Saturday, January 29, 2022

BALOZI MULAMULA: MISINGI YA SERA YA MAMBO YA NJE HAIJABADILIKA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) amesema kuwa Misingi ya Sera ya Mambo ya Nje haijabadilika na iko imara, kusisitiza umoja na kutoshabiana kisiasa na upande wowote pamoja na kuwaunga mkono wale wote wanaokandamizwa.

Balozi Mulamula ameyasema hayo wakati alipokutana katika kikao kazi na watumishi wa Wizara ya leo Jijini Dodoma na kuwasihi watumishi kujenga mahusiano na kutekeleza kwa ufanisi Diplomasia ya Uchumi.

“Uchumi wa Tanzania unakuwa kutokana na juhudi zetu, na mtakumbuka kuwa Wizara ya Mambo ya Nje majukumu yake ni mtambuka kwani yanagusa kila sekta, na lengo la kikao hiki ilikuwa kukumbushana maagizo ya Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,”

“Nashukuru sana katika kukutana kwenye kikao na wafanyakazi binafsi nimehamasika na kuwa na ari mpya ya kuchapa kazi, na pia wafanyakazi wamehamasika mara baada ya kikao cha leo,” 

Katika awamu ya Sita, Serikali imefungua balozi mbili mpya na Konseli mbili na naamini kutokana na msisitizo wa Mhe. Rais Samia wa kutekeleza Diplomasia ya uchumi kwa vitendo tutaendelea kufungua balozi nyingine zaidi kadri tutakapokuwa tunapata uwezo…….kile tulichonacho tukitumie vizuri kwani milango imefunguka.

Mazingira ni mazuri na ndiyo maana tunaendelea kuhamasisha wawekezaji na wafanyabiashara kuja kuwekeza Tanzania.

Mwana Diplomasia namba moja Mhe. Rais Samia amekuwa mstari wa mbele kutusaidia katika hili na hata juzi alipokutana na mabalozi na wakuu wa mashirika ya kimataifa aliweza kuwaeleza kuwa Tanzania ipo pamoja na kwamba tunaenda wote katika kufanikisha malengo ya watanzania yaweze kuboreka Zaidi.

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Nassor Mbarouk (Mb), Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine pamoja na Naibu katibu Mkuu Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Fatma Rajab.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akifurahia jambo alipokuwa akizungumza na Watumishi wa Wizara jijini Dodoma
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Nassor Mbarouk (Mb), akizungumza na watumishi wa Wizara kwenye kikao kilichofanyika jijini Dodoma 

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akizungumza na watumishi wa Wizara kwenye kikao kilichofanyika jijini Dodoma 

Kutoka kushoto; Naibu katibu Mkuu Mhe. Balozi Fatma Rajab, Naibu Waziri Mhe. Balozi Nassor Mbarouk (Mb), Waziri Mhe. Balozi Liberata Mulamula, Mkurugenzi Msaidizi Menejimenti ya Rasilimali Watu Bw. Peter Bunyazu wakiwa kwenye kikao na Watumishi wa Wizara kilichofanyika jijini Dodoma
Sehemu ya Wakuu wa Idara na Vitengo (mstari wa mbele) wakifuatilia Kikao kilichokuwa kikiendelea baina Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula na watumishi wa Wizara.
Kikao kikiendelea

Kikao kikiendelea

Picha ya pamoja Meza Kuu na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Picha ya pamoja Meza Kuu na Wakuu wa Taasisi zilipo chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Picha ya pamoja Meza Kuu na baadhi ya Watumishi wa Wizara

TANZANIA NA MAURITIUS ZASAINI MKATABA WA JUMLA

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Mauritius zimesaini Mkataba wa Jumla (General Framework Agreement - GFA)

