Tuesday, October 31, 2023

BALOZI MBAROUK AMPONGEZA DKT. TULIA KWA USHINDI URAIS IPU

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb.) katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson.

Balozi Mbarouk aliambatana na Mabalozi watatu  (3) waliohusika kwenye Kampeni ya IPU walipoenda kumpongeza kwa ushindi huo na kumhakikishia Ushirikiano wa Wizara katika utekelezaji wa Majukumu yake Mapya.

Mabalozi watatu ni pamoja na  Naibu Mwakilishi wa Kudumu, Uwakilishi Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,  Balozi Seiman Suleiman, Naibu Mwakilishi wa Kudumu, Uwakilishi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Geneva, Balozi Hoyce Temu pamoja na Balozi Robert Kahendaguza.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akisalimiana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson katika Ofisi za Bunge Dodoma

Mazungumzo baina ya Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson yakiendelea katika Ofisi za Bunge Dodoma

Mazungumzo baina ya Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson yakiendelea katika Ofisi za Bunge Dodoma

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson katika Ofisi za Bunge Dodoma

Picha ya Pamoja




RAIS WA UJERUMANI FRANK-WALTER STEINMEIER ATAMBELEA TWIGA CEMENT YA JIJINI DAR ES SALAAM


Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier ametembelea kiwanda cha kuzalisha saruji cha Twiga (Twiga Cement) kilichopo Tegeta jijini Dar es Salaam. 

Rais Frank-Walter Steinmeier amepata fursa ya kujionea shughuli mbalimbali za uzalishaji saruji zinazoendelea kiwandani hapo. 

Kiwanda hicho cha Twiga Cement kinachotarajia kuongeza uwekezaji wake kufikia Dola za Marekani Milioni 500 kilijengwa nchini mwaka 1967. 

Kiwanda cha Twiga Cement kina ubia na Kampuni ya Scancem International ya nchini Ujerumani.
Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier akikarubishwa katika Kiwanda cha kuzalisha saruji cha Twiga (Twiga Cement) jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier akiangalia ramani ya Kiwanda cha kuzalisha saruji cha Twiga (Twiga Cement) jijini Dar es Salaam
Kiwanda cha kuzalisha saruji cha Twiga (Twiga Cement) jijini Dar es Salaam akiangalia taswira ya Kiwanda cha kuzalisha saruji cha Twiga (Twiga Cement) kilichopo Tegeta jijini Dar es Salaam
Kiwanda cha kuzalisha saruji cha Twiga (Twiga Cement) jijini Dar es Salaam akiangalia shughuli mbalimbali za uzalishaji alipotembelea Kiwanda cha kuzalisha saruji cha Twiga (Twiga Cement) kilichopo Tegeta jijini Dar es Salaam
Taswira ya Kiwanda cha kuzalisha saruji cha Twiga (Twiga Cement) kilichopo Tegeta jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier akiangalia moja ya malighafi zinazotumika katika uzalishaji wa saruji alipotembelea Kiwanda cha kuzalisha saruji cha Twiga (Twiga Cement) kilichopo Tegeta jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier akizindua jengo la Kiwanda cha kuzalisha saruji cha Twiga (Twiga Cement) kilichopo Tegeta jijini Dar es Salaam

TANZANIA YASHIRIKI MAONESHO YA KIMATAIFA YA UTALII YA JAPAN (JAPAN TOURISM EXPO 2023) KWA MAFANIKIO

Tanzania imeshiriki kwa mafanikio makubwa katika Maonesho ya Kimataifa ya Utalii ya Japan (Japan Tourism EXPO 2023), yaliyofanyika kuanzia tarehe 26 - 29 Oktoba 2023 Jijini Osaka, Japan.  

Maonesho hayo, yamekuwa ya kwanza kufanyika katika jiji hilo baada ya janga la UVIKO – 19 na yameshirikisha takriban makampuni ya watalii 1,275 kutoka nchi zipatazo 70 duniani.

