Spika, Serikali ya Tanzania imeanza kunufaika
na mtandao wa kupeana taarifa za biashara (IORA Trade Repository) ikiwemo mfumo
wa kodi, uasili wa bidhaa, taratibu za forodha na upatikanaji wa leseni za
uingizaji wa bidhaa kwa kila nchi iliyo ndani ya Jumuiya uliozinduliwa rasmi
mwezi Agosti 2017.
Umoja
wa Afrika
85.
Mheshimiwa Spika, Wizara iliratibu ushiriki wa Tanzania
kwenye Mkutano wa 30 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika
uliofanyika Addis Ababa mwezi Januari 2018. Katika Mkutano huo, Mheshimiwa
Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
alimuwakilisha Mheshimiwa Rais ambapo pamoja na mambo mengine, mkutano huo
ulijadili taarifa ya Mheshimiwa Paul Kagame, Rais wa Jamhuri ya Rwanda na
Mwenyekiti wa Kamati ya Kuhuisha Mifumo ya Kitaasisi ya Umoja wa Afrika.
Mkutano huo uliazimia nchi wanachama ziendelee na majadiliano ya namna bora ya
kutekeleza mapendekezo ya mabadiliko ya kuhuisha
Mifumo
ya Kitaasisi ya Umoja wa Afrika ili kufikia muafaka 39
kwa
nchi zote. Aidha, mkutano huo ulizindua soko moja la usafiri wa anga Afrika.
Hadi sasa nchi wanachama 21 zimesaini Mkataba wa soko hilo unaotarajiwa
kuchochea utalii na kuongeza ajira.
86.
Mheshimiwa Spika, katika Mkutano wa 29 wa Wakuu
wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika uliofanyika Addis Ababa mwezi Julai
2017, Tanzania ilipata nafasi ya kuchaguliwa kuwa miongoni mwa wajumbe wanne wa
Bodi ya Ushauri ya Umoja wa Afrika kuhusu Masuala ya Rushwa ambapo Bi. Sabina
Seja anaiwakilisha Tanzania. Wajumbe wengine kwenye Bodi hiyo ni Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo, Algeria na Misri.
87.
Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na Wizara
ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji iliratibu na kushiriki katika Mkutano wa
Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika uliofanyika Kigali
mwezi Machi 2018. Madhumuni ya mkutano huo yalikuwa kupitia mkataba na itifaki
tatu za uanzishwaji wa eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA). Hatua hiyo ni
utekelezaji wa maazimio ya Wakuu wa Nchi na Serikali yaliyofikiwa mwaka 2012
kutaka kuanzisha Eneo Huru la Biashara Afrika ambapo majadiliano yake
yalizinduliwa rasmi mwaka 2015 na kukamilika mwaka 2017. Katika mkutano huo
nchi wanachama 44 zilitia saini mkataba huo na hatua inayofuata ni nchi
kuridhia ili utekelezaji wake uanze rasmi.
88.
Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa mkataba huo utazisaidia
nchi za Afrika kukua kiuchumi kwa kushiriki kwenye soko la pamoja ambalo lina
watu zaidi ya bilioni moja na pato ghafi linalokadiriwa kuwa na jumla ya zaidi
ya Dola za Marekani trilioni 3.4. Ni muhimu kwa Tanzania kuongeza uzalishaji na
kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji wa mitaji ili kutumia vyema fursa
ya soko hilo.
Mkutano
wa Masuala ya Mipaka ya Nchi za Umoja wa Afrika
89.
Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza maazimio ya
Umoja wa Afrika yaliyofikiwa Addis Ababa mwezi Juni
2007,
Serikali imeendelea kuchukua hatua za kuhakiki na kuimarisha mipaka yake na
nchi tunazopakana nazo na tayari tumeanza kuhakiki mipaka kati ya Tanzania na
nchi za Kenya na Uganda.
90.
Mheshimiwa Spika, napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu
kuwa mbali na utekelezaji wa azimio hilo, zoezi la uhakiki wa mipaka ya nchi
yetu ni endelevu, na linalenga kuweka usimamizi mzuri wa maeneo ya mipaka;
kuimarisha ulinzi na usalama wa nchi yetu; kurahisisha ukusanyaji wa mapato
mipakani; kudhibiti uhalifu katika maeneo ya mipaka; kuweka mipango ya
maendeleo na utoaji wa huduma za msingi za jamii; na kuimarisha mahusiano
mazuri yaliyopo baina ya jamii za mipakani.
Umoja
wa Mataifa
91.
Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza jukumu lake la
kuratibu masuala ya kimataifa, Wizara yangu iliratibu na kushiriki mikutano
mbalimbali. Baadhi ya Mikutano hiyo ni pamoja na: Mkutano wa 72 wa Baraza Kuu
la Umoja wa Mataifa; UN-HABITAT; UNIDO; Mkutano wa Kamisheni ya Umoja wa
Mataifa kuhusu Hali ya Wanawake; Mikutano ya Kimataifa inayohusu wakimbizi na
uhamiaji; Baraza la Haki za Binadamu; Shirika la Chakula Duniani (FAO); na
Mkutano wa 25 wa Wakuu wa Serikali wa Jumuiya ya Madola.
92.
Mheshimiwa Spika, Wizara yangu iliratibu na kushiriki
katika Mkutano wa 72 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa uliofanyika New York,
Marekani kuanzia mwezi Septemba hadi Desemba 2017. Nilipata fursa ya
kumwakilisha Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania katika vikao vya ngazi ya juu vilivyokutanisha Wakuu wa
Nchi na Serikali za nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa. Masuala muhimu
yaliyojadiliwa wakati wa vikao hivyo yalihusu uhusiano wa kidiplomasia, ajenda
ya uendelezaji wa viwanda, biashara, uwekezaji, hali ya usalama na amani
duniani na mapambano dhidi ya ugaidi.
93.
Mheshimiwa Spika, pamoja na masuala mengine, Tanzania
ilitumia fursa hiyo kuelezea jitihada za Serikali
42
ya
Awamu ya Tano ya kuendelea kuimarisha ushirikiano na Umoja wa Mataifa na
Mashirika yake. Vilevile, Tanzania ilieleza hali ya utekelezaji wa ajenda ya
Umoja wa Mataifa ya mwaka 2030 (Malengo ya Maendeleo Endelevu) na hatua
zinazochukuliwa na Serikali katika kuwaletea maendeleo watu wake ikiwemo
mapambano dhidi ya rushwa; dawa za kulevya; uwindaji haramu; kuimarisha
ukusanyaji wa mapato ya ndani na kuziba mianya ya ukwepaji kodi; na kusimamia
uwajibikaji na nidhamu ya utumishi wa umma. Aidha, Tanzania ilitumia fursa hiyo
kuomba mashirika ya kimataifa na wadau wengine wa maendeleo kuendelea kutoa
misaada ya fedha, teknolojia na utaalam ili kuunga mkono juhudi za Serikali za
kuleta maendeleo endelevu na kuondoa umaskini nchini.
94.
Mheshimiwa Spika, Tanzania kama zilivyo nchi wanachama
wengine wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) ilishiriki katika Mkutano Mkuu wa 39 wa Shirika hilo
uliofanyika Paris mwezi Oktoba 2017. Ajenda kuu ya Tanzania katika Mkutano huo
ilikuwa kuwasilisha uamuzi wake wa kutekeleza mradi mkubwa wa umeme wa Stigler’s
Gorge. Katika kutekeleza azma hii, ujumbe wa Tanzania uliungana na wajumbe
wengine wa nchi zinazoendelea kusisitiza umuhimu wa Shirika hilo kuweka uwiano
kati ya uhifadhi wa maeneo ya urithi wa dunia na kuwekeza kwenye miradi ya
maendeleo kwenye maeneo husika. Aidha, nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania
zilitumia mkutano huo kuomba msaada wa kuimarisha miundombinu katika
95.
