Monday, November 30, 2015

Balozi Mulamula akutana kwa mazungumzo na Kamishna wa masuala ya Afrika wa Ujerumani

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Balozi Georg Schmidt, Kamishna anayeshughulikia  masuala  ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani ambaye yupo katika ziara ya kikazi hapa nchini. Mazungumzo yao yalijikita kwenye masuala ya kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizi mbili hususan kwenye maeneo ya biashara na uwekezaji.
Mazungumzo yakiendelea
Mkurugenzi wa Idara y Ulaya na Amerika, Balozi Joseph Sokoine (kushoto), na Afisa Mambo ya Nje, Bi. Olivia Maboko wakifuatilia mazungumzo kati ya Balozi Mulamula na Balozi Schmidt  (hawapo pichani)
Mazungumzo yakiendelea
Balozi Mulamula akiagana na mgeni wake Balozi Schmidt mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.



Picha na Reginald Philip

Rais Magufuli Aonana na Mabalozi wa China na Korea Kusini, Ikulu jijini Dar Leo

Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Balozi wa Korea ya Kusini hapa nchini Mhe. Chung IL, wakati akimkaribisha na kufanya nae mazungumzo, Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 30, 2015.
Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Korea ya Kusini hapa nchini Mhe. Chung IL, Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 30, 2015.
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu Youqing, Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 30, 2015.
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu Youqing, Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 30, 2015.

Saturday, November 28, 2015

UN wakishirikiana na Ubalozi wa Palestina wafanya maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya mshikamano na watu wa Palestina

Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Abdallah Kilima (katikati), Kaimu Balozi wa Palestine Derar Ghannam (kulia) pamoja na Balozi wa Sudan nchini Tanzania, Dkt. Yassir Mohammed Ali wakikata utepe kwa ajili ya maonesho ya picha za matukio mbalimbali yanayoendelea nchini Palestina hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mshikamano na watu wa Palestina yaliyofanyika katika Chuo cha Diplomasia, Kurasini jijini Dar. 
Kaimu Balozi wa Palestina Derar Ghannam (wa kwanza kulia) akimuonyesha picha Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Abdallah Kilima (katikati) za matukio ya mauaji ya watu nchini Palestina yanayofanywa na Waisraeli ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mshikamano na watu wa Palestina yaliyofanyika katika Chuo cha Diplomasia, Kurasini jijini Dar. 

Afisa habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi Stella Vuzo (kulia) akitazama picha za wananchi wa Palestina waliouliwa na kutokana na mapigano ya Palestina na Israel yanayosababisha vifo vya watu wengi wasiokuwa na hatia.  
Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Abdallah Kilima akisoma hotuba yake mbele ya Mabalozi, wanafunzi wa chuo cha Diplomasia pamoja na wageni waalikwa waliofika kwenye maadhimisho ya ya siku ya kimataifa ya mshikamano na watu wa Palestina yaliyofanyika katika Chuo cha Diplomasia, Kurasini jijini Dar. 
Balozi wa Sudan nchini Tanzania, Dkt. Yassir Mohammed Ali akisoma hotuba yake wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mshikamano na watu wa Palestina.  
Baadhi ya Mabalozi waliofika kwenye maadhimisho hayo wakiendelea kufuatilia yanayojiri.  
Naibu Mkurugenzi wa Mipango Utawala na Fedha wa Chuo cha Diplomasia, Dk.Bernard Achiula akizungumza jambo wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika chuoni hapo. 
Prof Josephat Kanywanyi ,Chairperson Tanzania- Palestine Solidarity committee akitolea ufafanuzi kuhusu mahusiano ya Tanzania na Palestina wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mshikamano na watu wa Palestina.  
Wanafunzi wa Chuo cha Diplomasia wakiendelea kusikiliza kwa makini kinachozungumzwa kutoka meza kuu.  
Baadhi ya Mabalozi waliofika kwenye maadhimisho hayo wakiendelea kufuatilia yanayojiri. 
Mgeni rasmi akiwa kwenye picha ya Pamoja na Viongozi mbalimbali pamoja mabalozi.  
Viongozi wakiwa kwenye picha na wanafunzi wa Chuo cha Diplomasia.


