Thursday, October 17, 2013

Wiki ya Umoja wa Mataifa kuadhimisha miaka 68 yazinduliwa


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Umoja wa Mataifa  itakayoanza kuadhimishwa tarehe 17 hadi 24 Oktoba, 2014. Wiki hiyo ambayo huadhimishwa kila mwaka itajumuisha matukio mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mjadala wa Wazi utakaofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tarehe 22 Oktoba, 2013 na maonesho ya shughuli mbalimbali za Umoja wa Mataifa na Wizara ya Mambo ya Nje yakayofanyika Viwanja vya Karimjee tarehe 23 na 24 Oktoba, 2013 . Kilele cha maadhimisho hayo ni tarehe 24 Oktoba ambapo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) atakagua Gwaride rasmi na kupandisha Bendera ya Umoja wa Mataifa. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni "Tanzania ya Kesho Tunayoitaka". Mwingine katika picha ni Alberic Kacou, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini.
 

Waandishi wa Habari kutoka mashirika mbalimbali ya habari hapa nchini wakimsikiliza kwa makini Bw. Kacou na Balozi Gamaha walipozungumza nao kuhusu maadhimisho ya Wiki ya Umoja wa Mataifa.

Bw. Kacou akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa mkutano wa uzinduzi wa Wiki ya Umoja wa Mataifa.
 
Sehemu ya Waandishi wa Habari pamoja na Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakimsikiliza Balozi Gamaha alipozungumza nao kuhusu maadhimisho ya Wiki ya Umoja wa Mataifa. Kushoto ni Bi. Maulidah Hassan na Bw. Lucas Mayenga, Maafisa Mambo ya Nje.

 
Picha na Reginald Philip Kisaka

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.