Thursday, October 31, 2013

Membe: Vifo vya Askari ni chachu kwa Watanzania


Mhe. Bernard K. Membe (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akizungumzia ushiriki wa Tanzania katika operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa popote pale duniani.


Waziri Membe akiendelea na mahojiano yake na Mwandishi Fredy Mwanjala wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten ofisini kwake leo, jijini Dar es Salaam. 

Waziri Membe akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mahojiano na mwandishi Fredy Mwanjala (kushoto) na mpiga picha Bi. Fauzia Yusuph (kulia), wote wanatoka Kituo cha Televisheni cha Channel Ten.



Membe:  Vifo vya Askari ni chachu kwa Watanzania

Na TAGIE DAISY MWAKAWAGO


Tanzania itaendelea kushiriki operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa popote pale duniani.

Msimamo huo wa Tanzania uliwekwa wazi na Mhe. Bernard K. Membe (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika mahojiano maalum na Mwandishi Fredy Mwanjala wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, yaliyofanyika leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam

Katika mazungumzo yao yaliyolenga kutaka kufahamu msimamo wa Tanzania kufuatia vifo vya askari wake huko Darfur, Sudan na hivi karibuni huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Kongo (DRC), Waziri Membe alisema moja ya Sera ya Mambo ya Nje katika awamu ya nne ya Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete ni ulinzi na amani.

Hivyo, Tanzania itaendelea kushiriki katika operesheni hizo za kulinda amani ambazo zimeiletea Tanzania heshima kubwa katika medani ya kimataifa.

Waziri Membe alisema inawezekana kuwa wanajeshi wa Tanzania wanalengwa na kundi la waasi la M23, kwa kuwa Tanzania ni mwiba mkali kwa kikundi hicho kutokana na umahiri wake unaofahamika vyema katika nchi za Maziwa Makuu.

“Umwagikaji wa damu Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Kongo (DRC) ni chachu kwa Watanzania dhidi ya kikundi cha waasi cha M23,” alisema Mhe. Bernard Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.  

Hivi karibuni mwezi Agosti, kikosi cha M23 kilishambuliwa na kuteketezwa kwa mujibu wa taarifa za kiitelijensia zilizoripotiwa na vyombo vya habari.  Lakini inasemekana kuwa kuna kundi lingine limezuka tena hivi karibuni kwa jina hilo hilo la M23 kama vile chem-chem ya maji, alieleza Waziri Membe.

“Ni muhimu ieleweke kuwa Tanzania haitosita kamwe kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kupambana na hizi vita za nchi jirani zisizoisha,” alisema Waziri Membe.  Aliongeza na kusema kuwa Tanzania imekuwa kinara cha medali za kimataifa katika kutetea na kulinda amani na usalama wa nchi yetu na barani Afrika.

“Sisi ni taifa ambalo liko tayari kujitolea kupigana na kumwaga damu katika kutetea amani na kutatua migogoro ya majirani zetu,” alisema Waziri Membe.  Alieleza kuwa Tanzania imeshiriki kwa namna moja au nyingine katika vita vya ukombozi wa amani barani Afrika katika nchi za Msumbiji, Afrika Kusini, Zimbabwe, Comoro, Uganda, Mashariki ya Kongo-DRC na nchi nyingine nyingi. 

Akizungumzia kupoteza maisha kwa Askari wa Tanzania nchini Kongo-DRC, Waziri Membe alisema kuwa ni msiba mkubwa wa Kitaifa na wa Umoja wa Mataifa.  Alieleza kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea salamu za rambirambi kutoka Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Umoja wa Ulaya (EU), Serikali ya Kongo, Serikali ya Angola, Serikali ya Afrika ya Kusini na nchi nyingine duniani.

Tanzania ni mojawapo ya nchi zinazounda Brigedi Maalum ya umoja wa mataifa (MONUSCO) kulinda na kusimamia amani huko Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Kongo (DRC).  Kuna batalioni moja yenye askari zaidi ya 1,270 ambao wanaunda sehemu ya Brigedi hiyo Maalum ya MONUSCO. 



Mwisho. 




Jumuiya ya EAC na talaka rejea


Mhe. Bernard K. Membe (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akielezea kuhusu hisia za kutengwa kwa Tanzania katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).   Waziri Membe alikuwa katika mahojiano maalum na Mwandishi Fredy Mwanjala wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten ofisini kwake leo, jijini Dar es Salaam.

