TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
FURSA
ZA UFADHILI WA MAFUNZO KWA WATUMISHI WA UMMA
Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki imepokea fursa za ufadhili wa masomo ya muda
mrefu katika sekta ya miundombinu chini ya program iitwayo “Global Infrasructure Development Scholarship
Program (GIDSP) kutoka Jamhuri ya Korea.
Mafunzo haya ambayo ni kwa
ajili ya Watumishi wa Umma yatafanyika katika Chuo Kikuu cha Seoul (UOS) nchini
Korea kuanzia mwezi Agosti 2018 hadi Desemba 2019.
Waombaji wa mafunzo haya wanatakiwa
kutuma maombi yao moja kwa moja kwenye Chuo Kikuu cha Seoul (UOS). Maelezo ya
ziada kuhusu mafunzo haya na namna ya kutuma maombi yanapatikana kupitia tovuti
ya http://isus.uos.ac.kr au maombi yatumwe kwa
barua pepe ifuatayo: mipd@uos.ac.kr. Mwisho
wa kutuma maombi ni tarehe 18 Mei, 2018.
Mafunzo haya yanaratibiwa na
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam
03 Mei, 2018
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.