Sunday, May 31, 2015

Rais Kikwete aongoza Mkutano wa Pili wa Dharura wa Wakuu wa Nchi wa EAC kuhusu Burundi


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (wa kwanza kulia) kwa pamoja na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museven (wa pili kulia), Rais wa Afrika Kusini, Mhe Jacob Zuma (wa tatu kutoka kulia), Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi, Mhe. Alain Nyamitwe (wa tatu kushoto) na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt. Richard Sezibera (wa pili kushoto), wakiimba wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, kabla ya kuanza rasmi kwa Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kujadili hali ya siasa na usalama nchini Burundi. Mkutano huo ulifanyika Ikulu, Dar es Salaam tarehe 31 Mei, 2015. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula (wa pili kutoka kulia) akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bibi Joyce Mapunjo na  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje (kulia)  nao wakiimba wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Dkt. Richard Sezibera akisoma maazimio yaliyofikiwa mara baada ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kumalizika.
Kundi la Watu Maalum la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalofuatilia hali ya siasa na usalama nchini Burundi chini ya uongozi wa Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Jaji Joseph Sinde Warioba  wakifuatilia mkutano wa Wakuu wa Nchi wa EAC. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini.
Juu na Chini ni Wajumbe mbalimbali wakifuatilia mkutano wa wakuu wa nchi wa EAC
Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Mhe. Radhia Msuya (katikati) akiwa pamoja na Mkurugenzi Msaidizi katika Ubalozi wa Tanzania nchini Burundi, Bibi Victoria Mwakasege nao wakifuatilia mkutano
Maafisa Mambo ya Nje nao wakifuatilia kwa makini mkutano 
Sehemu ya Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini nao wakifuatilia mkutano 
Mkurugenzi wa Idara ya Habari,  Bw. Assah Mwambene (katikati) kwa pamoja na Afisa Habari wa Sekretarieti ya Maziwa Makuu Bw. Macdonald Mwakasendile (kushoto) wakirekodi matukio 
Rais Kikwete akifuraia jambo na Rais wa Afrika Kusini Mhe. Zuma pamoja na Rais wa Uganda Mhe. Museveni mara baada ya kumaliza mkutano.
Rais Kikwete akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Bi.Nkoosazana Dlamini-Zuma kabla ya kuanza mkutano. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe akiongozana na Rais wa Kenya, Mhe. Uhuru Kenyatta tayari kwenda kuanza mkutano wa kujadili hali ya usalama nchini Burundi .
Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje, Balozi Liberata Mulamula akizungumza jambo na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya,, Bw. Vervaeke.

....Kuwasili kwa viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje Balozi Mulamula akisalimiana na Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta
Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyetta akipita kwenye Gwaride la Heshima mara baada ya kuwasili nchini
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Harrison Mwakyembe akimtambulisha Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na UShirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula kwa Rais wa Uganda mara baada ya kumpokea Rais huyo alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Rais Museven akipita katikati ya  Gwaride la heshima. 
Balozi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini Balozi Radhia Msuya akisalimiana na Rais wa Afrika ya Kusini alipowasili nchini
Picha ya Pamoja baada ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
Picha na Reginald Philip


Saturday, May 30, 2015

Waziri Membe afungua rasmi Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa EAC

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akifungua rasmi Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 30 Mei, 2015. Mkutano huo ambao ni maandalizi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa EAC utakaofanyika tarehe 31 Mei, 2015,  pamoja na mambo mengine utapokea na kujadili taarifa zitakazowasilishwa na Jopo la Watu Maalum wanaofuatilia hali ya siasa na usalama nchini Burundi, Taarifa ya Wanasheria Wakuu kutoka Nchi Wanachama na Taarifa ya Mawaziri waliotembelea nchini Burundi hivi karibuni kwa ajili ya kutathmini hali. Kulia ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt. Richard Sezibera.
Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Mb.) akifurahia jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri.
Waziri mpya wa Mambo ya Nje wa Burundi, Mhe. Alain Nyamitwe (katikati) ambaye anaongoza ujumbe wa Serikali ya Burundi kwenye mkutano huo wa Baraza la Mawaziri
Ujumbe wa Uganda ukifuatilia hotuba ya ufunguzi ya Mhe. Membe (hayupo pichani)
Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Mhe. Amina Mohammed (wa pili kushoto) akiongoza ujumbe wa Kenya wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Baraza la Mawaziri wa EAC
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya (wa pili kulia mstari wa kwanza) kwa pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Innocent Shiyo (kushoto) nao wakifuatilia kwa makini hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri iliyotolewa na Waziri Membe (hayupo pichani)