Na Mwandishi wetu

UN Tanzania ikishirikiana na Ubalozi wa Palestina nchini waadhimisha Siku ya Kimataifa na Mshikamano na watu wa Palestina na Tanzania katika Chuo cha Diplomasia Kurasini jijini Dar es salaam mwishoni mwa juma na kukutana na mabalozi wa wa nchi mbalimbali akiwepo Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Abdallah Kilima, Kaimu Balozi wa Palestina Derar Ghannam na Balozi wa Sudan nchini Tanzania, Dkt. Yassir Mohammed Ali ambapo ikiwa kuendeleza ushirikiano pamoja na mfululizo wa maonesho ya picha mbalimbali za matukio yanayoendelea huko nchini Palestina.

Mabalozi hao ambao walikutana katika jijini Dar es salaam kwaajili ya kuadhimisha siku hiyo ya kumbukumbu za picha za mapigano ya Palestina kwa ajiri ya kudumisha upendo na mshikamano pia mabalozi hao wameuomba umoja wa mataifa kuweza kuchukua hatua za ziada zitakazo pelekea nchi hiyo kuwa huru na kuweza kuendelea kufanya shughuli mbalimbali za kimaendeleo.

Mshauri Mwandamizi wa Utawala kutoka UNDP, Steve Lee akizungumza kwa niaba ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez alisema kuwa uhusiano wa Palestina na Umoja wa Mataifa katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mshikamano na watu wa Palestina alisisitiza kuwa na na umoja baina ya nchi zote mbili hususani Palestina kuweza kupata uhuru na kutambulika kuwa ni nchi nyenye mipaka yake binafsi ili kuepusha mapigano hayo yasiweze kutokea na kila mtu aweze kuishi na amani akiwa ndani ya nchi yake na kuweza kufanya maendeleo ya nchi. Na aliweza kuziomba nchi mbalimbali kulitambua taifa la Palestina kama nchi kamili tofauti na inavyotambulika kwa sasa.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo ya ufunguzi wa siku ya maonesho ya picha Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Abdallah Kilima amesema wamefanya hivyo kwani ni hari ya kuwatakia heri Wapalestine wote kwani watu wote waparestine walipoteza uhuru na kwa sasa wanautafuta uhuru kwani nchi wanayo lakin hawako huru kwahiyo ni lazima tuwaunge mkono kwa kuweza kuadhimisha siku hii sehemu mbalimbali tunayoishi.

Kwa upande wa Afisa habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa(UNIC), Bi Stella Vuzo amesema wameamua kuwa na maadhimisho kwani ndani ya miaka 50 Palestina wamekuwa hawajatambulika kama taifa lenye mipaka yake ambapo kumekuwa na migogoro ya mda mrefu ambao unawahusu wa Palestine na wayahudi ambao upo tangu mwaka 1947,wakati katika maadhimio walio fikiana ni kuwa na mataifa mawili ndani ya eneo moja ambap mpaka sasa Israel pekee ndo iliyo pata kuwa hali ya taifa lenye mipaka yake wakati .


Kila siku Israel huwa wanaleta vita ndani ya Palestine, sasa maadhimisho haya ni kwa ajili ya kuwaunga mkono kwa vitendo vinavyo endelea huko si vizuri. Pia aliwaomba viongozi wa pande zote mbili kuweza kuketi na kuweza kuweka maadhimio mapya kwaajili ya kuepusha mapigano yanayokuwa yakitokea kila siku baina ya nchi hizo mbili. Pia katika siku hiyo waliweza kuzindua picha za matukio ya vifo pamoja na watu walioumia kutokana na vita Palestina na Israel zilizo kuwa zimeandaliwa kwa Tanzania kwa ajili ya kuonyesha dunia matukio yanayoendelea katika nchi za Mashariki ya mbali hii yote ni kwa kuwa Palestina ina ushirikiano na Tanzania na kuwaombea katika kuelekea hali ya utulivu.

Friday, November 27, 2015

Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje amuaga Balozi wa Korea Kusini

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula (kulia) akimkabidhi zawadi ya mchoro wa picha ya binti wa kimaasai na shati la kitenge alipokuwa akimuaga Balozi wa Jamhuri ya Korea Kusini, Mhe. Chung II ambaye amemaliza muda wake wa uwakilishi nchini. 
     
