Wednesday, November 18, 2015

Rais Magufuli asaini Kitabu cha Maombolezo katika Ubalozi wa Ufaransa, awasili Mjini Dodoma kwa Gari

Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisaini kitabu cha Maombolezo
katika Ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es salaam kufuatia vifo vya Watu zaidi ya 120 vilivyotokana
na mashambulizi ya kigaidi jijini Paris majuzi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimpa pole Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Mama Malika Berak kufuatia vifo vya Watu zaidi 120 vilivyotokana na
mashambulizi ya kigaidi  majuzi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph  Magufuli akizungumza na
Balozi wa Ufaransa nchini Mama Malika Berak mara baada ya kusaini Kitabu cha Maombolezo na kutoa salamu za pole kwa Rais wa Ufaransa Mhe.  Francois Hollande kufuatia vifo vifo vya Watu zaidi 120 vilivyotokana na mashambulizi ya kigaidi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wa pili akiwa katika picha ya
pamoja na Balozi wa Ufaransa (kushoto) pamoja na Maofisa mbalimbali wa Ubalozi huo mara baada ya kutia saini kitabu cha maombolezo.
 
Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwasili mkoani Dodoma na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa
wa Dodoma Mhe. Chiku Galawa. Rais Magufuli amesafiri kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma kwa kutumia usafiri wa Gari.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.