Kongamano likiendelea |
Mhe Dau amefanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo nchini Indonesi Dkt. Amran Sulaiman, katika mazungumzo yao yaliyojikita katika kushirikiana na kukuza sekta ya kilimo baina ya Tanzania na Indonesia. |
*********************
Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Thailand, Philippines, Cambodia, Brunei, Laos pamoja na Indonesia Mhe Dkt Ramadhani Kitwana Dau, leo ameshiriki katika Kongamano la Kitaifa kujadili zao la nazi kwenye mji wa Gorontalo Indonesia .
Balozi Dau
alishiriki kwenye mjadala huo (panellist) kwa kutoa historia ya zao la nazi
Tanzania ikiwemo uzalishaji na changamoto zake. Mkutano huo wa siku 2 umeanza
leo na unashirikisha Wadau wote wa zao la nazi nchini Indonesia. Indonesia
inaongoza katika uzalishaji wa nazi Duniani kwa kulima hekta 3.6 milioni na
kuzalisha nazi zaidi ya tani 17 milioni. Kwa upande wake, Tanzania inaongoza
kwa zao hilo Barani Afrika lakini inalima hekta 350,000.
Zao la nazi
kwa sasa linaongoza kwa bei kwenye soko la Dunia na kulipita zao la chikichi na
hata mafuta ya Petroli . Nchini Indonesia mnazi mmoja unatoa kati ya nazi 100
hadi 150 ingawa wastani wa kitaifa Ni nazi 70 kwa mnazi mmoja.
Aidha katika
mkutano huo Balozi Dau alipata fursa ya kuzungumza na Waziri wa Kilimo wa
Indonesia Mhe Dr Amran Sulaiman ambapo walikubaliana kukuza zaidi ushirikiano
kwenye kilimo baina ya nchi hizi mbili.
Pamoja na zao la nazi, Indonesia inaongoza Duniani kwenye mazao kadhaa yakiwemo muhogo, Mahindi ya njano. Balozi Dau anatarajia kukutana na wawekezaji wa sukari michikichi na mihogo kwa madhumuni ya kuwashawishi kuja kuwekeza Tanzania .
Pamoja na zao la nazi, Indonesia inaongoza Duniani kwenye mazao kadhaa yakiwemo muhogo, Mahindi ya njano. Balozi Dau anatarajia kukutana na wawekezaji wa sukari michikichi na mihogo kwa madhumuni ya kuwashawishi kuja kuwekeza Tanzania .
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.