Balozi Mulamula akizungumza na Balozi Chung II .
Balozi Chung II naye akimweleza jambo Balozi Mulamula wakati wa mazungumzo yao.
Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Balozi Mbelwa Kairuki (kushoto) na Afisa Mambo ya Nje, Bw. Khatibu Makenga nao wakifuatilia kwa  mazungumzo kati ya  Balozi Mulamula na Balozi Chung II (hawapo pichani).  
Balozi Mulamula (kulia) na Balozi Chung II wakifurahia jambo kwa pamoja wakati wa mazungumzo yao
Mazungumzo yakiendelea
 Balozi Mulamula akiagana na Balozi wa Jamhuri ya Korea Kusini aliyemaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini Mhe. Chung II mara baada ya kumaliza mazungumzo

Picha na Reginald Philip 

=============================================


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula amempongeza Balozi wa Jamhuri ya Korea Kusini hapa nchini, Mhe. Chung II kwa kuiwakilisha vyema nchi yake na kupelekea miradi mingi ya maendeleo ikiwemo ile ya miundombinu kukamilika.   
       
Balozi Mulamula alitoa pongezi hizo leo alipokutana na Balozi Chung II ambaye alifika Wizarani kwa lengo la kuaga baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini.

Balozi Mulamula alisema kuwa Jamhuri ya Korea Kusini imekuwa ni miongoni mwa nchi ambazo Tanzania inashirikiana nazo kwa karibu katika kutekeleza miradi ya maendeleo. Alieleza kuwa, nchi hiyo imeshiriki kikamilifu kutekeleza miradi  yenye manufaa makubwa kwa Tanzania  katika Sekta mbalimbali zikiwemo za kiuchumi, biashara na uboreshaji wa miundombinu. 

"Nakupongeza Mhe. Balozi kwa uwakilishi wako mzuri kwani katika kipindi chote ulichokuwepo nchini na kupitia Serikali yako umeweza kukamilisha miradi mikubwa ukiwemo ule wa Daraja la Kikwete lililojengwa katika Mto Malagarasi huko Kigoma” alisema Balozi Mulamula.

Aidha, alimhakikishia ushirikiano kutoka Wizarani na Serikalini kwa ujumla kwa Balozi mpya atakayeteuliwa na nchi hiyo kuja nchini.

Kwa upande wake, Balozi Chung II ambaye amekuwepo nchini kwa kipindi cha miaka mitatu aliishukuru Wizara na Serikali kwa ujumla kwa ushirikiano mzuri aliokuwa akiupata wakati wote wa uwakilishi wake. Pia aliahidi kuendelea kuitangaza Tanzania nchini kwake ili kuendeleza mahusiano mazuri yaliyopo kati ya nchi hizi mbili.

-Mwisho-





 
 

Thursday, November 26, 2015

Katibu Mkuu akutana kwa mazungumzo na Balozi wa Kuwait

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Liberata Mulamula (kulia), akizungumza na Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem Ibrahim Al-Najem alipokuja kumtembelea Wizarani. Mazungumzo hayo yalijikita katika kuimarisha mahusiano zaidi kati ya Tanzania na Kuwait katika sekta mbali mbali zikiwemo zile kiuchumi na biashara. Pia Balozi Jasem Ibrahim Al-Najem alitumia fursa hiyo kuipongeza Wizara na Watanzania kwa kumpata Rais wa Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mazungumzo yakiendelea huku Afisa Mambo ya Nje Bw. Tahiri Bakari (wa kwanza kulia) akisikiliza na kunukuu.

Picha na Reginald Philip

Azimio kuhusu watu wenye Ualibino lapitishwa kwa kauli moja


Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi akiwasilisha mbele ya wajumbe wa Kamati ya Tatu ya Baraza Kuu la Umoja wa Matifa Azimio kihusu watu wenye ualibino. Azimio hilo lililipitishwa kwa kauli moja na wajumbe wa Kamati hiyo.
Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Tatu ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wakiwa katika mkutano wao siku ya jumanne ambapo pamoja na kupitisha Azimio kuhusu watu wenye ualibino, azimio lililoandaliwa kwa pamoja kati ya Tanzania na Malawi, pia Kamati hiyo ilipitisha maazimio mengine kadhaa yanayohusiana na masuala mtambuka kama yale ya haki za mtoto,haki za binadamu, maendeleo ya vijana, usawa na uwezeshaji wa wanawake na utokomezaji wa umaskini.