Mkataba huo umesainiwa na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Mauritius mwenye makazi yake Harare Zimbabwe Mhe. Prof. Emmanuel Mbennah pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kikanda na Biashara za Kimataifa ya nchini Mauritius Mhe. Balozi Haymandoyal Dillum na kushuhudiwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kikanda na Biashara za Kimataifa Mhe. Alan Ganoo  

Mkataba huo pamoja na mambo mengine utaimarisha uhusiano wa kiuchumi, kisayansi na kiutamaduni. Mkataba huo pia utaanzisha Tume ya Pamoja ya Kudumu baina ya Nchi itakayokuwa ikifuatilia utekelezaji wa masuala mbalimbli kuhusu ushirikiano wa Tanzania na Mauritius. Hafla ya Uwekaji saini ilihudhuriwa pia na Viongozi wa Serikali na Taasisi kutoka Sekta Binafsi.

Aidha, kwa nyakati tofauti Balozi Mbennah alikutana kwa mazungumzo na Waziri mwenye dhamana na masuala ya Biashara Mhe. Soodesh Satkam Callichurn na Waziri mwenye dhamana na masuala ya Viwanda Mhe. Soomilduth Bholah. 

Mazungumzo na viongozi hao yalijikita katika utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi ili Tanzania na Mauritius ziweze kunufaika na fursa zilizopo katika Nchi hizo.

Balozi waTanzania nchini Mauritius Mhe. Prof. Emmanuel Mbennah pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kikanda na Biashara za Kimataifa ya nchini Mauritius Mhe. Balozi Haymandoyal Dillum wakisaini Mkataba wa Jumla (General Framework Agreement - GFA) na kushuhudiwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kikanda na Biashara za Kimataifa Mhe. Alan Ganoo

Balozi waTanzania nchini Mauritius Mhe. Prof. Emmanuel Mbennah katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kikanda na Biashara za Kimataifa ya nchini Mauritius Mhe. Balozi Haymandoyal Dillum na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kikanda na Biashara za Kimataifa Mhe. Alan Ganoo mara baada ya kusaini Mkataba wa Jumla (General Framework Agreement - GFA) 

Balozi waTanzania nchini Mauritius Mhe. Prof. Emmanuel Mbennah akibadilishana Mkataba wa Jumla na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kikanda na Biashara za Kimataifa ya nchini Mauritius Mhe. Balozi Haymandoyal Dillum  

Balozi wa Tanzania nchini Mauritius Prof. Emmanuel Mbennah akizungumza na Waziri Mkuu Mhe. Pravind Kumar Jugnauth, ambapo Mhe. Jugnauth ameipongeza Tanzania na Mauritius kuweka saini Mkataba wa Jumla ambao utaongeza wigo wa ushirikiano kwa nchi hizo mbili 


Thursday, January 27, 2022

MKUTANO WA 19 WA MAWAZIRI WA MAMBO YA NJE WA AFRIKA NA NORDIC KUFANYIKA JUNI 2022 FINLAND


Na Mwandishi Wetu, Dar

Mkutano wa 19 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Afrika na nchi za Nordic unatarajiwa kufanyika mwezi Juni 2022 nchini Finland.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Finland nchini Mhe. Riitta Swan leo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Katika kuendeleza na kuimarisho ushirikiano wa nchi hizo mbili viongozi hao wamependekeza kufanikisha ziara ya Mhe. Waziri Mulamula nchini Finland pamoja na ushiriki wake katika mkutano wa 19 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Nordic utakaofanyika nchini Finland mwezi Juni 2022. 

Katika mazungumzo ya viongozi hao, Balozi Mulamula amemhakikishia Balozi Swan kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana kwa karibu na Finland katika kuhakikisha Mataifa hayo yanashirikiana kijamiii, kisiasa na kiuchumi.

"Finland amekuwa mdau Mkubwa wa Maendeleo hapa nchini kwetu hasa katika sekta ya fedha hususan katika masuala ya kodi, mazingira, tehama, uongozi pamoja na uwezeshaji wa wanawake........pia tumekubaliana kuendeleza ushirikiano wetu kwa Maendeleo endelevu," amesema Balozi Mulamula.