Katika ufunguzi wa Maonesho hayo, Balozi wa Tanzania nchini Japan, Mhe. Baraka Luvanda aliinadi Tanzania kuwa ni nchi yenye vivutio mbalimbali vya utalii hususan, Ngorongoro, Serengeti, Kilimanjaro na Zanzibar.  

Kadhalika, Balozi Luvanda aliwataka mawakala wa utalii wa Japan waliojumuika na mawakala wa Tanzania kuchangamkia fursa mbalimbali za utalii. Aidha, alifanya mazungumzo na Kamishna wa Taasisi ya Utalii ya Japan kuhusu fursa mbalimbali za uwekezaji kwenye sekta ya utalii, kwenye mikutano ya pembezoni mwa Maonesho hayo. 

Balozi Luvanda alitumia fursa hiyo kuelezea Maonesho ya Utalii ya Kimataifa ya Swahili (Swahili Internation Tourism Expo – S!TE) ya mwaka 2024 yatakayofanyika nchini mwezi Oktoba 2024 ambapo wadau mbalimbali wa utalii wa Japan wamehamasika kujiandikisha ili waweze kushiriki kwa lengo la kujiunganisha kibiashara na mawakala wa utalii wa Tanzania. 

Pamoja na mambo mengine, Tanzania imepata fursa ya kuzindua rasmi filamu ya The Tanzania Royal Tour Jijini Osaka, iliyotafsiriwa kwa lugha ya Kijapani, tukio ambalo limepata muitikio mkubwa na hamasa kubwa miongoni mwa wajapani wanaoishi katika jiji hilo na majiji jirani. Tukio kama hilo lilifanyika mwaka jana Jijini Tokyo, wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya Utalii nchini Japan ya mwaka 2022.

Taasisi za utalii za Tanzania zilizoshiriki katika maonesho hayo ni Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) na makampuni binafsi ya utalii ya Tanzania yakiwemo, GOSHEN Afrika Safari na MAULY Tours. 

Jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan zinalenga kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta ya utalii ili hatimaye kufikia watalii milioni tano na mapato bilioni sita kwa mwaka 2025. 

Katika Maonesho hayo, mawakala wa utalii Japan wamevutiwa na vivutio vya utalii vya Tanzania pamoja na uwekezaji katika sekta ya utalii ikiwa ni pamoja na kuingia ubia na makampuni ya utalii ya ndani. Aidha, wajapani wengi wamevutiwa kuitembelea Tanzania hususan, baada ya Serikali ya Japan kufungua mipaka yake hivi karibuni kufuatia kupungua kwa janga la UVIKO-19.

Japan ni soko linalochipukia (emerging market) baada ya janga la UVIKO – 19 na ni nchi yenye watu takriban milioni 123 ambapo, inaelezwa kuwa watu takriban milioni 23 sawa na asilimia 45 wana tabia ya kutoka kwenda kutalii nje ya nchi. 

Balozi wa Tanzania nchini Japan Mhe. Baraka Luvanda akielezea jambo kwa wawakilishi wa Taasisi ya Utalii ya Japan katika Maonesho ya Kimataifa ya Utalii ya Japan (Japan Tourism EXPO 2023), yaliyofanyika tarehe 26 - 29 Oktoba 2023 Jijini Osaka, Japan

Balozi wa Tanzania nchini Japan Mhe. Baraka Luvanda akielezea jambo kwa wawakilishi wa Taasisi ya Utalii ya Japan katika Maonesho ya Kimataifa ya Utalii ya Japan (Japan Tourism EXPO 2023), yaliyofanyika tarehe 26 - 29 Oktoba 2023 Jijini Osaka, Japan

Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania nchini Japan, Dkt. Kazusue Konoike akielezea bidhaa za Tanzania kwa washiriki wa Maonesho ya Kimataifa ya Utalii ya Japan (Japan Tourism EXPO 2023), yaliyofanyika tarehe 26 - 29 Oktoba 2023 Jijini Osaka, Japan