Waziri Membe akiendelea na mahojiano hayo, wakati Bi. Fauzia Yusuph wa Channel Ten akirekodi tukio hilo. 




Jumuiya ya EAC na talaka rejea

Na TAGIE DAISY MWAKAWAGO


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) ameelezea hisia za sintofahamu kuhusu kutengwa kwa Tanzania katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), na kuhoji kuwa iwaje nchi yetu itengwe na nini maana ya Jumuiya hiyo?

Aliyasema hayo katika mahojiano maalum na Mwandishi Fredy Mwanjala wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, yaliyofanyika ofisini kwake leo, jijini Dar es SalaamMazungumzo hayo yalijikita zaidi katika kujua msimamo wa Tanzania kidiplomasia wakati huu wa sintofahamu ya Jumuiya hiyo inayoendelea, hususan Tanzania ikionekana kutengwa na nchi za Uganda, Rwanda na Kenya.

“Huu ni muungano wa watu wenye woga,” alisema Waziri Membe na kuongeza kuwa Jumuiya hiyo ilishawahi kuvunjika mnamo mwaka 1977.  

“Jumuiya hiyo ilishawahi kuvunjika na kuungwa tena, na Tanzania hatukuathirika.  Tuko tayari kupewa au kutoa talaka, na ikiwezekana labda kutakuwa na talaka rejea,” alisema Waziri Membe.  Jumuiya hiyo ya EAC inazijumuisha nchi za Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi na Tanzania.

“Sisi ndio ‘center of gravity’ na ndio soko kubwa la bidhaa katika ukanda wa Afrika Mashariki - tuna rasilimali zaidi ya majirani zetu, tuna utajiri wa ardhi na bandari nne ambazo ni ufunguo wa kutumia bahari kubwa na kufikia nchi nyingine duniani,” alifafanua Waziri Membe.  Bandari hizo ni za Mtwara, Tanga, Dar es Salaam na bandari ya Bagamoyo ambayo ipo katika ujenzi wa kuifanya iwe bandari kubwa ya kimataifa barani Afrika.

Waziri Membe alisema cha kushangaza ni kwamba majirani zetu wanatakiwa kutambua kuwa Tanzania ni nchi ambayo ni mfano pekee wa kuigwa kwa uzoefu wa muungano.  “Sisi ni taifa na sio muungano wa makabila matatu au manne,” alisema Waziri huyo.

“Hauwezi leo ukaitaifisha ardhi ya nchi nyingine na kuviacha vizazi vijavyo bila mali,” alisema Waziri Membe na kuongeza kuwa “kwa vyovyote vile, jumuiya hii ya Afrika Mashariki lazima iende kwa taratibu.”

Aidha, Waziri Membe alienda mbali zaidi na kusema kuwa huenda chokochoko ya kutengwa kwetu inatokana na wivu au gere kwa Tanzania kupeleka majeshi yake huko Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, jambo alilosema huenda halijawafurahisha baadhi ya watu katika Jumuiya hiyo.

Vilevile alisema kuwa kitendo cha Tanzania kukataa ardhi kuwa sehemu ya mali ya Afrika Mashariki huenda pia imepelekea mchango mkubwa kwenye choko choko hizo.

Waziri Membe amewaambia Watanzania kuwa “wakae wakijua kwamba akufukuzae hakwambii toka, utaona tuu mambo yanabadilika.”


Mwisho.



Wednesday, October 30, 2013

TANZIA





TANZIA

TUNASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA MFANYAKAZI MWENZETU ANNE FRANCIS MUKAMA (NAIBU KAMISHNA UHAMIAJI) KILICHOTOKEA TAREHE 29 OKTOBA 2013 SAA 1:00 ASUBUHI KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI.

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE MILELE AMEN.


UTAWALA


29 OKTOBA, 2013


Tuesday, October 29, 2013

Rais Kikwete kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa wa 'Open Government'

Tanzania congratulates Turkey for marking 90th National Day


H.E. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania has sent a congratulatory message to H.E Abdullah Gül, President of the Republic of Turkey on the occasion of the National Day of Turkey.

The message reads as follows.