Bunge lapitisha Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) akisoma Hotuba ya Bajeti ya Wizara yake Bungeni mjini Dodoma jana tarehe 29 Mei 2015.
Kutoka kushoto mstari wa mbele ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Balozi Liberata Mulamula, Naibu Katibu Mkuu, Balozi Hassan Simba Yahya, Mkurugenzi wa chuo cha Diplomasia, Mhe. Dkt. Mihammed Maundi wakifuatilia kwa makini hotuba ya bajeti.
Wageni waalikwa akiwemo Mke wa Waziri Membe, Mama Dorcas Membe (wa pili kushoto) wakiwa katika ukumbi wa Bunge wakifuatilia hotuba ya bajeti iliyokuwa ikiwasilishwa na Waziri Membe.
Waheshimiwa Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali duniani nao wakifuatilia hotuba ya bajeti.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga naye akifuatilia Hotuba ya Bajeti ilipokuwa inawasilishwa na Waziri Membe (hayupo pichani)
Mkurugenzi Mtendaji wa  Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), Bw. Elishilia Kaaya na wageni wengine nao wakifuatilia Hotuba ya Bajeti ya Mambo ya Nje ilipowasilishwa Bungeni
Ujumbe kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa uliaoambatana na Mhe. Waziri Membe ukifuatilia hotuba ya Wizara Bungeni.
Sehemu nyingine ya Ujumbe kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakiwemo Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali duniani wakifuatilia hotuba ya bajet ya Wizara.
Wageni wa Mhe. Membe nao wakifuatilia Hotuba 
Ujumbe wa Mabalozi wanao wanaowakilisha nchi zao hapa nchini wakiongozwa na Mkuu wa Mabalozi ambaye pia ni Balozi wa DRC, Mhe. Juma Alfan Mpango (kushoto) wakifuatilia hotuba ya Mhe. Membe
Mama Membe (wa pili kushoto) pamoja na Balozi wa Malawi hapa nchini, Mhe.Hawa Ndilowe (wa pili kulia) na wageni wengine wakisikiliza hotuba ya bajeti ya Waziri Membe
Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo Cha Diplomasia wakisikiliza Hotuba ya Bajeti iliyokuwa inawasilishwa na Waziri Membe, wakiongozwa na Mwalimu wao Bw. Jambo
Mbunge Dkt. Hamisi Kigwangala akimpongeza Waziri Membe baada ya Bunge kupitisha Bajeti wa Wizara yake
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria, Balozi Irene Kasyanju (katikati) na Balozi Filiberto Sebregondi wa Umoja wa Ulaya wakizungumza jambo nje ya Ukumbi wa Bunge baada ya Bunge kupitisha Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje. 
Waziri Membe (Wa kwanza kushoto), Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje Balozi Liberata Mulamula, Mbunge wa Simanjiro Mhe. Christopher Ole Sendeka na Katibu wa Waziri, Bw. Thobias Makoba wakifurahia jambo mara baada ya hotuba ya Wizara kupitishwa na Bunge 
Mbunge wa Maswa Magharibi, Mhe. John Magale Shibuda akisalimiana na Afisa Habari wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa pamoja na Reuben Mchome katika Viwanja vya Bunge
Waziri Membe akihojiwa na Paschal Mayala Mkuu wa Kampuni ya PPR kuhusu mipango ya Wizara katika mwaka wa fedha ujao 2015/2016
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Membe (wanne kutoka kulia) akiwa katika Picha ya Pamoja na wananchi wa Jimbo la Mtama

Picha na Reginald Philip

Bunge lapitisha Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) akisoma Hotuba ya Bajeti ya Wizara yake Bungeni mjini Dodoma jana tarehe 29 Mei 2015.
Kutoka kushoto mstari wa mbele ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Balozi Liberata Mulamula, Naibu Katibu Mkuu, Balozi Hassan Simba Yahya, Mkurugenzi wa chuo cha Diplomasia, Mhe. Dkt. Mihammed Maundi wakifuatilia kwa makini hotuba ya bajeti.


Wageni waalikwa wakiwa katika ukumbi wa Bunge wakifuatilia hotuba ya bajeti iliyokuwa ikiwasilishwa na Waziri Membe.


Waheshimiwa Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali duniani nao wakifuatilia hotuba ya bajeti.


Wageni waalikwa wakiwamo wananchi wa jimbo la Mtama la Mhe. Waziri Membe nao wakifuatilia hotuba ya bajeti ya Waziri Membe.


Kundi lingine la Waheshimiwa Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali duniani wakifuatilia hotuba ya bajeti.


Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo Cha Diplomasia wakisikiliza Hotuba ya Bajeti liyokuwa inawasilishwa na Waziri Membe, wakiongozwa na Mwalimu wao Bwa. Jambo
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Liberata Mulamula (Wa kwanza Kushoto), Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria Balozi Irene Kasyanju (katikati) na Balozi Filiberto Sebregondi wa Umoja wa Ulaya wakizungumza jambo nje ya Ukumbi wa Bunge baada ya Bunge kupitisha bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje. 
Mbunge Dkt. Hamisi Kigwangala akimpongeza Waziri Membe baada ya Bunge kupitisha Bajeti wa Wizara yake
Waziri Membe akihojiwa na Paschal Mayala Mukuu wa Kampuni ya PPR
Picha na Reginald Philip