Katika tukio jingine, Waziri Mulamula amekutana kwa mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Benki ya Stanbink Tanzania Bw. Kevin Wingfield
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula katika mazungumzo na Balozi wa Finland nchini Mhe. Riitta Swan leo katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akiteta jambo na  Balozi wa Finland nchini Mhe. Riitta Swan pamoja na Afisa kutoka Ubalozi wa Finland nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na Balozi wa Finland nchini Mhe. Riitta Swan, wengine ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushrikiano wa Afrika Mashariki Balozi Swahiba Mndeme, Bi. Kisa Mwaseba Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje pamoja na Afisa kutoka Ubalozi wa Finland 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akiwa katika mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Benki ya Stanbink Tanzania Bw. Kevin Wingfield yaliyofanyika katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam



TANZANIA NA INDIA KUONGEZA MAENEO YA USHIRIKIANO

Na Mwandishi wetu, Dar

Tanzania na India zimeahidi kuongeza maeneo mapya ya ushirikiano katika kuhakikisha maendeleo endelevu kwa maslahi mapana ya pande zote mbili.

Ahadi hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula wakati akihutubia sherehe za maadhimisho ya 73 ya Jamhuri ya India jana jioni Jijini Dar es Salaam.

Tanzania na India zimedhamiria kufanya kazi kwa karibu katika kutafuta njia bora ya kufungua fursa mpya na kuimarisha fursa mpya za biashara na uwekezaji zilizopo kati ya nchi hizo.

“Kuanza kwa safari za ndege za moja kwa moja kutoka Dar es Salaam hadi Mumbai kwa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) na kufunguliwa kwa soko la parachichi nchini India ni miongoni mwa hatua zilizochukuliwa ili kuimarisha na kukuza uhusiano wetu katika sekta za biashara na uwekuzaji pamoja na utalii kati ya India na Tanzania,” Amesema Balozi Mulamula. 

Pamoja na mambo mengine, Balozi Mulamula ameongeza kuwa Tanzania na India kwa sasa zimeanzisha ushirikiano katika usambazaji wa nishati, ujenzi wa miundombinu na Kilimo. Matarajio ya kuimarisha ushirikiano unaoendelea kati ya nchi hizi mbili ni mazuri na yanatia matumaini. 

“Uwekezaji wa India pamoja na idadi ya Wahindi wanaotembelea Tanzania kwa madhumuni ya kuwekeza katika sekta za madini, utalii, viwanda, kilimo, usindikaji wa mazao ya kilimo, nishati, usafirishaji, ujenzi, huduma za fedha na maendeleo ya rasilimali watu unaendelea kuongezeka kwa kasi,” amesema Balozi Mulamula.

Kwa upande wake, Balozi wa India nchini, Mhe. Binaya Srikanta Pradhan amesema kuwa Tanzania imekuwa na uhusiano mzuri na India ambapo uhusiano huo umekuwa ni chachu ya maendeleo kwa mataifa yote mawili na umepelekea kuongeza maeneo mapya ya ushirikiano.

“Ushirikiano na mshikamano uliopo baaina ya mataifa yetu mawili umekuwa chachu ya maendeleo na lengo la ushirikiano wetu yetu ni kukuza uchumi wetu,” amesema Balozi Pradhan 

Aidha, Balozi Pradhan amebainisha kuwa Tanzania itaendelea kuwa ya kipekee kwa taifa la India kutokana na mshikamano ambao umepelekea mataifa haya kufanya biashara, uwekezaji, kujenga uwezo, ujenzi wa miundiombinu pamoja na maendeleo ya kiuchumi.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akihutubia sherehe za maadhimisho ya 73 ya Jamhuri ya India jana jioni Jijini Dar es Salaam

Balozi wa India nchini, Mhe. Binaya Srikanta Pradhan akihutubia sherehe za maadhimisho ya 73 ya Jamhuri ya India jana jioni Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula. 

Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akisalimiana na Kiongozi wa Mabalozi nchini ambaye pia ni Balozi wa Visiwa vya Comoro nchini Mhe. Dkt. Ahmada El Badaoui Mohamed 

Sherehe za maadhimisho ya 73 ya Jamhuri ya India zikiendelea jana jioni Jijini Dar es Salaam

Balozi Mulamula na baadhi ya Mabalozi wakifuatilia sherehe za maadhimisho ya 73 ya Jamhuri ya India jana jioni Jijini Dar es Salaam

Sehemu ya Mabalozi wakifuatilia sherehe za maadhimisho ya 73 ya Jamhuri ya India jana jioni Jijini Dar es Salaam

Sherehe za maadhimisho ya 73 ya Jamhuri ya India jana jioni Jijini Dar es Salaam

Mabalozi na wageni waalikwa wakifuatilia sherehe za maadhimisho ya 73 ya Jamhuri ya India  

Sehemu ya Mabalozi wakifuatilia sherehe za maadhimisho ya 73 ya Jamhuri ya India  


Wednesday, January 26, 2022

TANZANIA, MOROCCO ZAKUBALIANA KUIMARISHA USHIRIKIANO

Tanzania na Morocco zimekubaliana kuimarisha ushirikiano katika nyanja za biashara na uwekezaji, elimu, utalii, uwezeshaji wa kiuchumi kwa wanawake na vijana.

Makubaliano hayo yamefikiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Morocco Bw. Nasser Bourita walipofanya mkutano wa kwa njia ya mtandao. Balozi Mulamula ameshiriki katika mkutano huo akiwa katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

“Tumezungumzia masuala ya kuimarisha uhusiano wetu baina ya Tanzania na Morocco na tumepitia makubaliano yaliyofikiwa wakati wa ziara ya Mfalme wa Morocco alipotembelea Tanzania mwaka 2016 pamoja na kuangalia mikataba mbalimbali iliyotiwa saini wakati wa ziara ya Mfalme wa Morocco ……… laikini pia tumejadili umuhimu wa kuwa na tume ya pamoja ya ushirikiano,” Amesema Balozi Mulamula.

Katika mkutano huo, viongozi hao wamejadili na kukubaliana kuimarisha ushirikiano wa karibu katika sekta za biashara na uwekezaji, utalii, elimu hasa katika kuongeza idadi ya ufadhili wa masomo kwa watanzania kutoka wanafunzi 30 hadi 50.

“Morocco ni nchi inayopata watalii wengi, hivyo tumekubaliana kushirikian kwa karibu zaidi ili kuweza kupata uzoefu ni njia gani wanatumia katika kukuza sekta ya utalii,” ameongeza Balozi Mulamula.

Katika tukio jingine, Balozi Mulamula amekutana na kufanya mazungumzo na Kaimu Balozi wa Oman nchini Dkt. Salim Saif Al Harbi katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam. 

Mazungumzo ya viongozi hao yamelenga kujadilia masuala mbalimbali ya kuendeleza na kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya Serikali ya Tanzania na Oman.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akishiriki mkutano wake na Waziri wa Mambo ya Nje wa Morocco Bw. Nasser Bourita. Mkutano huo umefanyika kwa njia ya mtandao.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akifuatilia mkutano 
Waziri wa Mambo ya Nje wa Morocco Bw. Nasser Bourita akimsikiliza Balozi Mulamula (hayupo pichani) katika mkutano uliofanyika kwa njia ya mtandao 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akimueleza jambo Kaimu Balozi wa Oman nchini Dkt. Salim Saif Al Harbi walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Kikao baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula na Kaimu Balozi wa Oman nchini Dkt. Salim Saif Al Harbi kikiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam



HOTUBA YA WAZIRI MULAMULA KWENYE DIPLOMATIC SHERRY PARTY IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

BOFYA HAPA KUSIKILIZA HOTUBA YA MHE. WAZIRI MULAMULA KWENYE DIPLOMATIC SHERRY PARTY ILIYOFANYIKA TAREHE 24 JANUARI 2022, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM


Tuesday, January 25, 2022

HABARI PICHA DIPLOMATIC SHERRY PARTY IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan jana aliwaalika Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini pamoja na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa katika Sherehe za Mwaka Mpya 2022 kwa Mabalozi (Diplomatic Sherry Party) Ikulu – Dar es Salaam.

Pamoja na mambo mengine, katika sherehe hizo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alisema Sera Mpya ya Mambo ya Nje itaendelea kuzingatia Diplomasia ya Uchumi na kuakisi maendeleo mapya kama vile uchumi wa bluu, mabadiliko ya tabianchi, uchumi wa kidigitali pamoja kukuza lugha ya Kiswahili kama lugha ya kidiplomasiana kibiashara. 

Awali, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula aliwahakikishia Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini pamoja na Waakilishi wa Mashirika ya Kimataifa kuwa Tanzania chini ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kuimarisha uhusiano wake kila wakati. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongea na Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini pamoja na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa katika Sherehe za Mwaka Mpya 2022 kwa Mabalozi (Diplomatic Sherry Party) Ikulu – Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akitoa hotuba yake wakati wa Sherehe za Mwaka Mpya 2022 kwa Mabalozi (Diplomatic Sherry Party) Ikulu – Dar es Salaam

Kiongozi wa Mabalozi nchini ambaye pia ni Balozi wa Visiwa vya Comoro nchini Mhe. Dkt. Ahmada El Badaoui Mohamed akihutubia wakati wa Sherehe za Mwaka Mpya 2022 kwa Mabalozi (Diplomatic Sherry Party) Ikulu – Dar es Salaam

Sehemu ya Uongozi wa Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ukifuatilia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa Sherehe za Mwaka Mpya 2022 kwa Mabalozi (Diplomatic Sherry Party) Ikulu – Dar es Salaam

Baadhi ya Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa wakiwa katika  Sherehe za Mwaka Mpya 2022 kwa Mabalozi (Diplomatic Sherry Party) Ikulu – Dar es Salaam

Baadhi ya Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa wakiwa katika  Sherehe za Mwaka Mpya 2022 kwa Mabalozi (Diplomatic Sherry Party) Ikulu – Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Balozi wa Finland hapa nchini Mhe. Riitta Swan wakati wa Sherehe za Mwaka Mpya 2022 kwa Mabalozi (Diplomatic Sherry Party) 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi mbalimbali katika Sherehe za Mwaka Mpya 2022 kwa Mabalozi (Diplomatic Sherry Party) 






Saturday, January 22, 2022

BALOZI MULAMULA AFANYA MKUTANO KWA NJIA YA SIMU NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA SWEDEN

 Na Mwandishi wetu, Dar

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) amefanya mkutano kwa njia ya simu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Sweden Mhe. Ann Linde katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Viongozi hao pamoja na mambo mengine, wamejadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Sweden ikiwemo vipaumbele vya pande zote mbili kuelekea Mkutano wa Wakuu wa Nchi baina ya nchi za Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika (European Union - African Union Summit) uliopangwa kufanyika tarehe 17 – 18 Februari 2022.