Na Mwandishi Maalum, New York

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imewashukuru wajumbe wa Kamati ya Tatu ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa kupitisha kwa kauli moja Azimio linalotaka pamoja na mambo mengine Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuwasilisha taarifa kuhusu watu wenye ualibino.

Azimio hilo na ambalo liliandaliwa kwa pamoja kati ya Wakilishi za Kudumu za Tanzania na Malawi katika Umoja wa Mataifa, limepitishwa siku ya Jumanne baada ya majadiliano ya kina na jumuishi yaliyowashilikisha nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa.
Akiwasilisha Azimio hilo mbele ya wajumbe wa Kamati hiyo ambayo inahusika na masuala ya Haki za Binadamu, Utamaduni na Maendeleo ya Jamii, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi amesema
“Azimio hilo linalenga katika kuitaka jumuiya ya kimataifa kutambua na kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazowakabili watu wenye ualibino”

Akabainisha kwamba ni kwa kutambua changamoto hizo zikiwano za kielimu, kiafya na kiuchumi pamoja na hatari zinazowakabili kwa sababu tu ya kuwa na ualibino ndio maana Tanzania kwa kushirikiana na Malawi ziliamua kuanda na hatimaye kuwaalika nchi wanachama si tu kulijadili na kuboresha mapendekezo yaliyomo katika azimio hilo bali pia kuliunga mkono.

Balozi Tuvako Manongi akawaeleza wajumbe wa Kamati ya Tatu ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwamba, katika eneo la afya watu wenye ualibino wanakabiliwa na tatizo kubwa la kansa ya ngozi kutoka na hali hiyo. Tatizo alilosema linahitaji ushirikiano wa pamoja katika kuwasaidia.

“Azimio hili linalenga katika kuelezea pengo lililopo kuhusiana na changamoto zinazowakabili watu wenye ualibino hususani katika elimu, afya, na ajira . Matatizo yao na changamoto zao na kwa kuwa yanaingiliana yanahitaji ushiriano kati yetu sisi sote na ufumbuzi wa muda mrefu” akabinisha Balozi Manongi.

Na kuongeza kuwa hakuna matibabu au uponyaji kwa watu wenye ualibino lakini kuna baadhi ya nchi chache ambazo zimeweza kubuni sera za kijamii na za afya za kuwasaidia watu wenye ualibino. Na kwamba ushirikiano kati ya nchi hizo chache ambazo zina sera nzuri za afya na zile ambazo hazina uwezo mkubwa wa raslimali ni jambo ambalo Tanzania inapenda kupitia azimio hilo kuona ukiimarishwa na kuwa shirikishi.

“Tunawashukuru wale wote ambao wameshirikia katika majadiliano ya awali ya maandalizi ya Azimio hili kwa mchango wao wa mawazo lakini pia kwa kuliunga mkono Azimio hili. Hapashaka Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa atawasilisha taarifa yake kama alivyoombwa kupitia Azimio hili.

Kwa mujibu wa Azimio hilo,Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anatakiwa kuwasilisha Taarifa kuhusu watu wenye ualibino wakati wa kipindi cha Baraza Kuu la 72 la Umoja wa Mataifa.

Katika miaka ya hivi karibuni tatizo na changamoto zinazowakabili watu wenye ualibino limekuwa likipewa uzito wa aina yake katika Jumuiya ya Kimataifa.

Mwaka jana Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha Azimio ambalo lilitamka kwamba Juni 13 ya kila mwaka inakuwa siku ya Kimataifa ya watu wenye ualibino. Na mwezi Machi mwaka huu Baraza la Haki za Binadamu liliteua mtaalamu wa kujitegemea kuhusu haki za binadamu za watu wenye ualibino.

Azimio lililoandaliwa na Tanzania na Malawi ni mwendelezo wa juhudi kutafuta namba bora na jumuishi za kuwasaidia na kuwaendeleza watu wenye ualibino.