Mheshimiwa Spika, Wizara yangu inaendelea kushirikiana
na wadau wengine kusukuma ajenda ya kitaifa ya kufikia uchumi wa viwanda
ifikapo mwaka 2025. Katika kutekeleza azma ya kukuza viwanda, Wizara iliratibu
ujio wa Dkt. Li Yong, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Maendeleo ya Viwanda Duniani (UNIDO) mwezi Machi 2018. Moja
ya manufaa ya ziara hiyo ilikuwa ni kusainiwa kwa tamko la kusudio la kuiingiza
Tanzania katika mpango maalum wa ushirikiano wa kuendeleza viwanda unaojulikana
kama Program for Country Partnership. Kwa kuwa mpango huu umefanyika kwa
mafanikio katika nchi za Ethiopia, Senegal na Peru, Tanzania inaendelea na
majadiliano ya karibu na UNIDO ili nayo iingizwe katika mpango huo wenye fursa
kubwa katika kusukuma maendeleo ya viwanda ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya
viwanda.
96.
Mheshimiwa Spika, katika ziara hiyo Shirika la UNIDO
lilitoa msaada wa vifaa vya kilimo vyenye thamani ya Dola za Marekani 80,000
kwa wakulima wa zao la mwani Zanzibar. Vifaa hivyo vitatumika kwa ajili ya
shughuli za kilimo, usafirishaji na usindikaji wa mwani jambo ambalo litasaidia
kuongeza thamani ya zao hilo katika soko la dunia.
97.
Mheshimiwa Spika, mwaka jana nililijulisha Bunge lako
Tukufu kwamba Serikali ipo katika hatua za mwisho za
44
kuridhia
Mkataba wa Paris chini ya mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya
Tabianchi ambao Bunge lako Tukufu liliridhia mwezi Aprili 2018. Napenda
kulishukuru Bunge lako Tukufu kwa hatua hiyo na tayari Mheshimiwa Rais alisaini
hati ya kuridhia na hivyo kuwezesha nchi yetu kutambuliwa rasmi kama mwanachama
wa makubaliano hayo. Naomba kutumia fursa hii kukushukuru wewe Mheshimiwa
Spika, kuwashukuru Waheshimiwa Wabunge na wadau wengine wote ndani na nje ya
Serikali kwa ushirikiano mkubwa waliotoa kuwezesha suala hili kufanikiwa. Ni
dhahiri kwamba makubaliano haya yana manufaa kwa nchi yetu na dunia nzima.
Kushughulikia
Masuala ya Wakimbizi
98.
Mheshimiwa Spika, moja ya nguzo za Sera ya Mambo
ya Nje ya Tanzania ni kulinda utaifa wetu, mipaka ya nchi na uhuru wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania. Katika kusimamia nguzo hii muhimu, mwezi Januari 2018,
Serikali ilifanya uamuzi wa kujitoa kwenye mpango maalum wa majaribio wa
kuhudumia Wakimbizi ujulikanao kama Comprehensive Refugees Response Framework
(CRRF). Mpango huo unalenga kuwanufaisha wakimbizi kwa kupanua wigo wa hifadhi
yao na kuwawezesha kujitegemea kwa Serikali kuwapatia ardhi, uhuru wa kutembea
mahali popote na vibali vya kufanya kazi popote nchini.
99.
Mheshimiwa Spika, uamuzi wa Serikali kujitoa kwenye
Mpango huo umezingatia maslahi mapana ya
45
Taifa
letu hususan masuala ya usalama. Nitumie fursa hii kulihakikishia Bunge lako
Tukufu kuwa pamoja na nia yetu nzuri ya kuwasaidia wakimbizi; usalama, amani na
ulinzi wa Taifa letu ndivyo vipaumbele namba moja vya Taifa letu.
100.
Mheshimiwa Spika, pamoja na Serikali kutokuafiki mpango
huo bado Tanzania itaendelea kupokea na kuhifadhi wakimbizi pale inapolazimika
kwa kuzingatia sheria za nchi na mikataba ya kikanda na kimataifa. Aidha,
tunaendelea kutoa wito kwa wakimbizi kurudi makwao kwa hiari pale ambapo hali
ya usalama kwenye nchi zao inapotengemaa.
Jumuiya
ya Madola
101.
Mheshimiwa Spika, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, alimwakilisha Rais kwenye
mkutano wa 25 wa Wakuu wa Serikali wa Jumuiya ya Madola uliofanyika London
mwezi Aprili 2018. Mkutano huo, pamoja na mambo mengine, ulipitisha maazimio
matano yanayosisitiza kuifanya dunia kuwa mahali penye ustawi na salama zaidi
ili kuchochea maendeleo, kuleta usawa, utunzaji wa mazingira, amani, haki za
binadamu na demokrasia. Maazimio hayo pia yameweka msisitizo kwenye mapambano
dhidi ya ugaidi, usafirishaji haramu wa binadamu, utumwa, makundi yenye
misimamo mikali na uhalifu mwingine wa kimataifa.
102.
Mheshimiwa Spika, Wakuu wa Serikali kwa kauli moja
walikubaliana kufanya kila liwezekanalo kuongeza biashara na uwekezaji miongoni
mwa nchi wanachama. Tanzania ilifanikiwa kuingiza ajenda ya viwanda, nishati ya
uhakika na kukuza uchumi kuwa sehemu ya majadiliano na hatimaye kuingia kwenye
tamko la mwisho la mkutano huo.
103.
Mheshimiwa Spika, wakati wa mkutano huo, Mheshimiwa
Makamu wa Rais alifanya mazungumzo na viongozi wa nchi mbalimbali wakiwemo Rais
wa Uganda, Waziri Mkuu wa Australia, Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa
Uingereza na Mjukuu wa Malkia, Prince William. Katika mikutano hiyo, viongozi
hao waliahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala mbalimbali
yakiwemo ya elimu, biashara na uwekezaji na mapambano dhidi ya ujangili na
biashara haramu ya wanyamapori. Prince William ni mmoja kati ya viongozi
wanaounga mkono jitihada za Tanzania katika mapambano dhidi ya ujangili na
uwindaji haramu.
104.
Mheshimiwa Spika, akiwa London, Mheshimiwa Makamu
wa Rais alikutana na viongozi wa makampuni sita yanayowekeza na yenye nia ya
kuwekeza nchini Tanzania. Kwenye mikutano hiyo, Mheshimiwa Makamu wa Rais
aliwathibitishia na kuwahakikishia kuimarika kwa mazingira ya uwekezaji nchini
na kukaribisha wawekezaji wengine.
KUSIMAMIA MIKATABA NA MAKUBALIANO YA KIMATAIFA
105.
Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka wa fedha
2017/18 Wizara iliratibu na kusimamia kusainiwa kwa mikataba, hati za
makubaliano na kumbukumbu za mazungumzo baina ya Tanzania na nchi mbalimbali.
Mikataba na makubaliano hayo ni kiashiria kikubwa katika kuimarisha uhusiano wa
kidiplomasia baina ya nchi yetu na nchi nyingine, mashirika ya Kikanda na
Kimataifa katika kuongeza kasi ya kuvutia uwekezaji, kukuza biashara na kutangaza
utalii. Wizara inaendelea kufuatilia utekelezaji wa mikataba hiyo kwa
kuzingatia maslahi mapana ya nchi yetu. Orodha ya mikataba na hati za
makubaliano zilizosainiwa katika kipindi hicho ni kama inavyooneshwa kwenye Kiambatisho.