Katika tukio jingine, Balozi Mulamula amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Somalia nchini Mhe. Zahra Ali Hassan katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam ambapo mazungumzo yao yamelenga kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Somalia
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akizungumza kwa njia ya simu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Sweden Mhe. Ann Linde

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akizungumza kwa njia ya simu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Sweden Mhe. Ann Linde. wengine ni Maafisa waandamizi Wizarani Bw. Charles Mbando na Bi. Agnes Kiama. 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Balozi wa Somalia nchini Mhe. Zahra Ali Hassan katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Mazungumzo baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula na Balozi wa Somalia nchini Mhe. Zahra Ali Hassan yakiendelea


Friday, January 21, 2022

BALOZI MULAMULA APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO UNHCR, UNFPA

Na Mwandishi wetu, Dar

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) amepokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) Bibi. Mahoua Parums pamoja na Mwakilishi Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu (UNFPA) Bw. Mark Bryan Schreiner katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Balozi Mulamula amewaeleza Bibi. Parums na Bw. Schreiner kuwa UNHCR na UNFPA zimekuwa na mchango mkubwa kwa kuiunga mkono Serikali ya Tanzania katika kushughulikia masuala ya wakimbizi pamoja na kukuza maendeleo.

“Tumekubaliana na UNHCR kuendelea kushirikiana kwa karibu pamoja na Wizara ya Mambo ya Ndani katika mchakato wa kurudisha wakimbizi wa Burundi nchini kwao kusudi hali ya Burundi iendelee kutengamaa kwani kurudi kwa wakimbizi hao kutachangia maendeleo ya Burundi,” amesema Balozi Mulamula.

Balozi Mulamula ameongeza kuwa itakumbukwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye alipofanya ziara ya kitaifa hapa nchini Oktoba 2021 alitoa rai ya wakimbizi wa Burundi warudi nchini kwao ili kuweza kuchangia maendeleo ya Taifa hilo.  

Pia Balozi Mulamula ameongeza kuwa Mwakilishwa wa UNFPA amekuja wakati muafaka ambapo Serikali inatarajia kuanza zoezi la Sensa mwezi Augusti 2022 na hivyo kutoa rai kwa Shirika hilo kuwashirikisha na kuwawezesha vijana na wanawake wa kitanzania katika maendeleo ya teknolojia.  

“Rai yangu kwao ni kuwahusisha vijana na wanaweke kwani UNFPA mbali na kushughulika na idadi ya watu wana program ya kuwashirikisha na kuwawezesha vijana ni vyema washirikiane kwa pamoja na Mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa kwa maendeleo ya pande zote mbili,” Amesema Balozi Mulamula.

Kwa upande wake Mwakilishi wa UNHCR Bibi. Parums ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuwapokea na kuwalinda wakimbizi kwa muda mrefu.

“Tumekubaliana kushirikiana kwa pamoja na Serikali katika kuwalinda na kuwasaidia wakimbizi na kuwapatia baadhi ya mahitaji muhimu……tunaomba tuendeleze ushirikiano huu kwa maendeleo yetu,” amesema Bibi. Mahoua.

Nae Mwakilishi wa UNFPA, Bw. Schreiner amesema UNFPA itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuhakikisha kuwa inasonga mbele kimaendeleo ikiwa ni pamoja na kusaidia katika zoezi la Sensa linalotarajiwa kufanyika Augosti 2022 ili kuiwezesha Tanzania kupata takwimu sahihi kuhusu idadi ya watu na kuiwezesha kusonga mbele kimaendeleo.

Katika tukio jingine, Waziri Mulamula amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Bibi. Sarah Gordon-Gibson.

Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamejadiliana masuala mbalimbali ya kuendeleza na kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya Serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania na WFP.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) Bibi. Mahoua Parums katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Mwakilishi Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu (UNFPA) Bw. Mark Bryan Schreiner katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Mwakilishi wa UNHCR, Bibi. Mahoua Parums akiteta jambo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula 

Kikao baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na Mwakilishi wa UNHCR, Bibi. Mahoua Parums kikiendelea 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimueleza jambo Mwakilishi wa UNFPA Bw. Mark Bryan Schreiner katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam



Mwakilishi wa UNFPA Bw. Mark Bryan Schreiner akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Bibi. Sarah Gordon-Gibson