TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Dkt, Mahiga atembelea taasisi ya Save the Children
Haert ya Israel
Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga ameshukuru
Ushirikiano kati ya Taasisi ya Moyo ya Save the Children Heart ya Israel na
Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kwa kuokoa maisha ya watu wengi nchini,
hususan watoto.
Waziri Mahiga
alitoa shukrani hizo leo alipoitembelea taasisi hiyo jijini Tel Aviv, Israel
akiwa anaendelea na ziara yake ya siku tatu aliyoianza jana. "Zamani
nilijua kuwa mtu akizaliwa na maradhi ya kurithi, mtu huyo hawezi kuishi lazima
atakufa, lakini uwepo wa taasisi yenu kumenifanya niondoe itikadi hiyo"
Dkt. Mahiga alisema.
Taasisi ya Moyo ya
Save the Children Heart imeisifu Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kuwa ni moja
ya Taasi bora kusini mwa Jangwa la Sahara na kwamba ina uwezo na wataalam wa
kufanya upasuaji bila ya kupeleka wagonjwa nje ya nchi. "Serikali
inachotakiwa kufanya ni kuiboresha taasisi hiyo kwa kujenga majengo mapya na
kuipatia vifaa zaidi na itakapofanya hivyo itaokoa maisha ya watu na fedha
nyingi ambazo zingelitumika kugharamia matibabu nje ya nchi". Mkurugenzi wa taasisi hiyo alishauri.
Mkurugenzi wa
Taasisi hiyo alimweleza Dkt. Mahiga kuwa taasisi ilianzishwa miaka ya 90 kwa madhumuni ya kuokoa maisha ya watoto
wenye maradhi ya moyo duniani kote, hususan katika nchi zinazoendelea. Hadi
sasa imeshatoa matibabu kwa zaidi ya watoto 460,000 wenye maradhi ya moyo
kutoka Afrika, Amerika, Asia na kwingineko.
Shughuli za taasisi
hiyo inajumuisha kutibu wagonjwa, kutoa mafunzo kwa madaktari na wakufunzi na
kusambaza madaktari katika nchi mbalimbali kuendesha upasuaji kwa kipindi
maalum. Madaktari waliopewa mafunzo na taasisi hiyo wanaendelea kupata miongozo
ya taasisi wanaporejea katika nchi zao kwa ajili ya kufanya matibabu.
Mhe. Waziri
alipokuwa katika taasisi hiyo alipata fursa ya kuonana na Watanzania wanaosoma
na wengine wanaopata matibabu ya maradhi ya moyo katika taasisi hiyo. Aidha,
alioneshwa watoto wawili wanaougua maradhi ya moyo kutoka Nymmar na Romania
ambao kwa mujibu wa Mkurugenzi alisema ndio wa kwanza kupokelewa kutoka nchi
hizo.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Israel
10 Mei 2017
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.