KURATIBU NA KUSIMAMIA MASUALA YA WATANZANIA WAISHIO
UGHAIBUNI
106.
Mheshimiwa Spika, kwa kutambua Watanzania wanaoishi
ughaibuni kama wadau muhimu wa maendeleo, Wizara yangu imeendelea kubuni mbinu
mbalimbali za kuwashirikisha katika kuchangia maendeleo ya nchi. Moja ya mbinu
hizo ni kuandaa makongamano ndani na nje ya nchi ambapo mwezi Agosti 2017,
Wizara yangu kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar iliandaa
Kongamano la Nne la Diaspora lililowakutanisha Watanzania zaidi ya 200 kutoka
nchi mbalimbali na wadau
wa
maendeleo hapa nchini. Kupitia kongamano hilo, Diaspora walihimizwa kushiriki
kikamilifu katika ujenzi wa Taifa letu kwa kuhamasisha uwekezaji wa mitaji
kutoka nje.
107.
Mheshimiwa Spika, mwezi Aprili 2018 lilifanyika kongamano
lingine lililoandaliwa na Diaspora jijini Dallas Marekani, ambalo pamoja na
masuala mengine, lililenga kutangaza vivutio vya utalii nchini pamoja na
kuhamasisha wawekezaji kwenye sekta mbalimbali ikiwemo utalii.
108.
Mheshimiwa Spika, mchango wa Diaspora katika
maendeleo ya nchi unajidhihirisha katika maeneo mbalimbali ya kiuchumi na
kijamii. Yafuatayo ni baadhi ya maeneo hayo:
i.
Diaspora imenunua nyumba zenye thamani ya Shilingi bilioni
29.7 kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa ajili ya nyumba za makazi,
ofisi, maeneo ya biashara na viwanja mbalimbali kati ya mwaka 2011 hadi 2017.
ii.
Takwimu za Benki Kuu ya Tanzania zinaonesha kuwa kwa
kipindi cha miaka mitano iliyopita 2013-2017, Diaspora kwa ujumla wao walituma
nchini kiasi kisichopungua Dola za Marekani bilioni 2.3.
iii.
Timu ya madaktari wa kitanzania waishio Marekani kupitia
taasisi ya afya, elimu na maendeleo (Head Inc.) ilitoa huduma ya afya bila
malipo na vifaatiba katika hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar, vyenye thamani ya
zaidi ya shilingi bilioni moja;
iv.
Jumuiya ya Watanzania nchini Marekani (DICOTA) iliandaa
jukwaa la afya mwezi Novemba 2017 ambalo lilihudhuriwa na wataalam wa afya
zaidi ya 130 kutoka Tanzania na Marekani ili kubadilishana ujuzi, uzoefu na
kutathmini njia madhubuti za kuendeleza sekta ya afya nchini Tanzania. Juhudi
hizi ziliwezesha kupatikana kwa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi na wafanyakazi
zaidi ya 60 kutoka vyuo vikuu na hospitali nchini ikiwemo Chuo Kikuu cha Tiba
KCMC, Hubert Kairuki, Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili na
hospitali ya Bugando.
v.
Aidha, Dkt. Frank Minja mtanzania mtaalam wa Radiolojia wa
Chuo Kikuu cha Yale Marekani amesaidia kuimarisha mfumo wa teknolojia ya kisasa
ya radiolojia katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
109.
Mheshimiwa Spika, wakati ambapo kipaumbele cha
kitaifa ni viwanda, tunahitaji kufikiria ujuzi maalum
50
walionao
Watanzania wanaoishi katika Diaspora, na vile vile mchango wa kifedha ambao
wanaweza kuchangia kutoka kwenye vyanzo vyao binafsi au kwa kushirikiana na
raia wa nje, mabenki na taasisi nyingine za nje. Ili kuwezesha viwanda vyetu
kuuza nje, tunahitaji kutambua, kupima na kupenya katika masoko mbalimbali ya
kigeni. Watanzania walioishi nchi za kigeni na watoto wao wanaweza kuchangia
zaidi kutokana na ujuzi wao kwa kupata masoko kwa kutumia ujuzi wao wa lugha za
kigeni.
110.
Mheshimiwa Spika, watanzania wengi walio Diaspora
wanachangia sana maendeleo ya kijamii na uchumi wa familia zao na Tanzania kwa
ujumla, na wako tayari kushiriki katika jukumu kubwa la kujenga uchumi wa Taifa
hili. Pengine tunahitaji kuwa na mfumo wa kisheria na sera ya kutoa huduma hiyo
kwa uhalali na uhakika.
TATHMINI YA HALI YA DUNIA Hali ya usalama
111.
Mheshimiwa Spika, hali ya usalama duniani imeendelea
kuimarika pamoja na kwamba changamoto kadhaa zimeendelea kuwepo katika baadhi
ya maeneo. Changamoto hizo ni pamoja na migogoro ya kisiasa katika baadhi ya
nchi, matukio ya kigaidi na kuongezeka makundi yenye itikadi kali na athari za
kiusalama zinazosababishwa na mabadiliko ya tabianchi. Katika kukabiliana na
changamoto hizo, Tanzania imeendelea kuunga mkono
jitihada
za kikanda na za Umoja wa Mataifa za kuimarisha amani na usalama duniani.
112.
Mheshimiwa Spika, kuhusu migogoro ya kisiasa
katika baadhi ya nchi, naomba nitumie fursa hii kuizungumzia kama ifuatavyo:
Lesotho
113.
Mheshimiwa Spika, hali ya siasa, ulinzi na usalama nchini
Lesotho bado hairidhishi. SADC ilituma misheni maalum ya ulinzi wa amani ili
kusaidia nchi hiyo kutekeleza maazimio ya kurejesha amani. Naomba niliarifu
Bunge lako Tukufu kuwa misheni hiyo ilizinduliwa rasmi tarehe
2
Desemba 2017 na ina jumla ya maafisa 269. Serikali ya Lesotho imetakiwa
kutekeleza maazimio yanayohusu maboresho ya mifumo ya Serikali kwa kipindi cha
mwaka mmoja.
Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo
114.
Mheshimiwa Spika, hali ya ulinzi na usalama nchini
DRC hairidhishi. Hivi sasa Serikali ya nchi hiyo inaendelea na maandalizi ya
Uchaguzi Mkuu ambao umepangwa kufanyika tarehe 23 Desemba 2018. Maandalizi ya
uchaguzi huu yanaendelea vizuri ikiwa ni pamoja na kukamilika kwa zoezi la
kuandikisha wapiga kura na kupitisha sheria mpya ya uchaguzi. Natoa rai kwa
wadau wa ndani na nje kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa utulivu kama
ulivyopangwa. Hata hivyo, DRC inahitaji kusaidiwa kwa hali na mali katika
kuandaa uchaguzi huo
hususan
ikizingatiwa kuwa nchi hiyo ni kubwa kuliko nchi yoyote Barani Afrika.
Madagascar
115.
Mheshimiwa Spika, hali ya siasa nchini Madagascar hairidhishi
na SADC imetuma ujumbe wa Baraza la ushauri la masuala ya uchaguzi nchini humo
ili kufanya tathmini ya utayari wa nchi hiyo kufanya uchaguzi mkuu Novemba
2018. Aidha, SADC ilimtuma Mheshimiwa Joaquim Chissano, Rais Mstaafu wa
Msumbiji na mjumbe maalum wa SADC tarehe 8 hadi 13 Mei 2018 kwa lengo la
kusaidia kuweka mazingira ya amani kabla ya uchaguzi mkuu.