Baadhi ya wahudhuriaji kwenye Banda la Tanzania wakipokea maelezo ya bidhaa za Tanzania wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya Utalii ya Japan (Japan Tourism EXPO 2023), yaliyofanyika tarehe 26 - 29 Oktoba 2023 Jijini Osaka, Japan

Balozi Tanzania nchini Japan Mhe. Baraka Luvanda kwenye picha ya pamoja na washiriki wa Tanzania katika Maonesho ya Kimataifa ya Utalii ya Japan (Japan Tourism EXPO 2023), yaliyofanyika tarehe 26 - 29 Oktoba 2023 Jijini Osaka, Japan



RAIS WA UJERUMANI KUTEMBELEA MAKUMBUSHO YA MAJIMAJI, SONGEA

Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani, Mhe. Dkt Frank Walter Steinmeier anatarajiwa kutembelea Makumbusho ya Kumbukumbu ya Vita vya MajiMaji Songea tarehe 1 Novemba 2023. Makumbusho hiyo ina historia kubwa ya Vita vya MajiMaji wakati wa harakati za ukombozi dhidi ya ukoloni wa Wajerumani.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Kanali Laban Thomas amesema maandalizi ya kuupokea ugeni huo yamekamilika ambapo baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Songea ataenda moja kwa moja katika Makumbusho hiyo ya Vita vya MajiMaji.

Amesema akiwa katika Makumbusho hiyo atapata historia ya makumbusho hiyo na kutoa heshima kwa mashujaa waliokufa katika vita hivyo vilivyopiganwa mwaka 1905- 1907.

Kanali Thomas ameongeza kuwa pamoja na kutoa heshima kwa mashujaa wa Vita vya Majimaji, Rais huyo wa Ujerumani  atakutana na baadhi ya wahanga wa vita hivyo na kutembelea Shule ya Msingi MajiMaji.

Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Kamshna  Benard Wakulyamba amesema Wizara ya Maliasili na Makumbusho ya Taifa wanaosimamia Makumbusho ya  MajiMaji wamekamilisha maandalizi kwa ajili ya kumpokea Rais huyo wa Ujerumani.

Mhe. Dkt. Frank-Walter Steinmeier yupo nchini kwa Ziara ya Kikazi ya siku tatu kuanzia tarehe 30 Oktoba hadi tarehe 01 Novemba 2023. 

Ziara hii mbali na kudumisha uhusiano wa kidiplomasia na ushirikiano wa kimaendeleo kati ya Tanzania na Ujerumani, pia imelenga kukuza na kuimarisha misingi ya biashara na uwekezaji.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Kanali Laban Thomas akizungumzia maandalizi ya kumpokea Rais wa Ujerumani, Mhe. Dkt Frank Walter Steinmeier wakati atakapotembela Makumbusho ya Kumbukumbu ya Vita vya MajiMaji Songea Mkoani Ruvuma, tarehe 1 Novemba 2023

Majadiliano yakiendelea kuhusu mapokezi ya Rais wa Ujerumani, Mhe. Dkt Frank Walter Steinmeier wakati atakapotembela Makumbusho ya Kumbukumbu ya Vita vya MajiMaji Songea Mkoani Ruvuma, tarehe 1 Novemba 2023

Majadiliano yakiendelea kuhusu mapokezi ya Rais wa Ujerumani, Mhe. Dkt Frank Walter Steinmeier wakati atakapotembela Makumbusho ya Kumbukumbu ya Vita vya MajiMaji Songea Mkoani Ruvuma, tarehe 1 Novemba 2023



TANZANIA – UJERUMANI KUJIKITA ZAIDI KATIKA USHIRIKIANO WA KIUCHUMI


Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani zimeeleza dhamira yao ya kujikita zaidi katika kuendeleza na kukuza ushirikiano wa kijamii na kiuchumi kwa maendeleo ya pande zote mbili.

