Friday, November 6, 2015

Balozi Mulamula akutana na Wageni mbalimbali Wizarani

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula (kulia) na Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi Mhe. Alain Aime Nyamitwe, walikutana leo na kufanya mazungumzo hapa Wizarani, Mazungumzo yao yalijikita katika kukuza na kuimarisha Ushirikiano kati ya Tanzania na Burundi katika sekta mbalimbali
Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Mhe. Rajab Gamah (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Samweli Shelukindo (katikati) na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bi. Mindi Kasiga nao wakifuatilia kwa makini mazungumzo yaliyo kuwa yakiendelea kati ya Baozi Mulamula na Waziri Nyamwite (hawapo pichani).  
Waziri Nyamitwe hakusita kuelezea furaha yake ya kupata fursa ya kuhudhuria sherehe za Uapisho wa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli hapo jana.
Mazungumzo yakiendelea kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Mulamula (wa tatu kushoto) na Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi (wa pili kutoka kushoto), na wakwanza kushoto ni Balozi wa Burundi nchini Mhe. Issa Ntambuka

=====================
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula (kulia) amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Ubelgiji nchini Tanzania, Mhe. Paul A. Cartier. Viongozi walijadiliana namna ya kuboresha  mahusiano kati ya Tanzania na Ubekgiji katika sekta za Kiuchumia, Biashara na Kijamii

Balozi Mulmula akizungumza huku Balozi Cartier (wa kwanza kushoto) akimsikiliza. Mwingine katika picha ni Afisa Mambo ya Nje, Bi. Felista Rugambwa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na UShirikiano wa Kiamataifa, Balozi Liberata Mulamula akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Mhe. Dkt. Josephine Ojiambo (kushoto) aliyeiwakilisha Jumuiya hiyo kwenye sherehe za uapisho wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli hapo jana 
Balozi Mulamula akizungumza na Dkt. Ojiambo alipotembelea Wizarani leo
Balozi Liberata Mulamula akiwa katika picha ya pamoja na Dkt. Ojiambo
Picha ya pamoja


Picha na Reginald Philip

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.