Sudan
Kusini
116.
Mheshimiwa Spika, hali ya usalama nchini Sudan Kusini
imeendelea kuwa ya wasiwasi kutokana na uhasama kati ya Serikali na upinzani.
Aidha, hatua ya waliokuwa viongozi wa juu wa jeshi la nchi hiyo kuamua kuunda
vikundi vya uasi imezidi kuchochea mgogoro huo. Hadi sasa mgogoro huo
umesababisha zaidi ya watu milioni mbili kukimbilia nchi jirani na wengine
zaidi ya 230,000 kulazimika kuyakimbia makazi yao na kuhifadhiwa kwenye makambi
ya Umoja wa Mataifa nchini humo.
117.
Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa mkataba wa mwezi
Agosti 2015 wa kugawana madaraka umeendelea kusuasua licha ya jitihada za
Jumuiya ya Maendeleo ya IGAD za mwaka 2017 za kufufua utekelezaji wa
makubaliano
hayo.
Jumuiya ya Afrika Mashariki, Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya zinaendelea
kutafuta suluhu ya kudumu ya mgogoro huo. Tanzania inaunga mkono jitihada zote
zinazofanywa kutafuta suluhu ya kudumu nchini humo.
Somalia
118.
Mheshimiwa Spika, hali ya usalama na siasa nchini Somalia
inaendelea kuimarika baada ya kuwa na Katiba mpya na uchaguzi wa Bunge
kufanyika. Kwa kupitia jitihada kubwa za Jeshi la Serikali ya Somalia kwa
kushirikiana na AMISOM, Serikali imerejesha zaidi ya asilimia 80 ya maeneo
yaliyokuwa yanashikiliwa na kikundi cha kigaidi cha al-Shabaab. Hata hivyo,
pamoja na mafanikio hayo kikundi hicho kimeendelea kuwa ni kikwazo cha kuleta
amani nchini humo.
119.
Mheshimiwa Spika, kwa upande mwingine majeshi
ya AMISOM yameanza kuondoa askari wake na kuhamasisha Jeshi la Somalia kuanza
kuchukua jukumu la kulinda usalama wa nchi yake. Katika kipindi cha mwezi
Oktoba na Desemba 2017, jumla ya askari 1,000 wa AMISOM waliondolewa na
kurudishwa katika nchi zao. Tanzania inaitakia Serikali ya Somalia na watu wake
mafanikio katika mipango ya kurejesha na kuimarisha amani na usalama nchini
humo.
120.
Mheshimiwa Spika, hali ya amani na usalama nchini
Libya ni tete. Hali hiyo imechangiwa na Dola kukosa udhibiti wa nchi,
kuongezeka kwa makundi yanayokinzana na kukwama kwa mazungumzo ya amani.
Tanzania inaunga mkono juhudi za kimataifa zinazoendelea kupitia Umoja wa
Afrika za kuupatia ufumbuzi mgogoro huo.
121.
Mheshimiwa Spika, siku za hivi karibuni, imeripotiwa
kuibuka kwa biashara haramu ya binadamu na utumwa katika baadhi ya maeneo
nchini Libya. Tanzania inalaani kwa nguvu zote kuwepo kwa biashara hiyo na
kuitaka jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua stahiki kwa wale waliohusika.
Burundi
122.
Mheshimiwa Spika, kuhusu mgogoro wa kisiasa nchini
Burundi napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kwamba jitihada kubwa zinazofanywa
na Jumuiya ya Afrika Mashariki, chini ya usuluhishi wa Mheshimiwa Yoweri Kaguta
Museveni, Rais wa Uganda akisaidiwa na Mwezeshaji Mheshimiwa Benjamin William
Mkapa, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zimesaidia kurejesha
hali ya amani na utulivu nchini Burundi tofauti na ilivyokuwa mwaka 2015
mgogoro huo ulipoibuka.
123.
Mheshimiwa Spika, Wizara iliratibu na kushiriki katika
mazungumzo ya kutatua mgogoro wa kisiasa nchini Burundi uliofanyika Arusha,
mwezi Novemba 2017. Mazungumzo hayo yalijumuisha Serikali ya Jamhuri ya Burundi
na makundi yanayohusika na mgogoro huo wakiwemo wanasiasa, Marais wastaafu,
viongozi wa dini, vyama vya siasa na vyama vya kiraia.
Syria
124.
Mheshimiwa Spika, mgogoro wa Syria bado unaendelea
kuwa moja kati ya ajenda muhimu kwenye jumuiya ya kimataifa. Mgogoro huo
unazidi kuwa mgumu kutokana na mvutano wa mataifa makubwa. Tunayasihi mataifa
yanayohusika na mgogoro huo kushirikiana ili kurejesha amani nchini humo kwa
njia ya mazungumzo. Hii inatokana na ukweli kwamba vita vinavyoendelea baina ya
makundi mbalimbali yanayoungwa mkono na nchi za kigeni huzidisha uhasama na
kusababisha hasara kubwa kwa maisha ya binadamu wasio na hatia pamoja na
uharibifu wa miundombinu ya nchi hiyo.
Yemen
125.
Mheshimiwa Spika, Tanzania ina imani kwamba wananchi
wa Yemen wana haki ya kujiamulia mustakabali wa nchi yao. Kutokana na mgogoro
huo idadi ya vifo, raia wanaokimbia nchi yao na wanaopoteza makazi inazidi
kuongezeka. Tanzania inaamini kuwa mgogoro huu
unaweza
kupatiwa suluhu kwa pande zinazohasimiana kukaa pamoja na inaunga mkono juhudi
za usuluhisho wa mgogoro huo, kupitia jumuiya za kimataifa.
Iran
126.
Mheshimiwa Spika, mwaka 2015 nchi wanachama wa
kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na Ujerumani ziliingia
makubaliano na Iran kuhusu mpango wake wa nyuklia ili kuondolewa vikwazo vya
kiuchumi. Mkataba huo ulitoa matumaini ya ushirikiano wa kimataifa katika
juhudi za kuondokana na silaha za nyuklia. Hata hivyo mwanzoni mwa mwezi Mei
2018, mmojawapo wa wadau wakuu ametangaza kujitoa katika mkataba huo. Tanzania
inazisihi pande zote zinazohusika kuendelea kuheshimu mkataba huo na kama kuna
dosari katika mkataba huo zitatuliwe kwa njia ya mazungumzo.
Rasi
ya Korea
127.
Mheshimiwa Spika, Rasi ya Korea ni miongoni mwa
maeneo yenye historia ya mgogoro wa muda mrefu na kutishia hali ya amani na
usalama duniani. Hata hivyo, hali hiyo imeanza kubadilika kufuatia tukio la
kihistoria lililoshuhudiwa mwezi Aprili 2018 wakati Marais wa Korea Kaskazini
na Korea Kusini walipokutana katika eneo la mpaka wa nchi hizo (Demilitarized
Zone) baada ya zaidi ya miaka 50 ya uhasama. Marais hao walikutana kujadili
namna ya kumaliza tofauti zao na kushirikiana. Aidha,
mkutano
huo umefanyika baada ya miaka 10 tangu viongozi watangulizi wa nchi hizo mbili,
Rais Kim Jong Il na Rais Roh Moo-hyun kukutana mwaka 2007.
128.