Hayo yamebainishwa na Viongozi Wakuu wa mataifa hayo mawili rafiki, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika mkutano huo Rais Samia ameeleza kuwa licha ya Tanzania na Ujerumani kuwa ushirikiano mzuri na wa muda mrefu katika shughuli mbalimbali za maendeleo hususani katika sekta ya Afya, elimu, usambazaji wa maji safi na salama, hifadhi ya mazingira, ulinzi na usalama, haki za binadamu na utawala bora na hifadhi ya maliasili bado kuna fursa kubwa ya kukuza zaidi ushirikiano wa kibiashara na uchumi kwa manufaa ya watu wa pande zote mbili. 

“Katika mazungumzo yetu tumeelekeza timu za pande zote mbili kukaa na kufanya majadiliano ya mara kwa mara ili kubaini maeneo mapya ya ushirikiano ambayo yatatusaidia kupiga hatua kwa haraka zaidi katika kukuza biashara na uwekezaji kwa manufaa ya watu wetu” Alisema Rais Samia. 

Katika hatua nyingine Rais Samia ameeleza kuwa katika mazungumzo na mgeni wake Rais Frank-Walter Steinmeier wamekubaliana kufungua majadiliano katika masuala kadhaa ya kihistoria ikiwemo kuhusu suala la mabaki ya kale ya Tanzania yaliyohifadhiwa nchini Ujerumani. 

Kwa upande wake Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier ameeleza kuwa Ujerumani itaendelea kufungua milango ya ushirikiano zaidi kwa Tanzania katika kijamii na kiuchumi kwa maendeleo ya sasa na vizazi vijavyo. 

“Ujerumani tutatendelea kujikita katika kuangazia maeneo mapya ya ushirikiano ikiwemo kuongeza nguvu ya kusaidia maendeleo ya nishati jadilifu nchini Tanzania na uchumi wa kidijiti ambao utatengeneza ajira nyingi zaidi kwa vijana. Tunafanya haya yote tukiamini kuwa hatusherekei urafiki wetu pekee bali maendeleo ya kiuchumi” Alieleza Rais Frank-Walter Steinmeier

Mbali masuala ya biashara na uchumi Rais Frank-Walter Steinmeier ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita ikiongozwa na Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa hatua kubwa iliyopiga katika kuboresha mazingira ya Demokrasia, Haki za Binadamu na Utawala Bora. 

Rais Frank-Walter Steinmeier ametumia fursa hiyo kuzishukuru familia za wahanga wa Vita vya Majimaji za jijini Songea kwa kumwalika kuzitembelea huku akieleza kuwa ni faraja kubwa kwake ikiwa ni mwendelezo wa ishara ya utayari wa kusonga mbele pamoja licha ya yaliyojiri katika historia. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizingumza na waandishi wa habari kuelezea yaliyojili kwenye mazungumzo na mgeni wake Rais wa Ujerumani Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier Ikulu jijini Dar es Salaam 
Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier akizingumza na waandishi wa habari kuelezea yaliyojili kwenye mazungumzo na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Ikulu, jijini Dar es Salaam 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier wakizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuhitimisha mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Y. Makamba (Mb,) akifuatilia mkutano wa Rais Samia na Rais wa Ujerumani Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier na waandishi wa habari uliokuwa ukuiendelea Ikulu jijini Dar es Salaam. 
Baadhi Viongozi wa Serikali wakifuatilia mkutano kati ya Rais Samia na Rais wa Ujerumani Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier na waandishi wa habari uliokuwa ukuiendelea Ikulu jijini Dar es Salaam
Sehemu ya watendaji wa Serikali wakifuatilia mkutano kati ya Rais Samia na Rais wa Ujerumani Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier na waandishi wa habari uliokuwa ukuiendelea Ikulu jijini Dar es Salaam
Baadhi Viongozi wa Serikali wakifuatilia mkutano kati ya Rais Samia na Rais wa Ujerumani Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier na waandishi wa habari uliokuwa ukuiendelea Ikulu jijini Dar es Salaam
Waziri wa Utalii na Mambo ya kale Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akifuatilia mkutano kati ya Rais Samia na Rais wa Ujerumani Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier na waandishi wa habari uliokuwa ukuiendelea Ikulu jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Balozi Mindi Kasiga akifuatilia mkutano kati ya Rais Samia na Rais wa Ujerumani Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier na waandishi wa habari uliokuwa ukuiendelea Ikulu jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na America Balozi Swaiba Mndeme akifuatilia mkutano kati ya Rais Samia na Rais wa Ujerumani Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier na waandishi wa habari uliokuwa ukuiendelea Ikulu jijini Dar es Salaam

