Wednesday, July 6, 2011

Rais Kikwete atembelea Banda la Wizara ya Mambo ya Nje Sabasaba

Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na taasisi zake, wakiwa kwenye picha ya pamoja na Rais Kikwete leo mchana alipotembelea banda lao lililopo ndani ya Banda Kuu la Jakaya Kikwete. Kutoka kushoto ni Tagie Mwakawago, Charles Faini, Mindi Kasiga, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Assah Mwambene, Andes Seiya na Cleophace Ntongani leo tarehe 6.07. 2011.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha wageni katika banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa leo tarehe 6.07.2011. Pembeni kwake ni mtoto wa Rais Rashid Kikwete ambaye anapenda kuwa mwanadiplomasia. Kulia ni Afisa Mawasiliano wa Wizara Mindi Kasiga.

Afisa Mambo ya Nje Charles Faini akifafanua umuhimu wa kuwa na mahusiano mazuri na nchi mbalimbali kwa wananchi waliokuwa wakimiminika kwa wingi kwenye banda la Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwenye viwanja vya sababasaba leo tarehe 6.07.2011.


Watoto wa Rais Kikwete wakiwa kwenye banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakitambua bendera za nchi mbalimbali zenye mahusiano ya kidiplomasia na Tanzania.

Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Kificho akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa leo tarehe 6.07.2011.

Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Katinda Kamando akijibu swali la mwananchi kuhusu sera moya ya mambo ya nje kwenye banda la Wizara hiyo leo tarehe 6.07.2011 kwenye maonesho ya sabasaba.