Mheshimiwa Spika, baada ya Rais wa Jamhuri ya Korea
Moon Jae-in kuingia madarakani mwaka 2017, moja ya agenda za serikali yake
ilikuwa ni kukaa katika meza ya majadiliano na Korea ya Kaskazini ili kutafuta
suhuhu. Nia hiyo njema ya kiongozi huyo iliimarishwa na hotuba ya Rais wa Korea
Kaskazini ya mwaka mpya 2018, ambapo alimtakia heri na mafanikio Rais wa Korea
Kusini katika kuwa mwenyeji wa mashindano ya olimpiki ya majira ya baridi ya
Februari 2018. Baada ya salamu hizo Rais wa Korea Kusini alimwalika mwenzake
kushiriki ufunguzi pamoja na kutuma timu kushiriki katika mashindano hayo.
Mwanzo huo mzuri ulizaa matunda na dunia iliendelea kushuhudia mazungumzo
mbalimbali katika ngazi za juu za Maofisa wa usalama wa nchi hizo mbili na
hatimaye mkutano huu wa kihistoria.
129.
Mheshimiwa Spika, Tanzania kama nchi mwanachama
wa Umoja wa Mataifa, ambayo imekuwa ikichangia sana katika harakati za
kuimarisha amani na usalama duniani, na kusimamia suluhu ya migogoro kupitia
mazungumzo inapongeza kwa dhati hatua hii ambayo imeonesha umuhimu wa
diplomasia katika kutatua migogoro kwa njia ya mazungumzo. Dunia inasubiri kwa
hamu matokeo ya mazungumzo kati ya Rais Donald Trump wa Marekani na rais Kim
Jong-un wa Korea ya Kaskazini
58
yatakayofanyika baadae mwaka huu.
Bahari
ya Kusini ya China (South China Sea)
130.
Mheshimiwa Spika, Tanzania imekuwa ikifuatilia kwa
makini hali ya usalama katika Bahari ya Kusini ya China na visiwa vyake.
Tunaunga mkono msimamo wa China unaotaka pawe na mazungumzo baina ya nchi
zinazohusika katika kutatua mgogoro na kuondoa tofauti zilizopo kati ya nchi
hizo kwa mazungumzo ili kufikia suluhu kwa njia ya amani.
Nchi
za Ghuba
131.
Mheshimiwa Spika, Tanzania inafuatilia kwa makini
mwelekeo wa siasa na tofauti zilizopo katika nchi za ghuba, hususan Saudi
Arabia, Falme za Kiarabu, Bahrain na Misri kwa upande moja na Qatar kwa upande
mwingine, nchi zote hizi zina uhusiano mzuri na Tanzania. Nchi hizi zina
rasilimali kubwa ya mafuta na gesi ambayo ni muhimu kwa uchumi wao na dunia kwa
ujumla. Tanzania inazisihi nchi hizi ambazo ni muhimu kwa amani na uchumi wa
dunia kuzungumza na kufikia muafaka wa tofauti zao kwa amani.
132.
Mheshimiwa Spika, uchumi wa dunia umeendelea kuimarika
ambapo kwa sasa unakadiriwa kukua kwa asilimia 3 ikilinganishwa na asilimia 2.4
mwaka 2016. Ukuaji huo umechangiwa zaidi na kuimarika kwa uchumi wa mataifa
yaliyoendelea, uwekezaji wa mitaji kwenye nchi zinazoibukia kiuchumi, pamoja na
kupanda kwa bei za bidhaa. Hali hii inatoa matumaini ya kuimarika kwa biashara
ya bidhaa hususan kutoka nchi zinazoendelea.
133.
Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Afrika, shughuli
za kiuchumi zimeendelea kuimarika zikisaidiwa kwa kiasi kikubwa na kuimarika
kwa uchumi wa mataifa yaliyoendelea pamoja na masoko yanayoibukia. Uchumi wa
Afrika unakadiriwa kukua kwa asilimia 3.1 mwaka 2018 kutoka asilimia 1.5 mwaka
2016. Ukuaji huu unatarajiwa kuendelea kutokana na kuimarika kwa hali ya soko
la fedha la nje (external financial market conditions). Hali hii itasaidia
kuongezeka kwa uwekezaji katika miundombinu ya kimkakati kama vile reli,
bandari na barabara. Hata hivyo, ukuaji wa uchumi katika Afrika unatarajiwa
kuwa na viwango tofauti ambapo nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zinatarajiwa
kuendelea kuimarika zaidi. Aidha, Tanzania inatarajiwa kuendelea kuwa kinara
katika ukuaji wa uchumi ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na hata katika
Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika.
134.
Mheshimiwa Spika, hali hii nzuri ya ukuaji kiuchumi
kwa ujumla wake, unaweza kuathiriwa na baadhi ya matatizo ya kimfumo hususan
kwenye sekta ya fedha na kodi. Jumuiya ya kimataifa inapaswa kuweka mfumo
mahsusi wa ushirikiano wa masuala ya kodi kwa ajili ya kuondoa ushindani wa
kukusanya kodi na kuyalazimisha makampuni ya kimataifa kulipa kodi stahiki
kwenye nchi yanapowekeza. Aidha, Tanzania inahamasisha ushirikiano madhubuti wa
kimataifa kwa ajili ya kukabiliana na uhamishwaji haramu wa fedha ili kupambana
na vitendo vya rushwa vya kimataifa. Kwa sasa thamani ya fedha zinazohamishwa
kutoka nchi zinazoendelea kwenda nchi tajiri ni kubwa kuliko thamani ya misaada
ya maendeleo inayotolewa kwa nchi zinazoendelea hivyo ni muhimu kuwa na mkakati
wa pamoja kudhibiti uhalifu huu unaokwamisha jitihada za maendeleo Afrika na
kwingineko. Changamoto hizi zinahitaji ushirikiano wa kimataifa kuzitatua na
kuimarisha mifumo ya kisiasa na kiusalama ili kuweka mazingira mazuri ya
kujenga uchumi imara kwa watu wote.
135.
Mheshimiwa Spika, tangu kuanzishwa kwake Shirika
la Biashara Duniani (WTO), limekuwa muhimili mkubwa katika kuhakikisha biashara
duniani zinaendeshwa kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizojadiliwa
na kukubalika na nchi zote wanachama. Kama leo hii pasingekuwepo na WTO ili
kusimamia uendeshaji wa biashara na hasa kulinda maslahi ya nchi zinazoendelea
kama Tanzania, dunia ingekuwa siyo mahali salama pakufanya biashara. Migogoro
na mivutano ya
kibiashara ingekuwa mingi na
ingezorotesha maendeleo.
136.
Mheshimiwa Spika, hivi sasa Shirika hili linapitia changamoto
zinazotishia uwepo wake na ustawi wa biashara duniani tangu kuanzishwa kwake
miaka zaidi ya 20 iliyopita. Hali hii inasababishwa na kuongezeka kwa maamuzi
ya nchi moja moja (unilateralism) badala ya kuzingatia misingi ya kuamua kwa
pamoja (multilateralism) iliyojengwa na WTO. Nchi zinazoendelea zikiruhusu
hili, zitakuwa za kwanza kuangamia. Natoa wito kwa nchi zote hususan
zilizoendelea kuheshimu na kulinda misingi ya ushirikiano wa kimataifa katika
kufanya maamuzi ya biashara duniani. Pale panapotokea sintofahamu, ni vizuri
kufuata taratibu za usuluhishi za kimataifa zinazokubalika.
137.
Mheshimiwa Spika, naomba kuliarifu Bunge lako Tukufu
kuwa Tanzania itaendelea kusimamia na kutetea misingi ya ushirikiano wa
kimataifa katika kufikia maamuzi yanayohusu mustakabali wa dunia kwenye nyanja
zote.
TAASISI
ZILIZO CHINI YA WIZARA
138.