UHUSIANO KATI YA MISRI NA ZANZIBAR NI MZURI LICHA YA MISRI KUFUNGA UBALOZI MDOGO ZANZIBAR

Serikali imeeleza leo kwamba, Uhusiano kati ya Misri na Zanzibar umeendelea kukua na kuimarika licha ya Serikali ya Misri kufunga Ubalozi wake mdogo Zanzibar kwenye miaka ya 1990.

Hayo yalielezwa Bungeni leo na Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alipokuwa akijibu Swali la nyongeza la Mhe. Ali Juma Mohamed, Mbunge wa Shaurimoyo, aliyetaka kujua sababu za nchi ya Misri kufunga Ubalozi wake Mdogo Zanzibar.

Mheshimiwa Naibu Waziri alifahamisha kwamba Misri haikutoa sababu za kufunga Ubalozi wake mdogo Zanzibar. Hata hivyo, alieleza zaidi kuwa pamoja na kufungwa kwa ofisi hizo, mahusiano na ushirikiano kati ya Misri na Zanzibar yameendelea kukua na kuimarika siku hadi siku kupitia Ubalozi wake uliopo Dar es Salaam.

Awali, katika suala lake la msingi, Mhe. Mohamed alitaka kujua idadi ya Balozi ndogo zilizopo Zanzibar, ambapo alijibiwa kuwa hadi kufikia Agosti, 2023, nchi zilizofungua Ofisi ndogo za Ubalozi Zanzibar ni China; India; Msumbiji; Oman na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Aidha, Mheshimiwa Naibu Waziri alieleza kuwa suala la kufungua na kufunga Ubalozi ni suala la kawaida katika ulimwengu wa Kidiplomasia. Alitaja sababu za nchi kufunga Ubalozi kuwa ni pamoja na; Kutetereka au kuharibika kwa mahusiano ya nchi husika; nchi kubadili mwelekeo wa kimaslahi na kistrategia; kukosekana kwa usalama katika nchi husika; na mwisho ni hali ya kiuchumi ambapo nchi hufunga Ubalozi au Konseli Kuu kwa ajili ya kubana matumizi.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akijibu swali Bungeni jijini Dodoma 

Waheshimiwa Wabunge wakisikiliza majibu ya swali kutoka kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk 


Monday, October 30, 2023

RAIS WA JAMHURI YA SHIRIKISHO LA UJERUMANI MHESHIMIWA FRANK-WALTER STAINMEIER AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI

Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier amewasili nchini leo tarehe 30 Oktoba 2023 kwa ziara ya kikazi ya siku tatu (3) kuanzia tarehe 30 Oktoba hadi 1 Novemba 2023, na kupokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Y. Makamba (Mb.) katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier akikabidhiwa maua alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Y. Makamba (Mb.) wakati alipompokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier akisalimian Balozi wa Ujerumani nchini Tanzani Mhe. Thomas Terstegen alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na America katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Swaiba Mndeme alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Y. Makamba na Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier  wakizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Hassan Mwamweta
kwenye hafla ya mapokezi ya Rais huyo katika 
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam  
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Y. Makamba na Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier wakifurahia ngoma za jadi (hawapo pichani) kwenye hafla ya mapokezi ya Rais huyo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam  
Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier akiwasalimia Watanzania waliojitokeza kumlaki (hawapo pichani) alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam  

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA WAKATI WA MAPOKEZI