“His Excellency Abdullah Gül,
  The President of the Republic of Turkey,
  Ankara,
  TURKEY.
            Your Excellency and Dear colleague,

On behalf of the people and the Government of the United Republic of Tanzania, and indeed on my own behalf, I wish to convey my sincere congratulations to you and through you to the Government and People of the Republic of Turkey, my heartfelt congratulations on the occasion of the National Day of Turkey.

Turkey and Tanzania have over the years enjoyed good bilateral relations and witnessed an increased trade and investment cooperation. It is a great honor and privilege to mark your country’s 90th National Day by reiterating my personal desire and that of my Government to working with You and Your Government in strengthening further these long ties of friendship, co-operation and partnership in areas such as trade, industry, infrastructure, tourism and investment.

I wish Your Excellency, personal good health and prosperity for the people of the Republic of Turkey.

Please accept, Your Excellency, my personal regards and best wishes for your continued good health and success.


Jakaya Mrisho Kikwete
PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA


ISSUED BY: 

THE MINISTRY OF FOREIGN AFFAIRS AND INTERNATIONAL CO-OPERATION,

DAR ES SALAAM.

29TH OCTOBER, 2013



Mhe. Membe akutana na Mkuu wa chombo kipya cha EU kuhusu Usalama Majini



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza na Bw. Etienne de Poncins,  Mkuu wa Chombo kipya chini  ya Jumuiya ya Ulaya (EUCAP Nestor) kinachoshughulika  na utoaji mafunzo katika masuala ya Usalama  Majini kwa nchi za pembe ya Afrika. Bw. Poncins alifika Wizarani kwa ajili ya kuwasilisha rasmi ombi kwa Serikali ya Tanzania la kujiunga na Chombo hicho ambacho lengo lake kuu ni kutoa mafunzo, misaada ya kiufundi na kisheria ili kuziwezesha nchi washirika kukabiliana na matukio mbalimbali ya Uharamia na Ugaidi yanayotokea katika Bahari Kuu ikiwemo Pwani ya Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika.

Balozi wa Jumuiya ya Ulaya hapa nchini, Mhe. Filiberto Cerian Sebregondi (kulia) akimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) alipozungumza nao kuhusu masuala mbalimbali ya Usalama Majini.


Mhe. Membe akimsikiliza Bw. Poncins akielezea utendaji kazi wa Chombo hicho cha EUCAP Nestor.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Dora Msechu (katikati) akiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (kushoto) na Bibi Victoria Mwakasege, Mkurugenzi Msaidizi katika Idara ya Ulaya na Amerika wakimsikiliza Bw. Poncins (hayupo pichani).

Mazungumzo yakiendelea

Mhe. Sebregondi akichangia jambo wakati wa mazungumzo kati ya Mhe. Membe na Bw. Poncins (hawapo pichani)

Maafisa kazini! Kutoka kushoto ni Bi. Zulekha Fundi na Bw. Frank Mhina, Maafisa Mambo ya Nje wakinukuu mazungumzo kati ya Mhe. Membe na Bw. Poncins (hawapo pichani).

Mhe. Membe akisisitiza jambo kwa Mhe. Sebregondi na Bw. Poncins baada ya kumaliza mazungumzo yao

 
Picha ya pamoja.
 




Monday, October 28, 2013

RAIS KIKWETE NA MAMA SALMA KIKWETE WATOA POLE KWA MJANE NA FAMILIA YA BALOZI ISAAC SEPETU LEO


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akiweka saini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa Balozi Isaac Sepetu  alipokwenda  nyumbani kwa marehemu Sinza Mori, Dar es salaam, kutoa pole. Marehemu Sepetu aliyefariki jana katika jijini Dar es salaam.
 Mama Salma Kikwete  akiweka saini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa Balozi Isaac Sepetu  nyumbani kwa marehemu Sinza Mori, Dar es salaam. . Marehemu Sepetu aliyefariki jana katika jijini Dar es salaam.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa pole mjane wa Balozi Isaac Sepetu, Mama Miriam Sepetu, alipokwenda na Mama Salma nyumbani kwa marehemu Sinza Mori, Dar es salaam, kutoa pole kwa mjane huyo na familia ya Marehemu Sepetu aliyefariki jana jijini Dar es salaam.  (Picha zote na Ikulu)