Mheshimiwa Spika, Wizara inasimamia taasisi tatu
ambazo ni Chuo cha Diplomasia, Taasisi ya Mpango wa Kujitathmini Kiutawala Bora
Barani Afrika na Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha, ambacho pia
kinasimamia Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere kilichopo Dar
es Salaam. Naomba nichukue fursa hii kutoa taarifa juu ya utekelezaji wa
majukumu ya taasisi hizo kama ifuatavyo:
139.
Mheshimiwa Spika, Chuo kimeendelea kutekeleza majukumu
ya kutoa mafunzo, kufanya tafiti na kushauri
Wizara
katika masuala ya diplomasia na uhusiano wa kimataifa. Mafunzo yanayotolewa
chuoni hapo yamejikita zaidi katika programu ya diplomasia ya uchumi ili kwenda
sambamba na dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kufanya mageuzi ya uchumi
wa Tanzania kuwa wa viwanda.
140.
Mheshimiwa Spika, katika kujiimarisha, Chuo kinatekeleza
mradi wa upanuzi na uboreshaji wa miundombinu yake ili kuongeza udahili wa
wanafunzi. Madhumuni ya hatua hizi ni kutoa nafasi zaidi ya elimu kwa umma na
kukiongezea chuo mapato na hatimaye kupunguza utegemezi wa fedha za uendeshaji
kutoka Serikalini. Katika kufanikisha hilo, Wizara inaendelea kutenga fedha
zaidi kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya chuo hicho.
Kituo
cha Kimataifa cha Mikutano Arusha
141.
Mheshimiwa Spika, Kituo cha Kimataifa cha Mikutano
Arusha (AICC) kimeendelea kuwa kitovu cha diplomasia ya mikutano hapa nchini na
kuchangia katika kukuza uchumi. Hadi kufikia mwezi Machi 2018 Kituo kilikuwa
mwenyeji wa mikutano 257 ambapo kati
ya hiyo, mikutano 57 ni ya kimataifa
na 200 ya kitaifa ambayo imeingiza
jumla ya Shilingi 2,036,218,423.
142.
Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka wa
fedha 2018/19, Kituo kimepanga kuingiza mapato ya Shilingi 16,743,620,893. Kati ya fedha hizo, Shilingi
15,587,877,637 ni kutoka vyanzo mbalimbali vya ndani; na Shilingi 1,155,743,256 zitatokana na mkopo. Aidha, Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius
Nyerere (JNICC) kinategemewa kuingiza kiasi cha Shilingi 3,338,800,000.
143.
Mheshimiwa Spika, Kituo cha AICC kinategemea kukopa
Shilingi 1,155,000,000 kwa ajili ya
mradi wa upanuzi wa Hospitali ya AICC. Aidha, kituo kinaendelea kufanya
taratibu za kuwezesha ujenzi wa kituo mahsusi cha mikutano kitakachoitwa Mt.
Kilimanjaro International Convention Centre (MK-ICC). Kituo hicho ndicho
kitakachokuwa suluhisho la utekelezaji wa diplomasia ya mikutano ya kimataifa
na maonesho hapa nchini. Vilevile, Kituo kimeiomba Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi kupatiwa eneo kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha mikutano
jijini Dodoma.
Mpango wa Kujitathmini Kiutawala Bora Barani Afrika (APRM)
144.
Mheshimiwa Spika, APRM ni mpango wa nchi za Afrika
wa kujitathmini katika masuala ya utawala bora. Tanzania ilijiunga na Mpango
huo mwaka 2004, na uliridhiwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka
2005. Lengo la APRM ni kuziwezesha nchi za Afrika kuimarisha utawala bora kwa
kushirikisha wananchi wake kubainisha changamoto na kuzigeuza kuwa fursa za
64
maendeleo ili kubaini mambo mazuri ya kuendelezwa kwa
faida ya nchi yenyewe na hata kuwa mfano wa kuigwa na nchi nyingine.
145.
Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka wa fedha
2017/18, kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, APRM Tanzania iliendelea kutekeleza shughuli zilizopangwa kwenye
mpangokazi kama ifuatavyo:
(i)
Kuandaa taarifa ya utekelezaji wa mpango kazi wa APRM kwa
ufadhili wa jumla ya Dola za Marekani 100,000 kutoka Shirika la Maendeleo la
Umoja wa Mataifa (UNDP) Tanzania;
(ii)
Kusimamia uzinduzi wa Ripoti ya nchi uliofanywa tarehe 19
Julai 2017 na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania;
(iii)Kufanya
warsha ya kuwajengea uwezo watendaji wa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ili kuunganisha mipango ya maendeleo ya nchi
pamoja na mpangokazi wa APRM;
(iv) Kushiriki
mikutano ya APRM kulingana na Mkataba wa Makubaliano wa kujiunga na APRM; na
(v)
Kuendelea kutoa taarifa kwa wananchi kuhusu utekelezaji wa
shughuli za APRM.
146.
Mheshimiwa Spika, kwa kutambua umuhimu wa
misingi ya utawala bora, Wizara yangu itaendelea kuiwezesha APRM kutekeleza
majukumu yake.
UTAWALA
NA MAENDELEO YA RASILIMALI WATU
147.
Mheshimiwa Spika, Wizara ina jumla ya watumishi 456
wa kada mbalimbali. Kati ya hao, 347 wapo Makao Makuu ya Wizara na 109 wapo
katika Balozi zetu nje ya nchi.
Ajira
Mpya
148.
Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2017/18,
Wizara ilipata kibali cha kuajiri watumishi 10 wa kada mbalimbali ambapo hadi
sasa watumishi 5 tayari wameripoti kazini na watumishi 5 taratibu za ajira zao
zinaendelea.
Upandishaji
vyeo watumishi
149.
Mheshimiwa Spika,
katika kipindi
cha mwaka
2017/18, Wizara imepata kibali kutoka Ofisi ya Rais,
Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora cha
kuwapandishavyeowatumishi97.Taratibuzakuwapandisha
vyeo watumishi hao zinaendelea
kukamilishwa.
Uteuzi
150.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/18, Mheshimiwa
Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
alifanya uteuzi wa mabalozi watano ambapo kati yao watatu wamepangiwa vituo na
wawili taratibu za kuwapangia vituo zinaendelea.
Mafunzo
151.
Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuwajengea uwezo
Watumishi kwa kutoa mafunzo ya muda mrefu na muda mfupi ndani na nje ya nchi.
Watumishi 31 walihudhuria mafunzo ya muda mfupi na watumishi 9 wanaendelea na
mafunzo ya muda mrefu katika ngazi ya Shahada ya Uzamili. Aidha, Wizara
ilipokea nafasi 5,220 za mafunzo kutoka nchi 27 wahisani na marafiki. Kati ya
nafasi hizo mafunzo ya muda mfupi ni 4,650 na ya muda mrefu ni 570. Wizara iliratibu
fursa hizo kwa kuzitangaza kwa umma wa watanzania kupitia vyombo vya habari,
tovuti ya wizara, mitandao ya kijamii na nyingine ziliwasilishwa moja kwa moja
kwenye Wizara na Idara za kisekta ili watanzania wenye sifa waweze kuomba
nafasi hizo.
152.
Mheshimiwa Spika, Wizara iliandaa Semina Elekezi
kwa Wabunge wa Tanzania katika Bunge la
Afrika Mashariki
iliyofanyika mwezi Januari, 2018, 67
Jijini
Dar es Salaam. Lengo la Semina hiyo lilikuwa ni kuwajengea uelewa Waheshimiwa
Wabunge hao katika masuala yatakayowawezesha kutekeleza majukumu yao,
wakihakikisha kuwa wanawasilisha na kutetea hoja zenye manufaa na maslahi
mapana kwa ustawi wa nchi yetu wakati wa mijadala ndani ya Bunge hilo.
