|
Mtendaji Mkuu wa
Makumbusho ya Taifa ya Oman Mheshimiwa Jamal al-Moosawi akisini kitabu cha wageni alipowasili katika
Makumbusho ya Kunduchi jijini Dar es Salam, kulia ni Balozi wa Oman nchini Mheshimiwa Saud bin Hilal Alshaidani
|
|
Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Taifa ya Oman Mhe. Jamal al-Moosawi akitembelea magofu ya Makumbusho ya Kunduchi jijini Dar es Salaam alipotembelea makumbusho hiyo |
|
Mtendaji Mkuu wa makumbusho ya Taifa
ya Oman Mhe. Jamal al-Moosawi akiangalia mabaki ya magofu yanayopatikana katika Makumbusho ya
Kunduchi jijini Dar es Salaam alipotembelea makumbusho hiyo |
|
Mtendaji Mkuu wa makumbusho ya Taifa
ya Oman Mhe. Jamal al-Moosawi na ujumbe wake wakiangalia mabaki ya magofu yanayopatikana katika Makumbusho ya
Kunduchi jijini Dar es Salaam walipotembelea makumbusho hiyo |
|
Mtendaji Mkuu wa makumbusho ya Taifa
ya Oman Mhe. Jamal al-Moosawi na ujumbe wake wakiangalia mabaki ya magofu yanayopatikana katika Makumbusho ya
Kunduchi jijini Dar es Salaam walipotembelea makumbusho hiyo |
Ujumbe
wa Makumbusho ya Taifa ya Oman ukiongozwa na Mtendaji Mkuu wa
Makumbusho ya Taifa ya Oman Mheshimiwa Jamal al-Moosawi umetembelea
Makumbusho ya Kunduchi jijini Dar es Salam.
Katika Makumbusho hiyo
yamehifadhiwa magofu ya Kale ambayo ni Makaburi ya masultani waliozikwa
na binti vigori wakiwa hai ili kumsindikiza sultan katika safari yake
hiyo ya kaburini na Msikiti uliotumika tangu karne ya 15.
Ujumbe huo
kutoka Oman ambao uko nchini uliambatana na Mkurugenzi wa Idara ya
Mashariki ya Kati Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Balozi Abdallah Kilima na Balozi wa Oman nchini Tanzania
Mheshimiwa Saud bin Hilal Alshaidani.
Ujumbe huo pia uliambatana na
Mwenyekiti wa Bodi ya Makumbusho ya Taifa Dkt. Oswald Masebo na
Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt. Noel Lwoga.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.