153.
Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka wa fedha
2017/18 Wizara yangu imekabiliana na changamoto mbalimbali za kimfumo wa dunia,
pamoja na zile za kiutendaji. Hata hivyo, pamoja na changamoto hizo Wizara
imeendelea kutekeleza majukumu yake kwa weledi na ufanisi mkubwa kwa kuendelea
kuimarisha ushirikiano na wadau wote wa ndani na nje kuhakikisha kwamba malengo
ya Serikali kwenye ushirikiano wa kimataifa yanatimia bila kujali uwepo wa
changamoto hizo. Napenda kutumia fursa hii kuhimiza wadau kuendelea
kushirikiana na Wizara yangu ili kwa pamoja tuweze kutimiza azma ya Serikali ya
kukuza uchumi na kuboresha maisha ya wananchi wote.
SHUKRANI
154.
Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee naomba kuchukua
fursa hii kuwashukuru Mabalozi, Wawakilishi wa Taasisi za Umoja wa Mataifa na
Mashirika mengine ya Kimataifa kwa ushirikiano mkubwa wanaoutoa kupitia nchi na
mashirika yao kufanikisha mipango mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na
Serikali.
155.
Mheshimiwa Spika, Serikali ya Awamu ya Tano imeendelea
kupata mafanikio makubwa kutokana na mchango wa wadau na washirika wa maendeleo
kutoka nchi na asasi mbalimbali za kitaifa, kikanda, kimataifa pamoja na sekta
binafsi. Naomba nitumie fursa hii kuzishukuru nchi za Afrika Kusini, Algeria,
Australia, Austria, Brazil, Canada, China, Cuba, Denmark, Finland, Hungary,
India, Italia, Ireland, Israel, Iran, Japan, Korea Kusini, Kuwait, Malaysia,
Marekani, Malta, Misri, Morocco, New Zealand, Norway, Oman, Pakistan,
Palestina, Poland, Qatar, Saudi Arabia, Sweden, Singapore, Sri-Lanka, Thailand,
Ubelgiji, Ufaransa, Uhispania, Uholanzi, Uingereza, Ujerumani, Umoja wa Falme
za Kiarabu, Ureno, Urusi, Uswisi, Uturuki na Vietnam kwa kuchangia mafanikio
hayo muhimu kwa Taifa.
156.
Mheshimiwa Spika, shukrani ziwaendee pia Umoja wa
Ulaya, Benki ya Maendeleo ya Afrika, African
Capacity Building Facility, Benki
ya Dunia, IAEA, Shirika la Fedha Duniani
(IMF), Investment Climate Facility for
Africa, UNDP na Mashirika mengine yote ya Umoja wa Mataifa, TradeMark East Africa, Benki ya Kiarabu
kwa Maendeleo ya Kiuchumi ya Afrika
(BADEA), The Association of European Parliamentarians with Africa, WWF, The Belinda and Bill gates Foundation, Global Fund, International Committee of the Red Cross, International Federation of the Red Cross and Red Crescent Societies, Medecins Sans Frontieres pamoja na Mifuko na Mashirika mbalimbali ya
Misaada. Ni dhahiri kuwa mafanikio tuliyoyapata yamechangiwa kwa misaada
MALENGO YA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2018/19
157.
Mheshimiwa Spika, kwa muhtasari miongoni mwa malengo
yaliyopangwa kutekelezwa na Wizara yangu katika mwaka wa Fedha 2018/19 ni
pamoja na:
i.
Kuendelea
kulinda na kutetea misingi ya Taifa;
ii.
Kuendelea kuratibu na kusimamia utekelezaji wa Sera ya
Mambo ya Nje ikiweka msisitizo kwenye diplomasia ya uchumi kuelekea Tanzania ya
viwanda;
iii.
Kuendelea kuvutia fursa za uwekezaji katika sekta
mbalimbali, biashara pamoja na kutangaza vivutio vya utalii;
iv.
Kuratibu Tume za Pamoja za Kudumu za Ushirikiano (JPC);
v.
Kufuatilia mwelekeo wa siasa na uchumi duniani na
kutathmini matokeo yake kwa siasa ya mambo ya nje ya Tanzania;
vi.
Kuendelea kuratibu utekelezaji wa makubaliano ya kikanda
na kimataifa ikiwemo agenda ya
Umoja
wa Afrika ya 2063; na agenda ya Umoja wa Mataifa ya 2030;
vii. Kufuatilia
fursa mbalimbali zinazotokana na ushiriki wa Tanzania katika mtangamano wa kikanda
na mashirika ya kimataifa;
viii.Kuendelea kuongeza uwakilishi wa
Tanzania nje kwa kufungua Balozi mpya, Konseli Kuu, kutumia Konseli za Heshima
sambamba na kuongeza umiliki wa nyumba za makazi ya watumishi na ofisi
balozini;
ix.
Kuendelea kufuatilia utekelezaji wa maelekezo ya Viongozi
Wakuu wa Kitaifa;
x.
Kuendelea kufuatilia utekelezaji wa mikataba mbalimbali
iliyosainiwa kati ya nchi yetu na nchi nyingine na kufuatilia ahadi mbalimbali
zilizotolewa kwa nchi yetu na nchi wahisani na mashirika ya kimataifa;
xi.
Kuongeza mshikamano na jumuiya za watanzania wanaoishi
ughaibuni na kuweka utaratibu madhubuti utakaowawezesha kuchangia kwenye
maendeleo ya Taifa;
xii. Kuendelea kushirikiana na Wizara,
Taasisi za
Serikali, Sekta Binafsi, Asasi za Kiraia na vyombo vya
habari katika kuelimisha umma juu ya fursa mbalimbali zitokanazo na ushiriki wa
Tanzania katika Jumuiya za kikanda na kimataifa;
xiii.Kuendelea kutafuta nafasi za
masomo, misaada na kushawishi nchi na mashirika kutufutia madeni; na
xiv. Kuendelea kujenga uwezo wa
watumishi Wizarani.
MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA KWA MWAKA WA
FEDHA 2018/19
158.
Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2018/19,
Wizara yangu imetengewa bajeti ya kiasi cha Shilingi 177,006,232,000. Kati ya fedha hizo Shilingi 154,810,812,000 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo, Shilingi 11,795,420,000 ni kwa ajili
ya mishahara na Shilingi 10,400,000,000 ni
kwa ajili ya bajeti ya maendeleo.
159.
Mheshimiwa Spika, katika bajeti ya matumizi mengineyo,
Shilingi 116,010,729,689 ni kwa
ajili ya matumizi ya vifungu vya Balozini, Shilingi
35,324,806,566 ni kwa ajili ya vifungu vya makao makuu ya Wizara, Shilingi 1,077,362,234 ni kwa ajili ya Mpango wa Kujitathmini Kiutawala bora Tanzania, Shilingi 1,000,000,000 ni kwa ajili ya
fedha za matumizi mengineyo ya Chuo cha Diplomasia, Shilingi 1,239,633,751 ni kwa ajili ya Mahakama ya Afrika ya Haki
za Binadamu na Watu na
Shilingi 158,279,760 ni kwa ajili ya Bodi ya Ushauri wa Masuala ya Rushwa ya Umoja wa Afrika.
160. Mheshimiwa
Spika, katika fedha za bajeti ya maendeleo, kiasi cha Shillingi 10,400,000,000 zilizopangwa
kwa mwaka wa fedha 2018/19, kiasi cha Shilingi
6,180,676,000 zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa jengo la ofisi ya ubalozi wa Tanzania Muscat, Oman; Shilingi 1,819,324,000 ni kwa ajili ya ukarabati
wa majengo ya ofisi na makazi
yaliyopo ubalozi wa Tanzania Khartoum, Sudan; na Shilingi 2,400,000,000 ni kwa ajili ya upanuzi na uboreshaji wa
miundombinu ya chuo cha diplomasia.
161.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2018/19,
Wizara kupitia balozi zake, inatarajia kukusanya kiasi cha Shilingi 28,564,158,100 ikiwa ni maduhuli ya Serikali.
HITIMISHO
162.
Mheshimiwa Spika, ili kuweza kutekeleza kikamilifu
majukumu ya Wizara, kwa mwaka wa fedha 2018/2019, naomba Bunge lako Tukufu
liidhinishe jumla ya Shilingi
177,006,232,000. Kati ya fedha hizo Shilingi
166,606,232,000 ni kwa ajili ya
matumizi ya kawaida na Shilingi 10,400,000,000 ni kwa ajili ya
bajeti ya maendeleo.
163.
Mheshimiwa Spika, naomba kuchukua nafasi hii kukushukuru
wewe binafsi na waheshimiwa wabunge kwa kunisikiliza.
164.
Mheshimiwa
Spika, naomba
kutoa hoja.
ORODHA YA MIKATABA ILIYORATIBIWA NA WIZARA KWA MWAKA WA
FEDHA 2017/2018.
Katika
kipindi cha mwaka wa Fedha 2017/2018, Wizara ilisimamia na kuratibu uwekaji
saini wa Mikataba na Makubaliano ya Kimataifa kama ifuatavyo:-
Mikataba Baina ya Tanzania na Nchi Nyingine (Bilateral
Agreements)
(a)
Hati ya Makubalino kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Uganda kuhusu ushirikiano wa Sekta ya
Nishati kusaidia eneo la Nangoma lililopo mpakani mwa Tanzania na Uganda,
iliyowekwa saini Julai, 2017, Bukoba, Tanzania.
(b)
Mkataba wa Ushirikiano katika masuala ya elimu kati ya
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Hungary kupitia
Wizara zenye dhamana na masuala ya Elimu, uliowekwa saini tarehe 27 Septemba,
2017, Hungary.
(c)
Hati ya Makubalino kati ya Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Idara ya Sayansi na Teknolojia
ya Jimbo la Hanan ya Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China, kuhusu ushirikiano
katika Sekta ya Elimu, iliyowekwa saini tarehe 25 Septemba, 2017, China.
(d)
Hati ya Makubalino kati ya Shirika la Habari la Utangazaji
la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Shirika la Habari la
Utangazaji la Serikali ya Jamhuri ya Uganda kuhusu masuala ya utangazaji
iliyowekwa saini tarehe
10
Novemba, 2017, Msaka, Uganda .
(e)
Mkataba wa Ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na Saudi
Arabia
kuhusu masuala ya Usafiri wa Anga, uliowekwa saini tarehe 7 Desemba,
2017-Colombo, Sri Lanka.
(f)
Mkataba wa Ushirikiano baina ya Serikali ya Jamhuri wa
Muungano wa Tanzania na New
Zealand
kuhusu masuala ya Usafiri wa Anga uliowekwa saini tarehe tarehe 7 Desemba,
2017- Colombo, Sri Lanka.
(g)
Hati ya Makubalino baina ya Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na Uswisi kuhusu masuala ya Usafiri wa Anga iliyowekwa
saini tarehe 7 Desemba, 2017- Colombo, Sri Lanka.
(h)
Hati ya Makubalino kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania na Jordan kuhusu masuala ya Usafiri wa Anga iliyowekwa saini tarehe
7 Desemba, 2017- Colombo, Sri Lanka.
(i)
Hati ya Makubalino kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania na Serikali ya
Marekani
kuhusu masuala ya Usafiri wa Anga iliyowekwa saini tarehe 7 Desemba,
2017-Colombo, Sri Lanka.
(j)
Kumbukumbu ya Mazungumzo (Records of Discussions) kati ya
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Japan kuhusu masuala ya Usafiri
wa Anga yaliyowekwa saini tarehe 7 Desemba, 2017- Colombo, Sri Lanka.
(k)
Kumbukumbu ya Mazungumzo (Agreed Minutes) kati ya Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zambia kuhusu masuala ya Usafiri wa Anga
yaliyowekwa saini
tarehe
7 Desemba, 2017- Colombo, Sri Lanka.
(l)
Kumbukumbu ya Mazungumzo (Records of Discussions) kati ya
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Uturuki kuhusu masuala ya
Usafiri wa Anga yaliyowekwa saini tarehe 7 Desemba, 2017- Colombo, Sri Lanka.
(m)
Kumbukumbu ya Mazungumzo kati ya Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na
Oman
kuhusu masuala ya Usafiri wa Anga yaliyowekwa saini tarehe 7 Desemba,
2017-Colombo, Sri Lanka.
(n)
Kumbukumbu ya Mazungumzo (Agreed Minutes) kati ya Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Sri Lanka kuhusu masuala ya Usafiri wa
Anga yaliyowekwa saini tarehe 7 Desemba, 2017- Colombo, Sri Lanka.
(o)
Hati ya Makubalino kati ya Wizara ya Maliasili na Utali ya
Wizara ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wizara ya Utalii
Serikali ya Jamhuri ya Kiarabu ya Misri kuhusu ushirikiano katika masuala ya
utalii, iliyowekwa saini tarehe 10 Januari, 2018, Misri.
(p)
|
Hati ya
Makubaliano
|
kati
|
ya Serikali
|
ya
|
|
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali
|
|
ya Jamhuri
ya Kiarabu ya
Misri kuhusu
|
|
ushirikiano katika nyanja ya kilimo, iliyowekwa
|
|
saini
tarehe 10 Januari, 2018, Misri.
|
|
(q)
|
Hati ya
Makubaliano
|
kati
|
ya Chuo
|
cha
|
|
Diplomasia cha
|
Serikali ya
Jamhuri
|
ya
|
|
Muungano wa Tanzania na Taasisi ya Mafunzo
|
|
ya
Kidiplomasia ya
|
Jamhuri
ya Kiarabu ya
|
|
Misri kuhusu
|
ushirikiano
|
katika masuala
|
|
ya
diplomasia,
|
iliyowekwa
saini tarehe
|
10
|
|
|
|
|
|
|
|
Januari,
2018, Misri.
(r)
Hati ya Makubaliano kati ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
na Shirika la Maendeleo la Taifa la Israel (Mashav- Israel Agency for
International Developement Cooperation kuhusu kuboresha huduma za afya,
iliyowekwa saini tarehe 22 Januari, 2018 Dar es Salaam, Tanzania.
(s)
Hati ya Makubaliano kati ya Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto na Serikali ya Palestine kuhusu ushirikiano katika masuala ya afya,
iliyowekwa saini tarehe 5 Machi, 2018, Dar es Salaam, Tanzania.
(t) Mkataba wa Ushirikiano kati ya Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
Serikali
ya
Jamhuri Rwanda kuhusu mradi wa pamoja
wa ujenzi wa reli ya kisasa (Standard Gauge
Railway-SGR),
uliowekwa saini tarehe 9 Machi,
2018,
Kigali, Rwanda.
(u)
Itifaki kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China inayohusu Madaktari kutoka
China kuja kufanya kazi Tanzania, iliyowekwa saini tarehe 4 Aprili, 2018, Dar
es Salaam, Tanzania.
(v)
Hati ya Makubaliano kati ya Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na Serikali ya Brazil
kuhusu
ushirikiano katika nyanja ya Siasa, iliyowekwa saini tarehe 16 Aprili, 2018,
Dar es Salaam, Tanzania.
78
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.